Kikwete awataka
wapinzani wasione haya kuipigia CCM
Na Rashid Zahor, Mkuranga
MGOMBEA Urais wa Jamhuri ya Muungano kwa tiketi ya CCM, Jakaya Kikwete amewataka
wafuasi wa vyama vya upinzani wasione aibu kukipigia kura chama hicho kwa vile
hakuna mgombea urais wa vyama hivyo atakayeweza kushinda wadhifa wa urais.
Kikwete alitoa rai hiyo juzi na jana alipokuwa akihutubia mikutano ya kampeni
iliyofanyika Utete na Mkuranga mkoani Pwani.
"Hakuna mgombea urais wa upinzani
akayemshinda mgombea wa CCM.
mpe kura yako mgombea urais wa CCM, wabunge na madiwani ili uharakishe maendeleo
ya jimbo lako," alisema.
"
hata
kishindo, lakini ukweli unabaki kuwa nao mwenyewe moyoni mwako," alisema.
Mgombea wa CCM aliwatahadharisha Watanzania wawe macho na viongozi wa vyama vya
upinzani wanaotangaza matokeo ya uchaguzi kwamba wanafanya makosa kwa vile kazi
hiyo ni ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi.
Alitoa mfano wa matokeo ya uchaguzi
mkuu wa Rais na Wawakilishi wa
yaliyotangazwa na CUF kwamba hayakuwa sahihi na yalilenga kuwapotosha Watanzania.
"CUF wanadai kwamba Maalim Seif alishinda kwa asilimia 50.6 na Karume alishinda
kwa asilimia 49.3. Ukijumlisha asilimia hizi unapata asilimia 100.
"Kule Zanzibar wagombea walikuwa sita na wote walipata kura. Sasa unapotoa takwimu
za kura za CCM na CUF ambazo ukizijumlisha unapata asilimia 100, kura za wagombea
wengine ziko wapi?
Wakati huo huo, akihutubia mkutano mkubwa wa kampeni Mburahati Barafu jijini Dar
es Salaam jana, Kikwete, ameahidi kuwa serikali ya awamu ya nne itahakikisha
walimu nchini wanajengewa nyumba bora za kuishi.
Alisema katika mkutano huo uliohudhuriwa na mamia ya wananchi na wapenzi wa CCM
kuiwa, baada ya serikali ya awamu ya tatu kukamilisha ukarabati wa shule za
msingi, katika awamu ijayo, serikali itatoa kipaumbele kwa walimu.
"Huko vijijini nyumba za walimu zinatisha. Wanafanya kazi kwa moyo. Tumeanza na
madarasa, sasa itakuwa zamu ya nyumba za walimu.
"
kwenye nyumba nzuri," aliongeza.
Kikwete pia aliahidi kuwa serikali ijayo ya CCM itatilia mkazo ajira kwa vijana
kwa vile ukosefu wa ajira ni bomu la kutega, ambalo yeye binafsi linamtisha.
Alisema karibu kila mwaka vijana 800,000 wanamaliza vyuo na shule za msingi, hali
inayoonyesha kuwa tatizo
serikali ijayo itapambana nalo.
Wananchi Bukoba Mjini
wasusia mkutano wa Seif
Na Angela Sebastian, Bukoba
WANANCHI wa Bukoba Mjini wamesusia mkutano wa kampeni wa chama cha CUF uliokuwa
ukihutubiwa na Katibu Mkuu wa chama hicho, Maalim Seif Shariff Hamad.
Tofauti na mikutano ya chama hicho kujaa mamia ya mashabiki, juzi hali ilikuwa
tofauti ambapo Maalim Seif alijikuta akiwahutubia viongozi wa wilaya wa chama
chake, wafuasi wachache na watoto.
Wananchi wengi waliususa mkutano huo uliyofanyika juzi katika viwanja vya Uhuru
mjini hapa, ambapo wengi waliamua kusikiliza sera za kumnadi mgombea ubunge wa CCM
katika jimbo la Bukoba Mjini, Khamis Kagasheki, uliofanyika katika viwanja vya
Bunena mjini hapa.
Hali hiyo imetafisiriwa na wakazi wengi wa hapa kuwa ni dalili inayoonyesha
kupungua kwa umaarufu wa CUF mjini hapa, jimbo ambalo lilikuwa likishikiliwa na
mbunge wa chama hicho, Wilfred Lwakatare. Hali hiyo inatoa nafasi nzuri zaidi ya
ushindi katika uchaguzi wa Desemba
14, mwaka huu, kwa CCM kuchukua jimbo
"Hivi huyu mtu aliyeshindwa
hii ni
mkutano wa CCM.
Hali hiyo ya wananchi kuukimbia mkutano wa Seif, inasemekana kumechangiwa na
kiongozi huyo kukosa ushindi huko
waandishi wa habari, ambapo wananchi walidai hawawezi kupoteza muda wao kwenda
kusikiliza sera zinanopalilia matusi, kashfa na vurugu.
Kundi moja lililokuwa pembeni mwa uwanja huo wa Bunena llililokuwa likiongozwa na
mzee mmoja aliyejitambulisha kwa jina la Salimu Swahibu mkazi wa mjini Bukoba
lilisikika likisema “sera za CUF ni kujenga chuki ndani ya mioyo ya wananchi,
kashfa na sasa wamecheza ngoma wasiyoijua".
"Itikadi ya vyama vingi si mapanga, marungu na fujo bali ni kuboresha demokrasia
na maendeleo ya Taifa la
Walisema kuwa siku hizi watu wameelewa kwa hiyo wanatafuta viongozi bora
watakaoweza kutatua matatizo
binafsi.
Wananchi hao walisema kuwa matusi yanayotolewa na viongozi wa CUF hayatawafaidisha
wananchi, bali viongozi watoa
matusi nia
Wakati huo huo, Mgombea ubunge kupitia tiketi ya CCM Khamisi Kagasheki alipokuwa
akihutubia katika mkutano wake wa kampeni jana uliofanyika katika kata ya
Rwamishenye, alisema kuwa nia ya kugombea ubunge katika
jimbo
bali kutaka kushirikiana na wananchi wa Bukoba kuleta maendeleo na kuwatumikia.
Mkutano huo ambao ulikuwa mkutano wa uzinduzi wa kampeni kwa mara ya pili
ulihudhuriwa na maelfu ya wananchi na wakazi wa mji wa Bukoba wakiimba nyimbo za
kuwanadi wagombea wa CCM.
Msome aasa
kuendelezwa kwa amani na utulivu
Na Mwandishi Wetu
CHAMA cha Mapinduzi kimewataka viongozi na wafuasi wa vyama vya siasa nchini
kujiepusha na vitendo vya fujo, chuki na uhasama wakati wa kampeni za uchaguzi
mkuu zinazoondelea ili kudumisha na kuendeleza umoja, amani, utulivu na mshikamano
wa taifa.
Wito huu umetolewa na Katibu wa
Organaizesheni wa Chama Cha Mapinduzi,
Msome katika mikutano ya kampeni za uchaguzi iliyofanya katika wilaya za Uyui na
Tabora, wiki hii.
Msome alisema hayo kufuatia mfululizo wa matukio ya kuhatarisha amani yaliyotokea
mkoani Tabora na sehemu kadhaa nchini ambayo yanaaminika kufanywa na wafuasi wa
vyama vya upinzani.
Akitoa mfano wa vitendo vya uvunjaji wa amani, Msome alivitaja vitendo vya hivi
karibuni vya ushambuliaji wa wana- CCM, uchomaji wa nyumba, uwekaji wa vinyesi
katika kuta za nyumba na visima vya maji na upigaji wa watu wakiwemo waandishi wa
habari ni baadhi ya mambo ambayo hayana budi kukemewa na jamii.
Msome alisema Watanzania wanachotaka kuona na kusikia ni sifa za wagombea, ubora
wa sera na rekodi ya vyama, wala si vitendo vinavyokiuka sheria za uchaguzi na
kuhatarisha misingi ya taifa.
Aliwakumbusha wananchi kuwa mfumo wa vyama vingi vya siasa haukuanzishwa ili
kuvunja misingi ya utaifa ambayo imejengwa kwa muda mrefu na waasisi wa Taifa letu
ambao ni Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere na Mzee Abeid Amani Karume,
bali kuiendeleza na kuiboresha kwa maendeleo ya Taifa.
"Kwa maana hiyo, chama chochote cha siasa kinachotishia misingi hiyo kikataliwe na
kunyimwa nafasi ya kuongoza nchi yetu," alisema
Msome ambaye pia ni Mjumbe wa kamati Kuu ya CCM, amewaomba Watanzania kuendelea
kukiunga mkono Chama cha Mapinduzi ambacho kimekuwa daima mtetezi mkubwa wanyonge,
udumishaji na uendelezaji wa umoja, amani na maendeleo ya taifa.
Msome amemaliza ziara ya siku nne mkoani Tabora ambayo ilikuwa ya lengo la
kuwanadi wagombea wa CCM wa nafasi za urais, ubunge na udiwani. Baadaye wiki hii
ataanza ziara
RPC Mbeya aagizwa
kuondoa tofauti na wana habari
Na Mohammed Mhina, wa Jeshi la Polisi
MAKAO Makuu ya Jeshi la Polisi nchini limemuagiza kamanda wa Polisi wa Mkoa wa
Mbeya Kamishna Msaidizi wa Polisi Suleimani Kova, kudumisha na kuendeleza uhusiano
mwema na waandishi wa habari mkoani humo kwa manufaa ya jamii inayowazunguka.
Msemaji wa Jeshi la Polisi nchini
Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi
Mwmaunyange, alisema jana uongozi wa polisi umeshtushwa na kusikitishwa na taarifa
ya chama cha waandishi wa habari wa mkoa wa Mbeya kuwa wametishia kususia kufanya
kazi na kamanda wa polisi wa mkoa huo kwa sababu za kutoaminiana.
Mwamunyange alisema Jeshi la Polisi kwa maana ya Makao Makuu na makamanda wa
polisi wa mikoa na vikosi, wakati wowote wanakuwa na uhusiano mwema na wa karibu
na wa moja kwa moja na waandishi ama vyombo vya habari kwa nia ya kuelimisha umma
juu ya masuala ya uhalifu na usalama.
Alisema hakuna haja ya kutofautiana ama kulumbana kati ya pande hizo mbili kwa
masuala ya kiutendaji kwani wote ni wadau katika suala la kuhakikisha kwamba
ulinzi na usalama na elimu kwa
jamii inawanufaisha wananchi katika maeneo
Jeshi
kutojenga tabia ya kutishia ama kususia kutoa taarifa za viongozi ama taasisi ya
mtu binafsi, taasisi au idara ya serikali kwani kwa kufanya hivyo kunawakosesha
wananchi haki
njia ya habari.
Msemaji huyo alisema hakuna haja ya baadhi ya waandishi ama vyombo vya habari
kujenga chuki na viongozi wa serikali ama taasisi kutokana na kuhitilafiana au
kutiliana mashaka kwani kwa kufanya hivyo hasara kubwa ni kwa jamii.
Mwamunyange alisema kwa vile makamanda wa polisi wa mikoa na wakuu wa vikosi vyote
vya polisi hapa nchini wapo chini ya Mkuu wa Jeshi la Polisi ni vema mtu ama
taasisi ikiona inahitalifiana na mmoja wa makamanda kutoa taarifa makao makuu
kabla ya kuchukua hatua dhidi ya mhusika kwa ushauri na maelekezo zaidi.
Jeshi
kuhakikisha usalama wa waandishi wa
habari katika kazi zao, maisha
zao ukiwa pia ni wajibu wa msingi katika jamii nzima ya Kitanzania.
'Ondoeni dhana ya
dawa ya jino kuling'oa'
Na Mwandishi Wetu
WIZARA ya Afya imewataka madaktari wa meno nchini kuondoa dhana iliyojengeka kwa
wananchi kwamba dawa ya jino ni kuling'oa.
Hayo yalisemwa jana na Mkurugenzi wa Huduma za Hospitali katika Wizara ya Afya Dk.
Zacharia Berege ambaye alitoa hotuba ya ufunguzi wa mkutano kwa niaba ya Katibu
Mkuu wa Wizara ya Afya Mariam Mwaffisi kwenye warsha ya siku tatu ya Chama cha
Madaktari wa Meno
Berege katika hotuba hiyo alisema changamoto waliyonayo madaktari hao kutoka
sehemu mbalimbali za
wa meno ya binadamu
kung'oa.
Aliwataka madaktari pia kulizungumzia kwa kina suala la maambukizi ya ukimwi kwa
mate na njia ya damu.
Berege aliwataka madaktari hao kutilia manaani changamoto wanazopata ili
kurekebisha sehemu zinazoonekana zina kasoro.
Alisema suala la msingi kwa binadamu ni pamoja na mazungumzo na mazungumzo
yanakuwa mazuri pale harufu inayotoka mdomoni inakuwa nzuri.
Naye Mwenyekiti wa Chama cha Madaktari wa Meno Tanzania Dk. Flora Fabian katika
hotuba yake ya kumkaribisha mgeni alisema kuwa wanatarajia katika mkutano huo
watatoka na maazimio ya kuendeleza afya ya meno.
Ukata wasababisha
mgombea ubunge kupitia TLP Handeni kushindwa kufanya kampeni
Na Mwandishi Wetu, Handeni
MGOMBEA ubunge wa Jimbo la Handeni kwa tiketi ya Tanzania Labour (TLP) Mwajabu
Sufiani Mhina ameshindwa kufanya kampeni kutokana na kukosa fedha.
Akizungumza na waandishi wa habari jana Ofisini kwake mjini hapa, Mwajabu alisema
mbali na uwezo wake mdogo wa kifedha pia amekosa ushirikiano na uongozi wa TLP
mkoa wa Tanga.
"Nimeshindwa kufanya kampeni sababu uwezo wangu wa kifedha ni mdogo...lakini
sikupata ushirikiano wala kutembelewa na viongozi wa mkoa, sielewi ni kwanini,
wakati niliteuliwa kihalali kugombea nafasi hiyo," alisema Mwajabu.
Mwajabu aliendelea kusema alifuata taratibu zote za kisheria hadi kuteuliwa,
lakini kinachomshangaza ni uongozi wa mkoa huo kutomjali.
Mgombea huyo ambae ni Mwenyekiti wa chama hicho wilayani hapa na ni Mjumbe wa
Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama hicho, alisema mgombea uraisi kupitia TLP
Augustine Mrema ilikuwa afanye ziara ya kampeni wilayani hapa miezi miwili
iliyopita lakini alishindwa kufanya hivyo.
"Sio uongo mgombea wetu (Mrema) ilikuwa aje na nilipigiwa simu kutoka makao makuu
nifanye maandalizi ya ugeni huo, tulishirikiana na uongozi wa wilaya na kata,
tulifanya maandalizi makubwa tuliandaa mabango, bendera na vipeperushi vya kila
aina tukatangaza ujio wa Mwenyekiti," alisema Mwajabu na kuwa pamoja na yote
hakutokea.
"Wakati maandalizi hayo yakiwa yamekamilika usiku wa ujio wa mgombea wetu
nikapigiwa simu na Katibu wa Vijana wa chama hicho mkoa Omari Chombo kuniambia
Mrema hatokuja Handeni," alisema Mwajabu.
Aliendelea kuwa: "Nilipata ugonjwa wa moyo, nilijiuliza nitawaambia nini wananchi
je wale waliopo njiani itakuaje,
kulipokucha nilipata wakati mgumu
nilijifungia ndani chumbani nilishindwa kutoka."
Mgombea huyo alifafanua kua kutokana na kutokufika kwa Mrema baadhi ya ngome za
chama hicho zimevunjika kutokana na watu kukasirika.
Mwajabu katika kinyang'anyiro hicho cha ubunge anachuana na Mjumbe wa Kamati Kuu
ya CCM Taifa ambaye pia ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Mipango na Ubinafsishaji)
Dk. Abdallah Kigoda na Saidi Mbweto wa CUF.
Tawi la TLP Kitunda lavunjika
L Wanachama wajiunga CCM
Na Nashon Maingu
TAWI la chama cha TLP liitwalo Ngurwi katika kata ya Kitunda, Manispaa ya Ilala
lenye wanachama 59, limevunjika baada ya wanachama wake kukihama na kujiunga na
Chama cha Mapinduzi.
Kufa kwa tawi
kuzielewa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ambayo inatangazwa katika kampeni zinazoendelea
za uchaguzi mkuu wa mwaka huu.
Tawi
walikabidhiwa kadi za CCM na mgombea wa udiwani kata ya Kitunda, Johannes Kisano
(Jaluo). Mwezi uliopita katibu wa CUF wa kata hiyo alijiunga na CCM.
Akikabidhi kadi hizo, Kisano aliwataka wananchi wengine waingie CCM na kuachana na
vyama vya ubabaishaji
Akijibu hoja hiyo ya mgombea udiwani, Mwenyekiti wa tawi jipya la CCM,
lililofunguliwa baada ya kufungwa la TLP, Hussein Mkukila, alisema walikuwa
wanachama wa CCM, lakini baada ya kulaghaiwa mwaka jana, walijiunga na TLP na
kuwa sasa wanakiri kuwa mtoto akimkosea mzazi wake na kuondoka nyumbani, iko siku
atarudi tu.
Katibu wa Tawi
kutowatembelea. Pia alisema hakuna kiongozi yeyote wa wilaya ama mkoa aliyewahi
kulitembelea tawi
Mwandishi wa habari hizi alipomhoji Katibu wa siasa na uenezi CCM, kata ya
Kitunda, Francis Kalokola, kuhusu mwenendo wa kampeni na matumaini ya CCM katika
kata hiyo, alisema wagombea wa CCM wanakubalika kutokana na sera nzuri za chama na
wana uhakika wa kupata ushindi wa zaidi ya asilimia 90.
"Ni kweli lilikuwepo kundi la wanachama na viongozi waliokuwa wakipinga chama
kutokana na matokeo ya kura za maoni, lakini mambo sasa ni shwari na ndiyo maana
tunatamba kwa jeuri kuwa tutapata ushindi zaidi ya asilimia 90," alisisitiza
Katibu huyo wa siasa na uenezi .
Kata ya kitunda ina matawi 16 na lengo ni kufikisha matawi 20 kabla ya mwisho wa
mwaka huu.
Dk. Sheni: Umoja na mshikamano ndiyo siri ya ushindi uchaguzi ujao
Na Mwandishi Wetu, Korogwe
Mgombea mwenza wa urais kwa tiketi ya CCM, Dk. Ali Mohammed Sheni, amesema umoja
na mshikamano miongoni mwa wanachama na wapenzi wa CCM ndio silaha kubwa
itakayowezesha kupata ushindi wa kishindo katika uchaguzi mkuu ujao.
Dk. Sheni aliyasema hayo alipokuwa akihutubia mkutano wa kampeni uliofanyika Mombo
wilayani Korogwe.
"Sote tushikamane, walio wanachama, wapenzi, wakereketwa wa CCM na wapenda amani,
letu liwe moja, ifikapo Disemba 14 tuipigie CCM kura zote za ndiyo za urais kwa
Jakaya Kikwete, wabunge na madiwani wote wa CCM.
"Umoja na mshikamano wetu ndio utatuwezesha kukata 'kilomolomo' chao
wapinzani...tuwanyoe kwa wembe ule
ule kama ilivyotokea
hakuna chama mbadala katika nchi hii zaidi ya CCM," alisema.
Dk. Sheni alisema wananchi wana kila sababu ya kuichagua CCM kwa kuwa ina historia
kubwa ya ukombozi na ujenzi wa nchi kiasi kwamba maendeleo yanaonekana katika
sekta mbalimbali zikiwemo za uchumi na huduma za jamii.
Mgombea Mwenza huyo amebainisha kuwa muda wa upinzani umekwisha na kilichobaki
wakusanye nguvu waipigie kura CCM, maana wapinzani watake, wasitake CCM itashinda
kwa kuwa inapendwa na watu wengi na ndio wanaokiweka madarakani.
"Waambieni hao wapinzani muda wa kukaa huko umekwisha wajikusanye nguvu waipigie
kura CCM maana watake wasitake CCM itashinda kwa sababu inawekwa madarakani na
nyinyi wananchi." alifafanua.
Dk. Sheni alikamilisha ziara yake ya kampeni mkoani Tanga kwa kupokea wanachama
164 wa kutoka vyama vya upinzani wilayani Korogwe wakiwemo 107 TLP, 27 CUF, 28
CHADEMA na wengine wawili kutoka NCCR-MAGEUZI na UDP.
Akiwa njiani kwenda Arusha, ambako alianza ziara ya kampeni jana, Dk Sheni
alisalimiana na wananchi wa Hedaru, Same, Mwanga, njia panda Himo na Hai mkoani
Kilimanjaro, ambapo aliwakumbusha juu ya uchaguzi mkuu ujao na kuwataka kupiga
kura kwa utulivu na wala wasibabaike na wapinzani.
Aliwataka wananchi wasikosee waendelee kuichagua CCM kwa kuwa viongozi wake wana
uwezo na uzoefu mkubwa wa kuongoza nchi tofauti na viongozi wa vyama vingine ambao
amewaelezea kuwa bado ni wachanga.
Hongera Tibaigana kwa kuwaepusha madaktari wahuni kupigwa mawe
NIMEMSIKIA
na kumwona Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoa wa
Tibaigana, akiwaeleza madaktari kuacha mpango wao wa kuandamana kwenda eti Ikulu
kuwasilisha malalamiko
Sababu alizotoa Afande Tibaigana kuwazuia madaktari hao, hasa wa hospitali kubwa
ya Muhimbili, kutoandamana ni kwamba ofisi yake haijapokea taarifa kutoka Ofisi
Kuu (Ikulu) kwamba maandamano
Kutokana na hatua yake hiyo, Tibaigana akawaambia madaktari hao kwamba iwapo
wanaona upo umuhimu wa kuendelea na
maandamano
kuelekea kiwanja chochote, lakini si Ikulu.
Nakiri kwamba uamuzi wa afande huo umeonyesha anavyoweza kutumia kichwa chake
kuepusha shari na dhahama ambazo zinaweza kutokea panapofanyika maandamano holela
na kutaka kuingia Ikulu bila kufuata taratibu zilizopo.
Hata hivyo, Afande Tibaigana ameshindwa kuwaeleza madaktari sababu nyingine muhimu
zaidi hata ya hiyo ya kufuata utaratibu wa kuingia Ikulu, kwamba ‘nguvu ya umma’
ingeweza kabisa kusababisha maafa
kwa madaktari hao kutokana na hatua
kugoma kuwahudumia wagonjwa, na
kuacha wengine wakipoteza maisha
rahisi iwapo wangeandamana.
Nasema amewaepusha na ‘nguvu ya umma’ kutokana na ukweli kwamba, baada ya
madaktari kutangaza mgomo wao kutokana na sababu wanazoeleza kuwa ni ujira mdogo,
ikiliganishwa na majukumu
kuielezea kuwa ni ya kinyama.
Kugoma kwa madaktari maana yake ni kuruhusu vifo vinavyoweza kuzuiwa kutokea
kutokana na wagonjwa kukosa huduma zinazohitajika kwa haraka kuokoa maisha.
Hata hivyo, serikali baada ya kukiri kuwepo kwa malipo kidogo, si kwa madaktari
tu, bali kwa kada zote za ajira za serikali na hata kwa watu binafsi, iliamua
kupandisha mishahara ya madaktari kwa viwango tofauti, huku waliokuwa wakipokea
zaidi ya sh. 200,000 kwa mwezi wakiongezewa hadi sh. 400,000 na ushei.
Madaktari waligoma wakiishinikiza serikali kuwalipa zaidi ya sh. milioni 1.2 ili
eti waweze kuishi kwa raha, huku wakitoa huduma kwa wagonjwa kwa ufanisi mkubwa.
Hao madaktari cha kushangaza, baada ya kutangazwa kwa nyongeza hiyo, ‘wakakaza
kamba’ kwamba hawawezi kuendelea na kazi hadi watakapohakikishiwa malipo ya sh.
milioni 1.2, kima cha chini, kwa mwezi, tena kwa kuanza kulipwa mara moja, si
kusubiri hadi Januari, mwakani
Wakielezea msimamo wao huo, madaktari hao walionekana wakiselebuka kwa ‘magoma
motomoto’ ndani ya viwanja vya hospitali ya Muhimbili eti wakifurahia kuendelea na
mgomo wao huku wagonjwa wakiendelea kufa na wengine wakichukuliwa na ndugu zao
kwenda hospitali binafsi.
Kitendo cha madaktari kuendelea na mgomo, huku wakionyesha kejeli kwa wagonjwa
kwa kucheza muziki na kuwapiga madaktari wenzao wenye moyo na huruma, waliokuwa
wakiendelea kutoa huduma, ni kitendo ambacho kimewakasirisha mno wananchi.
Wananchi wanashindwa kabisa kuwaelewa wasomi hao, wengi wao wakiwa wametumia kodi
za wananchi hao hao wanaowasusa kuwapa tiba leo baada ya kuwa wamepata kazi.
Kitendo cha madaktari kugoma na kuruhusu vifo zaidi ni cha kinyama na hakina
chembe ya ubinadamu wala Utanzania ambao tumeuzoea kwa miaka mingi.
Madaktari wamekuwa kimbilio la wagonjwa miaka nenda rudi, lakini leo vijana wa
kileo walioidandia fani hiyo sasa wanaonekana sawa na mashetani wekundu ambao wao
kutoa roho siyo ‘issue’. Ni kazi ya dakika moja tu ilimradi wanapata ujira wao.
Iweje madaktari hao wajione kwamba ndio wanastahili kupata malipo makubwa zaidi
eti kwa kuwa tu wamesomea taaluma
njia fulani na uhai wa binadamu na kusahau kwamba kada zote ni muhimu na
zinazotegemeana katika kuendesha maisha ama maendeleo ya nchi?
Ni wasomi wa namna gani ambao wanajitanabaisha kwa ujinga wa mambo ambayo hata
watoto wa chekechea wanaweza kuelewa baya na zuri kabla ya kuchukua uamuzi wa
hovyo
Uhakika ni kwamba
kwenda Ofisi Kuu na wakiwa njiani lazima wangekumbana na dharuba ya mawe na
marungu yanayokwenda sambamba na bakora kwani hakuna mwananchi anayekubaliana na
‘watoa roho’ (baada ya kugoma) hao
ambao wanajali zaidi ubinafsi wa matumbo
ya wategemezi wao na kupuuza uhai wa ndugu zao unaopotea kutokana na uamuzi wa
kijinga.
Taarifa ambazo nadhani hata Afande Tibaigana hakuwa nazo ni kwamba baadhi ya
wananchi walikuwa tayari wameandaa bakora kuwacharaza madakatari hao wakiwa njiani
kuelekea Ikulu kuwasumbua viongozi wetu ambao wako katika mchakato mzito wa
kupambanua mustakabali wa nchi hii.
Kejeli zaidi zilijitokeza juzi kwa madaktari hao kudai kwamba hawana wasiwasi na
ajira zao kwani serikali haina ubavu wala thubutu ya kuwafuta kazi. Kwamba hakuna
wa kufanya kazi zao ikiwa watafukuzwa! Kumbe watu hao wanajua umuhimu wao kwa
maisha ya Watanzania, sasa iweje waendekeze maamuzi ya hovyo na kijinga namna hiyo
huku wakicheza muziki nje ya wodi za wagonjwa?
Wengi tunafahamu kwamba ingekuwa enzi za ujamaa uliokomaa na ukomunisti uliofikia
kikomo, madaktari hao wasingekuwa na thubutu hiyo kwani kufumba na kufumbua
‘wangemwagika’ Wachina na Wacuba kama mvua kuwatibu wagonjwa wetu na kuwatupilia
mbali hao wanaojidai na taaluma
Ninachowaomba madaktari ni kwamba, pamoja na kuwa na hoja zenye mwangwi wa uhalali
wa madai
wao wanavyodhani kwamba wanaikomoa serikali ambayo kimsingi haiumwi. Wanaoumwa ni
binadamu
Wanapaswa kufikiria upya njia nzuri zaidi za kudai ujira mkubwa badala ya kuvaa
roho ya paku na kuruhusu binadamu wenzao kufa eti kwa kuwa wanaomba mlo zaidi kwa
matumbo
Mijadala ndiyo daima imekuwa njia ya kistaarabu kwa watu wasomi
waungwana kutafuta suluhu ya
matatizo
huku wahusika wakishuhudia watu wakiteseka na kufa, huku wagomaji wakicheza dansi.
Unyama gani huo mlionao nyie mnaoitwa madaktari!
Bodi iondoe adha hii ya wanafunzi kuhemea mikopo
KWA mara nyingine katika kipindi kisichozidi miezi miwili, Bodi ya Mikopo kwa
Wanafunzi wa Elimu ya Juu nchini imelazimika kushinikizwa na wanafunzi ndipo
iwapatie mikopo
Baada ya lililowahusu wanafunzi wa
Chuo Kikuu cha
miwili iliyopita, tukio la hivi sasa ni la juzi ambapo baadhi ya wanafunzi wa Chuo
cha Uhasibu Arusha (IAA) walisafiri kwa mabasi madogo manne waliyokodi kutoka
chuoni kwao mjini Arusha hadi
katika ofisi za bodi hiyo mjini
kufuatilia mikopo
Walipowasili eneo la ofisi hizo juzi alfajiri, walianza ufuatiliaji kwa maofisa
husika baada ya saa za kazi kuanza, huku wakiahidi kukesha hapo mpaka baada ya
kukamilishiwa malipo
kila mwanafunzi alichangia msafara huo sh. 3,000, na kwamba wanafunzi wapatao 100
ndio waliotumwa
Tunafarijika kwa taarifa
iliyotolewa na uongozi wa Bodi hiyo kwamba suala
lilikuwa tayari linashughulikiwa baada ya kuwasiliana na wanafunzi hao, na kwamba
lengo lilikuwa ni kuhakikisha fedha hizo, kiasi cha sh. milioni 168, zinalipwa
jana na hivyo wanafunzi kurejea chuoni.
Lakini pamoja na kufarijika kwa taarifa hiyo, inashangaza kwa nini utaratibu wa
utoaji mikopo hiyo uwe ni wa kusuasua namna hiyo, ambapo hatima yake ni kuwapa
usumbufu wanafunzi ambao wanastahili kuwa vyuoni wakiendelea na masomo bila ya
bughudha
Wakati utekelezaji wa utaratibu huu mpya wa kuwapatia mikopo wanafunzi wa elimu ya
juu unaanza Septemba, mwaka huu, Bodi ilieleza katika taarifa yake namna uitikiaji
wa wanafunzi kujaza na kuwasilisha fomu ulivyokuwa ukienda taratibu mno, na
kulazimika kuwahimiza kuharakisha kujaza fomu hizo ili kuepuka usumbufu.
Lakini kinyume kabisa na taarifa hiyo ya awali ya Bodi, uongozi hivi sasa unaeleza
kwamba wanafunzi wengi mno wamejitokeza katika vyuo mbalimbali kuomba mikopo zaidi
ya ilivyokuwa imekisiwa. Waliojitokeza wanatajwa kuwa ni 37,500 ambapo waliokisiwa
ni 35,194, hali ambayo imeelezwa kuwa inahitaji maandalizi ya ziada kufanikisha
utoaji wa mikopo.
Haja ya kuwepo maandalizi ya ziada ni sawa, lakini maandalizi hayo yazingatie hali
halisi ya umuhimu wa mikopo hiyo kwa mahitaji ya wanafunzi. Fedha zinazotolewa ni
pamoja na za chakula kwa muda ambao wanafunzi watakuwa vyuoni, ada na vitabu.
Yote hayo ni mahitaji muhimu, mengine yakiwa ni ya lazima na ya msingi kwa
binadamu
hawatarajiwi kufanya miujiza kujitosheleza katika mahitaji hayo, hasa ikizingatiwa
halisi ya uduni wa mapato ziliyonayo familia nyingi katika nchi yetu. Matokeo yake
ni kuwaweka wanafunzi katika uwezekano wa kubangaiza huku na kule, wakati mwingine
kuwa katika hatari ya kujiingiza katika vitendo visivyofaa.
Kwamba Bodi inakiri idadi ya wanafunzi waliojitokeza kuomba mikopo ni zaidi ya
ilivyotarajiwa, tulidhani ingekuwa busara kwa Bodi hiyo kuwa na mkakati maalum wa
kutekeleza majukumu yake, ikiwa pamoja na kufanya kazi kwa wakati wa ziada.
Ushughulikiaji maombi mengi namna hiyo lazima ukabiliwe kwa kukusanya nguvu zaidi
na muda mrefu zaidi kwa watendaji wake ili kuwaondolea matatizo wanafunzi. Bila
kufanya hivyo tutazidi kushuhudia ofisi za Bodi zikifurika wanafunzi kutoka chuo
kimoja hadi kingine kila kukicha. Wanafunzi waepushwe na adha hii.