HOTUBA YA RAIS WA JAMHURI YA
MUUNGANO WA
DAR ES SALAAM, UKUMBI WA
DIAMOND JUBILEE,
DAR ES SALAAM, TAREHE 14
FEBRUARI, 2008
Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa;
Waheshimiwa Wazee Wangu wote
mliopo hapa;
Waheshimiwa Viongozi
wenzangu;
Mabibi na Mabwana:
Wazee Wangu;
Nawashukuru Wazee wa Chama na Serikali wa Mkoa wa
Nilikuwa na mawazo ya kufanya mabadiliko katika Baraza la
Mawaziri, lakini siyo wakati huu. Kwa
fikra yangu tungefanya baada ya Bunge na baada ya mgeni wetu kuondoka. Yangekuwa
mabadiliko ya kawaida. Tumefikia miaka
miwili, tulianza zoezi la kufanya tathmini ya hali ya utendaji ya kila mmoja
wetu ili tujue turekebishe wapi na vipi!
Sikutarajia kufanya mabadiliko makubwa kiasi hiki. Lakini ya Mwenyezi
Mungu huyajui. Mwanadamu unakuwa na yako
na Mwenyezi Mungu anakuwa na yake usiyoyajua wala kuyategemea. Lakini kila linalotokea lina heri yake.
Wazee Wangu;
Kama nilivyosema jana, nilikuwa nimepanga kikao changu cha
Baraza la Mawaziri Jumanne tarehe 06 Februari, 2008 pale
Lakini, mtakumbuka kuwa katika kikao kilichopita cha Bunge,
Wabunge waliamua kuunda Kamati Teule kuchunguza tuhuma zihusuzo utoaji wa
zabuni kwa Kampuni ya
Nalitaja jambo hili kwa sababu nasikia watani zetu wanadai
ati ya
Shelukindo ni wa CUF, hivi
Mwakyembe ni wa CHADEMA? Hivi Anne
Kilango niwa TLP? Au Seleli ni wa
UMD. Ukweli ni kwamba jambo hili liliwahusisha Wabunge wa Pande zote. Lilianzia kwa Mzee Shelukindo wa CCM kwa
maana ya wazo na uchunguzi ukafanywa na Dr.
Mwakyembe wa CCM na wenzake wa CCM na mmoja wa CUF. Leo kugeuzwa la upinzani na
siyo la CCM sielewi.
Lakini, kabla ya kuletwa Bungeni na kuamuliwa Kamati Teule
ya Bunge iundwe, Kamati ya Uongozi ya
CCM Bungeni ilikutana kulijadili suala
Wazee Wangu;
Naomba mniruhusu nilizungumzie kidogo suala la Kamati ya
Chama ya Bunge kwani kumekuwepo na upotoshaji kuhusu kuwepo kwake na kazi zake.
Kwanza ipo kwenye Katiba ya CCM ibara 104(7) inasema “Kutakuwa na Kamati ya Wabunge wote wa CCM”
Ipo pia Kamati
Kuwa na Kamati ya Chama Bungeni ni jambo tulilorithi toka
kwa waasisi wa Chama chetu na Taifa letu.
Tumekuwa nayo tangu wakati wa Chama kimoja mpaka sasa. Ni jukwaa muhimu na mambo mengi makubwa
yamefanywa kupitia kikao hiki. Hatuna
budi kuuenzi mfumo huo na kuuimarisha. Napenda kurudia tena pongezi zangu kwa
Kamati ya CCM Bungeni kwa kazi nzuri inayoendelea kuifanya. Inawezekana kuwepo mapungufu ya hapa na pale,
ninawaomba Waheshimiwa Wabunge wasisite, wazungumze kwa uwazi na kufanya
marekebisho stahiki. Mimi naamini hakuna kasoro yoyote iwe ya muundo au ya watu
binafsi ambayo haizungumziki na kurekebishika.
Wazungumzaji ni Wajumbe wenyewe wa kikao hicho ambao ni Wabunge
wetu. Ni watu makini na watu
jasiri. Katika kikao kilichopita cha
Kamati Kuu, tulisisitiza umuhimu wa Kamati ya Chama kutumika ipasavyo. Hakuna badala yake. Vinginevyo itakuwa kuburuzana kwa maslahi
binafsi ya watu Bungeni badala ya maslahi ya Chama na Taifa.
Wazee Wangu;
Nilisema mwanzoni kuwa, nilipokwenda
Baadae usiku nilipokea taarifa ya vikao hivyo viwili vya
Chama chetu. Baada ya kufuatilia mjadala Bungeni siku iliyofuata na kusikiliza hisia za watu nchini ndipo tukafikia kwenye
maamuzi yale magumu na mazito tuliyofanya. Maamuzi ambayo yalipelekea kuvunjwa kwa
Baraza la Mawaziri. Ni maamuzi magumu,
lakini yalikuwa hayana budi kufanyika kwa maslahi ya utangamano wa taifa
letu. Uamuzi mwingineo tofauti ulikuwa unaliingiza taifa letu kwenye matatizo
makubwa zaidi. Ni uamuzi mgumu kwa sababu
unawahusu watu ambao ni wenzangu wa karibu kimaisha na kikazi kwa miaka mingi.
Na pia kwa sababu unaona wazi kuwa
Wazee Wangu;
Wananchi Wenzangu;
Napenda kuitumia nafasi hii kumshukuru
Nawashukuru
Wazee wangu;
Ni ukweli ulio wazi kuwa hiki kipindi cha wiki moja kilikuwa
kigumu
Nawashukuru
Hali iliyojitokeza na jinsi tulivyoishughulikia pia ni
kielelezo cha wazi cha kukomaa kwa demokrasia ya nchi yetu. Licha ya hofu na msukosuko mkubwa tulioupata tumeweza kuvuka
salama. Nchi yetu tayari imerudia hali
yake ya kawaida na kila mmoja wetu anaendelea na shughuli zake. Hili nalo ni jambo jema la kujivunia
Ndugu zangu, Wazee Wangu;
Kule kwenye shaka tulikokuwa
tayari tumeshapita. Baraza jipya la
Mawaziri limeshapatikana. Kazi iliyo mbele yetu
Ripoti ya Kamati ya Mhe. Mwakyembe ina mapendekezo
mazuri. Bunge letu linaendelea kuijadili
taarifa hiyo. Tunayasubiri kwa hamu
mapendekezo ya Bunge mwishoni mwa mjadala.
Nia yangu kuwa yale yanayoihusu Serikali tuyafanyie kazi mapema iwezekanavyo.
Ndugu Wananchi, Wazee
Wangu;
Kabla ya kumaliza naomba kurudia niliyoyasema. Nimesema nchi yetu imepita kipindi kigumu,
kipindi kilichotuletea mtikisiko mkubwa.
Lakini kwa dua zenu na sala zenu tumevuka salama. Kazi iliyo mbele yetu sasa
ni kuwatumikieni kwa uwezo wetu wote ili kutimiza ahadi zetu kwenu.
Daima tujitahidi kuwa watumishi wenu makini. Kila mara tutahakikisha kuwa tunafanya
maamuzi yenye manufaa na tija kwa taifa na wananchi wetu. Hatutasita kuchukua hatua kwa mambo yote
yanayopingana na maslahi ya watu wetu.
Nawashukuru tena kwa utulivu wenu, uelewa wenu na
mshikamano wenu mliouonyesha. Nawaomba tuendeleze moyo huo wa uzalendo na
mapenzi makubwa kwa nchi yetu.
Nitakuwa mwizi wa fadhila
Ndugu Wananchi;
Aidha, namshukuru Waziri Mkuu wetu mpya, Mheshimiwa Pinda
kwa kukubali kubeba jukumu
Naomba mniruhusu pia nitumie fursa hii kuwataarifu tena
kuwa keshokutwa tunao ugeni mkubwa na wa
kihistoria wa kutembelewa na Rais wa Marekani, Mheshimiwa George W. Bush. Rais Bush na Mkewe mama laura Bush na Ujumbe
wake watawasili hapa nchini kesho kutwa siku ya Jumamosi Februari 16. Ujio wake ni heshima kubwa kwa nchi
yetu. Hii ni mara ya pili kwa nchi yetu
kutembelewa na Kiongozi wa taifa
Hivyo kupitia kwenu Wazee wangu naomba sote tujitokeze
kumlaki mgeni wetu huyo kwa furaha na ukarimu wa Watanzania. Tumuonyeshe kuwa
sisi Watanzania ni watu wema na wakarimu, tunaojali na kuthamini urafiki wetu
na mataifa mengine. Tuhakikishe kuwa
mgeni wetu huyo awapo hapa nchini yupo salama na anarejea salama.
Mwisho kabisa nawashukuruni tena Wazee wangu kwa kuacha kazi
zenu na kuja kuzungumza nami. Niliona ni busara tubadilishane mawazo kuhusu hali iliyojitokeza na jinsi tulivyoikabili
sote
Asanteni kwa
kunisikiliza.