Wavumilia Mvua Kumsikiliza Mgombea
 
Na Abihudi Saideya, Geita, 11/09/2005 = Dk. SHEIN
 
Mamia ya wakazi wa Kata ya Nyarugusu, Wilaya ya Geita
Mkoani Mwanza jana (10/10/2005) walistahimili mvua
kusikiliza hotuba ya Mgombea Mwenza wa Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya CCM, Dk. Ali
Mohamed Shein.
 
Mvua hiyo ilianza kunyesha mara baada ya msafara wa
kampeni za uchaguzi wa Dk. Shein kuwasili Nyarugusu
ukitokea kata ya Kharumwa ambako pia alihutubia
mkutano wa hadhara.
 
Akihutubia mkutano huo Dk. Shein aliwashukru wakazi wa
Kata hiyo kwa mapokezi ya kishindo bila kujali mvua
ilikuwa ikinyesha.
 
"Mkutano huu Mungu ameutia barakha,mvua hii ni dalili
ya ushindi wa Chama Cha Mapinduzi," alisema na
kusisitisa kuwa kunyesha kwa mvua ni ishara ya neema.
 
Hata hivyo mvua hiyo iliendelea kupungua polepole na
kutoa nafasi ya mkutano huo kufanyika bila usumbufu
kama amabavyo wengi wangetarajia.
 
Katika hotuba yake Dk. Shein aliwaomba wananchi
kuwachagua wagombea wa CCM katika uchagauzi mkuu wa
Oktoba akisema CCM ndicho Chama chenye sera nzuri na
uzoefu wa uongozi.
 
Alisema wagombea wa upinzani hawana uzoefu wa uongozi
na vyama vyao vimenza siasa katika siku za karibuni
ikilinganishwa na CCM ambayo imetokea tangu enzi za
TANU na Afro-Shiraz (ASP). 
 
Dk. Shein alisema Serikali ya CCM ya awamu ya nne
ikiingia madarakani itaendeleza utawala bora kwa
kuimarisha idara ya mahakama na kuondoa sheria
zilizopitwa na wakati hasa zile zinazokandamiza
wanawake na watoto.
 
Pia alisema seikali itajenga vyuo vya ufundi stadi
(VETA) katika kila wilaya ili kuwawezesha wanafunzi
wanaokosa nafasi za kuendelea na elimu ya sekondari
kujifunza stadi za ujasilimali.
 
Leo Dk. shein anaendelea na ziara ya kamapeni wilaya
ya Magu Mkoani Mwanza na kesho ataanza ziara ya Mkoa
wa Mara.
(Mwisho)
*ABIHUDI SAIDEYA ni Mwandishi wa Habari - Contact:
0744-268961 au 0787-052221.