HOTUBA YA MHE.
JAKAYA MRISHO KIKWETE, RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA
Mhe. Ali Mohammed Shein, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa
Mhe. Amani Abeid Karume, Makamu Mwenyekiti wa CCM na
Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya
Mhe. Mhe. Pius Msekwa, Makamu Mwenyekiti wa CCM
Makamu Mwenyekiti Mstaafu, Mzee Rashid Mfaume Kawawa;
Mwenyeji wetu hapa Butiama, Mama Maria Nyerere;
Wajumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa;
Wajumbe Wenzangu wa Halmashauri Kuu ya Taifa;
Nianze kwa kuwashukuru wenyeji wetu,
wanakijiji wa hapa Butiama, wakiongozwa na Mama yetu, Mama Maria Nyerere,
kwanza, kwa kutukubalia tufanye mkutano wetu huu hapa kijijini kwao; na, pili,
kwa kutupokea na kutukaribisha vizuri sana. Tunawashukuru
Nawashukuru
na kuwapongeza wanachama na viongozi wa CCM wa Mkoa wa Mara kwa mapokezi mazuri
na kwa maandalizi mazuri ya mkutano huu. Mmetupokea vizuri na mmetupangia
ratiba nzuri. Wajumbe wa NEC wamepita
maeneo mengi, wameona mambo mengi ya maendeleo ya Chama na Mkoa yanayotia
moyo. Wameona juhudi kubwa wazifanyazo wanachama,
wapenzi na washabiki wa CCM mkoani Mara za kujiletea maendeleo na kujenga Chama
chao. Tumeona raha zenu na karaha
zenu. Tunawapongeza kwa mafanikio na
kuwahakikishia kuwa tumeona, tumesikia, tuko pamoja nanyi.
Napenda
kutumia nafasi hii kutoa pongezi mahsusi kwa Mhe. Nimrod Mkono, Mjumbe mwenzetu
wa NEC na Mbunge wa Musoma Vijijjini, kwa kazi kubwa aliyoifanya na mchango
wake muhimu uliowezesha kufanikisha mkutano huu kufanyika kwa kiwango
hiki. Amesimamia kwa ufanisi mkubwa
ujenzi wa ukumbi huu. Ahsante
Ndugu Wajumbe wenzangu wa Halmashauri Kuu ya Taifa,
Ndugu Wageni Waalikwa,
Tulipoamua
kufanya mkutano wetu huu hapa Butiama, sikujua kwamba uamuzi huo ungezua
mjadala na matumaini makubwa kuliko matarajio halisi ya sisi tulioamua. Kwangu
mimi na wenzangu katika Halmashauri Kuu ya Taifa, tulitaka kurudia utaratibu
mzuri wa zamani ambapo vikao vya NEC vilikuwa vinafanyika mikoani kwa
mzunguko. Yaani, Mkoa ambao ulikuwa
tayari kuwa mwenyeji uliwaalika Wajumbe wa NEC kwenda kufanya mkutano wao
kule. Hapo katikati, kwa sababu
mbalimbali, utaratibu huo ukaachwa na vikao vyote vikawa vinafanyika
Tuliona
ni busara sasa turudie kwenye ule utaratibu wetu wa zamani. Tuliamua hivyo baada ya kupima manufaa
makubwa tutakayoyapata ya kuhamasisha uhai wa Chama katika Mikoa mwenyeji. Pia ni fursa ya kuwafanya viongozi wa ngazi
ya juu wa Chama chetu wakijue vizuri zaidi Chama na waijue kwa undani zaidi
nchi ambayo wana dhamana ya kuiongoza. Ni
kutokana na shabaha hiyo, karibu kwa muda wa siku tatu, Wajumbe wa NEC
wametembelea Wilaya zote za Chama za Mkoa huu kukagua uhai wa Chama, kuzungumza
na viongozi na wanachama wa CCM. Aidha,
wamekagua shughuli za maendeleo na kuzungumza na wananchi. Ni ukweli ulio dhahiri kwamba ziara hizo za
Wajumbe wa NEC zitakuwa zimepanda mbegu itakayochipua mmea mzuri wa kudumisha
na kuendeleza uhai wa Chama chetu siku za usoni.
Baada
ya NEC kuamua hivyo, Mkoa wa Mara ulikuwa ndiyo Mkoa wa kwanza kuwa tayari kuwa
mwenyeji wa mkutano wa NEC katika utaratibu huu mpya. Naambiwa Mkoa wa
Ndugu
Wajumbe;
NEC
ilipoamua kuwa Mkoa wa Mara uwe wenyeji wa kikao hiki, tuliona ni vyema mkutano
huu tuje kuufanyia hapa Butiama, kwa sababu nzuri. Hapa ndipo alipozaliwa na kuzikwa muasisi wa
Chama hiki na Taifa letu. Hii ni mara ya
kwanza NEC nzima inakuwa Mkoani Mara kwa pamoja tangu alipotutoka mzee wetu
huyu kipenzi. Ni mahali muafaka kabisa
kuja kufanyia mkutano. Tuwape nafasi
wasiopajua Butiama wapajue. Watu wapate
nafasi ya kuzuru kaburi lake. Lakini pia tulitaka kuiweka hai kumbukumbu ya
mahali muhimu kwa Chama chetu na Taifa letu.
Kwa kufanya hivyo, tunaiweka hai kumbukumbu ya Mzee wetu hayati Mwalimu
Julius Kambarage Nyerere.
Pamoja
na hayo, tutumie nafasi hii kujikumbusha juu ya mema mengi ambayo Mwalimu
amelifanyia taifa letu na Chama hiki alichokiasisi. Tujikumbushe kuhusu moyo wa kujitolea kwa
ajili ya wengi na moyo wa uzalendo kwa nchi.
Tujikumbushe wajibu wa viongozi kuzingatia misingi ya uadilifu na
uaminifu. Rais wa zamani wa Marekani,
John F. Kennedy, alisema: “mifano ya watu mashuhuri huzaa watu wa
kiwango hicho”. Kuja hapa kutatupa
ari ya kuishi na kutumikia taifa na watu wake kwa mfano wa Mwalimu Julius
Kambarage Nyerere.
Ndugu
Wajumbe, huu ni mwanzo tu wa hatua za kuiweka kumbukumbu ya Baba wa Taifa. Tutafanya mambo mengine ambayo yatafanya watu
wawe wanamkumbuka Baba wa Taifa na wanaikumbuka Butiama. Kwa mfano, mwenge wa Uhuru utazimwa Butiama
mwakani. Pia, siku za usoni, hapo
tutakapofikia uamuzi wa kuigawa wilaya ya Musoma kiserikali, nitapenda,
Matumaini Makubwa
Ndugu Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya
Taifa;
Kwetu
sisi tulioamua mkutano huu ufanyike hapa, tuliona kuwa tumefanya uamuzi wa
kawaida tu kwa ajili ya kikao cha kawaida cha Halmashauri Kuu ya Taifa. Kumbe
hatukujua kuwa kwa sababu ya uhusiano wa Baba wa Taifa imejengeka imani kuwa
kikao hiki ni maalum kwa ajili ya kufanya maamuzi mazito. Kwa namna fulani, wanaofikiria hivyo
hawajakosea, kwani NEC ni kikao kikubwa
Na
hata kwenye kikao hiki, yatakuwepo maamuzi muhimu yatakayofanyika. Tutatoa taarifa mwisho wa kikao. Lakini napenda kusema kuwa maamuzi hayo
hayatahusu mageuzi ya kisera au kiitikadi.
Nalisema hili kwa sababu wapo watu wanaotumaini au wenye hofu kuwa hapa
Butiama kutatokea tamko la kurudia tena kutaifisha
Napenda
kuwahakikishia kuwa hili halitatokea na wala siyo makusudi ya kikao cha Butiama
kuja na maamuzi ya kugeuka nyuma kwenye mageuzi ya kisiasa na kiuchumi
tuliyoyafanya. Mageuzi ambayo pamoja na
matatizo ya hapa na pale yameliweka taifa letu katika msingi mzuri wa maendeleo
ya sasa na siku za usoni.
Ndugu
Wajumbe,
Nawashukuru
KIDUMU CHAMA
CHA MAPINDUZI