| "Mimi naamini kabisa kwamba tutasaidia nchi yetu,
kuimarisha Umoja wake na Mapinduzi yake
na hivyo kuwa na uwezo mkubwa zaidi wa kusaidia
kuleta Umoja na Mapinduzi ya Afrika ikiwa sasa bila kusita tena tuaviunganisha vyama vyetu na kuwa Chama kimoja cha Mapinduzi."
— Mwalimu Nyerere — Mwalimu Julius K. Nyerere na wanachama na viongizi wa TANU na ASP walio wengi walikuwa na matarijo makubwa kwa Chama kimoja cha Mapinduzi. Miongoni mwa matarajio hayo ni kukamilisha Muungano wa Tanzania; kuleta maendeleo ya pamoja na haraka kwa nchi yetu; kumkomboa Mtanzaina na Mwafrika kifikra, kisiasa, kiuchumi na kijamii; na kusaidia kuharakisha kufikia lengo la kujenga nchi inayofuata siasa ya Ujamaa na Kujitegemea. Aidha, Chama kimoja cha Mapinduzi kilitarajiwa kushiriki kwa ukamilifu katika kutokomeza ukoloni katika Bara la Afrika na kwingineko duniani na kuendeleza siasa ya kutofungamana na upande wowote hasa kwa kuzingatia kwamba katika miaka ya 1970 na 1980 dunia ilikuwa bado imegawanyika kisiasa, kiuchumi na kiulinzi katika kambai mbili zenye uhasama. Kambi hizo ni ya Magharibi ikiongozwa na Marekani na ile ya Mashariki ikiongozwa na Umoja wa Kisovieti. Waasisi wa TANU na ASP walitambua kwamba kuwepo kwa vyama viwili katika mazingira ya siasa ya chama kimoja kulipunguza upeo, nguvu na umoja wao katika kuendeleza mapambano ya kujenga Ujamaa nchini na kushiriki kwa pamoja na kwa ukamilifu katika harakati za mapinduzi ya Tanzania, Afrika na dunia kwa jumla.
Endelea |