Ni unafiki wapinzani kudai kumuenzi Mwalimu Nyerere wakati wanamchoma kwa matendo
Na Lucas Kisasa
Kampeni za uchaguzi mkuu ambao sasa umepangwa kufanyika Desemba 14, mwaka huu hivi
sasa zinaendelea kwa kasi kubwa huku vyama vya siasa na wagombea wao wakipitapita
huku na kule kujinadi ili wachaguliwe hii ikiwa ni katika ingwe ya pili ya kampeni
hizo.
Uchaguzi Mkuu ulikuwa ufanyike Oktoba 30, mwaka huu lakini ukaahirishwa kufuatia
kifo cha mgombea mwenza wa nafasi ya urais kwa tiketi ya CHADEMA, Jumbe Rajab
Jumbe, kilichotokea Oktoba 26, mwaka huu.
Kwa upande wa
nafasi ya Rais wa
Uchaguzi wa Desemba 14 utakuwa kwa nafasi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Kampeni hizi za sasa na hasa kwa
nafasi ya urais wa
mpya, huku wagombea wote wa nafasi hiyo kutoka vyama 10 vya siasa wakiwa
wamejiandaa kutoa pigo kubwa la mwisho tayari kwa siku hiyo ya uchaguzi mkuu.
Siasa ni mchezo mchafu. Huu ni usemi ambao umezoeleka duniani kuhusiana na masuala
ya siasa na hasa siasa za uchaguzi. Huku vyama vya siasa vikiwa vinadi sera katika
kipindi hiki cha uchaguzi, lakini wakati huo huo wako wanasiasa ambao wanayo
mikakati ya "kupakaziana" kwa lengo la kudhoofisha upande mwingine katika
kinyang'anyiro cha madaraka.
Hivi sasa kwa mfano wako wanasiasa wanaopita huku na huko wakitumia jina la
Mwalimu Nyerere kwa lengo la kujinufaisha kisiasa. Wote tunafahamu umaarufu wa
jina la Mwalimu Nyerere, siyo katika nchi yetu tu, bali kimsingi kwa dunia nzima.
Mwalimu Nyerere ndiye mwasisi wa taifa letu, ni Baba wa taifa hili.
Kwa siasa za
amseme vibaya Mwalimu Nyerere. Ni kweli wako wanasiasa ambao hawakubaliani au
hawakukubaliana na Mwalimu Nyerere, wakiwemo akina Christopher Mtikila na wengine,
lakini kwa ujumla wake wanasiasa wengi wakiwemo wa upinzani hupenda kujipambanua
kuwa wao ndio wako msitari wa mbele katika kumuenzi Mwalimu Nyerere.
Hivi sasa, kwa mfano, wanasiasa kadhaa wa upande wa upinzani wakiwemo wagombea wa
nafasi ya urais katika mikutano
wanaomuenzi Mwalimu Nyerere na kwamba Chama tawala, CCM, wamezitupa fikra zote za
Baba wa taifa.
Ni maoni ya safu hii kuwa wale wote , na hasa kwa upande wa upinzani, wanaojinadi
kuwa wao ndio wanaomuenzi Mwalimu Nyerere, ikiwa ndio mkakati wao wa kujipatia
kura, wanatenda kosa kubwa na kimsingi siyo tu kwamba kitendo hicho ni cha unafiki
mkubwa bali pia ni matusi kwa Baba wa taifa.
Katika kuchambua unafiki wa watu wanaolitumia jina la Mwalimu Nyerere ni muhimu
kwanza tukaainisha mambo yale muhimu ambayo Mwalimu Nyerere aliyaamini na
kuyasimamia wakati wa uhai wake.
dhati kabisa na bila unafiki wowote. Katika matendo yake yote kamwe Mwalimu
Nyerere hakuisaliti nchi yake. Aliitetea kwa vitendo. Mwalimu Nyerere hakuwa
tayari kuona
hasa ya kibeberu. Ni katika enzi za
Mwalimu Nyerere ambapo heshima ya
ilikuwa juu kutokana na msimamo wake usioyumba.
Sasa hebu tujiulize ni akina nani hao kwa upande wa upinzani wanaodai kuwa
wanamuenzi Nyerere na ambao
wanaipenda
wanachodai kuwa ni kutokana na mizengwe watahakikisha kuwa kunakuwepo na janga la
kitaifa?
Kama kweli wapinzani wanaipenda
kampeni ili
kiuchumi? Kama wanaipenda
siyo kwa bahati mbaya, katika
kuchochea maasi
Jambo la pili aliloliamini na kulisimamia Mwalimu Nyerere ni kwamba aliwapenda
wananchi wake. Mwalimu Nyerere aliwapenda Watanzania, na alifanya hivyo kikweli
kweli na kwa moyo wa dhati kabisa. Ajitokeze mpinzani hapa na atuambie kwa moyo
wake wa dhati
Kwa ujumla, vitendo vya wanasiasa wengi ni kuwa wanawapenda wananchi kwa nadharia
tu, lakini matendo ya wanasiasa hao ni kinyume kabisa na wanachohubiri kwenye
majukwaa ya kisiasa.
Mwalimu Nyerere aliwapenda wananchi na alipenda Watanzania wawe na maendeleo.
Mwalimu alipenda maendeleo ya wananchi na alikuwa msitari wa mbele kuhakikisha
kuwa wananchi wanaondokana na unyonge.
Sasa basi waje hao wanaojidai kuwa wanamuenzi Mwalimu Nyerere na watufahamishe
namna wanavyomuenzi kwa kupenda
wananchi na hata maendeleo
wamewafanyia nini wananchi. Katika hili wapinzani wanaweza wakaja na hoja kuwa
hawajawafanyia lolote wananchi kwa kuwa hawajapata madaraka. Sawa, lakini je,
wameshawahi kwenda huko vijijini kuhimiza maendeleo ya wananchi? Je, wamekwenda
huko vijijini au hata katika maeneo ya mijini kuishi na wananchi na kuhimiza
miradi ya kuondokana na umaskini?
Ambacho tumekuwa tukikishuhudia kutoka kwa wanasiasa wengi wa upinzani ni pita
pita zao na za hapa na pale huku wakipiga kelele za kwamba eti CCM ni wezi wa kura
kwa hiyo wasipewe madaraka.
Wapinzani ni
uongo dhidi ya Chama tawala kwamba eti kinapata madaraka kwa hadaa zitawasaidia
wapinzani hao kuingia Ikulu.
Wanachofanya wapinzani ni kulalamika na siyo kuchochea maendeleo. Tena basi wako
baadhi wanakwenda mbali zaidi kwa
kuhujumu hata
mbalimbali iliyopo kwa ajili ya wananchi. Hivi watu wa namna hiyo kweli
wanawapenda wananchi?
Katika mgomo huu wa madaktari wa Hospitali kubwa nchini, Muhimbili, ambao umeacha
baadhi ya wananchi wakikosa huduma
za matibabu na hata kuhatarisha maisha
wako wanasiasa uchwara waliounga mkono mgomo huo. Wamefanya hivyo kwa sababu za
kisiasa. Wanachojali wanasiasa hao ni maslahi
Mwalimu Nyerere alipenda na kusimamia amani, umoja na utulivu nchini. Mwalimu
Nyerere alifanya hivyo kwa vitendo. Alikuwa mkali kwa wale wote waliokuwa
wakihatarisha amani, utulivu na umoja wa kitaifa. Baba wa taifa pia alipenda
utawala wa sheria.
Sasa basi asimame mwanasiasa, na hasa wa upande wa upinzani, anayejidai kuwa
anamuenzi Mwalimu Nyerere atueleze ni namna gani anatekeleza aliyoamini Mwalimu
kuhusu suala la amani, umoja, utulivu nchini na utawala wa sheria.
Wanasiasa wengi wa upande wa upinzani wanakwenda kinyume na aliyoamini Baba wa
taifa. Wanachochea vurugu nchini. Wanawahamasisha wanachama na wafuasi wa vyama
vyao walale barabarani eti "mpaka kieleweke". Wanawachochea wafuasi wao waendeshe
vitendo vya hujuma. Na kweli, baadhi ya wafuasi wao wamekuwa wakitekeleza
maelekezo hayo ya wanasiasa wa upinzani katika "kuifanya nchi isitawalike".
Tumeshuhudia mauaji ya kisiasa yakitokea nchini mwetu. Kada wa CCM wa Tawi la
Chama (CCM) la Midizini, Manzese,
waliuawa katika tukio la kutisha
baada ya nyumba
Waliochoma moto nyumba hiyo ni akina nani? Ni wafuasi wa chama kimojawapo cha
siasa nchini. Kosa la kada huyo wa CCM aliyeuawa ni nini? Ni kuipenda na
"kuifagilia" CCM.
Huko Tanga nako katika kijiji kimojawapo mkoani humo kada wa CCM akiwa amevalia
sare zake za "Ari mpya, nguvu mpya na kasi mpya" na akipita njiani akiimba nyimbo
za "kuifagilia" CCM, alishitukia akidakwa na kundi la vijana wa chama cha siasa
cha upinzani ambapo walimsulubu na kumuua.
Baada ya kitendo hicho kiovu maiti ya Mtanzania huyo ikafungiwa ndani ya ofisi na
kuenezwa habari za uongo kuwa kada wa CCM amejinyonga. Baadhi ya waandishi wa
habari wakaidaka habari hiyo kama
walivyolishwa na kuandika kwenye magazeti
yanayodaiwa ni huru kwamba kada wa CCM akutwa amejinyonga.
Hatujasahau kilichotokea katika kijiji cha Piki huko
mkuu wa Oktoba 30, mwaka huu huko
uchumi la
wanaojiita wao ni ngangari. Mmoja wa askari hao akateleza
lakini mwenzake hakusalimika.
Askari huyo wa Jeshi la Kujenga
Uchumi la
na kuuawa. Baada ya kitendo hicho kiovu wanakijiji wote wa kijiji hicho wakaingia
msituni kukimbia mkono wa dola. Lakini ikapigwa propaganda na kudakwa na vyombo
kadhaa vya habari kwamba wanakijiji wa Piki wamewakimbia polisi ili
wasiwanyanyase. Kitendo cha baadhi
ya msingi isipokuwa mazungumnzo sasa yakawa ni namna wanakijiji waovu
walivyowakimbia polisi "wanyanyasaji".
Katika matukio yote haya ya mauaji ya kisiasa viongozi wa chama cha siasa ambacho
wafuasi wake walihusika hawakuomba radhi hata kidogo. Walifanya hivyo tu pale
waandishi wa habari walipopigwa katika ofisi ya chama kimoja cha upinzani kwa
kuogopa kuwa
Kwa wanasiasa wasioamini katika umoja wa kitaifa, amani na utulivu wala utawala wa
sheria ni matusi makubwa kusema kuwa eti wanamuenzi Baba wa taifa. Wanyamaze.
Wasipotoshe historia, wasimdhalilishe Mwalimu Nyerere huko aliko.
Simu: 0744-309858
E.mail: kisasa2000@yahoo.com