Na Abihudi Saideya, Biharamulo 18/10/2005 -DK. SHEIN
Mgombea Mwenza wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania kupitia tiketi ya Cham Cha Mapinduzi Dk. Ali
Mohamed Shein amesema wagombea wa uongozi katika
uchaguzi mkuu wapimwe kwa sifa na uwezo wa vyama vyao.
Dk. Shein alitoa mwito huo leo (18/10/2005) alipokuwa
akihutubia mkutano wa kampeni za uchaguzi mjini
Biharamulo Mkoani Kagera.
Alisema wapiga kura wasifanye makosa ya kuanagalia
sifa ya mgombea bila kuzingatia Chama chake.
Mfumo wa siasa hapa nchini, alisema unashindanisha
sera za vyama vya siasa na kwamba umaarufu wa mgombea
siyo sifa pekee ya kuzingatiwa.
Aliwataka wananchi kumchagua mgombea Urais wa CCM Bw.
Jakaya Marisho Kikwete na wagombea Ubunge na Udiwani
wa CCM akisema CCM ni chama chenye historia ya
ukombozi wa taifa na kimedhirisha uwezo na uzoefu
mkubwa wa uongozi.
Alisema vyama vya upinzani haviaminiki na baadhi ya
vyama hivyo vinaongozwa na wanasiasa waliofukuzwa CCM
kutokana na mapungufu yao katika uongozi wa Chama na
serikali.
Alisema CCM imeimarisha uchumi na huduma za kijamii na
kuiwezesha Tanzania kupata sifa kemkem ndani ya Afrika
na duniani.
Dk. Shein ambaye alikuwa akitubia kwenye uwanja wa
wazi huku mvua ikinyesha aliwaponda viongozi wa
upinzani wanaodai serikali ya CCM haijafanya chochote
wakati wao wenyewe wamesoma katika shule za serikali.
Alimtambulisha na kumwombea kura mgombea Ubunge wa CCM
jimbo la Biharamulo Magharibi Bw. Anatory Choya na
wagombea udiwani wa Kata za Walaya hiyo.
Dk. Shein aliwashukru wana-CCM,wapenzi wa CCM na
wananchi kwa kuendelea na mkutano huo licha ya mvua
iliyokuwa ikinyesha.
Mapema akimkaribisha Dk. Shein, Mwenyekiti wa CCM wa
Mkoa Bw.Pius Ngeze alisema mvua kubwa iliyonyesha mara
baada ya kuanza kwa mkutano huo ni dalili nzuri
inayoashiria ushindi wa Chama Cha Mapinduzi.
Hapo jana Dk. Shein alihutubia mikutano miwili ya
kampeni Wilayani Muleba. Katika mikutano hiyo alipokea
wanachama 130 waliohamia CCM kutoka vyama vya upinzani
wengi wao wakiwa wa TLP na CUF.
Kesho (19/10/2005) Dk. Shein anaendelea na ziara ya
kampeni Mkoani Shinyanga akianzia wilaya ya Kishapu
ambako anatarajiwa kuhutubia mkutano wa hadhara.
(mwisho)
*Abihudi Saideya ni Mwandishi wa Habari-Contact:
0744-268961 au 0787-052221.