UCHUKUAJI
WA FOMU ZA UBUNGE, UWAKILISHI WA MAJIMBO NA WA
VITI MAALUM (WANAWAKE) KWA TIKETI YA CCM
Chama Cha Mapinduzi kimeweka utaratibu wa ndani ya Chama wa namna ya kuwapata wana-CCM watakaogombea nafasi za Ubunge na Uwakilishi wa Majimbo na wa Viti Maalum Wanawake katika Uchaguzi Mkuu utakaofanyika Oktoba 30, 2005.
Kwa
mujibu wa utaratibu uliowekwa, siku ya Jumatatu tarehe 1/08/2005 ndiyo mwanzo
wa kuchukua fomu kwa wanachama wa CCM wote wanaotaka kugombea Ubunge na
Uwakilishi wa aina zote kwa tiketi ya CCM.
Mwisho wa kurudisha fomu hizo ni tarehe 3/08/2005 kabla ya saa 10 jioni.
Utaratibu mzima utakaotumika kuwapata watakaogombea nafasi hizo ni kama ifuatavyo:-
|
MWAKA |
NAFASI YA UONGOZI |
MWANZO WA KUCHUKUA FOMU |
MWISHO WA KURUDISHA FOMU |
|
2005 |
Ubunge |
1/08/2005 |
3/08/2005 kabla ya saa 10.00 jioni |
|
Uwakilishi |
1/08/2005 |
3/08/2005 kabla ya saa 10 .00 jioni |
|
MWAKA 2005 |
TUKIO |
|
4-6 Agosti 2005 |
Kura za maoni katika Majimbo |
|
7 Agosti 2005 |
Mikutano Mikuu ya UWT ya Mikoa kupendekeza wagombea 5 kwa kila mkoa |
|
8 Agosti |
Kamati za Siasa za Wilaya |
|
9 Agosti 2005 |
Kamati za Siasa za Mikoa zitajadili wagombea Ubunge, Uwakilishi na Viti Maalumu-Wanawake. |
|
10 Agosti 2005 |
Kamati Maalum ya Halmashauri Kuu ya Taifa kuwajadili wagombea Ubunge na Uwakilishi wa aina zote. |
|
11 Agosti 2005 |
Baraza Kuu la UWT kuandaa orodha ya wagombea wote nchini |
|
12-13 Agosti 2005 |
Sekretarieti ya Halmashauri Kuu ya Taifa. |
|
15 Agosti 2005 |
Kamati Kuu Maalumu |
|
16 Agosti 2005 |
Halmashauri Kuu ya Taifa kuteua wagombea Ubunge na Uwakilishi wa jimbo na Viti Maalumu-Wanawake |
|
Mapitio na uthibitishaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2005 |
|
|
17 Agosti 2005 |
Kutangaza Uteuzi |
|
20 Agosti 2005 |
Tume ya Taifa ya Uchaguzi kuteua wagombea |
|
21 Agosti 2005 |
Kuanza kwa kampeni za Uchaguzi Mkuu kwa Tanzania Bara |
|
03 Septemba 2005 |
Tume ya Uchaguzi Zanzibar kuteua wagombea |
|
05 Septemba 2005 |
Kuanza kampeni kwa upande wa Zanzibar |
|
29 Oktoba 2005 |
Kumalizika kwa Kampeni za Uchaguzi Mkuu nchi nzima |
|
30 Oktoba 2005 |
Siku ya Uchaguzi (Kupiga Kura) |