HISTORIA YA CCM TANGU TANU NA ASP
1.0 UTANGULIZI:
1.1
Maelezo
ya awali
Chama
cha Mapinduzi (CCM) kilizaliwa tarehe 5 Februari, 1977 kutokana na
kuvunjwa kwa vyama vya Tanganyika
African National Union (TANU) na Afro-Shirazi Party (ASP).
Tendo
Kupatikana
kwa uhuru wa
Katika
mazingira ya ubeberu duniani wakati huo na hali ya unyonge wa mataifa haya
machanga, yakielewa kuwa ‘umoja ni nguvu’,
Katiba ya CCM, katika Azimio
la Mkutano Mkuu wa Taifa wa Pamoja wa TANU na ASP tarehe 21 January, 1977,
inaeleza kuwa, (uk. 2-3), “...kwa kauli moja tunaamua na kutamka rasmi
kuvunjwa kwa Tanganyika African Union(TANU) na Afro-Shirazi Party (ASP) ifikapo
tarehe 5 Februari, 1977 na wakati huohuo kuundwa kwa Chama kipya cha pekee na
chenye uwezo wa mwisho katika mambo yote kwa mujibu wa Katiba.”
Muungano wa TANU na ASP ndio
uliowezesha CCM kuwa Chama chenye nguvu,
imara na madhubuti, hivyo kuwa Chama cha siasa pekee chenye uwezo wa hali ya
juu wa kuwaunganisha Watanzania. Aidha, CCM kimeweza kuwaongoza wananchi katika
mapambano ya kitaifa ya kiuchumi, kisiasa na kijamii kufuatana na mabadiliko
mbalimbali yanayojitokeza ndani na nje ya nchi.CCM kimeendelea kupewa dhamana
na wananchi ya kuunda serikali na kukamata dola tangu 1977 chini ya mfumo wa
demokrasia ya chama kimoja hadi sasa
katika mfumo wa demokrasia ya vyama vingi, kufuatia mageuzi yaliyoidhinishwa na
marekebisho ya Katiba ya Jamhuri ya Tanzania Juni 1992.
1.2 Umuhimu
wa kuielewa historia ya CCM na Vyama
vilivyokitangulia
Historia
ya CCM tangu TANU na ASP ina umuhimu wa pekee katika Taifa letu katika kuelewa
tulikotoka, tulipo hivi sasa na tunakoelekea.
Historia ya nchi yetu haiwezi kukamilika bila ya historia ya vyama hivi
vya ukombozi. Historia hutoa mafunzo na
ni mwelekezaji pia, kwa hiyo ni wajibu wa Watanzania, hasa wanachama wa CCM
kujifunza kutokana na historia yetu.
Kazi kubwa na ya msingi inayofanyika katika kujifunza historia hiyo, ni
kurithisha dhamira ya kujituma na
kudumisha uhuru wa nchi yetu. Hivyo, ili kuendelea kukijenga Chama, na
kuimarisha uwezo wa kuendelea kukamata dola barabara kwa namna endelevu, hapana
budi ihakikishwe kuwa historia ya CCM inabeba pia jukumu la msingi la
kusaidia:-
·
Kujua Chama kilikotoka, mahali kilipo na kinakoelekea
katika misingi ya sera, itikadi, malengo na wanachama.
·
Kuunganisha wanachama na kuwaweka pamoja kiimani,
kiitikadi na kiutendaji.
·
Wanachama kujitambua, kutambua wajibu na majukumu yao
na kujenga moyo wa kujiamini na kujithamini.
·
Kuinua kiwango cha ushiriki wa wanachama wa CCM na
wananchi katika kubuni na kutekeleza mkakati na mbinu sahihi za kutetea na
kuendeleza Chama na taifa kufuatana na hali ya wakati na mahali.
·
Kuweka misingi ya kufanya tathmini na hivyo kuwa na
uhakika katika kufanya maamuzi.
·
Kupanda mbegu bora za upendo, uzalendo na uchungu wa
kweli kwa uhai wa CCM na taifa kwa ujumla.
·
Kuwa na majibu sahihi wakati wote kwa hoja mbalimbali
zinazotolewa kuhusu Chama Cha Mapinduzi na taifa kwa ujumla.
·
Kuweka msingi wa kurithisha kutoka kizazi kimoja hadi
kingine maadili ya msingi wa uhai wa CCM.
·
Kuhifadhi kuweka na kueneza kumbukumbu sahihi ya
historia ya Chama, nchi, mchango wa Waasisi na wanachama na kuhakikisha
wapotoshaji hawapati fursa ya kueneza uongo.
Pamoja na kwamba Chama Cha
Mapinduzi kuwa kilizaliwa rasmi tarehe 5 Februari, 1977, chimbuko lake
linaanzia miaka mingi kabla, sambamba na historia ya uhai wa taifa la Tanzania.
Mizizi ya historia ya CCM imo ndani ya harakati za kukataa ukoloni na usultani,
zilizofanywa na wananchi wa Tanzania. Wahenga wetu kwa pamoja tangu enzi, walionyesha wazi
kukataa kwao kutawaliwa. Historia ya Tanzania inao utajiri wa mifano mingi ya
harakati hizo japokuwa zilijengwa katika misingi ya ukoo na ujirani, katika
wilaya na mikoa mbalimbali hata kabla ya kuundwa kwa vyama vya TANU na ASP.
Wananchi hao waliotutangulia
walikataa kunyonywa, kupuuzwa, kubaguliwa, kutawaliwa, kunyanyaswa na
kugawanywa katika misingi ya rangi, kabila, dini, jinsia, nk. Utu na uhuru wao
ulikuwa na thamani kubwa sana. Hivyo waliamua kupambana dhidi ya udhalimu huo.
Baadhi ya mifano ya jitihada za mapambano ya awali ni Vita ya Majimaji huko
Umatumbi na maeneo ya kusini, Mbiru huko Upare, Waluguru, Wameru, Wahehe na
mengineyo huko Unguja, Pemba, Kanda ya Ziwa na katika jamii za wafugaji. Ari,
utashi, uzalendo na dhamira ya kweli ya kutaka kujitawala vilivyojidhihirisha
katika harakati hizo, viliotesha mizizi iliyoshikilia uhai wa vyama vya TANU na
ASP.
2.1 TANU
ilizaliwa katika mazingira yaliyoandaliwa na
TAA
iliundwa 1948 kufuatia tukio la kutengana kwa African Association (AA) ya
Katiba
ya TAA ilitamka wazi kwamba Chama hicho hakikuwa na malengo ya kisiasa. Mwaka 1953 yalifanyika mabadiliko ya uongozi
katika TAA. Mwalimu Julius Kambarage
Nyerere alichaguliwa kuwa Rais wa TAA.
Chini ya uongozi mpya, Katiba ya TAA ilionekana kwamba isingeweza kukidhi malengo ya kisiasa. Mwalimu alipewa jukumu la kuandaa Katiba mpya
ya TAA ambayo ingezingatia malengo ya kisiasa.
Baada ya uandaaji wa Katiba hiyo kukamilika, haja ya kubadili jina
ilionekana dhahiri na majina mengi yalipendekezwa likiwemo la TANU. Nafasi ya TAA ilichukuliwa na TANU
iliyozaliwa tarehe 7 Julai, 1954.
TANU ilirithi matawi ya TAA, wanachama
na viongozi wa TAA katika maeneo mengi.
Waasisi
wa TANU ambao walihudhuria na kushiriki katika Mkutano wa kuzaliwa kwa TANU
walikuwa 17:
(1)
Mwalimu J.K.
Nyerere – Rais wa TAA/TANU
(2)
Geremano Pacha
– Jimbo la Magharibi
(3)
Joseph
Kimalando – Jimbo la Kaskazini
(4)
Japhet Kirilo –
Jimbo la Kaskazini
(5)
C.O. Milinga –
Jimbo la Mashariki
(6)
Abubakari
llanga – Jimbo la Ziwa
(7)
L.B. Makaranga
– Jimbo la Ziwa
(8)
Saadani A.
Kandoro – Jimbo la Ziwa
(9)
Suleman M.
Kitwara – Jimbo la Ziwa
(10)
Kisung’uta
Gabara – Jimbo la Ziwa
(11)
Tewa Said Tewa
– Jimbo la Mashariki
(12)
Dossa A. Aziz –
Jimbo la Mashariki
(13)
Abdu Sykes –
Jimbo la Mashariki
(14)
Patrick Kunambi
– Jimbo la Mashariki
(15)
Joseph K. Bantu
– Jimbo la Mashariki
(16)
Ally Sykes –
Jimbo la Mashariki
(17)
John Rupia –
Jimbo la Mashariki
2.2 TANU
ilizaliwa baada ya Vita ya Pili ya Dunia:
Katika
vita ya Pili ya Dunia (1939 – 1945), Watanganyika walishiriki wakiwa askari upande
wa Waingereza. Katika kushiriki huko,
baadhi
Baadhi
ya askari hao wa
2.3
TANU
ilizaliwa katika mazingira ya vyama vya
ushirika:
Katika
miaka 1950, wakulima walikwishajiunga na kuanzisha vyama vya kuuza mazao
·
Kilimanjaro
Co-operative Union Ltd (1933)
·
Ngoni – Matengo
Co-operative Union Ltd. (1936)
·
Rungwe African
Co-operative Union Ltd. (1949)
·
Bukoba
Co-operative Union Ltd. (1950)
·
Kwa
kuwepo vyama vya ushirika, ujumbe wa TANU kuwafikia wananchi
ulirahisishwa. Wanachama wa vyama vya
ushirika walijiunga na TANU. Wanachama
na viongozi wa vyama vya ushirika waliunga mkono TANU katika madai yake ya
kudai uhuru. Baadhi ya viongozi wa vyama
vya ushirika walichaguliwa kuwa viongozi wa TANU katika ngazi ya Taifa. Kwa mfano:-
·
Ndugu Nsilo
Swai
·
Sir George
Kahama
·
Ndugu Jeremiah
Kasambala
·
Balozi Paul
Bomani
·
Ndugu John
Mhavile.
TANU
nayo iliunga mkono vyama vya ushirika katika madai yake ya bei nzuri ya mazao
Baada
ya Uhuru, TANU iliuona ushirika kuwa ni chombo cha kuleta maendeleo hivyo wananchi
walihimizwa kuanzisha ushirika katika maeneo ambayo hayakuwa na vyama vya
ushirika. Hali hii inaendelea hadi hivi
sasa ambapo katika mfumo wa uchumi wa Soko, CCM inauona ushirika kuwa ni chombo
cha kumwezesha mwananchi kiuchumi katika kumiliki na kuendesha uchumi wa Taifa
lake.
2.4 TANU
ilizaliwa katika mazingira ya vyama vya
wafanyakazi:
Lengo
kuu la Vyama vya Wafanyakazi lilikuwa ni kutetea maslahi ya wafanyakazi. Baadhi ya vyama vya wafanyakazi ni:-
·
Chama cha
Wafanyakazi Serikalini (1929)
·
Chama cha
Makuli (1937)
·
Chama cha
Wapishi na Madobi (1939)
·
Chama cha
Wapishi na Watumishi wa Ndani
·
Chama cha
Madereva
·
Chama cha
Walimu
·
Chama cha
Wafanyakazi wa Reli
·
Chama cha
Wafanyakazi Mashambani
·
Chama cha
Wafanyakazi Viwandani.
Vyama
vya Wafanyakazi viliunda Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi (Tanganyika
Federation of Labour –TFL) tarehe 10
Oktoba, 1955.
Wafanyakazi
kupitia vyama vyao walikuwa na madai yafuatayo:-
·
nyongeza ya
mshahara
·
mapumziko ya
mchana siku ya kazi
·
umri wa
kustaafu na
·
kuondoa ubaguzi
katika ajira na huduma za jamii.
Vyama
vya wafayakazi vilisaidia kuvunja ukabila na hivyo kuwa chanzo cha umoja. Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi
lilisaidia kueneza TANU kwa njia zifuatazo:-
·
Kila Chama cha Wafanyakazi
chini ya Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi (TFL) kilitakiwa kuwashawishi na
kuwahimiza wanachama wake kujiunga na TANU.
·
Kila mwanachama
wa TANU aliyekuwa mwanachama wa Chama cha Wafanyakazi alitakiwa kulipa mchango
wake wa kila mwezi kwa TANU.
·
Vyama vya
Wafanyakazi, wakati mwingine kupitia TFL, viliweza kusaidia TANU kifedha fedha
hizo zilitokana na michango ya hiari.
·
Shirikisho la
Vyama vya Wafanyakazi lilisaidia
Vyama
vya Wafanyakazi vilifanya yote hayo kwa kuelewa kwamba uhuru ndio ungekuwa
suluhisho la kweli la matatizo
Kwa
upande wake, TANU iliunga mkono madai ya vyama vya wafanyakazi na migomo ya
wafanyakazi. Katika historia ya
Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi, mgomo wa wafanyakazi wa Shamba la Mazinde
huko Tanga na mgomo wa wafanyakazi wa Kiwanda cha Bia
Shamba
la Mazinde lilikuwa
Jitihada
za TFL kusuluhisha mgogoro huo kati ya Mwajiri na wafanyakazi
zilishindikana. TFL na TANU kwa pamoja
viliunga mkono mgomo wa wafanyakazi wa Shamba la Mazinde. TANU kupitia Mwalimu Nyerere ilitoa wito kwa
wananchi wa Mkoa wa Tanga kuwahifadhi
wafanyakazi waliofukuzwa kazi.
Wananchi waliitikia wito wa TANU na kuwapokea na kuishi nao. Aidha, TFL na TANU vilitoa wito kwa wananchi
kususia shamba la Mazinde. Wafanyakazi
hao hawakurejea kazini hata baada ya mmiliki kuwataka kufanya hivyo. Matokeo yake ni kwamba mmiliki huyu wa Shamba
la Mazinde hakuchukua muda akafilisika na akarejea kwao Uingereza.
Huu
ulikuwa ni ushindi wa TANU na TFL. TANU
ilitambuliwa na wafanyakazi mashambani na iliendelea kuimarika. Kwa kuwa ngome ya UTP, na baadaye African
National Congress (ANC) ilikuwa huko Tanga
pigo hili lilisababisha kifo cha UTP na kuzorota kwa ANC.
Kuhusu
mgomo wa Kiwanda cha Bia
Katika
kuonyesha mshikamano na wafanyakazi katika mgomo huu wa Kiwanda cha Bia, TANU
ilichukua hatua zifuatazo:-
·
Ilitoa wito kwa
nchi nzima kususia pombe zote za kigeni;
·
Iliwaomba
wananchi wa
·
Iliwaomba
wananchi wenye nyumba Ilala kuwapokea wagomaji katika nyumba zao pasipo
kuwatoza kodi ya nyumba.
Kama kawaida
2.5 TANU
ilizaliwa katika mazingira ya kero na adha za wananchi kutoka Serikali ya Kikoloni:
Malalamiko
hayo ya wananchi yalijidhihirisha katika maeneo yafuatayo:-
·
Upinzani huko
Upare dhidi ya ulipaji kodi kulingana na
mapato (Mbiru);
·
Wahehe kukataa
kuogesha ng’ombe wao;
·
Waluguru
kupinga juhudi za kuhifadhi mapori na kulima matuta;
·
Wafugaji
(Wasukuma) kupinga kodi ya ng’ombe na kupunguza idadi ya ng’ombe, kumi kwa kila
mia;
·
Wameru wapatao
3,000 walipinga kunyang’anywa ardhi
TANU ilitumia kero hizo za wananchi katika
kuwaunganisha wananchi na kuwaelekeza namna ya kutafuta haki zao.
Kuhusu
ardhi ya Wameru, Katika mkutano wake wa kwanza, TANU ilitoa tamko lifuatalo:-
“Mkutano huu unasikitika
2.6
Kuenea kwa TANU na Kupata Ushindi:
Dhumuni
la kwanza la TANU mwaka 1954 lilikuwa ni kuwatayarisha Watanganyika kujitawala
na kujitahidi kwa bidii mpaka
Katika
harakati za kuitangaza TANU, njia mbali mbali zilitumika:-
·
TANU ilifungua
matawi katika maeneo mbali mbali ya nchi yetu.
·
TANU ilitumia
mikutano ya hadhara katika kufikisha ujumbe wake kwa wananchi.
·
TANU ilitumia mikutano
ya ndani ya wanachama.
·
TANU ilitumia
vyombo vya habari, hususan magazeti,
2.7 Jumuiya
za TANU za Umoja wa Wanawake, Umoja wa Vijana na Wazazi zilifanya kazi kubwa katika kukieneza na
kukiimarisha Chama.
TANU
ilianzisha rasmi mwaka 1955 sehemu ya Wanawake wa TANU. Chama kilitambua kwamba mapambano ya kudai
uhuru yasingeweza kufanikiwa bila ya kulitumia jeshi kubwa la Wanawake. Chama kilimpata Bibi Titi Mohamed na kumpa
jukumu la kuwakusanya wanawake ili washiriki katika mapambano ya kudai
uhuru. Sehemu ya Wanawake ilipewa
majukumu yafuatayo:-
·
Kupata
wanachama wa TANU wengi;
·
Kueneza Chama
hasa vijijini kwa moyo wa kujitolea;
·
Kuona kwamba
viongozi wa Chama wako salama/ulinzi wa viongozi na
·
Kukipatia Chama
fedha kutokana na shughuli halali mbali mbali.
Katiba
ya TANU ya mwaka 1954, sehemu ya sita, ilitoa nafasi kwa vijana kuunda umoja
wao ili waweze kushiriki kwa ukamilifu katika mapambano ya kudai uhuru. Umoja wa Vijana ulikuwa na majukumu yafuatayo:
·
Kuwaandaa
vijana katika uongozi;
·
Kuwahimiza
vijana kujitolea kufanya kazi za TANU;
·
Kutekeleza
shabaha za TANU;
·
Kuunda makundi
ya starehe na maendeleo miongoni mwa wanachama
·
Kukusanya
habari na kufuatilia mwenendo wa kisiasa nchini;
·
Kushirikiana na
vyama vingine vya vijana visivyo na upinzani kwa TANU.
2.8 TANU
ilivyopambana na kuvishinda vikwazo na hila za Mkoloni
Jumuiya
ya Wazazi (Tanganyika Parent’s Association – TAPA) iliundwa mwaka 1955 chini ya
Ndugu Lawi Sijaona. TAPA ilikuwa ndiye mtekelezaji mkuu wa Azimio la Mkutano
Mkuu wa Tabora lililohusu upanuzi wa elimu.
Katika kutekeleza jukumu lake, TAPA ilifungua shule za msingi na
sekondari nyingi nchini na kuendesha kisomo cha Watu Wazima. Huu ulikuwa mkakati wa makusudi wa kuwaandaa
wananchi kushika madaraka baada ya uhuru.
Jinsi
TANU ilivyozidi kuimarika ndivyo hivyo ilivyopambana na vikwazo na hila za
Mkoloni:
·
Serikali ya
Kikoloni ilipitisha Sheria mwaka 1953 ya kuwakataza watumishi wa Serikali wa
mataifa yote kujiunga na vyama vya siasa.
Aidha, Tangazo la Serikali Namba 2 la 1954 lilifafanua kuwa hata Sukuma
Union kilikuwa ni Chama cha Siasa. Kwa
mujibu wa Tangazo la Serikali Namba 6 la 1954, maafisa wote wa Serikali
waliokuwa wanachama wa TANU na waliotaka kuendelea na utumishi serikalini
walitakiwa kujiuzulu mara moja. Aidha,
Sheria ya vyama vya siasa, 1954, ilitaka kila tawi la TANU lisajiliwe kabla ya
kuandikishwa kisheria. Sheria hii
iliiwezesha serikali ya mkoloni kusajili au kutokusajili tawi lo lote la TANU.
·
Mara tu baada
ya TANU kuundwa, Rais wake Mwalimu Nyerere alitakiwa na Serikali ya Kikoloni
achague moja kati ya mambo mawili ama kuendelea kuiongoza TANU au
kujiuzulu uongozi wa TANU na kuendelea
na kazi yake ya ualimu katika Shule ya Sekondari Pugu. Mwalimu aliamua kuendelea kuihudumia TANU hivyo akalazimika kujiuzulu
kazi ya ualimu. Bila shaka, Serikali ya
Kikoloni ilidhani kwamba Mwalimu asingejiuzulu ualimu. Katika suala hili, uamuzi wa Mwalimu haukuwa
rahisi hasa kwa kuzingatia kwamba kazi ya ualimu ndio alikuwa ameisomea, riziki
yake na ya familia ilitokana na ualimu na kwamba kuitumikia TANU wakati huo
ilikuwa ni kupambana na Serikali ya Kikoloni na hii ilikuwa ni hatari
kubwa. Kwa kujiuzulu ualimu, Mwalimu
alipata nafasi kubwa zaidi ya kuihudumia TANU.
·
Mwalimu Nyerere
mwaka 1958 alishitakiwa na Serikali ya Kikoloni kwa kosa la kuwakashifu
District Commissioners wa Songea, Geita
na Musoma. Kwamba kashfa hiyo aliifanya
kwa kupitia makala aliyoiandika kupitia Gazeti la “Sauti ya TANU” Toleo Namba
29 la tarehe 27 Mei, 1958. Katika kesi
hii iliyosikilizwa na Mahakama ya Dar es
Salaam, Mwalimu alihukumiwa faini ya
shs. 3,000/= (shilingi elfu tatu) au kifungo cha miezi 6. Mwalimu alilipiwa faini hiyo na TANU.
·
Serikali ya
kikoloni pia ilijitahidi kadri ilivyoweza kuwatumia baadhi ya machifu kuwa chombo cha kuzuia uenezaji wa TANU. Machifu walipewa madaraka makubwa zaidi na
zaidi ili wajisikie kuwa ni sehemu ya utawala na kwamba TANU ilikuwa na lengo
la kuwakosesha maslahi
·
Serikali ya
kikoloni ilihimiza kuundwa kwa United Tanganyika Party (UTP) ndani ya Baraza la
Kutunga Sheria mwaka 1956. UTP ilikuwa
ni chombo na Sauti ya Serikali ya kikoloni kwa sababu zifuatazo:-
(a)
Uongozi wa UTP
uliundwa na Wajumbe wa Baraza la Kutunga Sheria,
“
(b)
Wajumbe hao
waliteuliwa na Gavana na hivyo hawangeweza kupingana na siasa ya Serikali ya
Kikoloni.
Licha
ya hila na vikwazo vya mkoloni, TANU ilijikuta ina mtihani mgumu wa kuamua
kushiriki ama kutokushiriki katika Uchaguzi Mkuu wa kwanza mwaka 1958.
Akifungua kikao cha kwanza cha Baraza la Kutunga Sheria mwaka 1956,
Gavana Edward Twining alitangaza kuwa Serikali ilikuwa na mpango wa kufanya
Uchaguzi Mkuu wa kwanza mnamo 1958.
Sharti moja kubwa la uchaguzi huo lilikuwa kwamba kila mpiga kura apige
kura tatu: moja kwa Mzungu, moja kwa
Mwasia na moja kwa Mwafrika.
Suala
hili la kura ya Mseto lilijadiliwa kwa undani katika Mkutano Mkuu wa TANU
uliofanyika Tabora mwaka 1958 na kuhudhuriwa na Wajumbe 300 kutoka sehemu zote
za Tanzania Bara.
Mwalimu
Nyerere aliweza kuushawishi Mkutano kukubali kushiriki katika Uchaguzi Mkuu wa
kwanza mwaka 1958. Hoja za Mwalimu
zilikuwa ni kwamba
Matokeo
ya kukubali kura ya mseto, aliyekuwa Katibu Mwenezi wa TANU, Ndugu Zuberi
Mtemvu aliamua kuachana na TANU na kuanzisha African National Congress (ANC)
mwaka 1958. Hata hivyo toka kuanzishwa
kwake hadi kifo chake, ANC haikupata hata kiti kimoja katika Baraza la Kutunga
Sheria. Aidha, Ndugu Mtemvu alibwagwa
kwa kishindo na Mwalimu Nyerere katika kugombea Urais wa Jamhuri ya
Uchaguzi
Mkuu wa pili ulifanyika mwaka 1960.
Katika uchaguzi huo, TANU ilijikuta imefanikiwa kupitisha wagombea wake
58 bila ya kupingwa. Kati ya wagombea
hao 58 waliopita bila kupingwa, 8 walikuwa Wazungu, 11 Waasia na 39
Waafrika. Tarehe 30 Agosti, 1960
ulifanyika uchaguzi katika sehemu nyingine ambako kulikuwa na zaidi ya
mgombea mmoja katika jimbo la uchaguzi. Wagombea viti wote jumla walikuwa 25 kati ya
hao 11 walisimamishwa na TANU na walishinda isipokuwa mmoja tu wa kiti cha
Mbulu, Chifu Amri Dodo aliyeshindwa na Herman E. Sarwatt ambaye alikuwa mgombea
binafsi. Hata hivyo, Sarwatt alikuwa ni
mwanachama wa TANU.
Pamoja
na vikwazo hivi Msimamo sahihi usioyumba uongozi bora umoja mshikamano ari na
dhamira ya wananchi ya kutaka kujitawala vilikuwa chachu iliyosababisha TANU
kupata ushindi wa kishindo na kutokana
na ushindi huo, Gavana Richard Turnbull
alimwomba Rais wa TANU, Mwalimu Nyerere kuunda Baraza la Mawaziri ambalo
lilikuwa na jukumu la kuongoza nchi kwa jumla na kumshauri Gavana. Serikali ya Madaraka iliundwa na kuapishwa
tarehe 3 Septemba, 1960.
Uhuru
wa
·
Tanganyika ilikuwa chini ya Udhamini wa Umoja wa Mataifa
tofauti na nchi kama Kenya, Uganda, Zambia na Malawi zilizokuwa makoloni moja
kwa moja chini ya Serikali ya Kiingereza iliyokuwa na sauti ya mwisho. Chini ya
udhamini huo watawala wa
Kiingereza, walipaswa kuitawala nchi hii kwa mujibu wa masharti ya Umoja wa
Mataifa kuhusu makoloni ya udhamini.
·
Nafasi ya
Jamhuri ya Kisovieti (Urusi) (ilikuwa
miongoni mwa mataifa manne makubwa) katika Umoja wa Mataifa ilisaidia kutoa
msukumo kwa Umoja huo katika kufanikisha juhudi za TANU za kudai uhuru wa
·
Lugha ya
Kiswahili ilisaidia
·
Katika
·
·
Umoja wa Vijana
na Umoja wa Wanawake chini ya TANU, walitoa
msukumo mkubwa katika kudai uhuru.
Vikundi hivyo vilijawa na ari na moyo wa kimapinduzi; vilifanya kazi ya
kujitolea usiku na mchana.
·
Vyama vya Wafanyakazi
na Vyama vya Ushirika viliweza kuwabana vilivyo Wakoloni kwa njia ya migomo na
ususiaji wa bidhaa.
·
Uongozi bora wa
TANU, hususan uongozi wa Mwalimu Nyerere.
Uongozi bora wa TANU ndio uliokipa Chama msimamo thabiti na kuwafanya
wananchi kuwa na imani kubwa na TANU.
Aidha
TANU iliweza kushinda changamoto katika sura ya hila na vikwazo kadhaa na
kupata mafanikio
3.0 ASP NA
HARAKATI ZA MAPAMBANO DHIDI YA
UKOLONI WA KIINGEREZA NA USULTANI WA KIARABU
3.1
Mazingira
ambamo ASP ilizaliwa:
·
ASP ilizaliwa
katika mazingira yaliyokwisha andaliwa kisiasa na African Association (AA) na
Shirazi Association (SA); vyama ambavyo vilikuwa nusu vya siasa na nusu vya
kupigania maslahi ya Watumishi wa Kiafrika kazini. Katika mazingira hayo, waafrika na Washirazi
walielewa kwamba:-
(a)
Adui wa
Waafrika ni ukoloni wa Kiingereza na umwinnyi wa Kiarabu ukiongozwa na Sultani.
(b)
Umoja miongoni
mwa Waafrika ni muhimu ili kujipatia uhuru wa kisiasa.
(c)
Ukoloni wa
Kiingereza ulikuwa na nia ya kutoa uhuru kwa Waarabu wa
·
Aidha, ASP
ilizaliwa katika mazingira yaliyokuwa yamejaa manung’uniko dhidi ya ukoloni wa
Kiingereza na ubwanyenye/umwinyi wa Kiarabu.
Miongoni mwa manung’uniko hayo ni:-
(i)
Kutokuwepo na
demokrasia ya kweli katika utawala wa kikoloni.
(ii)
Kutokuwepo na
wawakilishi wa Waafrika katika baraza la Kutunga Sheria kuanzia mwaka 1926 hadi
1946
(iii)
Ubaguzi katika
kazi na huduma za jamii, hususan elimu na afya.
(iv)
Ardhi ilikuwa
inamilikiwa na kusimamiwa na Waarabu. Waafrika
walikuwa manokoa katika mashamba ya Waarabu.
(v)
Sheria ya
Serikali ya Kikoloni ya mwaka 1953 iliwazuia wafanyakazi Serikalini wasishiriki
katika shughuli za kisiasa.
·
ASP ilizaliwa
baada ya Zanzibar Nationalist Party (ZNP) au HIZBU kuwa imeundwa mwaka
1955. HIZBU ndicho chama kilichotoa
upinzani mkubwa kwa ASP.
·
ASP ilizaliwa
baada ya Vita Kuu ya Pili. Uingereza ilitoka vitani ikiwa maskini ajabu
ikilinganishwa na kipindi kabla ya vita na haikuwezekana tena kuendelea
kushikilia makoloni yake. Marekani
ilizuka katika vita ikiwa Taifa lenye nguvu zaidi kuliko mataifa yote ya Ulaya
Magharibi.
·
ASP ilizaliwa
baada ya vyama vya siasa vingine kuwa vimeibuka katika nchi nyingine za Afrika
hasa TANU ambayo ilikuwa na mahusiano ya
karibu na ASP. Hata kabla ya ASP,
kulikuwa na uhusiano wa kihistoria uliojengeka tangu kuanzishwa kwa AA Tanzania
Bara na
3.1
Kuzaliwa na Kuimarika kwa ASP:
Wazo
la kuunganisha nguvu za Waafrika liliwasilishwa kwenye Mkutano wa Pamoja wa
African Association (AA) na Shirazi Association (SA) uliofanyika tarehe 5 Februari, 1957. Mkutano huo ulikubaliana kuunganisha AA na SA
na kuanzisha Afro-Shirazi Party
(ASP). Sheikh Abeid Amani Karume
alichaguliwa kuwa Rais wa kwanza wa ASP na Sheikh Thabit Kombo alichaguliwa
kuwa Katibu Mkuu.
Waasisi
wa ASP waliohudhuria Mkutano huo na kupitisha uamuzi wa kuunganiisha AA na SA
ni:-
African Association
(AA): Shirazi Association (SA):
1. Sheikh
Abeid Amani Karume 1. Sheikh Thabiti Kombo
2. Sheikh
Mtoro Rehani 2. Sheikh Muhidini Ali Omar
3. Sheikh
Ibrahim Saadallah 3. Sheikh
Ali Ameir
4. Sheikh
Mtumwa Borafia 4. Sheikh
Ameir Tajo
5. Sheikh Bakari Jabu 5. Sheikh Ali Khamis
6. Sheikh
Rajab Swedi 6. Sheikh
Mdungi Ussi
7. Sheikh
Saleh Juma 7. Sheikh
Haji Khatibu
9. Sheikh
Abdullah Kasism Hanga 8. Sheikh
Othman Sharif
9. Sheikh Ali Juma Seif
10. Sheikh Mzee Salehe Mapete.
Chimbuko
la kuunganisha AA na SA lilitokana na Tangazo la Serikali ya Kikoloni kuhusu
Uchaguzi Mkuu wa
Msimamo
wa ASP ulikuwa kwamba
Licha
ya lengo kuu la kisiasa la kuleta uhuru, ASP pia ilikuwa na malengo ya kiuchumi
na kijamii. Miongoni mwa malengo hayo
ni:-
·
Kugawa upya
ardhi ili imilikiwe na wengi badala ya wachache tu;
·
Kutoa elimu
bure kwa wote;
·
Kueneza huduma
za afya;
·
Kuwapatia wananchi
makazi bora;
·
Kuondoa dhuluma
mbali mbali na;
·
Kujenga ujamaa
na ushirika.
3.2
Uchaguzi Mkuu wa
Katika
uchaguzi huo, ASP ilipata viti 5 kati ya 6.
Kiti hicho kimoja cha
Baada
ya uchaguzi huo,
Mwaka
1959 Sultan Khalifa bin Haroub alipata nafasi ya kutembelea Uingereza, mwanae Seyyid
Abdulla ndiye akawa Sultani wa muda na wakati huo akajiunga na ZNP. Mwanae Sultan kujiunga katika Chama cha siasa
ilikuwa ni mbinu ya kuwakandamiza
Waafrika.
Sultani
na Balozi Mkazi wa Kiingereza walijitahidi kwa nguvu zao zote kuiangusha
ASP. Balozi Mkazi wa Kiingereza aliwaita
Washirazi na kuwashawishi kuanzisha Chama
chao wakati Sultani naye aliwashawishi Washirazi wajitoe katika
ASP. Baadhi
Baraza
la Kutunga Sheria. Wajumbe hao wawili ni
Sheikh Abeid Amani Karume akiwakilisha
Jimbo la Ng’ambo na mwakilishi wa Unguja Kaskazini, Sheikh Daud Mahmoud.
Kitendo
cha kuzaliwa ZPPP kilifurahisha
3.3 Ziara
ya Ian Macleod, Waziri
wa Makoloni:
Ian
Macleod alitembelea Zanzibar Desemba 1959 na alifanya mazungumzo na viongozi wa
ASP, ZNP na ZPPP. Katika mazungumzo
hayo, Macleod alikubali mambo mawili:-
(a) Tume
iteuliwe kuchunguza Katiba (maendeleo ya kikatiba)
(b) Uchaguzi
Mkuu wa pili uliokuwa umepangwa kufanyika Julai, 1960 uahirishwe hadi hapo Tume
itakapokuwa imetoa mapendekezo yake.
Tume ya Hilary Blood iliteuliwa na kupata nafasi ya kusikiliza maoni ya
viongozi wa vyama vya siasa na viongozi
wa Jumuiya.
Mapendekezo ya Tume ya Sir Hilary
Blood:-
(1) Sultan
asijihusishe na mambo yoyote ya siasa kwa maana ya kujiunga na chama cha siasa
au kusaidia chama cho chote cha siasa.
(2) Kuhusu
muundo mpya wa Baraza la Kutunga Sheria, ilipendekezwa kwamba liwe na wajumbe
21 wa kuchaguliwa na 8 wa kuteuliwa.
Aidha, ilipendekezwa kwamba Baraza jipya liwe na Spika badala ya
kuongozwa na Balozi Mkazi wa Kiingereza.
(3) Baada
ya uchaguzi mkuu,
(4) Pawepo
na upande wa Upinzani katika Baraza la Kutunga Sheria na Kiongozi wa Upinzani
apangiwe mshahara kamili.
(5)
3.4
Uchaguzi Mkuu wa Pili Januari, 1961:
ASP,
ZNP na ZPPP walishiriki katika Uchaguzi Mkuu wa Pili uliofanyika Januari,
1961. Tangazo la tarehe 16 Januari, 1961
lililotolewa na Balozi Mkazi wa Kiingereza lilieleza wazi kwamba chama cho
chote kitakachopata viti zaidi katika uchaguzi mkuu wa pili ndicho
kitakachounda Serikali. Katika uchaguzi
huo, majimbo ya uchaguzi yalikuwa 22 yaani majimbo 13
Matokeo
ya uchaguzi huo yalikuwa ifuatavyo:-
ASP – viti 10 (viti 2
ZNP – viti 9 ( viti 4
ZPPP – viti 3 (viti 3
Kwa mujibu wa matokeo hayo, mshindi alikuwa ni
ASP. Hata hivyo, matokeo hayo
yalibadilika baada ya Wajumbe 2 wa ZPPP Sheikh Mohammed Shamte na Sheikh Bakari Mohammed Bakari kuamua kujiunga na
ZNP na
Mjumbe mmoja Sheikh Ali Shariff Mussa kujiunga na ASP.
Kwa kuzingatia kwamba ASP na ZNP walikuwa na viti
sawa katika Baraza la Kutunga sheria, uamuzi ulifikiwa wa kuunda Serikali ya
Mseto ambayo ilitakiwa kudumu kwa muda wa miezi sita.
3.5
Uchaguzi Mkuu wa Tatu Juni, 1961:
Katika
uchaguzi huo, majimbo ya uchaguzi yaliongezwa toka 22 hadi 23. Jimbo jipya la uchaguzi lilikuwa Mtambile,
Pemba Kusini ambapo ZPPP ilikuwa na nguvu.
ASP, ZNP, ZPPP vilishiriki katika Uchaguzi Mkuu wa Tatu. Hata hivyo,
ZNP
na ZPPP walikuwa na makubaliano kwamba anaposimamishwa mgombea wa ZNP
asisimamishwe mgombea wa ZPPP na kinyume chake.
ASP ilisimamisha wagombea wake katika majimbo yote 23 ya uchaguzi.
Matokeo
ya Uchaguzi Mkuu wa Tatu uliofanyika tarehe 1 Juni, 1961:
·
ASP – viti
10 (Unguja 8 na
·
ZNP – viti 10
(Unguja 5 na
·
ZPPP – viti 3 (
Unguja 0 na
Kuhusu
kura, waliojiandikisha kupiga kura ni 94,218
na waliopiga kura ni 90,595 sawa na asilimia 96.15. ASP ilipata asilimia 49.9 ya kura zote
zilizopigwa, ZNP asilimia 35.0, ZPPP
asilimia 13.7 na kura zilizoharibika zilikuwa
asilimia 1.4
Matokeo
haya yanaonyesha kwamba ZNP na ZPPP kwa pamoja walipata viti 13 na ASP
viti 10. Balozi Mkazi wa
Kiingereza alimwomba Sheikh Ali Muhsin Barwani, Rais wa ZNP kuunda Serikali ya
madaraka ambaye pia alitoa nafasi hiyo kwa Sheikh Mohammed Shamte, Rais wa ZPPP
kuwa Waziri Mkuu.
Uchaguzi
Mkuu wa Tatu ulitawaliwa na vurugu:-
·
Baadhi ya
wapiga kura walipiga kura mara mbili.
·
Katika baadhi
ya masanduku kura zilitumbukizwa kabla ya upigaji kura.
·
Siku ya
uchaguzi tarehe 1 Juni, 1961 kulikuwa na fujo iliyosababisha mapigano kati ya
wafuasi wa ASP na ZNP. Inakisiwa kwamba
watu wapatao 400 walijeruhiwa na 68 walikufa.
Machafuko hayo yalipamba moto zaidi tarehe 2 Juni , 1961 baada ya
taarifa kuwafikia wanachama wa ASP kuwa Serikali ya Madaraka ilikuwa imeundwa
na ZNP pamoja na ZPPP. Vikosi vya kuzuia
fujo kutoka
Mkutano
wa kwanza wa Katiba ulifanyika London Machi, 1962. ASP iliongozwa na Mzee Karume na Othman
Shariff wakati ZNP na ZPPP iliongozwa na
Ali Muhsin Barwani (ZNP) na Mohammed Shamte (ZPPP). Baada ya Mkutano huo, Umma Party chini ya
Abdurahaman Mohammed Babu ilizaliwa.
Umma party ilikuwa na fikra za kimapinduzi, hususan fikra za
kikomunisti. Babu alijitoa ZNP na
hili lilikuwa ni pigo kwa chama hicho.
3.6
Uchaguzi Mkuu wa Nne Julai, 1963:
Majimbo
ya uchaguzi yaliongezwa toka 23 hadi 31 yaani majimbo 17 Unguja na Majimbo 14
Pemba. Kwa mara ya kwanza katika
historia ya
Matokeo
ya uchaguzi huo:-
·
ASP – viti 13
(Unguja 11 na
·
ZNP – viti 12
(Unguja 6 na
·
ZPPP – viti 6
(Unguja 0 na
Kuhusu
kura, ASP ilipata kura 87,085 sawa na asilimia 54.21; ZNP na ZPPP kwa pamoja
zilipata kura 73,559 sawa na asilimia 45.79 ya kura zote halali zilizopigwa.
Kwa
matokeo hayo, Sheikh Mohammed Shamte alitakiwa na Balozi Mkazi wa Kiingereza
Kuunda Serikali ya Ndani tarehe 17 Julai, 1963.
Mkutano wa Pili wa Katiba ulifanyika London kuanzia tarehe 20 hadi 24
Septemba, 1963 na Zanzibar ilipewa uhuru
wake wa bandia tarehe 10 Desemba, 1963 kwa mujibu wa makubaliano ya Lancaster
House – London.
Mapinduzi:
Mara
baada ya uhuru, ASP ilianza maandalizi ya kufanya Mapinduzi. Kamati ya Mapinduzi ya watu 14 iliteuliwa na
Mzee Karume na kupewa jukumu la kuandaa na kuendesha mapinduzi. Wajumbe wa Kamati hiyo walikuwa:
(1) Seif Bakari
(2) Said Washoto
(3) Abdalla
Natepe
(4) Khamis
Hemed
(5) Said
Idi Bavuai
(6) Yussuf
Himid
(7) Pili
Khamis
(8) Mohammed
Abdalla
(9) Hafidh Suleiman
(10) Hamid
Ameir
(11) Ramadhani
Haji
(12) Khamis
Darwesh
(13) Mohammed
Mfaranyaki
(14) John
Okello
Kamati
hii ya watu 14 ilifanikisha Mapinduzi Matukufu tarehe 12 Januari, 1964 na
Jamhuri ya Watu wa
Baada
ya mapinduzi, Serikali ya Mapinzudi Zanzibar ilichukua hatua zifuatazo:-
·
Kuanzisha mfumo
wa Chama kimoja cha Siasa;
·
Kutaifisha
ardhi na wananchi kugawiwa ekari tatu tatu kutokana na mashamba makubwa
yaliyokuwa yakimilikiwa na makabaila;
·
Kupiga marufuku
ubaguzi wa aina zote;
·
Kujenga majumba
ya wazee;
·
Kuanzisha na
kuendeleza mradi wa nyumba za kuishi;
·
Kutoa elimu
bure na matibabu bure;
·
Kupiga marufuku
rehani;
·
Kuchoma moto
maringisha (rickshaws) ambayo ni aina ya mikokoteni ya raha iliyotumika
kuwasafirisha mabwanyenye na watalii.
4.0
CHAMA CHA MAPINDUZI
4.1
Kuzaliwa kwa
CCM
Katika
Mkutano Mkuu wa Pamoja wa TANU na ASP uliofanyika tarehe 22 Septemba, 1975 Rais
wa TANU, Mwalimu Nyerere alisisitiza kwamba Tanzania ni nchi yenye Chama
kimoja;
“Lakini kwa sababu kuna vyama viwili TANU na ASP,
Katiba inazungumza juu ya Chama kimoja, hicho Chama kimoja kwa kweli ni vyama
viwili … Siasa ya TANU na ASP ni moja
yaani Ujamaa na Kujitegemea. Midhali
Katiba ya Tanzania ni ya Chama kimoja, Katiba hiyo inataka hicho Chama chenye
Siasa ya Ujamaa na Kujitegemea kishike hatamu na uongozi wa nchi”. (Tathmini ya
Miaka 20 ya CCM, uk. 3-4).
Kwa
msisitizo huo, Mwalimu alipendekeza kuunganishwa kwa TANU na ASP na kuundwa kwa
chama kipya. Pendekezo
Wajumbe
wa Tume ya Watu 20 ya kuandaa Katiba ya CCM:-
Kutoka ASP: Kutoka
TANU:
1. Sheikh Thabiti Kombo 1. Ndugu Peter A. Kisumo
2. Ndugu Ali Mzee 2. Ndugu
Pius Msekwa
3. Ndugu A.S. Natepe 3. Ndugu
Daudi N. Mwakawago
4. Ndugu Seif Bakari 4. Ndugu
Kingunge Ngombale-Mwiru
5. Ndugu Hamisi Hemed 5. Ndugu
Jackson Kaaya
6. Ndugu Rajab Kheri 6. Ndugu
Peter S.Siyovelwa
7. Ndugu Asia Amour 7. Ndugu
Nicodemus M. Banduka
8. Ndugu Hassan N. Moyo 8. Ndugu Lawi N. Sijaona
9. Ndugu Juma Salum 9. Ndugu
Beatrice P. Mhango
10. Ndugu Hamdan Muhiddin 10. Ndugu Basheikh A. Mikidadi
Mkutano
Mkuu wa Pamoja wa vyama vya ASP na TANU uliofanyika tarehe 21 Januari, 1977
uliazimia ifuatavyo:-
“Sisi wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Taifa wa pamoja wa TANU na ASP
tuliokutana leo tarehe 21 Januati, 1977 mjini Dar es Salaam, chini ya uongozi
wa pamoja wa Mwalimu Julius K. Nyerere, Rais wa TANU na Ndugu Aboud Jumbe, Rais
wa ASP, kwa kauli moja tunaamua na kutamka rasmi kuvunjwa kwa Tanganyika African National Union (TANU)
na Afro Shirazi Party (ASP) ifikapo tarehe 5 Februari , 1977 na wakati huo huo
kuundwa kwa Chama kipya cha pekee na chenye uwezo wa mwisho katika mambo yote
kwa mujibu wa Katiba” (Katiba ya CCM).
Aidha, Azimio
“Chama tunachokiunda tunataka kiwe chombo
madhubuti katika muundo wake na hasa katika fikra zake na vitendo vyake vya
kimapinduzi vya kufutilia mbali aina zote za unyonyaji nchini …” (Katiba ya
CCM)
Mkutano
Mkuu huo wa pamoja ulipitisha pia Katiba ya CCM na kumchagua Mwalimu Nyerere
kuwa Mwenyekiti wa CCM, Sheikh Aboud
Jumbe kuwa Makamu Mwenyekiti wa CCM na Ndugu Pius Msekwa kuwa Katibu Mtendaji
Mkuu wa CCM.
Azma
ya CCM ilikuwa ni kuendeleza mazuri yote ya TANU na ASP na kuyaacha
mabaya. Miongoni mwa mazuri
yaliyoendelezwa na CCM ni pamoja na:-
·
Kuendelea
kuimarisha uhuru wa
·
Kuendelea
kuimarisha umoja na mshikamano wa kitaifa.
·
Kuendelea
kutekeleza siasa ya Ujamaa na Kujitegemea.
·
Kuendelea
kupanua na kuimarisha demokrasia ndani ya Chama na nchini ikiwa ni pamoja na
kufungua milango ya demokrasia
4.2
CCM katika
kipindi cha Mageuzi:
CCM
Mwalimu Julius Kambarage Nyerere alifariki dunia
tarehe 14 Oktoba, 1999 Jijini London katika Hospitali ya Mtakatifu Thomas. Kifo cha Baba wa Taifa kilikuwa ni pigo kubwa
kwa CCM na Taifa letu. Kwa Watanzania,
Mwalimu ni maarufu kwa sababu yeye ndiye mwanzilishi wa Taifa letu, ni
mwanzilishi wa TANU hadi kuleta uhuru; Mwalimu na Mzee Abeid Amani Karume ndio
walioasisi Muungano; Mwalimu na Mzee Aboud Jumbe ndio walioasisi CCM; Mwalimu
ndiye aliyelijenga na kutuachia Taifa lenye umoja, udugu na mshikamano. Afrika itamkumbuka
Chini ya mfumo wa Vyama vingi vya siasa CCM kimeweza
kufanya mageuzi makubwa ya kisiasa kiuchumi na kijamii. Mageuzi ya kiuchumi yanaendelea kwa mafanikio
makubwa kupitia Ubinafsishaji na mkakati wa Uwezeshaji chini ya mkakati mkuu wa
modenaizesheni. Mageuzi ya
kisiasa yameibua kuanzishwa kwa vyama 16 vya siasa vilivyosajiliwa. Hata hivyo CCM kimeweza kujiimarisha kisiasa
na kiuhalali kupitia ushindi wa chaguzi kuu za 1995 na 2000. Ilani ya Uchaguzi ya 2000 inaendelea
kutekelezwa kwa mafanikio makubwa. Mpaka
kufikia mwishoni mwa mwaka 2003 kasi ya kukua kwa uchumi wa
Aidha CCM inaendelea kuimarisha umoja na mshikamano
wa kitaifa ikiwa ni pamoja na kuhakikisha mfumo wa vyama vingi hauwi sababu ya
chuki na msambaratiko wa umoja wa kitaifa, amani na mshikamano. Katika msimamo huo CCM imeweza kufikia
MUAFAKA na CUF, hatua ambayo imetoa fursa kwa
5.0 HITIMISHO:
5.1 Tunajifunza
nini kutokana na historia ya TANU na ASP?
Historia ya TANU na ASP inaonyesha kwamba Chama chetu wakati wote
kimekuwa na sifa zifuatazo:
·
kuimarisha
umoja;
·
kujenga utaifa
na uzalendo;
·
kupanua
demokrasia ndani ya chama;
·
kubadilika mara
kwa mara kifikra na kimuundo kulingana na wakati;
·
pamoja na
kutambua na kushughulikia matatizo ya wananchi.
CCM
kinayo nafasi nzuri ya kujifunza mambo mengi mazuri kutokana na historia ya
TANU na ASP. Katika kipindi kinachotukabili
inabidi CCM kikabiliane na changamoto mbalimbali kwa kutumia mafunzo si tu
yatokanayo na historia ya TANU na ASP, bali pia kwa kuzingatia uzoefu wake hadi
sasa. Changamoto ya utandawazi na
majukumu ya kisiasa, kiuchumi kiutamaduni na kijamii hayana majibu katika
historia peke yake. Mada zinazofuata
zinatoa fursa ya kutafakari mustakabali, mbinu na mikakati ya kukabiliana na
changamoto mbalimbali zilizopo mbele ya CCM ili kiendelee kushinda na kuendelea
kuwa Chama Tawala kinachokidhi matakwa ya Watanzania.
Imetolewa
na Idara ya Itikadi na Uenezi kwa ajili ya Semina za Halmashauri Kuu za Taifa,
Mikoa na Wilaya. Inapatikana pia katika
kitabu cha Sera za Msingi za CCM
____________________________________________________________________________________________________________________
Makao Makuu
ya CCM