Ilani ya CCM Habari Mpya Historia ya TANU na ASP Kutoka Magazetini Hotuba

 

 

 

 

 

 

 

 

 

JARIDA LA MKEREKETWA

Baada ya hali ya amani na utulivu kurejea Zanzibar
 
  • Karume asambaza maendeleo Pemba na Unguja
  • Sera za ‘Jino kwa Jino’ zimefifia
  • Na heshima ya SMZ inang’ara
   
 

Matokeo ya Uchaguzi wa Rais wa Zanzibar yalitangazwa tarehe 7 Novemba, 2000. Kufuatia matokeo hayo, mgombea wa Urais kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mheshimiwa Amani Abeid Karume alishinda kwa kishindo kwa kupata kura 248,095 (65%), ambapo mgombea wa nafasi hiyo hiyo kupitia CUF, Seif Shariff Hamad alipata kura 122,000 (33%).Hata hivyo, kumalizika kwa Uchaguzi Mkuu wa 2000 kulizaa hali ya mivutano mikubwa ya kisiasa, vurugu baadhi ya nyakati na hujuma dhidi ya mali za Serikali na wananchi.
Mivutano hiyo ilipelekea fujo na maandamano haramu ya tarehe 26 na 27 Januari, 2001 huko Pemba, fujo zilizosababisha kupotea kwa maisha ya watu 23, wengine kujeruhiwa na baadhi ya wananchi kukimbilia Shimoni-Kenya. Tukio hili liliisikitisha sana Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar pamoja na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Kwa kutekeleza Ilani ya Uchaguzi ya CCM kuhusu ujenzi wa mshikamano na umoja wa Kitaifa, awamu ya pili ya mazungumzo ya kujenga maelewano ya kisiasa baina ya vyama vikuu vya siasa vya CCM na CUF yalifanyika. Baada ya miezi 9 ya majadiliano na mashauriano Muafaka ulifikiwa kati ya CCM na CUF na ulitiwa saini tarehe 10 Oktoba, 2001 Ikulu Zanzibar.

 
       
       
   
Katibu Mkuu wa CCM, Ndugu Philip Mangula akipeana mkono na Katibu Mkuu wa CUF, Seif Shariff Hamad baada ya kutiwa saini Muafaka baina ya vyama vyao viwili tarehe 10/10/2001 Ikulu Zanzibar
     
 

Hatua kadhaa zilichukuliwa na Serikali zote mbili za Muungano na ya Zanzibar ili kuhakikisha kwamba vurugu za aina hiyo zilizotokea Pemba hazirudiwi tena.
Faida zilizokwishapatikana kutokana na kutekelezwa kwa Muafaka ni pamoja na:-
.Hali ya maelewano katika jamii imerejea na umoja na mshikamano wa Kitaifa unaendelea kujengeka tena.
· Sera za chuki na uhasama (jino kwa jino) za CUF zilizokuwa zikiwavutia wafuasi wengi wa chama hicho zimefifia kwa kiasi kikubwa.
· Hadhi na heshima ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na Mheshimiwa Rais Amani Abeid Karume imerejea na inaendelea kuimarika siku hadi siku.
· Kupitishwa kwa marekebisho ya sheria za Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC) kumewezesha kufanyika kwa amani na utulivu chaguzi ndogo za majimbo 17 Kisiwani Pemba tarehe 18 Mei, 2003. Matokeo yake ni kwamba CUF ilipata viti 11 na CCM ilipata viti 6.
Kutokana na mafanikio hayo, mazingira mazuri yamejengeka Zanzibar ambayo yameiwezesha Serikali ya CCM ya Zanzibar kuendelea kutekeleza Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2000 kwa ufanisi mkubwa na kuharakisha maendeleo.

Katika kipindi cha mwaka 2000-2003 uchumi wa Zanzibar umekuwa kutoka asilimia 3.2 mwaka 2000 hadi asilimia 5.6 mwaka 2002. Mfumko wa bei umeshuka kutoka asilimia 6.2 mwaka 2000 hadi asilimia 5.2 mwaka 2002.
Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) ulioanzishwa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa mkopo wa Benki ya Dunia umesaidia kupunguza matatizo ya wananchi wa Zanzibar hasa vijijini. Mfuko huu umetenga shilingi bilioni 3 kwa ajili ya miradi ya maendeleo katika sekta za elimu, afya na huduma za maji.
Mpaka sasa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii umeshatekeleza miradi 65, Unguja 37 na Pemba 28. Miradi hii ina thamani ya shilingi bilioni 1,737,218,255. Katika fedha hizo, wananchi wamechangia shilingi milioni 239,505,855 kama nguvu kazi na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii umetoa shilingi bilioni 1,497,712,400. TASAF pia inaifadhili miradi miwili ya kilimo cha umwagiliaji maji katika vijiji vya Mtwango na Ndijani, Unguja. Halikadhalika TASAF inayafanyia utafiti maeneo ya mto Mwanakombo, Upenja, Chaani na Kibokwa kwa Unguja na Weni pamoja na Gae la Mtungi kwa Pemba ili kuangalia uwezekano wa kuyatumia maeneo hayo kwa ajili ya kilimo cha kumwagilia maji.

   
       
       
        “Sasa mambo safi”, Naibu Katibu Mkuu CCM (Zanzibar), Ndg. Saleh R. Ferou        
       
       
          Wake kwa waume wakishiriki katika mradi wa TASAF wa ujenzi wa kusambaza maji wa Kiuyu Mnungwini (Pemba)          
   
Tangu Serikali ilipozindua mpango wa kupunguza umaskini mwezi Mei, 2002 imekuwa ikiweka mkazo mkubwa katika uimarishaji wa sekta ya elimu, mawasiliano, afya na maji. Serikali imeshatekeleza mambo yafuatayo:-
· Imeandikisha asilimia 98 ya watoto waliofikia umri wa kwenda skuli.
·. Mpango Mkuu wa Elimu umefanyiwa mapitio.
· Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar kimeshatimiza mwaka wa pili tangu kilipofunguliwa rasmi mwaka jana. Chuo hiki kina wanafunzi 54 wanaochukua shahada ya ualimu na sanaa.
· Imejenga barabara zenye urefu wa kilomita 60 kwa kutumia fedha za Serikali.
· Zabuni ya utanuzi wa uwanja wa ndege wa Zanzibar tayari zimeshatangazwa.
· Inaimarisha huduma za maji safi katika maeneo mbalimbali ya Unguja na Pemba.
· Serikali ya Japani iko katika hatua za mwisho inashughulikia ombi la mradi wa maji katika Manispaa ya Zanzibar wenye thamani ya shilingi bilioni 11.
· Serikali imeyatengeneza majenereta ya umeme Pemba kwa thamani ya shilingi 497,000,000/=.
· Katika sekta ya kilimo, Serikali inakiimarisha Chuo cha Kizimbani kwa ajili ya shughuli za utafiti wa kilimo na mifugo. Serikali pia inayafanyia utafiti mabonde 57 ya Unguja na Pemba yenye ukubwa wa hekta 17,042.
Kwa kuwa Ilani ya Uchaguzi ya CCM inatilia mkazo suala la ustawi wa jamii wa wananchi wake katika utekelezaji wa ahadi za Serikali, suala la mafao ya wastaafu lilishguhulikiwa mara moja baada ya Rais Amani Abeid Karume kuchukuwa madaraka mwaka 2000.
Kuanzia Novemba 2000 hadi Juni 2003, jumla ya wafanyakazi 3,741 wameshalipwa viinua mgongo yenye thamani ya shilingi 2,914 milioni. Kadhalika wafanyakazi 1662 wameshalipwa malimbikizo ya pensheni zao.
Wakati Rais Karume anaingia madarakani, Serikali ilikuwa inadaiwa mafao ya viinua mgongo vya wastaafu wapatao 4967 yenye thamani ya shilingi 5,325 milioni.
Wastaafu 2293 pia walikuwa wanaidai Serikali shilingi 1,092.2 milioni kama malimbikizo ya pensheni.
Malipo hayo yamefanywa kwa wadai wote wa Unguja na Pemba.
Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar katika kutekeleza Ilani ya Uchaguzi ya CCM pia imeweka mkazo katika ujenzi wa barabara mijini na vijijini.
Katika kipindi cha miaka miwili na nusu ya utekelezaji wa Ilani, Serikali imeweza kujenga barabara Unguja na Pemba ili kuimarisha miundo mbinu ya uchumi.

UNGUJA barabara zilizojengwa ni:-

· Kitogani-Paje Kilomita 11-2
· Barabara ya Bambi – kilomita 6.0
· Jang’ombe-Mpendae – kilomita 0.6
· Kaebona-Kaepwani – kilomita 4.5
· Makunduchi-Mtende – Kilomita 5.5

PEMBA barabara zilizojengwa ni:-

· Chake-Wesha – kilomita 7.0
· Chake-Vitongoji – kilomita 7.0
· Kilindi-Micheweni – kilomita 6.0
Jumla ya shilingi 2,282 bilioni zimetumika kugharamia ujenzi wa barabara hizi. Kati ya hizo, shilingi 1.319 bilioni zimetolewa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na shilingi 963 milioni ni msaada wa lami kutoka Serikali ya Libya.
Barabara zinazoendelea kujengwa hivi sasa kwa nguvu za Serikali ni kwa upande wa Unguja barabara ya Mahonda-Donge yenye urefu wa kilomita 14; na Pemba ni barabara ya Mtu Haliwa-Chokocho ya kilomita 12.
Barabara nyingine zinazojengwa kwa msaada wa wafadhili ni:-
· Kidimni-Kitope – kilomita 29.6
· Mkoani-Chake – kilomita 30.5
Mafanikio yote haya yameweza kupatikana katika kipindi cha miaka miwili na nusu tu cha uongozi wa Rais Amani Abeid Karume.

 
   
 
    Rais Karume akikagua ujenzi wa barabara mpya ya Kilindini - Micheweni huko Pemba  
   
   
          Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM na Waziri Kiongozi wa SMZ akizindua mradi wa maendeleo Zanzibar.