KAMPENI ZA MGOMBEA URAIS MHE. JAKAYA MRISHO KIKWETE  MKOA WA PWANI

 

Mgombea  Urais Mh Jakaya Mrisho Kikwete aanza kampeni za pili kwa mafanikio,ambapo ameanzia Mkoa wa Pwani alipopata mapokezi makubwa na wapinzani wamekuwa wakivutika na kuamua kurudi CCM.

·        Apokea wanachama wapya wa CCM 894 na waliorudisha kadi kutoka vyama vyama vya upinzani ni 713 kati yao ni kama ifuatavyo:

·        CUF 713

·        CHAUSTA 174

·        Kutoka vyama vingine ni 115

 

Mh Kikwete ameanza kampeni  katika Mkoa wa Pwani ambapo alikuwa katika wilaya ya Rufiji na Mkuranga, alifanya mikutano ya hadhara mitano na kusalimia wananchi katika vijiji 20

 

Mgombea  aliwaaidi wakazi wa Mkoa Pwani endapo watampa ridhaa basi ataboresha zaidi mfuko wa barabara ambao utasaidia kujenga barabara vijijini kama Bungu hadi Nyamisati,Kibiti hadi Mtunda,Nyamwage hadi Utete, na kukikarabati kivuko cha rufiji.

 

Pia  upande wa kilimo ameaidi kuboresha upatikanaji wa pembejeo za kisasa zaidi ili kuongeza uwingi wa upatikanaji wa mazao na kutafuta masoko ya kuuzia bidhaa hizo.Kwa upande wa wachungaji amegusia zaidi swala la kufuga kuliko kuchunga,”inaonekana kwa Tanzania Mchungaji anamtumkia N’gombe zaidi unakuta mchungaji hanenepi wala Ng’ombe hanenepi nataka kuwatoa huko tuingie katika ufugaji tuondokane na uchungaji”ni maneno ya Mh Kikwete. Aidha alisisitiza juu ya uboreshaji wavuvi wadogo wadogo ili waweze kupata vifaa vya kisasa kama vile boti za kuvuli badala ya mitumbwi ya wanaotumia hivi sasa.

 

Mbali na hayo,Mh Kikwete aliongeza kuwa makusudio ya serikali ya awamu ya nne ni pamoja na kuenzi Amani,Umoja na Utulivu ambayo ndiyo sera ya CCM. Tofauti na vyama vingine vinavyo hubiri sera ya udini, ukabila na rangi, alisema vyama vya siasa sio mzizi wa fitina miongoni mwa wananchi.

 

 Pia kuyaenzi mafanikio yaliyotokana na serikali zote tatu, serikali ya awamu ya kwanza ya hayati Mwl. Nyerere, serikali ya awamu ya pili ya Mzee Ali Hassan Mwinyi na ya awamu ya tatu ya Rais Benjamin Willium Mkapa, katika nyanja za elimu, afya, maji na ukuwaji wa uchumi. Alisema kuhusu elimu serikali ya awamu ya nne itaboresha zaidi mafanikio yaliyojitokeza kwa ujenzi wa nyumba za walimu, shule za sekondari kutoka kila kata na kuongeza idadi ya vyuo vikuu hapa nchini.

 

Alisema kuwa msukumo mpya pindi akichaguliwa itakuwa ni kupambana na umaskini wa Mtanzani, kwanza kwa kuboresha shuguli ambayo alikuwa anaifanya kama vile kilimo, ufugaji, na uvuvi, pili kuwawezesha vijana kupata ajira au kujiajiri wao wenyewe na tatu kuwawezesha wanawake kiuchumi kwa kuwatafutia mazingira ambayo wanaweza kujikwamua kiuchumi. Watanzania ni masikini lakini wanawake ni masikini zaidiMh. Kikwete alisema.

 

Kuhusu huduma za jamii alisema, akichaguli na hana mashaka na hilo serikali yake itashughulikia kwa makini  ujenzi wa zahanati na vituo vya afya ili Taifa letu liwe la watu wenye afya njema. Pia alizungumzia dhamira aliyonayo kuhakikisha upatikanaji wa maji safi na salama. ambapo ifikapo mwaka 2010 asilimia 90 ya maji yatakuwa yanapatikana mijini na asilimia 65 itakuwa vijijini,alisemaNichagueni nihangaike nayo….tumeyaweza mengi hili haliwezi kutushinda”.

 

Mh. Kikwete aliwaomba wananchi  wakichague Chama Cha Mapinduzi kwani ndicho chenye sera za kuleta maendeleo kwa Mtanzania, hivyo alitumia nafasi hiyo kuwaombea Madiwani na Wabunge  wa CCM kura ili wamsaidie kuboresha maisha ya kila Mtanzania kwa Ari Mpya, Nguvu Mpya na Kasi Mpya.