Ilani ya CCM Habari Mpya Historia ya TANU na ASP Kutoka Magazetini Hotuba

 

 

 

 

 

 

 

 

 

JARIDA LA MKEREKETWA

TASAF
  Chachu ya maendeleo na inayoondoa umaskini nchini    
 
Chama cha Mapinduzi (CCM) kimewapongeza waanchi na Serikali kwa juhudi za waziwazi zinazoonekana za kuondoa umaskini nchini.
Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) ulianzishwa na Serikali mwaka 2000 kutokana na mkopo wa Dola za Kimarekani 60 milioni toka Benki ya Dunia. Serikali ya Jamhuri ya Muungano ya Tanzania nayo imetoa Dola za Kimarekani 3.2 milioni kuchangia juhudi za wananchi katika kuondoa umaskini.
TASAF imejitanua katika wilaya 40 za Tanzania Bara na wilaya zote za Unguja na Pemba ambapo imeshughulikia jumla ya miradi mingi kote nchini.
Inatazamiwa kwamba katika miaka miwili ijayo, shughuli za TASAF zitaenea katika wilaya zote za Tanzania Bara.
Miradi iliyokamilishwa hadi sasa ni pamoja na madarasa ya shule za msingi 1,888; nyumba za walimu 481; vyoo vya matundu 277; zahanati 272; nyumba za waganga 330; visima 244; mabwawa 6; barabara za vijijini kilomita 1,354; bustani za miche na mingineyo kadhaa.
Kwa mujibu wa taarifa ya Serikali liyowasilishwa hivi karibuni kwenye kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, TASAF hadi sasa imetoa ajira kwa wananchi 69,699 ambao kati yao hawa wanawake ni 32,800.
Halmashauri Kuu ya Taifa ambayo ilikutana chini ya Mwenyekiti wa CCM, Rais Benjamini Mkapa imeridhika na mafanikio haya makubwa yaliyokwisha patikana na imewataka wananchi kushiriki katika ujenzi wa miradi hiyo ili isaidie kuwaondolea au kuwapunguzia tatizo la umaskini.
 
         
     
       
Ujenzi wa Zahanati wa Zingwe Zingwe, Unguja ni moja ya miradi ya TASAF.
   
           
       
            Wananchi wakishiriki kutoa maoni yao juu ya ujenzi wa mira iliyo chini ya TASAF.          
Tovuti (Website) ya CCM hii hapa
 
Tovuti (Website) ya CCM ilizinduliwa rasmi tarehe 5 Februari, 2002 na Mwenyekiti wa CCM, Mheshimiwa Rais Benjamin Mkapa wakati wa sherehe za Jubilel ya miaka 25 ya Chama Cha Mapinduzi zilizofanyia Zanzibar.
Hata hivyo, muda mfupi baada ya uzinduzi huo, Tovuti ilikabiliwa na matatizo kadhaa yaliyosababisha isiwepo kwenye mtandao kwa kipindi kirefu.
Kutokana na kasoro hiyo, hatua za kuifufua Tovuti iyo zilichukuliwa hivi karibuni. Hivi sasa Tovuti ya CCM ambayo ni www.ccmtz.org au www.ccmtz.com imeundwa upya na ipo hewani. Taarifa nyingi za Chama Cha Mapinduzi zinaendelea kujazwa katika Tovuti hiyo.
Baadhi ya mambo muhimu yaliyowekwa ili kuitangaza CCM ni pamoja na Hotuba mbali mbali; Mwelekeo wa Sera za CCM katika miaka ya 2000 hadi 2010; Katiba ya CCM; ILANI ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2000; Historia ya TANU na ASP na mambo megine kadhaa.

Mtandao wa Internet:
Kazi ya uundaji wa Tovuti imekwenda sambamba na uunganishaji wa mtandao wa kisasa wa INTERNET katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba Dar es Salaam. Kazi hiyo imekwishakamilika na hivi sasa kompyuta ya Ofisi ya Katibu Mkuu wa CCM imekwisha unganiswa na INTERNET.
Ili kila kompyuta katika jengo iweze kupata INTERNET, kazi ya kuweka mtandao wa ndani (Local Area Network- LAN) imekwishaanza.