|
|
| JARIDA
LA MKEREKETWA
|
Sera
ya CCM ya Ubinafsishaji wa Mashirika
ya Umma ni ukombozi mkubwa |
|
- Ukuzaji
wa ajira umeongezeka
- Mapato
ya Serikali yameongezeka
-
Watanzania wanunua mashirika mengi
|
|
|
Marekebisho
ya Mazingira ya Tanzania yamegusa maeneo yote, yaani,
siasa, sheria, huduma za jamii, sekta ya fedha na uchumi
kwa jumla. Hata hivyo kutokana na mabadiliko yanayotokea
duniani hivi sasa tunahitaji pia kubadilisha utamaduni
wetu, mtazamo wetu na fikra zenu. Miaka zaidi ya 35
ya uchumi hodhi inatuhitaji tukabili zama hizi za uchumi
wa soko huria na utandawazi.
Ubinafsishaji ni moja ya mbinu za kurekebisha uchumi
wa nchi ambao ni kama asilimia 2 tu ya utaratibu wote
wa urekebishaji huo. Kimsingi Sera ya Ubinafsishaji
ambayo ni ya CCM imelenga katika kuifanya Serikali iachilie
kuhodhi nguzo kuu na nyenzo za kuzalisha mali na uchumi
na badala yake jukumu hili kuliachia Sekta Binafsi.
Serikali imebakia na jukumu la kuboresha masuala ya
sheria na utawala bora pamoja na uimarishaji wa miundo
mbinu na suala zima la kuendeleza huduma za jamii. Ubinafsishaji
huchukua moja kati ya sura zifuatazo:-
· Uuzaji wa kiwanda/shirika moja kwa moja
· Utaratibu wa Ubia
· Uuzaji na ununuzi wa hisa
· Ununuzi ufanywao na Menejimenti
· Ubinafsishaji wa Mashirika ya Miundo mbinu.
Chimbuko la sera hii lilianza miaka ya 1980 wakati tuliposhindwa
kabisa kihimili na kuyaendesha mashirika na kuyaendesha
mashirika yetu mengi. Hadi mwaka 1990 zaidi ya mashirika
400 yaliliingiza taifa hasara ya shs. 100 bilioni na
yalikuwa yanadaiwa kodi ya shs. 352 bilioni. Kiwango
cha uzalishaji viwandani ulifikia asilimia 25 ya uwezo.
Mashirika 70 tayari yalikwishafilisika na Watanzania
wengi kupoteza ajira. Tukumbuke wakati ule wa uhaba
wa bidhaa. Magendo na ulanguzi vilikithiri na urasimu
na menejimenti dhaifu vilitawala. Mashirika haya hayakuendelea
kwa maana ya kubadilisha teknolojia, kukuza mitaji,
ujuzi, rushwa ilikithiri ikiandamana na upendeleo. Kanuni
zote za kiuchumi zilikiukwa.
Hali hii ilikifanya Chama chetu cha CCM kuona ni njia
zipi zinahitaji kutekelezwa. Ilipofika mwaka 1992 Bunge
lilipitisha sheria kuruhusu Sekta Binafsi kumiliki,
kuendesha na kununua mashirika. Na mwaka 1993 Bunge
lilirekebisha sheria hiyo ili kuruhusu kuanzishwa kwa
Tume ya Rais ya Kurekebisha Mashirika ya Umma (PSRC).
Kimsingi madhumuni ya Ubinafsishaji yamelenga katika
kuendeleza tija, kupanua wajibu wa Sekta Binafsi, kukuza
nafasi za ajira, kuendeleza mitaji na teknolojia ili
kukuza uchumi wetu. |
|
|
|
|
|
|
Mashine
ya kisasa ya kupakia na kupakua mizigo kutoka kwenye
ndege. Mashine hiyo ni moja ya vitendea kazi vya kisasa
vinavyotumiwa na DAHACO baada
ya kubinafsishwa. |
|
|
|
Matokeo
yake ni kuwa hadi Machi 2003 mashirika 266 yalibinafsishwa
na 47 yaliwekwa chini ya ufilisi. Kati ya mashirika
yaliyobinafsishwa na 47 yaliwekwa chini ya ufilisi.
Kati ya mashirika yaliyobinafisishwa 134 yamenunuliwa
asilimia 100 kwa Watanzania kwa thamani ya shs. 63
bilioni. Zaidi ya mali 265 (non core assets) yamenunuliwa
na Watanzania.
Mashirika 16 yenye thamani ya shs. 4 bilioni yamenunuliwa
na “Wawekezaji kutoka nje wakati mashirika 116
yamenunuliwa kwa njia ya ubia kati ya Serikali, Wawekezaji
kutoka nje na Watanzania kwa thamani ya shs. 400 bilioni.
Aidha mashirika mengine 16 yamebinafsishwa chini ya
utaratibu wa MEBO kwa mfano NEDCO, KIUTA, Moshi Handtools,
Tanzania Publishing House n.k. wakati mashirika 116
yamenunuliwa kwa njia ya ubia kati ya Serikali, Wawekezaji
kutoka nje na Watanzania kwa thamani ya shs. 400 bilioni.
Aidha mashirika mengine 16 yamebinafsishwa chini ya
utaratibu wa MEBO kwa mfano NEDCO, KIUTA, Moshi Handtools,
Tanzania Publishing House n.k.
Vile vile Serikali kupitia Soko la Hisa la Dar es
Salaam mashirika kama vile DAHACO, Viwanda vya Saruji,
Kiwanda cha Biashara, Kiwanda cha Bia n.k. yameuza
hisa kwa Watanzania zaidi ya 80,000. Serikali vile
vile inaendelea na ubinafsishaji wa mashirika ya miundo
mbinu kama vile DAWASA, ATC, TANESCO, THA, NIC, TRC
na NMB.
Takwimu hizi zinaonyesha wazi kuwa mashirika/viwanda
vingi vimenunuliwa na Watanzania tukiacha upotoshaji
mkubwa unaoendelea hivi sasa kuwa Sera ya CCM ya Ubinafsishaji
ni uuzaji wa nchi. Huu ni uzushi wenye nia ya kuipaka
matope Sera hii nzuri ya CCM.
Mikakati ifuatayo inatumika na Serikali kuhakikisha
Watanzania wanashirikishwa katika kununua mashirika.
.Utaratibu
wa Wafanyakazi Wenyewe Kununua Mashirika (MEBO).
.Kuwauzia Watanzania kwa misingi ya thamani ya Vitabu
badala ya thamani ya Soko. Mashirika yote ya Usafirishaji
yameuzwa kwa utaratibu huu.
· Kufuta kodi kwa KAURU (shs. 251.8m), Mbeya
RETCO 9215.8m) na kodi za shs. 47.9m.
|
|
| |
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
Mjumbe
wa Kamati Kuu ya CCM ambaye pia ni Waziri wa Nchi katika
Ofisi ya Rais anayeshughulikia Mipango na Ubinafsishaji
Dk. Abdalah Kigoda akielezwa na mfanyakazi wa Kampuni
ya Sigara (TCC) jinsi walivyofurahishwa na ubinafsishaji. |
|
|
|
|
|
|
·
Ulipaji wa mafao ya kisheria ya wanaopunguzwa kazini.
Hadi sasa Serikali haina deni la mafao ya kisheria.
· Muda wa kulipia Mashirika hayo kwa Watanzania
umeongezwa na kuwa mrefu km. Shamba la Chai la Dabaga
n.k.
· Wawekezaji wa Tanzania wamekuwa wakipewa viwanda
pale wanapotoka.
Makundi Maalum yamepewa upendeleo wa makusudi hasa yale
ya ushirika na umoja kwa mfano Kiwanda cha Chai cha
Mponde kinachonunua majani ya Chai kutoka Vijiji vya
Lushoto na Korogwe, Kiwanda cha Chai cha Rungwe, Viwanda
vya Kahawa vya Mbozi, Mbinga, Kilimanjaro n.k.
· Ununuzi wa Hisa kupitia Soko la Hisa la Dar
es Salaam.
Utekelezaji wa Sera yoyote lazima uwe na mafanikio na
matatizo. Kimsingi Sera ya Ubinafsishaji katika miaka
10 iliyopita imeonyesha mafanikio makubwa sana.
Mafanikio yamepatikana katika ukusanyaji wa kodi kwa
Serikali kwani Mashirika na Viwanda sasa vinalipa kodi
Serikalini badala ya kungojea ruzuku itokanayo na fedha
za walipa kodi. Serikalini badala ya kungojea ruzuku
itokanayo na fedha za walipa kodi.
Uzalishaji Viwandani umeongezeka maradufu na ufanisi
na ubora wa bidhaa umeongezeka. |
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
Mtambo
wa kisasa wa kupikia pombe wa TBL unaoendeshwa kwa kompyuta.
Haya ni moja ya mafanikio ya teknolojia yaliyoletwa na
ubinafsishaji. |
|
|
|
|
·
Ukuzaji wa Ajira umeongezeka baada ya ubinafsishaji.
Ikumbukwe kuwa kabla ya zoezi hili mashirika 70 yalikwishafilisiwa.
Viwanda vya Saruji vimeongeza ajira, viwanda vya Sukari
vya Mtibwa. Kilombero na Kagera vimeongeza ajira; Viwanda
vya Tumbaku na Sigara nahivi sasa takriban Watanzania
500,000 wamepata ajira zilizotokana na matunda ya ubinafsishaji
kwa mfano – sekta za biashara, ujenzi, usafirishaji
n.k.
· Ubora wa bidhaa tunazozalisha umeongezeka.
· Teknolojia mpya imeongezeka viwandani.
· Ujuzi wa biashara umberoka pamoja na kuongezeka
kwa mishahara.
· Ununuzi wa hisa unazidi kuendelea.
Sekta ya Viwanda imeongeza mchango wake katika ukuaji
wa Pato la Taifa. Serikali ya CCM inaweza kwa kiwango
kikubwa kuhudumia na kuboresha sekta ya Huduma za Jamii,
Huduma za miundo mbinu ya kiuchumi, Serikali ya CCM
inapata viwango vikubwa vya kodi na gawio hivyo kukuza
mapato ya Serikali.
|
|
|
|
|
|