Ilani ya CCM Habari Mpya Historia ya TANU na ASP Kutoka Magazetini Hotuba

 

 

 

 

 

 

 

 

 

JARIDA LA MKEREKETWA

Tuna kila sababu ya kujivunia Mkapa na Karume kwani
 
  • Mkapa ana uwezo mkubwa wa uongozi
  • Karume ameirejeshea heshima Zanzibar
   
  Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama Cha Mapinduzi iliyokutana mwezi Septemba ilijadili kwa kina miongoni mwa mengine, hali ya kisiasa nchini.
Kwa jumla, Halmashauri Kuu ya Taifa imeridhika na hali ya amani na utulivu wa nchi ukiondoa matukio ya hapa na pale ya uhalifu.
 
   
Mwenyekiti mpya wa SADC, Rais Mkapa akivishwa beji baada ya kukabidhiwa
madaraka hayo na Rais Dos Santos wa Angola.
 
Halmashauri Kuu ya Taifa imempongeza kwa dhati Mheshimiwa Benjamin William Mkapa, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi kwa kuchaguliwa kuwa Mwenyekiti wa SADC kwa mwaka 2003/2004. Imempongeza pia kwa kufanikisha kwa kiwango kikubwa Mkutano wa Wakuu wa Nchi za SADC uliofanyika Mjini Dar es Salaam tarehe 26-27 Agosti, 2003.
Halmashauri Kuu ya Taifa imeendelea kumpongeza Rais Mkapa kwa uwezo wake mkubwa wa uongozi ambao umeijengea heshima kubwa Tanzania na Chama Cha Mapinduzi ndani na nje ya nchi yetu.
Rais Mkapa amejibainisha waziwazi kwa sasa kuwa tegemeo kubwa la kuzisemea nchi za Kiafrika na nyingine za Dunia ya Tatu katika medani za Kimataifa, hasa katika wadhifa wake wa heshima kubwa wa Mwenyekiti Mwenza wa Tume ya Utandawazi Duniani.
Lakini pia, kwa haiba yake ya uongozi, Rais Mkapa amejitokeza kuheshimika sana hata mbele ya macho ya nchi zilizoendelea. Kutokana na kuheshimika huko, ameweza kujenga imani kubwa ya nchi hizo siyo kwake yeye binafsi tu bali hata kwa nchi yetu. Imani hiyo inajidhihirisha katika mambo makuu yafuatayo miongoni mwa mengi mengine:-
(1) Tanzania ni miongoni mwa nchi chache sana zilizofanikiwa kuingia katika mpango wa kuzifuatia madeni nchi maskini duniani (HIPC).
(2) Tanzania hivi sasa inapokea misaada mingi na mikubwa ya wahisani kuliko wakati mwingine wowote; na tena misaada hiyo inaingizwa moja kwa moja katika bajeti ya Serikali ukiwa ni ushahidi wa kutosha wa jinsi wahisani wanavyotuamini kuwa tunazitumia vizuri fedha zao.
(3) Hivi sasa Tanzania ni miongoni mwa nchi zinazoongoza katika kuvutia vitega uchumi vya nje katika Bara la Afrika.
Halmashauri Kuu ya Taifa ilijadili pia hotuba ya ufunguzi wa Mwenyekiti ambayo ilibainisha mafanikio makubwa ya jumla katika maeneo ya siasa, uchumi na huduma za jamii wakati tukiwa tumemaliza nusu ya kipindi cha utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2000-2005.
Katika hotuba hiyo ambayo imechapishwa katika ukurasa wa pili wa jarida hili , Mwenyekiti alitoa changamoto kwa viongozi na wanachama wa CCM kuwa mstari wa mbele kutetea rekodi nzuri ya Chama na Serikali zake badala ya kuwaachia wapinzani wanaojaribu kupuuza au kukebehi rekodi hiyo, usahihi wa Sera za CCM na umakini wa utekelezaji wake.
Halmashauri Kuu ya Taifa imempongeza pia Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Amani Abeid Karume kwa kazi nzuri anayoifanya Zanzibar ambayo matunda yake yanaonekana. Uchumi wa Zanzibar hivi sasa umekua kutoka aslimia 3.2 mwaka 2000 hadi asilimia 5.6 mwaka 2002.
Mfumko wa bei umeshuka kutoka aslimia 6.2 mwaka 2000 hadi kufikia aslimia 5.2 mwaka 2002. Miundombinu hasa ya barabara na mawasiliano pamoja na shule imekuwa bora zaidi hivi sasa kote Unguja na Pemba na mabadiliko yanaonekana kwa kila mtu.
Tangu Serikali ilipozundua mpango wa kupunguza umaskini mwezi Mei 2002 imekuwa ikiweka mkazo mkubwa katika uimarishaji wa sekta ya elimu, mawasiliano, afya na maji.
Aidha, Rais Karume ameirejeshea Zanzibar heshima mbele ya Jumuiya ya Kimataifa kama inavyodhirishwa na kurejeshwa kwa misaada ya wahisani.
Kutokana na mafanikio hayo makubwa, Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM imezipongeza Serikali zote mbili, yaani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na ile ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa kutekeleza vizuri Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2000 na kuwataka Watanzania wajivunie mafanikio hayo.
Pia Serikali zote mbili zimepongezwa kwa juhudi zake za kuondoa kero mbali mbali za wananchi.
               
Madarasa ya Skuli ya Chwale, Wete, Pemba yaliyojengwa chini ya Mfumo wa Maendeleo ya Jamii (TASAF)