| JARIDA
LA MKEREKETWA
|
CCM
yatoa kadi mpya kwa wanachama wake |
|
|
|
|
- Mtindo
wa ‘papo kwa papo’ sasa basi
|
|
|
|
|
Halmashauri
Kuu ya Taifa ya CCM iliamua mwaka 2002 kwamba ufanyike
utaratibu wa uchapishaji upya wa Kadi za CCM kwa ajili
ya wanachama wake wote (wazamani na wapya) nchini.
Madhumuni ya uamuzi huo ni kuongeza ubora na udhibiti
wa kadi za CCM ili zisiweze kuingia katika mikono ya
watu wasiohusika.
Katibu Mipango wa CCM Taifa, Ndugu Jackson Msome ameliambia
jarida la Mkereketwa kwamba Sekretarieti ya Halmahauri
Kuu ya Taifa ya CCM (NEC) imeanza kutekeleza zoezi hilo
na hadi sasa jumla ya kadi mpya 470,000 zimekwisha chapishwa
na baadhi yake zimefikishwa mikoani.
“Lengo letu ni kuchapisha kadi mpya zaidi ya milioni
tatu (3,000,00) ili wanachama wetu wote wa zamani na
wale watakaojiunga na CCM waweze kupewa kadi hizo ambazo
zimetengenezwa kitaalamu na zina alama maalum za siri”,
aisema.
Katibu Mipango amewakumbusha Makatibu wa CCM wa Mikoa
kuzingatia utaratibu uliowekwa wa usambazaji wa kadi
hizo ili kudhibiti uchukuaji, ugawaji na mawasilisho
ya fedha.
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
Katibu
Mipango CCM Taifa, Ndg. Jackson Msome |
|
|
|
|
|
Alieleza
kwamba ili kufanikisha vizuri zoezi hili, Kamati Kuu
ya CCM imeagiza mambo yafuatayo yazingatiwe:-
Kadi mpya zichukuliwe kutoka Ofisi za CCM za Dodoma,
Dar es Salaam na Zanzibar na Makatibu wa CCM wa Mikoa
wenyewe. Mtu mwingine hatapatiwa kadi katika ofisi hizo
mpaka awe na kibali cha maandishi cha Katibu wa CCM
wa Mkoa anakotoka.
Makatibu wa CCM wa Mikoa wahakikishe kwamba wanatuma
mawasilisho ya fedha zinazohusika Makao Makuu ya CCM
bila kuchelewa. Sekretarieti ya NEC itakuwa karibu sana
na Mikoa ili kuratibu suala la uchukuaji wa kadi na
mawasilisho ya fedha kila mwezi.
Matawi ya CCM yaelekezwe kurejesha utaratibu wa Katiba
ya CCM ya kuwapokea wanachama wapya badala ya mtindo
wa “papo kwa papo”.
Ndugu Msome amewakumbusha Makatibu wa CCM wa Mikoa kutekeleza
agizo la Chama la kuanzisha “Mfuko wa Vifaa”
katika kila ngazi ya Chama ili itumike kununulia kadi
za CCM na kuendeshea shughuli nyingine za Chama.
Watendaji wa CCM wa ngazi zote wanatakiwa kuliendesha
zoezi hili muhimu kwa uangalifu na uadilifu wa hali
ya juu bila kuleta usumbufu kwa wanachama wa CCM. |
|
|
|
Mangula
aelezea utekelezaji wa ‘Muafaka’ ingereza |
|
|
|
- Aiwakilisha
CCM kwenye Mkutano wa Labour Party
|
|
|
|
Katibu
Mkuu wa CCM, Ndugu Philip Mangula hivi karibuni alialikwa
na Katibu Mkuu wa Chama cha Laour Party cha Uingereza,
David Triensman kuhudhuria Mkuano Mkuu wa chama chao
uliofanyika kwenye kituo cha kitaifa cha Bournemouth
kuanzia Septemba hadi Oktoba 2, mwaka huu.
Aidha, Katibu Mkuu wa CCM pia alialikwa na Serikali
ya Uingereza kutembelea sehemu mbalimbali za nchi hiyo
kwa muda wa wiki mbili.
Katika ziara hiyo, kiongozi huyo wa CCM alitumia fursa
hiyo kuwaeleza wenyeji wake kuhusu utekelezaji wa Muafaka
wa CCM na CUF, hali ya kisiasa nchini na maandalizi
ya CCM ya Uchaguzi Mkuu wa Serikali wa mwaka 2005. |
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
Katibu
Mkuu wa CCM, Ndugu Mangula akimsikiliza Mkuu wa Idhaa
ya Kiswahili BBC, Ndugu Dunstan Tido Mhando alipotembelea
Studio za BBC London. Kushoto
ni Jumbe Omar Jumbe wa BBC. |
|
|
|
|
|
Akiwa
Uingereza, Ndugu Mangula alikutana na watu kadhaa
mashuhuri wakiwemo Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Madola,
Bwana Donald Mac Kinnon; Mkurugenzi Mkuu wa Westminster
Foundation for Democracy, Bwana David French na Mkrugenzi
wa Jamuiya ya Afrika (Royal African Soceity), Bwana
Richard Dowden
Katibu Mkuu wa CCM alifanya mazungumzo na Watanzania
wanaoishi huko pamoja na wafanyakazi wa Ubalozi wetu
ambao aliwaeleza jinsi hali ya kisiasa ilivyo nchini
Ta-nzania na mae-ndeleo ya kuuje-nga uchumi wa Tanzania
pamoja na utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM
ya mwaka 2000.
Aidha, alifanya mahojiano na Shirika la Habari la
BBC kwa lugha zote mbili za Kiswahili na Kiingereza
ambapo alizugumzia mambo mengi kuhusu hali ya kisiasa
nchini, Itikadi ya CCM, Mwelekeo wa Sera za CCM na
mafanikio yaliyopatikana na Serikali zote mbili za
CCM za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali
ya Mapinduzi ya Zanzibar katika kutekeleza Ilani ya
Uchaguzi ya CCM.
|
|