HOTUBA YA MHE.
JAKAYA MRISHO KIKWETE, MWENYEKITI WA CCM NA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA
03 FEBRUARI, 2008
Mheshimiwa Amani
Abeid Karume, Makamu Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya
Mheshimiwa Ali
Mohammed Shein, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Mheshimiwa Shamsi
Vuai Nahodha, Waziri Kiongozi wa Serikali ya Mapinduzi ya
Waheshimiwa
Wajumbe wa Sekretariat, Kamati Kuu na Halmashauri Kuu ya Taifa;
Waheshimiwa
Waasisi wa TANU, ASP na CCM;
Wanachama
wenzangu wa CCM;
Waheshimiwa
Mabalozi;
Wageni Waalikwa,
Mabibi na Mabwana;
Nianze kwa kuwashukuru na kuwapongeza viongozi na wana-CCM
walioandaa sherehe hii kwa kazi nzuri
Leo ninayo furaha kubwa kujumuika nanyi kuadhimisha miaka
31 ya kuzaliwa kwa chama chetu, Chama Cha Mapinduzi. Leo ni siku ya kuangalia
tulikotoka, tulipo na tuendako katika uhai na ujenzi wa Chama chetu. Nawapongeza
viongozi na wanachama wa CCM kwa mafanikio makubwa tuliyoyapata katika kukijenga,
kukitunza na kukiimarisha Chama cha Mapinduzi katika uhai wake wa miaka 31.
Kuweza tu kudumu kwa miaka 31, na nusu ya miaka hiyo ikiwa ni ndani ya
ushindani wa vyama vingi, ni mafanikio makubwa ambayo wote hatuna budi
kujivunia nayo.
Lakini jambo
linalitia faraja ni ule ukweli kwamba Chama chetu kimeiongoza nchi yetu vizuri
na mafanikio yako wazi. Mwenye macho
haambiwi tazama. Hata asiyetupenda hawezi
kubisha kuwa tumefanya mengi mazuri na mazuri zaidi yanakuja.
Ndugu zangu,
viongozi wenzangu wana CCM wenzangu hatuna budi kujipongeza kwa yote
tuliyoyafanya. Na watani zetu nao
wanapotupinga, nao wawe wakweli kwa kuyatambua mengi mazuri tuliyoyafanya. “Baniani mpigeni, upati wake mpeni”. Nataka kuwahakikishia kuwa Serikali ya
Mapinduzi ya
Ndugu Wanachama wenzangu wa CCM;
Wakati tunajivunia uhai na uimara wa Chama chetu kwa
miaka 31 na mafanikio yaliyopatikana nchini chini ya uongozi wake hatuna budi
kukumbuka kuwa kazi ya kukiimarisha Chama cha Mapinduzi ni inayoendelea, yaani
ni kazi ya kudumu.
Kila uongozi wa CCM uliopita, umechukua hatua muafaka,
kulingana na mazingira ya kisiasa na kiuchumi ya wakati huo, kukiimarisha Chama
chetu. Na sisi tuliopo sasa kwenye uongozi wa CCM, tunaendelea na pale uongozi
uliopita uliishia. Tunachukua hatua thabiti za kuendelea kukiimarisha Chama cha
Mapinduzi.
Kazi
iliyo Mbele Yetu (2008)
Ndugu Viongozi, Wanachama,
Wapenzi na Washabiki wa CCM;
Katika mwaka huu mpya wa 2008, Chama chetu ni
muhimu kijielekeze katika kufanikisha majukumu saba yafuatayo:
Utekelezaji
wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM
Jukumu la kwanza, na kubwa zaidi, ni kuendelea kusimamia
utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM. Kazi hii tumekuwa tukiifanya tangu
Serikali hii iingie madarakani, lakini ningependa sasa, katika mwaka huu wa
2008, Chama chetu kiongeze nguvu na umakini zaidi katika kuhakikisha kwamba
Ilani na ahadi zake kwa Watanzania zinatekelezwa kwa ukamilifu na kwa kasi
inayoridhisha. Sasa tumefikia katikati ya safari yetu ya miaka mitano ya
uongozi wa Taifa letu. Wakati wa kurudi tena kwa wananchi hauko mbali.
Viongozi wa CCM ni
lazima wajue Chama chao kiliahidi mambo gani katika maeneo
Katika Ilani ya CCM kuna yale mambo ya kawaida,
tunayoyaongelea siku, yanayohusu ustawi
wa kiuchumi, kisiasa na kijamii wa
Na, hapa kuna
wajibu wa kimsimamo na kimtazamo, lakini vilevile kuna wajibu wa vitendo,
ambapo Ilani inawataka viongozi wa CCM waongoze kwa kuonyesha njia. Tunapopiga
vita rushwa inapendeza zaidi sisi wenyewe tukiwa waadilifu. Tunapohimiza
mapinduzi ya kilimo, na sisi viongozi, ambao tunalima, tuwe na mashamba ya
mifano. Ilani inawahimiza viongozi na wanachama wa CCM kuwa mfano wa kuigwa kwa
uchapakazi na kujitegemea katika maisha.
Ndugu zangu,
tukizingatia haya, na maagizo mengine ya Ilani kwa viongozi na wanachama wa
CCM, Chama chetu, sio tu kitakuwa kinaongoza mapambano dhidi ya umaskini, bali
kitakuwa kinatoa uongozi madhubuti katika maisha na ustawi wa watu wa nchi
yetu.
Maandalizi
ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa
Ndugu Wanachama wenzangu;
Jukumu la pili la Chama chetu kwa mwaka huu mpya wa 2008,
ni maandalizi ya uchaguzi wa Serikali za Mitaa utakaofanyika mwaka ujao, wa
2009.
Pia kuanza matayarisho ya Uchaguzi Mkuu wa 2010.
Na, katika kutafuta ushindi wa Serikali za Vijiji na
Vitongoji, matumaini yetu yapo kwa viongozi na watendaji wa CCM katika ngazi za
mashina, matawi na kata. Bahati nzuri mwaka wa jana Chama chetu kilikamilisha
kuunda safu ya uongozi katika ngazi hizo. CCM imejitengenezea mtandao mkubwa
katika ngazi zote za utawala nchini mwetu, ambao wahimili wake ni wanachama
wake na wapenzi wake. Tuhakikishe kwamba tunautumia mtandao huu kushinda katika
chaguzi zilizo mbele yetu. Nawaomba viongozi wa CCM ngazi za Wilaya, Mikoa na
Taifa, tuhakikishe kwamba tunazo orodha za vijiji na vitongoji vyote katika
maeneo yetu. Aidha, tuhakikishe kuwa safu za uongozi katika ngazi za vijiji na
vitongoji zimekamilika na tunawapatia viongozi hawa mafunzo yapasayo. Chama cha
Mapinduzi lazima kishiriki uchaguzi katika kila kijiji na kitongoji nchini.
Hivyo tuanze pia kuwatambua na kuwashawishi wanachama na makada kujiandaa kwa
uchaguzi.
Ushiriki
katika Zoezi la Kuboresha Daftari la Wapiga Kura
Ndugu Wananchi,
Chama cha Mapinduzi, katika mwaka huu, ni lazima kijielekeze
katika kuwahamasisha wananchi washiriki kwenye zoezi la Kuboresha Daftari la
Wapiga Kura. Hili ni jukumu la tatu kwa mwaka wa 2008.
Katika chaguzi zote, siri mojawapo kubwa ya ushindi wa
Chama chetu ni kuhakikisha kwamba wanachama, wapenzi na washabiki wa CCM
wanajiandikisha kupiga kura na siku ya kupiga kura wanajitokeza vituoni na
wanapigia kura wagombea wa CCM. Hii ni siri ya ushindi ambayo hatuna budi
kuikumbuka na kuifanyia kazi.
Sasa hivi kote nchini, Tume ya Uchaguzi inaendesha zoezi
la Kuboresha Daftari la Wapiga Kura. Wale ambao hawakuwa wameandikishwa mara ya
mwisho sasa wana nafasi hiyo. Na wale ambao walikuwa hawajafikia umri wa kupiga
kura kwenye uchaguzi uliopita, na sasa wamefikisha umri stahiki, pia wana fursa
ya kujiandikisha sasa na kushiriki kwenye chaguzi zijazo kuanzia sasa. Lakini
pia wapo wenzetu wengine ambao wamepoteza kadi zao za kupigia kura, nao pia
wajitokeze kujiandikisha wapewe kadi mpya.
Ndugu zangu, suala la kuhimiza wananchi kujitokeza
kujiandikisha ni jambo lenye maslahi makubwa kwa Chama chetu. Nasisitiza kuwa
tuhakikishe wanachama wetu, wapenzi na washabiki wa CCM wanajiandikisha. Pamoja
na hayo, hili ni jambo lenye maslahi mapana kwa kwa nchi yetu pia. Demokrasia
inasimama kwenye msingi wa wananchi kuchagua viongozi wao. Na, kwa mujibu wa sheria
ya nchi yetu, mtu huwezi kuchagua kiongozi ambaye
Chama cha Mapinduzi ni lazima kitoe uongozi kwenye zoezi
hili muhimu kwa maendeleo ya demokrasia nchini mwetu.
Kuimarisha
Uhusiano Baina ya CCM na Vyama vya Upinzani
Ndugu Wanachama wenzangu;
Mwaka huu pia ni mwaka wa kuimarisha mahusiano baina ya
Chama chetu na vyama vya upinzani nchini. Kwenye kuendesha mfumo wa siasa za
vyama vingi, kuna sehemu mbili. Sehemu ya kwanza ni ushindani. Na sehemu ya
pili ni ushirikiano. Ushindani ni wakati wa uchaguzi, na uchaguzi unapokwisha,
kwa kuwa wote tunajenga nchi moja, hatua inayofuata ni ushirikiano.
Kuimarisha
ushirikiano na mahusiano baina ya CCM au Serikali na vyama vya upinzani imekuwa
ni dhamira yangu tangu mnipe heshima ya kuliongoza taifa letu mwaka 2005.
Na, ndio maana
niliunda Wizara mahsusi katika Ofisi yangu, Wizara inayoongozwa na Mzee
Kingunge Ngombale Mwiru kwa ajili hiyo, pamoja na mambo mengine.
Niliwaahidi
Watanzania kwenye salamu zangu za mwaka mpya wa 2008 kwamba mwaka huu
tutaongeza juhudi katika kutimiza azma hii. Ningependa CCM ionyeshe uongozi
kwenye suala hili na pia kuonyesha njia kwamba siasa za upinzani hazina maana
ya uadui, chuki na kutokushirikiana.
Kwa sasa, nchi yetu
ina taasisi mbili ambapo vyama vya siasa vinaweza kuzitumia kushirikiana
vizuri.
Lakini pia ipo
taasisi ya Kituo cha Demokrasia
Ndugu zangu;
Kwa hapa Visiwani,
ambapo kwa muda mrefu sasa, mahusiano ya kisiasa baina ya CCM na CUF yamekuwa
sio mazuri, naomba niseme mambo yafuatayo;
Kuendelea
Kusimamia Maadili ya Viongozi na Uongozi
Ndugu Wanachama wa CCM;
Jukumu jingine kubwa lililo mbele yetu
Kimsingi, suala la maadili limesisitizwa na Chama chetu
ndani ya Ilani yake ya Uchaguzi wa 2005. Ibara ya 110 ya Ilani hiyo, pamoja na
mambo mengine, inazitaka Serikali na CCM “kuongeza juhudi za kuendelea kuchukua
hatua za kisheria, kiutawala na kinidhamu kwa wote watakaobainika kuhusika na
vitendo vya rushwa”.
Kwa maana hiyo, hatua ambazo Serikali na CCM imekuwa
inazichukua kupambana na rushwa, wizi na ubadhirifu wa nchi ni utekelezaji
thabiti wa maagizo hayo ya Chama kupitia Katiba ya Chama na Ilani ya CCM.
Ndugu zangu, kwahiyo basi, mwaka huu wa 2008, uwe ni
mwaka wa kuimarisha juhudi za kusimamia maadili ya viongozi wa Chama na
Serikali. Hivi majuzi, nimeelezea nia ya Serikali ya Muungano kuweka utaratibu
utakaowawezesha Wabunge na Mawaziri kutenganisha shughuli za biashara na
uongozi. Katika nchi
Kutekeleza
Mradi wa Kuimarisha Chama
Ndugu zangu;
Mwaka 2006, Chama chetu kilizindua Awamu ya Tatu ya Mradi
wa Kuimarisha Chama. Na, mwaka jana, tulizindua shughuli za utekelezaji wa
mradi huo kwa hapa
Lakini mwaka jana, tulijielekeza zaidi kwenye kufanikisha
zoezi la uchaguzi wa ndani ya Chama nchini, kwahiyo hatukutumia muda wa kutosha
kutekeleza Miradi hii ya kuimarisha Chama.
Ningependa kuona mwaka huu na kuendelea tunatoa msukumo maalum wa kuhakikisha kuwa madhumuni ya Mradi
yanafikiwa. Kubwa zaidi katika kutekeleza mradi huu ni kuhakikisha kwamba wanachama
wa CCM na jumuiya zake wanaongezeka. Wanachama ambao ni imara kukitetea na
kukilinda Chama chao. Wanaolipa ada zao kwa wakati na kuchangia maendeleo ya
Chama chao. Nafurahi leo kupokea wanachama wapya wengi. Kume inawezekana. Mtaji
wetu unazidi kukua. Pili, kuhakikisha kuwa Chama chetu kinao viongozi walio
madhubuti: yaani waaminifu kwa Chama, waadilifu, wachapakazi hodari na jasiri
katika kukipigania Chama chao; viongozi waliopatikana kidemokrasia. Na kwa
hapa, kuwa na viongozi wenye sifa hizo ni muhimu
Naomba tukubaliane
kwa dhati sasa kwamba viongozi wa Chama wanapofanya ziara katika maeneo
Uchaguzi wa Jumuiya
Mwaka huu ni mwaka
wa uchaguzi wa Jumuiya. Nawatakia kila
la heri, mambo yaende kwa mafanikio.
Hata hivyo, niwaombe viongozi wenzangu
kutambua wajibu wao wa kuhakikisha kuwa chaguzi hizi zinafanikiwa. Pia nawaomba wanajumuiya kuzingatia maadili
ya uchaguzi. Kasoro zilizokuwepo uchaguzi
uliopita tuziepuke. Ni jambo
lisilokubalika. Tuwe waadilifu.
Ndugu zangu,
Mwisho
Ndugu viongozi na wanachama wa
CCM;
Mimi naamini tukiyatekeleza kwa ukamilifu majukumu haya
saba katika mwaka huu wa 2008, tutakuwa tumepiga hatua kubwa katika kukiimarisha
Chama chetu na kuzidisha imani ya wananchi kwa CCM.
Mwisho, ndugu viongozi, naomba niongelee kwa kifupi jambo
moja muhimu na la kihistoria ambalo tumeamua ndani ya Chama tuliadhimishe kwa
pamoja na sherehe za miaka ya 31 ya kuzaliwa kwa CCM. Mwaka huu ni Jubilei (Miaka 50) ya Uamuzi wa
Busara wa Tabora, ambapo TANU iliamua kushiriki uchaguzi wa kura tatu. Uamuzi
ule, ambao ulipingwa
Lakini uamuzi ule una mafundisho makubwa
Hata hivyo,
Serikali ya Kikoloni ya Uingereza ilipanga uchaguzi wa Baraza la Kutunga Sheria
ufanyike kwa namna na misingi ambayo ni kinyume na imani hii ya msingi ya
TANU. Wakaloni waliamua watu wa
Kwahiyo, mjadala
ukaletwa mbele ya Mkutano Mkuu wa TANU mjini Tabora, tarehe 21 Januari 1958.
Je, TANU ishiriki kwenye uchaguzi ambao utaendeshwa kwa namna ambayo TANU
yenyewe na vyama vingine vya ukombozi
Barani Afrika vimekuwa vinaupinga hadharani siku zote?
Baada ya mjadala
mrefu na mkali, TANU, pamoja na kukiri kwamba mfumo wa kura tatu ni mbaya,
iliamua kushiriki uchaguzi ule. TANU ilishinda viti karibu vyote
vilivyogombaniwa na hivyo kuweza kutawala na kudhibiti mwelekeo na shughuli za
Baraza la Kutunga Sheria, hivyo kuwezesha kutungwa Sheria na kupitishwa kwa
maamuzi yenye tija na maslahi kwa Watanganyika. Hata kupatikana kwa uhuru wa
Fundisho kubwa tunalopata
kutokana na uamuzi ule ni kwamba wakati mwingine viongozi wa siasa tunawajibika
kufanya maamuzi magumu, ambayo wakati mwingine yanaendana kinyume na tunayoaamini
na kuyahubiri. Cha msingi ni kwamba maamuzi yoyote ya kisiasa ni lazima
yaangalie manufaa mapana zaidi ya Taifa.
Vilevile, kwetu
sisi katika CCM tunajivunia urithi wa viongozi na uongozi wa busara ambao siku
zote, yanapokuja maamuzi makubwa, maslahi ya Taifa yanawekwa mbele. Huu ni
urithi ambao hatuna budi kuuenzi na kuutafsiri kwa vitendo na kuupitisha kwa
vizazi vijavyo vya viongozi wa Chama chetu na Taifa letu.
KIDUMU
CHAMA CHA MAPINDUZI!
MAPINDUZIII!
Asanteni