Ilani ya CCM Habari Mpya Historia ya TANU na ASP Kutoka Magazetini Hotuba

 

 

 

 

 

 

 

 

 

"Mimi naamini kabisa kwamba tutasaidia nchi yetu,
kuimarisha Umoja wake na Mapinduzi yake
na hivyo kuwa na uwezo mkubwa zaidi wa kusaidia
kuleta Umoja na Mapinduzi ya Afrika ikiwa sasa bila kusita tena tuaviunganisha vyama vyetu na kuwa Chama kimoja cha Mapinduzi."

  Mwalimu Julius K. Nyerere na wanachama na viongizi wa TANU na ASP walio wengi walikuwa na matarijo makubwa kwa Chama kimoja cha Mapinduzi.

Miongoni mwa matarajio hayo ni kukamilisha Muungano wa Tanzania; kuleta maendeleo ya pamoja na haraka kwa nchi yetu; kumkomboa Mtanzaina na Mwafrika kifikra, kisiasa, kiuchumi na kijamii; na kusaidia kuharakisha kufikia lengo la kujenga nchi inayofuata siasa ya Ujamaa na Kujitegemea.

Aidha, Chama kimoja cha Mapinduzi kilitarajiwa kushiriki kwa ukamilifu katika kutokomeza ukoloni katika Bara la Afrika na kwingineko duniani na kuendeleza siasa ya kutofungamana na upande wowote hasa kwa kuzingatia kwamba katika miaka ya 1970 na 1980 dunia ilikuwa bado imegawanyika kisiasa, kiuchumi na kiulinzi katika kambai mbili zenye uhasama.

Kambi hizo ni ya Magharibi ikiongozwa na Marekani na ile ya Mashariki ikiongozwa na Umoja wa Kisovieti. Waasisi wa TANU na ASP walitambua kwamba kuwepo kwa vyama viwili katika mazingira ya siasa ya chama kimoja kulipunguza upeo, nguvu na umoja wao katika kuendeleza mapambano ya kujenga Ujamaa nchini na kushiriki kwa pamoja na kwa ukamilifu katika harakati za mapinduzi ya Tanzania, Afrika na dunia kwa jumla.

TANU na ASP toka mwanzo vilikuwa ni vyama vya ukombozi vilivyojengeka kwenye msingi wa demokrasia. Kwa mfano, pendekezo la Mwalimu Julius K. Nyerere la kuunganisha vyama lilipitishwa na TANU na ASP kwa njia ya kidemokrasia.

TANU na ASP walipeleka suala zima la kuunganisha vyama kwa wanachama wenyewe kwani ndio wenye vyama.

Wanachama hao katika matawi yao walitakiwa wajadili nakutoa maoni yao kuhusu suala la kuunganisha TANU na ASP ili kiundwa Chama kimoja cha Mapinduzi.

Kazi hiyo ilifanyika kwa ufanisi kama ilivyoagizwa na Halmashauri Kuu za Taifa za TANU na ASP. Licha ya wanachama kujadili na kutoa maoni yao, kwa Zanzibar viongozi wa ASP walipwewa nafasi ya kujadili na kutoa maoni yao katika vikao vyote vya Chama.

Wanachama walijadili na kutoa maoni yao kwanza ndipo wakafuata viongozi katika Halmashauri za vikao mbalmblai vya ASP. Angalia majedwali na. 1 na 2 ambayo yanaonyesha matokeo ya maoni ya wanachama wa TANU na ASP kuhusu kuunganishwa vyama. Matokeo ya Maoni ya Wnachama wa TANU kuhusu kuunganishwa TANU na ASP

Matawi
Idadi
Asilimia
Idadi ya Matawi ya TANU 6,639 100
yaliyokutana 6,427 96.81
yaliyokutana 212 3.19
yaliyokubali 6,424 99.95
yaliyokataa 3 0.05
Idadi ya matawi madogo ya TANU 38 100.
Matawi Madogo yaliyokutana 38 100
Matawi Madogo yaliyokubali 38 100
Matawi Madogo yaliyokataa Hakuna 0.00

Chanzo: Chuo cha CCM Kivukoni (1981) Historia ya Chama cha TANU 1954 hadi 1977, (Dar es Salaam : Mpiga Chapa wa Serikali)