Habari Mpya

 
 Vichwa vya Habari
 Habari Nyinginezo
 Rudi Mwanzo
 
 


Hotuba za Mwenyekiti wa CCM
Fungua www.ccmtz.org/0hotubamwenyekiti.htm
12 May 2008

TAMKO LA HALMASHAURI KUU YA TAIFA KUHUSU MAZUNGUMZO YA MUAFAKA BAINA YA CCM NA CUF.
Halmashauri Kuu ya Taifa katika kikao chake cha tarehe 29 na 30 Machi, 2008 pamoja na mambo mengine kilipokea na kujadili taarifa ya Kamati ya CCM ya Mazungumzo kuhusu kuupatia ufumbuzi wa kudumu mpasuko wa kisiasa Zanzibar.
10 Apr 2008

Waziri Mkuu akabidhiwa ripoti ya Richmond
Waziri Mkuu, Bw. Mizengo Pinda, jana alikabidhiwa ripoti ya Timu iliyoundwa na serikali kuyafanyia kazi mapendekezo ya Kamati Teule ya Bunge iliyochunguza mchakato wa zabuni ya kampuni ya ``Richmond Development Company``.
27 Mar 2008

CCM Mvomero watakiwa kuvunja makundi
CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), kimemtaka Mbunge wa Mvomero, Suleiman Saddiq na Mweka Hazina wa chama hicho Taifa, Amos Makalla kuvunja makundi yao wilayani Mvomero, na kuonya kuwa endapo watashindwa kufanya hivyo, watachukuliwa hatua za kinidhamu, ikibidi kuwanyang’anya uanachama wao.
22 Mar 2008

Posho ya mafunzo kwa wanafunzi vyuoni kuwa 10,000/
SERIKALI imesikia kilio cha wanafunzi wa vyuo vikuu baada ya kutangaza kuongeza posho kwa ajli ya mafunzo kwa vitendo kutoka Sh 6,000 zinazodaiwa kuwa hazitoshi hadi Sh 10,000 kwa siku.
21 Mar 2008

RIPOTI YA TIMU YA KUPITIA MAPENDEKEZO YA KAMATI TEULE YA KUCHUNGUZA RICHMOND KUWASILISHWA WIKI IJAYO KWA WAZIRI MKUU
TIMU ndogo ya wataalam kutoka idara mbalimbali za serikali, iliyopewa jukumu la kupitia upya mapendekezo ya Kamati ya Bunge iliyochunguza mchakato wa zabuni ya mkataba wa kuzalisha umeme wa dharura ulioipa ushindi Kampuni ya Richmond, imemaliza kazi yake na inatarajia kuwasilisha ripoti yake wiki ijayo.
20 Mar 2008

Dk. Shein ataka Watanzania kuitangaza nchi yao
MAKAMU wa Rais, Dk. Ali Mohamed Shein, amesema Watanzania wanapaswa kuunga mkono jitihada za serikali katika kuitangaza Tanzania ili kuweza kupata wawekezaji wa kuja nchini.
20 Mar 2008

Mbowe azidi kubanwa kuhusu ufisadi
.Atakiwa alipe deni badala ya kulalamika
.Aambiwa ufisadi si kuing’ang’ania CCM
20 Mar 2008

UZINDUZI WA SHINA JIPYA LA CCM SOUTHAMPTON,UINGEREZA
Shina jipya la Chama Cha Mapinduzi Jijini Southampton, Uingereza lilizinduliwa rasmi tarehe 15 Machi 2008.
19 Mar 2008

MAKAMBA ASISITIZA SUBIRA MAZUNGUMZO YA MUAFAKA - UHURU
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi, Yussuf Makamba, amewataka viongozi na wanachama wa CCM kuwa na subira kuhusu mazungumzo ya muafaka kati ya CCM na CUF.
19 Mar 2008

WALIOBOMOLEWA NYUMBA TABATA DAMPO WAISHUKURU CCM
Wananchi waliobomolewa nyumba zao eneo la Tabata dampo, Dar es Salaam wameshukuru Chama Cha Mapinduzi kwa kuonyesha huruma kwao.
18 Mar 2008

NEC KUFANYIKA BUTIAMA
KIKAO cha Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama Cha Mapinduzi kwa mara ya kwanza katika historia ya Chama, kitafanyika kijiji cha Butiama, Musoma, mkoani Mara, mwishoni mwa mwezi huu.
17 Mar 2008

CCM London yampongeza Kikwete kwa uteuzi wa Pinda, na kuwa mwenyekiti wa AU
CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) tawi la Uingereza kimempongeza Rais Jakaya Kikwete kwa uteuzi wa Wazir Mkuu Mpya, Mheshimiwa Bw. Mizengo Pinda na kuchaguliwa kwake kuwa Mwenyekiti mpya wa umoja wan chi za Afrika (AU).
14 Feb 2008

Mkutano Mkuu wa Taifa wa Nane wa CCM
Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama Cha Mapinduzi inawakaribisha Wajumbe wote Mkoani Dodoma kwa ajili ya kuhudhuria Mkutano Mkuu wa Nane wa Taifa, utakaofanyika tarehe 3 – 4 Novemba 2007. Mkutano huo utakuwa ni wa uchaguzi.
23 Oct 2007

Tamko la Chama Cha Mapinduzi Kuhusu Mjadala wa Filamu ya Darwin’s Nightmare
CCM inaamini kwamba filamu hiyo, kwa nia na maudhui yake, imejikita katika kulivunjia hadhi na heshima Taifa letu na kulihujumu kiuchumi.
16 Aug 2006

Radio Uhuru-Rais Kikwete leo ahitimisha ziara Dar es Salaam
Rais JAKAYA KIKWETE leo anahitimisha ziara yake ya siku tatu mkoani Dar es Salaam kwa kutembelea na kukagua shughuli mbalimbali za kimaendeleo katika Manispaa ya Temeke kabla ya kuwahutubia wananchi hao katika uwanja wa Mbagala Zakhem.
29 Jul 2006

Taarifa Idara ya Itikadi na Uenezi ya CCM Kwa Mhariri wa Habari Gazeti la Mtanzania Kuhusu Shutuma za CUF kwa Katibu Mkuu wa CCM Mhe. Yusuf Rajab Makamba - 16/07/2006
Chama Cha Mapinduzi kimesema kauli liyotolewa na Chama cha CUF kuwa Katibu Mkuu wa CCM amekuwa akitoa kauli za kibabe ni dalili ya kukata tamaa kisiasa.
26 Jul 2006

Sekretarieti Mpya ya Halmashauri Kuu ya Taifa
Halmashauri Kuu ya Taifa ilifanya kikao chake cha kwanza chini ya Mwenyekiti mpya wa CCM, Mheshimiwa Rais Jakaya Mrisho Kikwete tarehe 25 Juni, 2006 Mjini Dodoma, mara tu baada ya Mkutano Mkuu wa Taifa wa Saba wa kawaida wa CCM.
26 Jun 2006

Majumuisho ya Mkutano Mkuu wa Saba wa Taifa wa CCM uliofanyika Chimwaga - Dodoma Tarehe 24 - 25 Juni, 2006
Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Saba wa Taifa wa Chama Cha Mapinduzi uliofanyika tarehe 24 - 25 Juni, 2006, Chimwaga Dodoma, chini ya Mwenyekiti wake Nd. Benjamin W. Mkapa, pamoja na mambo mengine umejadili na kutafakari kwa kina taarifa zifuatazo:
25 Jun 2006

Mwenyekiti ya Kung’atuka na Kuaga
Hotuba ya Mwenyekiti ya Kung’atuka na Kuaga Chimwaga 25 Juni, 2006
25 Jun 2006

Mkutano Mkuu Maalum wa Saba Wafunguliwa
Hotuba ya Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Ndugu Benjamin William Mkapa, Akifungua Mkutano Mkuu Maalum wa Saba wa CCM; Chimwaga, Dodoma, 24 Juni 2006
24 Jun 2006

Taarifa ya Kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa
Katika kikao chake kilichofanyika leo tarehe 23 Juni, 2006 Mjini Dodoma chini ya Mwenyekiti wa Chama Ndugu Benjamin William Mkapa, Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM imepokea taarifa na kufanya maamuzi kama ifuatavyo:-
24 Jun 2006

Taarifa ya Katibu Mkuu kwa Wanahabari Kuhusu Maandalizi ya Mkutano Mkuu wa CCM, Utakaofanyika Mjini Dodoma Tarehe 24 Hadi 25 Juni, 2006
Tarehe 24 na 25 ya mwezi huu wa Juni, kuna Mkutano Mkuu wa CCM wa Taifa. Mkutano Mkuu huu ni wa kawaida ulioitishwa kwa mujibu wa kifungu cha 105 kifungu kidogo cha 3 cha katiba ya CCM Toleo la Mei 2005.
22 Jun 2006

Radio Uhuru-Nusu ya wakazi wa kusini mwa Jangwa la Sahara wana vimelea vya kifua kikuu
Takwimu zinaonesha kuwa zaidi ya nusu ya watu wanaoishi kusini mwa Jangwa la Sahara wanavimelea vya ugonjwa wa kifua kikuu.
16 Jun 2006

Radio Uhuru-Rais Kikwete awataka watumishi kutopokea rushwa
Rais JAKAYA KIKWETE amewataka watumishi wa serikali kutotumia mishahara midogo wanayopata kama kigezo cha kuomba na kupokea rushwa.
16 Jun 2006

Radio Uhuru-Kamati Kuu ya CCM kukutana kesho kutwa.
Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama Cha Mapinduzi –CCM itakutana kesho kutwa kwa kikao chake cha siku moja jijini Dar es Salaam.
16 Jun 2006

Radio Uhuru-Watakiwa kufichua watoto walemavu waliofichwa majumbani
Jamii imeombwa kufichua watoto wenye ulemavu wa aina mbalimbali ambao wamefichwa ndani na wazazi wao kwa madai kwamba kuwa na watoto hao ni aibu katika familia husika.
16 Jun 2006

Radio Uhuru-RC Dodoma apiga marufuku uuzaji na ununuzi wa mahindi ambayo bado hayajakauka vizuri
Serikali Mkoani Dodoma imepiga marufuku mara moja kuuza na kununua mahindi ambayo hayajakauka kwa kiwango kinachotakiwa pamoja na kufungasha mahindi au nafaka zingine kwa ujazo mkubwa.
16 Jun 2006

Radio Uhuru- Kutoa elimu ya shughuli za idara mbalimbali za serikali
Serikali kupitia Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma imelenga kuwaelimisha watumishi wa umma ili kuelewa maadili ya kazi zao ili kujenga uelewa wa kazi wanazozifanya.
16 Jun 2006

Radio Uhuru-Madiwani Moshi wapewa changamoto ya uanzishwaji wa SACCOS katika kata zao
Baraza la madiwani la Halmashauri ya wilaya ya Moshi vijijini limeombwa kuwahamasisha wananchi kujiunga na vyama vya kuweka na kukopa -SACCOS ili waweze kukopeshwa na kupata mitaji itakayowawezesha kubuni biashara pamoja na miradi mbalimbali ya kiuchumi.
16 Jun 2006

Radio Uhuru-Jaji Luanda awataka watumishi wa idara za serikali kusaidiana kupunguza msongamano gerezani
Watumishi wa Idara za Mahakama, Polisi, Uhamiaji, Taasisi ya Kuzuia Rushwa, Hospitali, Magereza na mawakili wa mkoa wa Kagera wametakiwa kuweka msukumo katika kesi mbalimbali zinapofikishwa mahakamani ili kupunguza mrundikano wa kesi na mahabusu katika magereza.
16 Jun 2006

Radio Uhuru-Polisi Kilimanjaro kuweka masanduku ya maoni kila kata
Polisi mkoani Kilimanjaro, imesema itaweka masanduku ya maoni katika ofisi za kila kata, ili kuwawezesha wananchi kutoa taarifa za kuwepo kwa matukio ya uhalifu au utendaji mbovu wa baadhi ya askari.
14 Jun 2006

Radio Uhuru-Kampeni ya ukimwi kwa kupanda Mlima Kilimanjaro yaingiza Shilingi Milioni 350
Safari ya kupanda mlima Kilimanjaro iliyoandaliwa na kampuni ya uchimbaji wa madini ya Geita imefanikisha kupatikana kwa zaidi ya shilingi milioni 350 ambazo zitatumika kwa ajili ya mapambano dhidi ya ugonjwa wa ukimwi nchini.
14 Jun 2006

Radio Uhuru-Mhe.Wasira:Miradi ya Maji sasa kutekelezwa kwa haraka
Imeelezwa kuwa miradi ya maji inayofadhiriwa na benki ya dunia itatekelezwa haraka nchini katika kipindi cha mwaka wa fedha 2006/2007 kutokana na utaratibu wa benki hiyo uliopo sasa kurahisisha jukumu hilo
kwa kupeleka fedha hizo hazina.
14 Jun 2006

Radio Uhuru-Viongozi watakiwa kuwa mstari wa mbele kupima afya zao
Katibu wa Jumuiya ya Umoja wa Wanawake Mkoa wa Dar es Salaam –UWT- Bibi SAUDA MPAMBALYOTO ametoa wito kwa viongozi kuwa mfano wa kuigwa katika kupima ugonjwa wa ukimwi badala ya kusimama katika majukwaa na kuwalazimisha wananchi kwenda kupima.
14 Jun 2006

Radio Uhuru:Nagu-Serikali kutokata rufaa kuhusu marekebisho ya sheria ya uchaguzi ya 2000
Serikali imesema kuwa haitakata rufaa dhidi ya uamuzi wa Mahakama Kuu kuhusu marekebisho ya sheria ya uchaguzi ya mwaka 2000.
14 Jun 2006

KUPANGIWA VITUO VYA KAZI MAKATIBU WA CCM WA WILAYA
Katika kikao chake cha tarehe 27 Aprili, 2006 kilichofanyika mjini Dodoma, Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ilifanya uteuzi wa Makatibu wa Wilaya 17 wapya
24 May 2006

Serikali imesema kuna mafanikio katika utatuzi wa kero za Muungano
Waziri Mkuu Mheshimiwa EDWARD LOWASA na Waziri Kiongozi wa Zanzibar Mheshimiwa SHAMSI VUAI NAHODHA wamesema wamefanikiwa kwa kiasi kikubwa kujadili kwa pamoja kero zinazoukabili Muungano wa Tanzania.
22 May 2006

Ndg.Mangula asema Daraja la Ruvuma ni mwendelezo wa ukombozi
Imeelezwa kuwa kujengwa kwa daraja la mto Ruvuma ni mwendelezo wa harakati za ukombozi katiika nchi za kusini mwa Afrika ,ambapo baada ya uhuru nchi hizo sasa zinapambana kujikomboa kiuchumi kwa kupamba na umaskini.
22 May 2006

Dk.Shein asema matatizo ya Muungano ni lazima yafanyiwe kazi
Makamu wa Rais Dokta ALI MOHAMED SHEIN amesema matatizo ya Muungano hayatamazika iwapo maamuzi yanayochukuliwa na vikao halali katika kuyapatia ufumbuzi matatizo hayo hayatafanyiwa kazi.
22 May 2006

Rais Kikwete awataka watanzania kuuza kwa wingi bidhaa zake Nje
Rais JAKAYA KIKWETE ametoa wito kwa Watanzania kuzalisha kwa wingi bidhaa zinazounzwa nje, ili kulinda akiba ya fedha za kigeni ambayo inapungua kutokana na kasi ya kuongeza kwa bei ya mafuta duniani.
22 May 2006

Radio Uhuru-Waziri Kiongozi wa Zanzibar asisitizia umuhimu wa elimu bora
Waziri Kiongozi wa Zanzibar Mheshimiwa SHAMSI VUAI NAHODHA amesema Serikali katika kipindi cha mwaka 2005/2010 imelenga kuimarisha Elimu kwa kuwa na walimu bora zaidi.
18 May 2006

Radio Uhuru-Rais Bush wa Marekani ausifu uongezi wa Rais Kikwete
Rais GEORGE BUSH ameeleza kuridhishwa na kufurahishwa kwake kwa namna ambavyo Rais Jakaya Kikwete ameanza kazi ya kuongoza Tanzania.
18 May 2006

Radio Uhuru-Waziri Mkuu azungumzia wakulima wa kahawa
Waziri Mkuu Mheshimiwa EDWARD LOWASSA ameagiza asilimia 70 ya pato linalopatikana katika uuzaji wa zao la kahawa kupatiwa mkulima kutokana na gharama wanazotumia wakati wa upandaji hadi uvunaji wa zao hilo kuwa kubwa.
18 May 2006

Radio Uhuru-uchimbaji wa Gesi ya Mnazi Bay kukamilika Mwezi wa Nane mwaka huu
Kampuni ya ARMATUS ya Canada inayochimba gesi katika eneo la Mnazibay mkoani Mtwara inatarajia kukamilisha uchimbaji wa visima vya kutoa gesi itakayotumika kuzalishia umeme ifikapo Agusti mwaka huu.

18 May 2006

Radio Uhuru-Serikali yaanza kuboresha sekta ya sheria
Serikali imeanza mkakati wa kuboresha sekta ya sheria katika juhudi za kuboresha mazingira ya kazi.
18 May 2006

Radio Uhuru- Makatibu wilaya wapya wa CCM wapangiwa vituo vya kazi.
Sekretarieti ya Halmashauri kuu ya Taifa ya Chama cha Mapinduzi –CCM- imewapangia vituo vya kazi makatibu wa CCM wapya 17 wa Wilaya ambao waliteuliwa hivi karibuni mjini Dodoma.
18 May 2006

Radio Uhuru-Mhe. NAHODHA amesema kuna umuhimu wa tafiti zinazofanywa nchini kutangazwa.
Waziri Kiongozi wa Zanzibar Mheshimiwa SHAMSI VUAI NAHODHA amesema kuna umuhimu wa matokeo ya tafiti zinazofanywa nchini kutangazwa kwa wananchi ili ziweze kufanyiwa kazi na kuifaidisha jamii.
08 May 2006

Radio Uhuru-IGP MWEMA mawasiliano na taasisi nyingine yatasaidia kukomesha vitendo vya uhalifu.
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini Inspekta Jenerali SAID MWEMA, amesema ili kusaidia kazi ya kukomesha vitendo vya uhalifu nchini ni lazima kuwepo na mawasiliano na mahusiano ya karibu na taasisi nyingine za serikali na watu binafsi.
08 May 2006

Radio Uhuru-Waziri SOPHIA SIMBA amesema benki ya wanawake kuanzishwa mwakani.
Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Mheshimiwa SOPHIA SIMBA, amesema benki ya wanawake nchini inatazamiwa kuanza kazi mwaka ujao.
08 May 2006

Jumuiya ya Wazazi Taifa inatazamia kufanya Mkutano wa Baraza Kuu la wazazi Taifa.
Kaimu Katibu mkuu wa Jumuiya ya Wazazi ya Chama Cha Mapinduzi –CCM Ndugu COSMAS HINJU amesema Jumuiya hiyo inatazamia kufanya mkutano wa Baraza Kuu la wazazi taifa Mei 12 na 13 jijini Dar es Salaam.
08 May 2006

Rais KARUME wa Zanzibar leo ameapishwa kuwa mjumbe wa baraza la Mawaziri.
Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Mheshimiwa AMAN ABEID KARUME leo ameapishwa kuwa mjumbe wa baraza la mawaziri la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
08 May 2006

Radio Uhuru-Sekretarieti ya NEC kesho kutwa inaanza ziara ya siku tatu mkoa wa Dar es Salaam.
Wajumbe wa Sekretarieti ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM wakiongozwa na Mwenyekiti wao ambaye ni Katibu Mkuu wa CCM, Ndugu PHILIP MANGULA watakuwa na ziara ya siku tatu kuona uhai wa Chama katika mkoa wa Dar es Salaam kuanzia keshokutwa.
08 May 2006

Rais Kikwete asema matatizo katika magereza nchini hayana budi kupatiwa ufumbuzi.
Rais JAKAYA KIKWETE amesema matatizo yaliyoko katika magereza mbalimbali nchini yanastahili kupatiwa ufumbuzi kwa kuwa wafungwa walioko katika magereza hayo ni binadamu licha ya kwamba walikosa na kuhukumiwa vifungo hivyo.
04 May 2006

Radio Uhuru- Mhe. Nahodha amesema maeneo ya kipaumbele hivi sasa ni Elimu na Afya.
Waziri Kiongozi wa Zanzibar Mheshimiwa SHAMSI VUAI NAHODHA ameeleza kuwa elimu na afya ni miongoni mwa vitu vitakavyopewa kipaumbele katika awamu ya pili ya mpango wa kupunguza umaskini Zanzibar ambao unatazamiwa kuanza mapema mwaka huu.
03 May 2006

Radio Uhuru- Rais Kikwete amewaonya watendaji wazembe na wala rushwa.
Rais JAKAYA KIKWETE ameonya kuwa si muda mrefu hatua kali zitachukuliwa kwa watendaji wabovu, wezi na wala rushwa katika Halmashauri za miji nchini walioshindwa kubadilika na kutekeleza majukumu yao kwa kufuata taratibu.
03 May 2006

Rais Kikwete kesho anatembelea magereza mkoani dar es Salaam.
Rais JAKAYA KIKWETE kesho anatazamiwa kufanya ziara katika Magereza yaliyo Mkoani Dar es Salaam.
03 May 2006

MAJUMUISHO YA MKUTANO WA HALMASHAURI KUU YA CCM.
MAJUMUISHO YA MKUTANO WA HALMASHAURI KUU YA
TAIFA YA CCM ILIYOKUTANA DODOMA
TAREHE 29 - 30 APRIL, 2006
02 May 2006

Hifadhi ya Saadani
Radio Uhuru; Hifadhi ya Taifa ya Saadani imekusanya shilingi milioni 24.301 kwa kipindi cha mwaka 2004/2005 kutoka kwa watalii walitembelea hifadhi hiyo.
01 May 2006

NEC yateua
Radio Uhuru; Halamshauri Kuu ya Taifa ya Chama cha Mapinduzi imeteua kamati ya kupendekeza utaratibu bora zaidi wa kuwapata wagombea wa CCM katika vyombo vya dola.
01 May 2006

NEC yazipongeza serikali kwa hatua inazochukua kukabiliana na ujambazi
Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM imezipongeza kwa dhati serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kwa hatua madhubuti inazochukua katika kukabiliana na ukame, upungufu wa chakula, tatizo la ukame, uhalifu na matukio ya ujambazi yaliyoikumba jamii katika kipindi hiki.
01 May 2006

NEC yakanusha vikali kuwepo kwa mpasuko ndani ya CCM
Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama cha Mapinduzi –CCM- imekanusha vikali kuwepo kwa mpasuko ndani ya chama hicho kama inavyodaiwa na baadhi ya vyombo vya habari nchini.
01 May 2006

Mwanamke afanya mauaji
Radio Uhuru; Jeshi la Polisi mkoani Tabora, linamshikilia mwanamke mmoja kwa tuhuma za kumuua mtoto wa jirani yake kwa kumkata kichwa kwa madai ya kulipiza kisasi.
01 May 2006

Serikali inakusudia kuanzisha mchakato wa mishahara minono kwa wafanyakazi.
Rais JAKAYA KIKWETE amesema serikali imeanza mchakato maalum utakaosaidia kuelekeza namna ya kumlipa mfanyakazi mshahara utakaomwezesha kuishi maisha yenye heshima.
01 May 2006

NEC yamteua Rais Kikwete kugombea nafasi ya Mwenyekiti wa CCM.
Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama Cha Mapinduzi -CCM imemteua kwa kauli moja Rais JAKAYA MRISHO KIKWETE kuwa mgombea wa nafasi ya Mwenyekiti wa CCM.
29 Apr 2006

Ndg. Nyantahe Mwenyekiti Mpya Bodi ya TIRDO.
Rais JAKAYA KIKWETE amemteua Dokta SAMWEL NYANTAHE kuwa mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Utafiti na Maendeleo ya Viwanda –TIRDO-kwa kipindi cha miaka 3.
29 Apr 2006

NEC yamteua Ndg.Naomi Kapambala kuwa katibu wa mkoa.
Mkutano wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama Cha Mapinduzi –NEC- unaoendelea mjini Dodoma umemteua Ndugu NAOMI KAPAMBALA kuwa Katibu wa CCM wa mkoa.
29 Apr 2006

Askofu Laiser aipongeza kasi ya serikali ya awamu ya Nne.
Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania limeipongeza serikali ya awamu ya nne kwa kuweza kuondoa kero za wananchi katika kipindi kifupi tangu iingie madarakani.
29 Apr 2006

Radio Uhuru- Rais Kikwete anaanza ziara yake ya siku moja nchini Zimbabwe.
Rais JAKAYA KIKWETE leo anaanza ziara ya kikazi ya siku mbili nchini Zimbabwe.
27 Apr 2006

Ujerumani yaizawadia JWTZ vifaa vya zaidi ya shilingi mill.600.
Serikali ya Ujerumani imelipatia Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania -JWTZ- msaada wa vifaa vya tiba vyenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 600.
27 Apr 2006

Radio Uhuru- Katibu wa CCM Mkoa wa Singida afariki dunia.
Katibu wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Singida Ndugu PERPETUA NGERERA amefariki dunia.
27 Apr 2006

Radio Uhuru- Mhe. Lowasa aipongeza serikali ya Uchina.
Waziri Mkuu Mheshimiwa EDWARD LOWASSA ameipongeza Serikali ya China kwa jinsi uchumi wake unavyokua kwa kasi nzuri na kusifu mabadiliko ya haraka ya kiuchumi ambayo nchi hiyo imeyapata.
27 Apr 2006

Ndg. Penza na Ndg. Mfungo waidhinishwa kuongoza vyombo vya habari vya CCM.
Kikao cha Kamati Kuu kilichoketi leo chini ya Mwenyekiti wake Mheshimiwa BENJAMIN MKAPA kimewateua wanahabari wawili wakongwe kuwa wakuu wa vyombo vya habari vinavyomilikiwa na CCM.
27 Apr 2006

RADIO UHURU- Mhe. Nahodha aishauri Tanga Cement kupunguza gaharama za bidhaa hiyo.
Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imeishauri kampuni ya saruji ya Tanga kuangalia uwezekano wa kupunguza gharama za uzalishaji wa bidhaa yao ili wananchi wa Zanzibar waweze kumudu kununua bidhaa hiyo kutoka kiwandani humo.
22 Apr 2006

RADIO UHURU-Mhe. Lowasa serikali haitawavumilia viongozi wanaowakumbatia wahamiaji haramu.
Waziri Mkuu Mheshimiwa EDWARD LOWASA amewataka wananchi kuisaidia serikali kuwafichua viongozi wa serikali wanaokula njama na wahamiaji haramu na kuwapatia maeneo ya kuishi kinyemela.
22 Apr 2006

RADIO UHURU-Polisi Tabora wakamata silaha 31 zikiwemo bunduki.
Jeshi la Polisi mkoani Tabora, limefanikiwa kupata silaha 31 zilizokuwa zikimilikiwa kinyume cha sheria, baada ya wamiliki wake kuamua kuzisalimisha.
22 Apr 2006

RADIO UHURU-Tendwa lazima chama cha siasa kiwe na sura ya Muungano.
Msajili wa Vyama vya Siasa, Bwana JOHN TENDWA, amesema ili chama cha siasa kiweze kupata usajili lazima kiwe na sura ya Muungano, ikiwa ni pamoja na kuwa na ofisi za kudumu Tanzania Bara na Zanzibar.
22 Apr 2006

RADIO UHURU-Majambazi yaua na kupora milioni 150 za NMB.
Majambazi yamevamia magari ya benki ya NMB yaliyokuwa yakisafirisha fedha za benki hiyo kutoka jijini Dar es Salaam kupeleka katika tawi la benki hiyo lililopo mkoani Morogoro na kupora shilingi Milioni 150.

20 Apr 2006

RADIO UHURU- Rais Kikwete amtumia salamu za rambirambi Rais Kibaki wa Kenya.
Rais JAKAYA KIKWETE amemtumia salamu za rambirambi Rais MWAI KIBAKI wa Kenya kufuatia vifo vya watu 14 wakiwemo manaibu waziri wawili wa nchi hiyo katika ajali ya ndege iliyotokea juzi kaskazini mwa nchi hiyo.
12 Apr 2006

RADIO UHURU-Serikali ina mpango wa kujenga chuo kikuu kingine.
Serikali ina mpango wa kujenga Chuo Kikuu Nchini kitakachokuwa na uwezo wa kuchukua wanafunzi kati ya Elfu-20 hadi-30 katika fani mbalimbali.
12 Apr 2006

RADIO UHURU- Profesa Mwakyusa ataka ripoti ya kifo cha mtoto katika hospitali ya Amana.
Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Profesa DAVID MWAKYUSA ametoa siku sita kwa hospitali ya manispaa ya Ilala, Amana kutoa ripoti kamili juu ya kifo cha mtoto ZENA RAMADHAN kilichotokea tarehe 10 ya mwezi huu.
12 Apr 2006

RADIO UHURU- Watu watatu wafa katika ajali ya gari mkoani Pwani
Watu watatu wamekufa na wengine 16 kujeruhiwa baada ya magari mawili kugongana uso kwa uso katika ajali iliyotokea katika eneo la Njuweni, Maili Moja wilaya ya Kibaha mkoani Pwani.
12 Apr 2006

RADIO UHURU-China yaisaidia Tanzania msaada wa njaa.
Serikali ya China imetoa msaada wa zaidi ya Shilingi bilioni moja kwa Tanzania kwa ajili ya kukabiliana na uhaba wa chakula uliotokana na ukame.
12 Apr 2006

RADIO UHURU- Waziri Khatib amesema Tanzania itaendelea kuheshimu uhuru wa vyombo vya habari.
Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo Mheshimiwa MOHAMMED SEIF KHATIB amesema Tanzania itaendelea kudumisha uhuru wa vyombo vya habari utaokaoheshimu mipaka, sheria na ujenzi wa umoja wa kitaifa nchini.
12 Apr 2006

RADIO UHURU-Rais Kikwete ataka nguvu zaidi katika ushirikiano wa kiuchumi na Namibia.
Rais JAKAYA KIKWETE amesema anaridhishwa na uhusiano mzuri wa kisiasa na kidiplomasia uliopo kati ya Tanzania na Namibia, lakini hafurahishwi na kasi ndogo ya uhusiano wa kiuchumi na kibiashara iliyopo kati ya nchi hizo mbili.
11 Apr 2006

KIKWETE yupo Namibia
Radio Uhuru; Rais JAKAYA KIKWETE amewasili nchini Windhoek, Namibia kwa ziara ya kikazi ya siku tatu kwa lengo l kujitambulisha kwa viongozi wa serilkali ya Namibia na wananchi wake.
11 Apr 2006

Asilimia 40 ya kodi jijini Tanga yatokana na mafuta yanayoingizwa
Radio Uhuru; Asilimia 40 ya kodi ya katika jiji la Tanga inatokana na mafuta yanayoingizwa kupitia bandari ya mji huo.
08 Apr 2006

Chama cha Maalbino chaomba msaada kwa serikali
Chama cha Maalbino Tanzania kimeiomba serikali kuweka mipango madhubuti itakayowezesha kupambana na ugonjwa wa kansa ambao umekuwa ni tatizo kubwa kwa maalbino nchini.
08 Apr 2006

Atafutwa kwa mauaji
Radio Uhuru; Polisi mkoani Mbeya wanamtafuta mkazi mmoja wa wilaya ya Chunya mkoani humo kwa tuhuma za kumuua mkewe baada ya kumpiga kichwani na mdomoni na kumzika kisiri.
08 Apr 2006

IGP MWEMA katika mapambano na uhalifu
Mkuu wa Jeshi la polisi nchini Inspekta Jenerali SAID MWEMA amewaagiza makamanda wa polisi wa mikoa yote kuweka visanduku ya maoni katika vituo ili kuwawezesha wananchi na askari wenye taarifa za vitendo vya uhalifu kufichua kwa njia hiyo.
08 Apr 2006

Dokta SHEIN atoa changamoto kwa wawakilishi
Radio Uhuru; Makamu wa Rais Dokta ALI MOHAMED SHENI ametoa changamoto kwa wajumbe wa Baraza la Wawakilishi kuwajibika ipasavyo kwa kufuata maadili ya kazi zao ili wananchi waweze kutambua kuwapo kwao.
08 Apr 2006

RADIO UHURU-Dk. Shein kufungua mafunzo kuhusu katika kwa wawakilishi.
Makamu wa rais Dk, ALLY MOHAMED SHEIN leo anafungua mafunzo ya siku tatu kuhusu katiba na utendaji wa baraza la wawakilishi Zanzibar.
08 Apr 2006

RADIO UHURU-Marais wa Tanzania na Afrika Kusini wametoa wito wa kunufaishana katika uhusiano baina ya nchi hizo mbili.
Marais THABO MBEKI na Rais JAKAYA KIKWETE wameagiza kufanyika kwa mkutano wa kwanza wa Kamisheni ya Marais ya Ushirikiano wa Kiuchumi, ili kuhakikisha Tanzania inanufaika na uhusiano wa kiuchumi na kibiashara uliopo kati yake na Afrika Kusini.
08 Apr 2006

RADIO UHURU-Mkuu wa mkoa wa Mtwara awataka watendaji kuwavutia wawekezaji.
Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Bwana HENRY SHEKIFU amewataka watendaji wa serikali wa ngazi zote mkoani Mtwara kuandaa mazingira yatakayowavutia wawekezaji kuwekeza mkoani humo.
08 Apr 2006

RADIO UHURU-Mkuu wa mkoa wa Mtwara awataka watendaji kuwavutia wawekezaji.
Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Bwana HENRY SHEKIFU amewataka watendaji wa serikali wa ngazi zote mkoani Mtwara kuandaa mazingira yatakayowavutia wawekezaji kuwekeza mkoani humo.
08 Apr 2006

RADIO UHURU-Rais Jakaya Kikwete akimpongeza Balozi Juma Mwapachu
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimpongeza Balozi Juma Mwapachu Mara baada ya kula kiapo kama katibu mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki jana mjini Arusha.
07 Apr 2006


Ndugu Mangula awataka viongozi wa CCM kuwa mstari wa mbele katika kutekeleza Ilani ya CCM
Chama Cha Mapinduzi kimewataka viongozi wake kuisoma Ilani ya uchaguzi kwa makini na kuona nini wanatakiwa kukifanya na nini wanatakiwa kuwaelekeza wananchi wao katika kuwaletea maendeleo yao kwa haraka.
03 Apr 2006

Rais Kikwete amesema serikali yake itahakikisha inafufua viwanda Tanga
Rais JAKAYA KIKWETE amesema serikali ya awamu ya nne itahakikisha inafufua viwanda vyote vilivyosimama kufanya kazi na vile vilivyokufa kabisa mkoani Tanga ili kuendeleza mkoa huo kiuchumi na kibiashara.
03 Apr 2006

RADIO UHURU-Rais Mahamoud Abbas wa Palestina afanya ziara Nchini.
Rais MAHMOUD ABBAS wa Mamlaka ya Palestina amesema ni lazima nchi yake na Tanzania zishirikiane katika nyanja mbalimbali za kimaendeleo ili kukuza uhusiano na ushirikiano wa kihistoria na wa muda mrefu uliokuwepo baina ya mataifa hayo mawili.
02 Apr 2006

Utafiti wa mbegu za tumbaku waendelea
Radio Uhuru; Taasisi ya Utafiti wa zao la tumbaku nchini imesema inaendelea kuzifanyia utafiti aina 20 za mbegu za zao hilo zilizoingizwa nchini na wadau wa zao hilo mapema mwaka jana.
02 Apr 2006

Ziara ya KIKWETE Pemba
Radio Uhuru: Rais JAKAYA KIKWETE wanachama wa vyama vya siasa nchini kuacha chuki na utengano baina ya vyama au ndani ya vyama vyao ili kudumisha umoja na ushrikiano na kuimarisha demokeasia nchini.
02 Apr 2006

Igunga yatekeleza agizo la LOWASSA
Radio Uhuru; Wilaya ya Igunga mkoani Tabora imefanikiwa kutekeleza agizo lililotolewa na Waziri Mkuu mheshimiwa EDWARD LOWASSA, linalowataka wanafunzi waliofaulu mtihani wa darasa saba mwaka jana na kushindwa kuchaguliwa katika shule za serikali, kuendelea na masomo yao.
02 Apr 2006

WanaCCM watakiwa kutekeleza ilani ya uchaguzi
Radio Uhuru; Mwenyekiti wa CCM tawi la la ofisi ndogo la lumumba Jijini Dar es salaam bwana VICENT MKUDE amewataka wanachama wa CCM kusimamia vema na kutekeleza kwa vitendo ilani ya uchaguzi ya Chama cha mapindzui.
02 Apr 2006

RADIO UHURU- Dk.Shein kulihutubia taifa leo kwa lengo la kuelezea viainishi vya uhifadhi wa mazingira.
Makamu wa Rais Dokta ALLI MOHAMED SHEIN leo anatazamiwa kutoa tamko la serikali kuhusu hatua za haraka za kuhifadhi mazingira ya ardhi na vyanzo vya maji zinazotakiwa kuchukuliwa hapa nchini.
01 Apr 2006

RADIO UHURU- Ndg.Mangula aipongeza Jumuiya ya wazazi kwa kufanikisha uchaguzi.
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi -CCM, Ndugu PHILIP MANGULA, ameishukuru na kuipongeza Jumuia ya Wazazi ya CCM kwa kushiriki kikamilifu katika uchaguzi mkuu uliopita.
01 Apr 2006

RADIO UHURU-Watendaji 22 wa wizara za SMZ wafukuzwa kazi kwa wizi.
Wafanyakazi 22 wa wizara mbalimbali za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar wamefukuzwa kazi kwa tuhuma za kuhusishwa na wizi wa fedha za serikali kwa kulipa wafanyakazi hewa.
01 Apr 2006

RADIO UHURU-Serikali imesema haitawavumilia watumishi wavivu.
Serikali imesema haitawavumilia watumishi ambao ni wavivu na wasiotekeleza wajibu wao kwa kufuata maadili ya kazi zao.
01 Apr 2006

RADIO UHURU-Dk. Shein kutoa tamko la serikali kuhusu jitihada za haraka za uhifadhi wa mazingira.
Makamu wa Rais Dokta ALLI MOHAMED SHEIN kesho anatazamiwa kutoa tamko la serikali kuhusu hatua za haraka za kuhifadhi mazingira ya ardhi na vyanzo vya maji zinazotakiwa kuchukuliwa hapa nchini.
31 Mar 2006

RADIO UHURU-Rais Kikwete asema siku 100 za kwanza zilikuwa za majaribio.
Rais JAKAYA KIKWETE ameeleza kuwa siku mia moja tangu kuingia kwake madarakani zilikuwa ni za kujifunza jinsi ya kuweka mikakati ya kuwatumikia wananchi katika kipindi cha miaka 5 ijayo.
31 Mar 2006

RADIO UHURU-Rais Kikwete leo kuwahutubia wazee wa Dodoma.
Rais JAKAYA KIKWETE leo atalihutubia Taifa kupitia mkutano wake na wazee wa mkoa wa Dodoma.
31 Mar 2006

RADIO UHURU-CCM yatuma salamu za Rambirambi kwa familia MOSHI WILLIAM kufuatia kifo cha mwanamuziki huyo.
Chama Cha Mapinduzi –CCM kimetuma salamu za rambirambi kufuatia kifo cha Mtunzi na mwimbaji wa Bendi ya Msondo Ngoma Marehemu MOSHI WILLIAM kilichotokea jana Alfajiri katika hospitali ya Taifa Muhimbili.
30 Mar 2006

RADIO UHURU-Rais Kikwete kesho kuwahutubia wazee wa Dodoma.
Rais JAKAYA KIKWETE kesho atalihutubia Taifa kwa kuzungumza na wazee wa Mkoa wa Dodoma.
30 Mar 2006

RADIO UHURU- Vodacom yachangia Bill.1 ya chakula cha njaa.
Kampuni ya Simu za Mkononi ya Vodacom Tanzania imemkabidhi Rais JAKAYA KIKWETE hundi ya shilingi bilioni Moja ukiwa ni mchango wake katika kukabiliana na tatizo la njaa nchini.
30 Mar 2006

RADIO UHURU-Hali duni ya wapandisha watalii Mt. Kilimanjaro yasababishwa na kutolipwa vizuri.
Serikali imekiri kutambua hali duni za wabeba mizigo inayotokana na kutolipwa vizuri na mawakala wa Utalii wanaopandisha watalii katika mlima Kilimanjaro.
29 Mar 2006