UHURU 16.11.2005
Karume
atangaza baraza la mawaziri
Na Mwandishi Wetu
RAIS wa
lenye mawaziri 13, wakiwemo wawili wapya ambao wanashika nafasi za uwaziri kwa
mara ya kwanza.
Katika Baraza
wa Naibu Waziri katika Baraza lililopita na mawaziri wawili wamerudi tena, baada
ya kuwa nje kwa
muda.
Mawaziri wapya
kabisa ni Asha Abdalla Juma, ambaye anakuwa Waziri wa Maendeleo ya
Vijana, Wanawake
na Watoto, na Zainab Omar Mohammed, anayekuwa Waziri wa Nchi
Ofisi ya Rais
(Kazi Maalum).
Aliyepandishwa ni
Sultan Mohammed Mugheiry, aliyekuwa Naibu Waziri wa Afya katika
Baraza
lililopita, ambaye anakuwa waziri mpya wa wizara hiyo, ambayo sasa inaitwa
Wizara ya Afya na
Ustawi wa Jamii.
Taarifa
iliyotolewa na Ikulu ya Zanzibar jana na gazeti hili kupata nakala yake,
ilionyesha kuwa
mawaziri waliyorejea katika Baraza hilo la mawaziri, ambao
waliwahi kuwa
mawaziri huko nyuma, ni Ramadhan Abdalla Shaaban na Amina Salum
Ali.
Ramadhan aliwahi
kuwa Waziri wa Habari, Utangazaji, Utamaduni na Televisheni na
Waziri wa Nchi
katika Ofisi ya Makamu wa Rais, wakati Amina Salum Ali, alikuwa
Waziri wa Fedha katika serikali ya awamu ya tano ya Dk. Salmin Amour.
Kwa mujibu wa
taarifa hiyo, Baraza la Mawaziri la sasa lina wizara 13, likiwa
limelizidi
lililopita kwa wizara moja. Lilikuwa na wizara 12. Pia, imeonyesha
kuwa mawaziri
watatu wa zamani wameachwa.
Waliyoachwa ni
Mussa Ame Silima, aliyekuwa Waziri wa Biashara, Viwanda na Masoko,
Mohammed Aboud,
aliyekuwa Waziri wa Kilimo na Mifugo na Salum Juma Othman,
aliyekuwa Waziri
wa Afya na Utibabu.
Mawaziri saba
wameendelea kushika nafasi hizo kutoka katika Baraza la Mawaziri
liliopita, ingawa
baadhi wamebadilishwa wizara.
Mawaziri hao ni
Ali Juma Shamuhuna, Suleiman Othman Nyanga, Mansoor Yussuf Himid,
Dk. Mwinyihaji
Makame Mwadini, Burhan Saadat Haji, Samia Suluhu Hassan na Haroun
Ali Suleiman.
Baraza kamili la
mawaziri lililotangazwa jana na wizara zao katika mabano ni Ali
Juma Shamuhuna
(Naibu Waziri Kiongozi na Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo);
Amina Salum Ali (Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Kiongozi); Dk. Mwinyihaji Makame
Mwadini (Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,
anayeshughulikia Fedha na Uchumi).
Zainab Omar Mohammed (Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Kazi Maalum); Haroun Ali
Suleiman (Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali); Sultan Mohammed Mugheiry (Waziri
wa Afya na Ustawi wa Jamii); Burhan Saadat Haji (Waziri wa Kilimo, Mifugo na
Mazingira).
Mawaziri wengine ni Brigedia Jenerali mstaafu Adam Mwakanjuki (Waziri wa
Mawasiliano na Uchukuzi); Suleiman Othman Nyanga (Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais,
Tawala za Mikoa na Vikosi vya SMZ); Mansour Yussuf Himid (Waziri wa Maji, Ujenzi,
Nishati na Ardhi).
Wengine ni Ramadhan Abdalla Shaaban (Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Katiba na
Utawala Bora); Samia Suluhu Hassan (Waziri wa Utalii, Biashara na Uwekezaji) na
Asha Abdalla Juma (Waziri wa Maendeleo ya Vijana, Wanawake na Watoto).
Uteuzi huo ulianza jana.
‘Wanafunzi walioanguka kwa kunywa dawa walikuwa na njaa
kali’
Na El-hadji Yuusuf, Tabora
WANAFUNZI wapatao 30 walianguka na kupoteza fahamu baada ya kupewa dawa za
kichocho na minyoo kwa sababu walizidiwa nguvu kutokana na kupewa dawa hizo bila
kula.
Juzi wanafunzi wa shule mbalimbali za mjini hapa walipoteza fahamu, mara baada ya
kupatiwa dawa za kutibu minyoo na
kichocho. Walizidiwa nguvu na dawa
hizo
kutokana na
kupatiwa dawa hizo bila ya kula chakula.
Kaimu Mganga Mkuu
wa Mkoa wa Tabora, Dk. Amos Nsheha, alisema kuwa kwa mujibu wa
Mwongozo kuhusu utoaji wa dawa hizo, hazikupaswa kutolewa kwa watoto bila ya
kupatiwa lishe ya kutosha kwanza.
Dawa zilizotolewa kwa wanafunzi hao ni aina ya Mebendazole kwa ajili ya kutibu
minyoo na Praziquentel ambayo hutibu kichocho, na kwamba inaelezwa kuwa na nguvu
nyingi na ambayo inaweza kusababisha madhara iwapo mtumiaji wake atakuwa hajapata
chakula na kushiba.
Alisema kuwa katika shule ambazo zoezi
hakukuwa na athari kubwa zilizotokea, katika kampeni maalum ya kuutokomeza
ugonjwa wa kichocho na minyoo hapa nchini.
Akiongea na waandishi wa habari, mara baada ya kumalizika kwa kikao cha dharura,
kilichoitishwa hospitalini hapo kwa ajili ya kutathmini hali iliyokuwa, Dk.
Nsheha, aliyekuwa sambamba na Mganga Mkuu wa Manispaa ya Tabora, Dk. Madaraka
Luganga, alisema kuwa watoto waliolazwa kutokana na tatizo
vizuri.
Alisema kuwa
mpango huo uliendeshwa katika mazingira ya tiba ya ugonjwa huo kwa
watoto wengi ili
kuweza kupunguza madhara ya minyoo kati ya aina tatu kwa watoto
na kutibu ugonjwa
wa kichocho ambao una madhara makubwa kwa binadamu.
Hata hivyo,
alikiri kuwepo kwa mkanganyiko kuhusu namna ya kuwapa dawa watoto
hao, kwa sababu
njia kuu iliyotumika ni ile ya kuwapa dawa baada ya kupimwa
urefu, badala ya
kuzingatia uzito halisi kwa watoto.
Alisema kuwa
shule nyingi zilizotekeleza tiba hiyo, hazikuwa na mizani kitu
ambacho alisema
kuwa wengi wao waliamua kuwapa tiba kwa kuzingatia urefu tu.
Dk. Nsheha,
alisema kuwa dawa hizo hazina madhara kabisa kwa watoto iwapo
wangepatiwa baada
ya kupata chakula na kushiba, na kwamba watoto waliopatiwa dawa
hizo baada ya kula
hawakuwa na athari zozote.
Alisema kuwa kati
ya shule 20 zilizoendesha mpango huo juzi, katika manispaa ya
Tabora, ni
wanafunzi wa shule nane ndio waliopata madhara hayo na hiyo inaashiria
kuwa kulikuwa na uzembe
uliofanywa na baadhi ya walimu.
Akijibu swali ni
kwanini dawa hizo zilitolewa na walimu badala ya watumishi wa
Idara ya Afya,
alisema kuwa hilo lilitokana na Mwongozo wa Serikali wa mwaka 2002
na kwamba
lilifanyika kutokana na manispaa kuwa na watumishi wachache wa idara
hiyo.
Dk. Nsheha, hata
hivyo, alisema kuwa watoto wenye magonjwa sugu, kama ukimwi,
kansa, ‘sickle
cells’, kifua kikuu na mengineyo, hawakupatiwa dawa hizo, kutokana
na Mwongozo kuzuia
wasipatiwe ili kuepusha madhara kwao.
Naye Mkuu wa
Wilaya ya Tabora, Alhaji Mussa Samizi, alisema dawa hizo hazina
madhara yeyote,
kama inavyovumishwa na watu mitaani, lakini alikiri kuwa madhara
yaliyotokeza
yalitokana na uzembe wa dhahiri.
Alisema kuwa
walimu waliobainika kufanya uzembe huo watachukuliwa hatua za
kinidhamu, kwa
sababu hawakutakiwa kuwapa watoto dawa hizo bila ya kuwapa chakula
kwanza, kama
Mwongozo unavyosema.
Aliwataka wazazi
na walezi wa watoto wanaosoma katika shule za msingi nchini,
wasihofu kutokana
na zoezi hilo, kwa sababu halina madhara na kuomba ushirikiano
wao ili kutokomeza
magonjwa ya kichocho na minyoo kwa vijana ili kuwafanya wawe
na afya bora.
Kwa upande wake,
Dk. Luganga, alisema kuwa dawa hizo ni za kutibu minyoo na
kichocho na siyo chanjo
dawa hizo pamoja na wazazi na walezi wao na kuripotiwa na vyombo vya habari.
Wizara ya Afya kwa upande wake, hadi jana jioni ilikuwa ikisubiri taarifa rasmi
kutoka Tabora.
Ofisa Mawasiliano
wa Wizara hiyo, Nsacris Mwamwaja alisema jana kwamba Wizara ya
Afya iliposikia
kupitia magazeti iliwasiliana na Ofisi ya Katibu Tawala Mkoa wa
Tabora ili kupata
taarifa zaidi na kwamba hadi jioni ilikuwa bado haijafika.
Mwamwaja alisema
kwa kawaida vidonge vinavyotolewa ni salama na kwamba vipo
kwenye mpango
maalum wa kupambana na magonjwa na ulizinduliwa na Waziri Mkuu
Frederick Sumaye
mjini Dodoma.
Wataoipigia
kura CUF hawaijui tabia yake - Mangula
Na Bashir Nkoromo,
Mbeya
KATIBU Mkuu wa
Chama Cha Mapinduzi Philip Mangula amesema watakaoipigia kura CUF
ni wale ambao
hawakijui chama hicho na tabia zake.
Mangula alisema
hayo juzi wakati akihutubia mkutano wa kampeni kwa ajili ya
mgombea ubunge wa
jimbo la Mbarali, Estheria Kilasi, uliofanyika katika Kata ya
Madibira mkoani
hapa.
Alisema kwa
Mtanzania mpenda amani anayeijua CUF na kuzifahamu fika tabia za
chama hicho, kamwe
hatathubutu kupigia kura mgombea wake yeyote katika uchaguzi
utakaofanyika
Desemba 14, mwaka huu.
Mangula alisema
CUF ni chama kilichobobea katika kujenga uhasama, ugomvi na
hamasa za vita na
umwagaji damu.
Alitoa mifano
kadhaa kwamba, wafuasi wa CUF waliwahi kuchinja hadi kumuua afisa
wa polisi huko
Pemba, pia wamewahi kuua kwa kumchomea katika nyumba mwanamke
mkereketwa wa CCM
na watoto wanne mjini Dar es Salaam.
Mangula alisema
wafuasi wa CUF wamekuwa wakifanya maandamano haramu Dar es Salaam
na kusababisha
maduka kuporwa na pia tukio la hivi karibuni la waandishi wa
habari kushambuliwa
na kuharibiwa vifaa vya kazi kwenye makao makuu ya CUF,
Buguruni.
Aliwataka
wananchi wa Mbarali na Watanzania kwa jumla kuipigia kura CCM kwa
sababu ndicho
Chama chenye tabia makini na ujenzi wa amani na utulivu tangu nchi
kupata uhuru.
Mangula alisema
kutokana na umakini wake CCM imeweza kuweka mazingira bora ya
wananchi kujiletea
maendeleo ambapo sasa yanaonekana kila kona ya Tanzania.
“Kazi ya serikali
si kuleta maendeleo. Maendeleo yanaletwa na wananchi huku kazi
ya serikali ikiwa
ni kuwajengea mazingira bora ya kufanya hivyo,” alisema
Mangula.
Alisema miongoni
mwa mazingira bora ni pamoja na hali ya utulivu na amani ambavyo
vinawawezesha
Watanzania kufanya shughuli zao bila wasiwasi na kukumbusha kuwa
mahali penye
vurugu na vita hakuna maendeleo yanayoweza kupatikana.
Mangula alisema
mazingira mengine ni uboreshaji wa miundombinu kama vile
barabara,
mawasiliano ya simu na huduma nyingine za kijamii.
Mapema kabla ya
mkutano huo, Mangula alizungumza na kamati ya wilaya ya Mbarali
ambapo ilimweleza
kuwa ina matumaini makubwa ya kupata ushindi katika uchaguzi wa
Desemba 14.
Baadaye alikwenda
kata ya Chimala ambako alihutubia mkutano wa ndani na kumpokea
muasisi wa TLP na
Katibu Kata wa chama hicho Kata ya Chimala, Isaya Mwakihwaya
ambaye alirejea
CCM na mkewe na wanachama wengine zaidi ya 20.
Maofisa Uhusiano
Mamlaka za maji watakiwa wawe kiungo
Na Mwandishi Wetu
MAOFISA Uhusiano
wa Mamlaka za Majisafi na Majitaka nchini wametakiwa kuwa kiungo
kati ya mamlaka na
umma katika kuhakikisha malengo ya mamlaka hizo yanafikiwa
ikiwa ni pamoja na
kuyatangaza kwa wadau wengine.
Wito huo
ulitolewa jana na Waziri wa Maji na Maendeleo ya Mifugo, Edward Lowassa,
katika hotuba yake
ya ufunguzi wa mkutano wa nne na uzinduzi wa Umoja wa
Waelimishaji na
Uhamasishaji Umma Sekta ya Maji (WEMMA).
WEMMA unaundwa na
maofisa uhusiano wa mamlaka za Majisafi na Majitaka nchini.
Uzinduzi huo
ulifanyika katika ukumbi wa mikutano wa Millenium Tower mjini Dar es
Salaam na
kuhudhuriwa na maofisa kadhaa wa mamlaka hizo.
Waziri Lowassa
alisema hilo linatokana na ukweli kwamba kupitia maofisa hao,
mamlaka hizo
zimeweza kuwasogeza karibu wadau mbalimbali wakiwemo wateja.
Alisema hilo
lilikwenda sambamba na kuongeza mwitikio wa wateja kwa mamlaka za
maji ikiwa ni
pamoja na kuwahamasisha kulipia ankara za maji na kuwashirikisha
katika upanuzi wa
huduma za majisafi na majitaka.
Waziri Lowassa
aliyataja mafanikio mengine ya sekta ya maji kuwa ni ongezeko la
makusanyo ya
mapato ya Mamlaka za Maji Mijini kutoka sh. milioni
400 mwaka 1995
hadi sh. bilioni 17.9 kufikia mwaka jana.
Alisema ongezeko
hilo kwa kiwango kikubwa limeziwezesha mamlaka hizo kujiendesha
kwa sehemu kubwa.
Pia alisema hadi
kufikia Juni mwaka huu, kamati za maji 9,283 ziliundwa katika
vijiji na kati
hizo kamati 8,099 zilikuwa zimeanzisha mifuko ya maji yenye
thamani ya sh. bilioni 1.07.
Mapema akitoa
maelezo ya WEMMA, Katibu wa umoja huo, Sebastian Warioba alisema
malengo ya
uanzishaji wa WEMMA umelenga katika kuelimisha na kuhamasisha umma
kuhusu masuala
yanayohusu usambazaji wa maji na uondoshaji wa majitaka katika
mazingira yaliyo
safi, salama na endelevu.
Pia umelenga
katika kujenga na kuendeleza mahusiano kati ya wadau wa sekta ya
maji ndani na nje
ya nchi.
Mkenya
akamatwa Arusha kwa wizi wa gari
Na Mohammed
Mhina, wa Jeshi la Polisi – Arusha
MKENYA
anashilikiwa na polisi mjini Arusha kwa tuhuma za kujihusisha na wizi wa
magari.
Kamanda wa Polisi
mkoa wa Arusha James Kombe, alisema jana kuwa mtuhumiwa huyo
Paulo Osumba
Kaserah (41) alikamatwa na Polisi akiwa na gari aina ya Toyota Hilux
iliyosajiliwa hapa
nchini kwa namba TZS 3809 ambazo zilibainika kuwa zilikuwa za
bandia.
Alisema kuwa
baada ya uchunguzi wa awali, Polisi ilibaini kuwa namba halali za
gari hiyo zilikuwa
ni KAR. 948T iliyosajiliwa nchini Kenya ambazo pia zilikuwa
zimeandikwa katika
vioo vyake na kubandikwa stika ili zisiweze kuonekana kwa
urahisi.
Kamanda Kombe
alisema Polisi pia walimkuta mtuhumiwa akiwa na hati nne za
kusafiria zikiwa
na majina tofauti na moja kati ya hizo ilikuwa imetolewa nchini
Tanzania na
nyingine tatu zilitolewa nchini Kenya.
Alisema
imebainika pia kuwa mtuhumiwa huyo alikuwa akitumia hati mbili
zilizotolewa Kenya
na zenye majina na picha tofauti kwa kusafiria katika nchi
mbali mbali.
Alisema katika
hati nyingine mtuhumiwa Osumba, alikuwa akitumia jina la Rojers
Ochieng Okuta.
Alisema polisi
kwa kushirikiana na Idara ya Uhamiaji nchini Kenya na Tanzania,
inawasaka watu
watatu wenye hati za kusafiria alizokutwanazo mtuhumiwa huyo.
Aliwataja watu
wanaotafutwa kuwa ni Alan Zomboko Bongonya (31), mwenye pasi namba
AB 048106
iliyotolewa hapa nchini, Beatris Gaseri Muthamia (25), mwenye pasi
nambari A. 687034
na Rojers Ocheng Okuta (21), mwenye pasi nambari A. 808100 zote
zilizotolewa
nchini Kenya katika vipindi tofauti.
Wakati huo huo
Majeshi ya Polisi Tanzania na Rwanda yamekubaliana kudumisha
ushirikiano na
uhusiano uliopo kwa nia ya kuimarisha ulinzi na usalama kwa nchi
za Maziwa Makuu.
Makubaliano hayo
yamefikiwa na Wakuu wa majeshi hayo Inspakta Jenerali Omari
Mahita wa
Tanzania na Kamishna Jenerali Andrew Rwigamba wa Rwanda, wakati wa
hafla fupi
iliyofanyika jana usiku kwenye Bwalo la Polisi Oysterbay.
Akizungumza
katika hafla hiyo, Mahita alisema ushirikiano uliopo kwa nchi hizi
mbili utaziwezesha
nchi hizi za Maziwa Makuu na ukanda wa Pembe ya Afrika kuweza
kudhibiti uhalifu
wa Kimataifa kwa pamoja.
Kwa upande wake
Kamishna Jenerali Rwigamba ambaye anaitembelea Tanzania kwa ziara
ya kikazi, amesema
kuwa Rwanda itaendelea kujifunza mengi kutoka kwa Jeshi la
Polisi nchini
Tanzania na kuhakikisha kuwa uhusiano na ushirikiano uliopo
unadumu.
Stashahada
fani ya ustawi wa jamii kuanza kutolewa mwaka ujao
Na Mwandishi Wetu
TAASISI ya Ustawi
wa jamii (ISW) itaanza kutoa shahada katika fani ya Ustawi wa
Jamii kuanzia
mwaka kesho ikiwa ni moja ya jitihada za kuimarisha elimu ya jamii
nchini.
Kaimu Mkurugenzi
Mkuu wa Taasisi hiyo Dk. Hosea Rwegoshora alisema hayo jana
alipozungumza na waandishi wa habari kuelezea maendeleo na mikakati mbalimbali ya
kuboresha taasisi
yake pamoja na maandalizi ya mahafali ya 29 yanayotarajiwa
kufanyika Ijumaa
ijayo.
Mgeni rasmi
wakati wa mahafali atakuwa Waziri wa Kazi, Maendeleo ya Vijana na
Michezo Profesa
Juma Kapuya na kwamba wahitimu 191 watapatiwa shahada za juu
,
shahada za kawaida
na vyeti mbalimbali.
Dk.Rwegoshora
alisema taasisi yake itaanza kutoa shahada ya ustawi mwaka
2006/2007 baada
ya kukamilisha maandalizi ambayo yanasimamiwa na Baraza la
Mitihani la Taifa
(NECTA).
“Tuliwaandikia
NECTA nia yetu na mipango ya utekelezaji katika kuanzisha masomo
ya shahada, nayo
NECTA ilipitia na kutoa ushauri wake wa mwisho ambao unafanyiwa
kazi ili kuanza
kufundisha masomo ya shahada,’’ alisema.
Alisema taasisi
yake itakuwa ya tatu nchini kutoa shahada maalum ambazo
zinatolewa na vyuo
vya kati badala ya vyuo vikuu pekee.
Vyuo vingine
ambavyo kwa sasa vinatoa shahada ni pamoja na Chuo cha Mipango
Dodoma na Chuo
cha Ufundi Dar es Salaam.
Taasisi ya ustawi
wa jamii ilianzishwa mwaka 1974 ikiwa na lengo la kufundisha
masuala ya ustawi
wa jamii, lakini ilizidi kuongeza kozi kulingana na mahitaji
ambapo sasa zipo
zaidi ya kozi saba za muda tofauti wa kusomea.
Dk. Rwegoshora
alisema taasisi hiyo pamoja na kozi nyingi zinazohusu ustawi wa
jamii, kwa sasa
inafundisha pia kozi juu ya masuala ya menejimenti ya rasilimali
watu ambayo pia
inafundishwa kwenye Chuo Kikuu cha Mzumbe.
Alisema taasisi
yake kwa sasa inao wanafunzi 900 ukilinganisha na wanafunzi 24
waliofungua chuo
wakati kinaanza.
Wanafunzi 1,470
walimaliza masomo kwenye taasisi hiyo na walitunukiwa vyeti na
stashahada za fani
mbalimbali. Waliotunukiwa stashahada za juu, kawaida na vyeti
ni pamoja na
wanafunzi wa nje 91 kutoka Afrika Kuisni, Lesotho, Swaziland,
Burundi, Kenya,
Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo, Gambia, Namibia na Sudan.
Wakati huohuo
Chuo cha sayansi jamii cha Kivukoni (KASS) kinatarajia kuwa na
mahafali yake siku
ya Novemba 26 mwaka huu ambapo wanafunzi 133 watatunukiwa
vyeti na
stashahada katika fani ya jinsia, sayansi jamii, na maendeleo ya uchumi.
Taarifa
iliyotolewa jana ilisema Rais Benjamin Mkapa anatarajiwa kuwa mgeni rasmi
kwenye mahafali
hayo na kwamba wahitimu saba watatunukiwa stashahada katika fani
ya uchumi wakati
wengine 60 watapata stashahada za sayansi jamii na wengine 37
watatunukiwa
stashahada za jinsia wakati wahitimu 29 watapatiwa vyeti vya fani ya
kazi za vijana.
Wengine wanne
Wajitoa CHADEMA Moshi Vijijini
Na Rodrick
Makundi,Moshi
KAMBI ya upinzani
katika jimbo la uchaguzi la Moshi Vijijini imeendelea kupata
pigo baada ya
wanachama wanne wa Chadema kujitoa kwenye chama hicho na kujiunga
na Chama Cha
Mapinduzi.
Wanachama
waliohama Chadema na kurejea CCM ni Mwenyekiti wa kitongoji cha Kifumbu
kata ya Uru Kusini
na Mwenyekiti wa kitongoji cha Okaseni chini, Anthony Komu.
Aidha viongozi wa
Chadema kata ya Mabogini wamerejea CCM ambapo walikabidhi kadi
za chama chao
walichotoka kwa Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Moshi vijijini.
Viongozi
waliorejesha fomu kutoka katika kata hiyo ni pamoja na Mwenyekiti wa
Chadema,Laurence Mbwambo,katibu wake Ally Mchomvu na katibu
msaidizi Sadick
Lukware ambao
walikuwa wahamasishaji wakubwa wa mgombea udiwani wa kata hiyo.
Wanachama hao kwa
pamoja walirejesha kadi zao kwa Mwenyekiti wa CCM,wilaya
ya
Moshi Vijijini
ambaye aliwapokea na kuwakaribisha kuwa wanachama wapya wa CCM.
Mwenyekiti wa CCM
wilaya ya Moshi vijijini Gabriel Masenga mara baada ya
kuwapokea
wanachama hao aliwataka kushirikiana kwa pamoja kwa kuwahamasisha
wanachama wengine
kuendelea kujiunga na CCM ili kuharakisha utekelezaji wa ahadi
za chama.
Wakizungumzia
azma yao ya kujiunga CCM,wanachama wa Mabogini
waliojiengua kutoka
Chadema,walisema uamuzi wao huo umetokana na sera madhubuti za
Chama ambazo
zimeonekana
kulenga kutekeleza ahadi zinazotolewa na wagombea wakati wa kampeni
za awali za chama
hicho kwenye kata hiyo.
“Tunafanya hivyo
kwa kuwa tunatambua kuwa malengo ya wagombea wa CCM,Mheshimiwa
Kikwete,kwa ngazi ya urais,Dk.Cyril Chami kwa ngazi ya ubunge na
Rodgers Mmary
kwa ngazi ya
udiwani kata ya Mabogini ni ya kuwaletea maendeleo wananchi wa
Tanzania,jimbo la Moshi Vijijini na hasa katika kata yetu ya
Mabogini”alisema
sehemu ya taarifa
hiyo.
Kwa upande wake
mwenyekiti wa Chadema kitongoji cha Kifumbu alisema dhamira yake
ya kurejea
CCM,inatokana na kukosa ushirikiano baina yake na chama hivyo kukosa
matumaini ya
kupata ushindi katika eneo lake na hata kwa jimbo.
Kwa upande wake
mgombea wa CCM,ngazi ya ubunge jimboni humo Dk.Cyril
Chami
aliwapongeza
wanachama hao kujiunga CCM na akawataka kueneza sera za chama.
Aliongeza kuwa
wanachama waliorejea CCM,wanatarajiwa kupewa mkono wa
pongezi na
Waziri Mkuu,Frederick Sumaye ambaye pia ni mlezi wa chama mkoa wa
Kilimanjaro
wakati wa ziara
yake kesho (leo) katika majimbo ya Moshi Vijijini na Vunjo
wilayani humo.
Waziri Mkuu
anatarajiwa kufanya ziara ya siku mbili mkoani hapa
Kilimanjaro,katika majimbo ya Moshi Vijijini ambako atamnadi mgombea
ubunge wa
jimbo hilo Dk.
Chami na katika jimbo la Vunjo, Sumaye atamnadi mgombea ubunge wa
CCM Aloyce Kimaro wa jimboni humo.
Pia aliyekuwa mgombea ubunge kupitia CUF,Steven Nguma ambaye alijitoa kugombea na
kujiunga na CCM,wagombea udiwani wa TLP na Chadema waliojitoa watakutana na
Sumaye kwa kukaribishwa rasmi katika Chama.
Mchanga wenye madini ya Almasi waibwa Mwadui
Kundi la watu
zaidi ya 100 lahusika
KUNDI la watu
zaidi ya 100 limevamia mgodi wa almasi wa Mwadui mkoani Shinyanga
na kuiba mchanga
wenye almasi unaosadikiwa kuwa na thamani ya mabilioni ya fedha.
Akizungumza na
PST ofisini kwake jana Kamanda wa Polisi mkoani Shinyanga Abdallah
Mssika alisema
kundi hilo pia limemuua mlinzi wa Kampuni ya Ulinzi ya Grey
Security Guard inayolinda mgodi huo.
Hata hivyo, Kamanda Mssika alisema katika msako uliofanyika hakuna madini
yaliyokamatwa katika mchanga ulioibwa katika uvamizi huo.
Kuhusiana na tukio
kuhusika na uvamizi huo na msako kwa watu wengine bado unaendelea.
Majina ya watu waliokamatwa yamehifadhiwa kwa sababu za uchuguzi zaidi wa
kipolisi.
Kwa mujibu wa taarifa ya polisi
kundi
lilifanya uvamizi
huo saa 12.30 jioni Alhamis iliyopita eneo la New Almasi namba
10 ndani ya mgodi
wa Mwadui.
Kundi la watu hao
huku wakiwa wamebeba, mapanga, marungu, makombeo na machekeche
ya mchanga wa
almasi lilivamia eneo hilo kwa lengo la kuiba mchanga wenye almasi.
Mssika alisema,
mlinzi aliyemtaja kuwa ni Aden Rage (29) akiwa doria alipoliona
kundi hilo la
wavamizi likivuka eneo la uzio wa mgodi alipiga risasi moja hewani
kuwatishia kwa ili
kuwatawanya lakini waliendelea kumfuata na kumkabili mlinzi
huyo.
Alisema Rage
alipoona wanaendelea kumkabili alijaribu kufyatua tena risasi ya
pili ili
kuwatanyawa lakini kwa bahati mbaya risasi hiyo ilikwama katika bunduki
yake aina ya
shotgun.
Kiongozi huyo wa
polisi alisema kitendo hicho kilitoa mwanya kwa kundi hilo
kumvamia na kuanza
kumpiga na kumchoma na kitu chenye ncha kali kifuani upande wa
kulia na
kusababisha kifo chake.
Wavamizi baada ya
kumuua, alisema Mssika walivunja kitako cha bunduki yake na
kuitupa bunduki
kando ya maiti na kisha kuanza kusomba mchanga unaosadikiwa kuwa
na thamani ya
mabilioni ya shilingi uliokuwa katika mashine moja ya kusomba
mchanga.
Kamanda alisema
wavamizi waliusomba mchanga uliokuwa katika mashine hiyo maarufu
kama kijiko"
kilichokuwa kikiendeshwa na mfanyakazi wa
mgodi Aloyce Zengo
(40) na kutoweka nao nje ya mgodi .
Serikali
kuboresha maslahi ya watumishi wa umma
Na Mwandishi
Maalum
SERIKALI
imedhamiria kuboresha mishahara na maslahi ya watumishi wa umma kufikia
kiwango cha kuweza
kujiwekea akiba kwa ajili ya maendeleo yao.
Hayo
yalibainishwa na Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi
wa Umma, George
Yambesi, alipokuwa akifungua mafunzo ya namna ya kuandaa makisio
ya ikama na bajeti
ya mishahara ya watumishi wa umma kwa maofisa utumishi wa
wizara, idara,
wakala na halmashauri za miji na wilaya.
Yembesi katika
mafunzo hayo yanayoendeshwa katika Chuo cha Ufundi Stadi -VETA,
mjini Morogoro
alisema nia hiyo ya serikali, itaweza kutekelezeka endepo ukuaji
wa uchumi wa taifa
utafikia kiwango cha juu katika kuchangia pato la taifa hivyo
kuwezesha serikali
kulipa mishahara na maslahi bora zaidi kwa watumishi wa umma.
Alisema kwa
kuzingatia hilo, ndio maana Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa
Umma, kupitia
Programu ya Kuboresha Utumishi wa Umma, imeamua kuendesha mafunzo
hayo kwa watendaji
wake ili kiasi kidogo kilichopo kiweze kutumika vizuri na
kutoa motisha kwa
watumishi hivyo kuwajengea ari.
Yambesi alikiri
kuwa tathmini ya hali halisi ilivyo hadi sasa imeonyesha bado
kuna baadhi ya
matatizo katika utendaji wa shughuli za utumishi wa umma ikiwemo,
uwajibikaji
usioridhisha katika kushughulikia maslahi ya watumishi wapya na
wanaopandishwa
vyeo.
Naibu katibu mkuu
huyo alisema kufuatia hali hiyo, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya
Utumishi wa Umma
tayari imetoa maelekezo kwa watumishi wote wenye dhamana za
kushughulikia
malipo ya mishahara kuhakikisha malipo yanafanyika bila
ucheleweshaji usio
wa lazima.
Naye Naibu
Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Misaada ya Kimaendeleo la Japan JICA
waliofadhili
mafunzo hayo, Naoki Takahashi ameihakikishia Serikali ya Tanzania
kuendelea
kufaidika na ufadhili wao katika programu mbalimbali za maendeleo
ikiwemo ya
Kuboresha Utumishi wa Umma (PSRP).
Mtendaji Mkuu wa Chuo cha Utumishi wa Umma, Dk. Richard Kavura, alisema chuo
chake kimefikia kiwango cha juu katika utoaji wa mafunzo ya menejimenti na
utawala kwa kada ya kati na juu sio tu kwa watumishi wa umma, bali pia hata
taasisi binafsi.
Mafunzo hayo yatahusisha maofisa zaidi ya 400 yataendeshwa kwa awamu 4 za maofisa
100 kila awamu na
yameandaliwa na Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma.
CCM Mwanza
yapinga kutenguliwa wenyeviti wake
Na Eva Musiba,
Mwanza
CHAMA Cha
Mapinduzi Mkoa wa Mwanza kimesema kuwa kinapinga hukumu iliyotolewa na
Mahakama ya
Hakimu Mkazi ya kutengua matokeo ya wenyeviti wake wawili wa mitaa
kata ya Mbugani
Halmashauri ya jiji la Mwanza.
Katibu wa CCM
mkoa wa Mwanza Mujuni Kataraia alisema kuwa chama chake
kinawasiliana na
msimamizi wa uchaguzi jiji la Mwanza ili kiweze kupata ufafanuzi
kuhusiana na
uamuzi huo wa mahakama.
Kataraia alisema
chama hicho hakikubaliani maamuzi hayo kwa kuwa
hakikushirikishwa
tangu mwanzo wa kesi na kinashangazwa kesi hiyo kuamuliwa
upande mmoja.
"Nimewasiliana
na msimamizi wa uchaguzi ambaye pia ni mkurugenzi wa jiji la
Mwanza kupata
ufafanuzi kuhusiana na suala hilo,naye amtueleza kuwa
haelewi ni
kwa nini maamuzi
hayo yalifanyika upande mmoja, ndio maana hatukubaliani na
maamuzi hayo na
tunajiandaa kupigania haki yetu," alisema.
Mkurugenzi wa jiji
la Mwanza Paul Baruti ambaye pia ni msimamizi wa uchaguzi
alisema kuwa ofisi
yake inashangazwa na maamuzi ya mahakama ya kusikiliza kesi
hiyo upande mmoja
pasipo kuishirikisha ofisi yake.
Baruti alisema
ofisi yake haikuwahi kuitwa mahakamani wakati wa usikilizwaji wa
shauri hilo
lililokuwa limefunguliwa na chama cha Civic United Front (CUF)
kupinga matokeo ya
uchaguzi wa wenyeviti wa mitaa kata ya Mbugani.
"Baada ya
kutolewa kwa hukumu hiyo nilimuita mwanasheria wa jiji kumuulizia
kuhusiana na
shauri hilo naye alinieleza kuwa ofisi yake haikuwahi kuitwa
mahakamani hivyo
kutokana na utata huo tunafuatilia ili kuweza kuchukua hatua
zaidi,"
alisema msimamizi huyo wa uchaguzi.
Katika hukumu
iliyotolewa, mahakam ilitengua uenyekiti wa mitaa ya Kreluu na
Serengeti kwa
madai kuwa taratibu za uchaguzi zilikiukwa.
Kufuatia kutolewa
kwa huku hiyo tayari msimamizi wa uchaguzi amewaandikia barua
wenyeviti wa mitaa
hiyo Ezekiel Bahebe (Kreluu) na Brown Aunice (Serengeti)
kuacha kufanya
shughuli za uenyekiti wa mtaa hadi pale uchaguzi utakapofanyika
tena.
TRA
Kilimanjaro yasema haina lengo la kufilisi watu
Na Rodrick
Makundi, Moshi
MAMLAKA ya Mapato
(TRA) mkoa wa Kilimanjaro imesema haijalenga kufunga au
kufilisi biashara
katika zoezi lake la kutoza kodi, badala yake imelenga kuwa ni
chombo cha kisasa
cha ukusanyaji wa kodi kwa ajili ya maendeleo ya Taifa.
Katika mkutano
kati ya TRA na wafanyabiashara wa mji wa Moshi, Meneja wa mamlaka
hiyo mkoa Patience
Minga alisema wamedhamiria kujenga uhusiano mzuri na wafanya
biashara ili
waondokane na kukwepa kodi bali watambue kuwa kulipa kodi ni wajibu
wao wa msingi.
Minga aliyasema
hayo juzi katika moja ya semina ambazo zinaendeshwa na TRA,
kupitia idara yake
ya elimu kwa walipa kodi ikiwa ni sehemu ya mkakati wa mamlaka
hiyo katika
kuwaelimisha walipa kodi.
Alisema
wafanyabaishara wakubwa na wadogo mkoani hapa hawana budi kuondoa fikra
potofu
zinazokwamisha uhusiano mzuri kati ya mamlaka na wafanya biashara.
Aliwataka
wafayabiashara hao kutokuwa na woga katika suala zima la ulipaji kodi
badala yake
wawasiliane na ofisi yake ili kupata ufafanuzi juu ya taratibu sahihi
zinazomstahili
mlipa kodi.
Alisema mamlaka
hiyo pia imeanzisha utaratibu wa kuwa na visanduku kwa ajili ya
walipa kodi kutoa
maoni yao juu ya huduma wanazopatiwa na mamlaka hiyo.
Minga alisema
walipa kodi wasioridhika na huduma za TRA, ama kuridhishwa watakuwa
wanajaza maoni yao
katika vikaratasi maalumu na kuviweka katika visanduku hivyo
kwa ajili ya
kufanyiwa kazi na kwamba vitasambazwa katika vituo vyote vya TRA,
wilayani na
mikoni.
Aliwataka
wafayabishara kujenga uaminifu kwani kwa njia hiyo mamlaka hiyo
haitawaona kama
maadui bali marafiki wema wanaostahili katika kuendeleza bishara
zao kwa manufaa ya
Taifa.
Mwili wa
askari aliyeuawa Pemba hatimaye wapatikana
Na Mwandishi Wetu
MWILI wa askari
wa kikosi cha Jeshi la Kujenga Taifa (JKU), Shariff Salum
aliyetekwa nyara
na wananchi wa kijiji cha Piki Pemba umeokotwa ukiwa umefichwa
kwenye kichaka.
Kwa mujibu wa
matangazo ya Idhaa ya Sauti ya Tanzania Zanzibar, mwili huo
uliokotwa jana
kufuatia msako uliofanywa kwa ushirikiano kati ya JKU na polisi.
Salum aliuawa na
watu wanaosadikiwa kuwa ni wafuasi wa CUF baada ya kutekwa nyara
Novemba Mosi,
mwaka huu, kufuatia vurugu zilizotokea Pemba, mara baada ya
uchaguzi mkuu
uliofanyika Oktoba 30.
Uchunguzi wa
awali kutoka hospitali ya Wete ambako mwili wa marehemu ulipelekwa
umebainisha kuwa
askari huyo aliuawa baada ya kupigwa na kitu kizito kichwani.
Mwili wa marehemu
Salum ulikabidhiwa kwa familia yake ambayo wiki iliyopita
ilianua tanga
baada ya kukata tamaa kufuatia kukwama kwa juhudi za kumtafuta.
Salum alikamatwa
na wanakijiji hao baada ya kuziba barabara wakati akirejea
kambini katika
kijiji cha Pujini, mkoa wa Kusini Pemba akitokea Utaani, Kaskazini
Pemba baada ya
pikipiki aliyokuwa akiendesha kushindwa kuendelea na safari
kufuatia magogo
yaliyokuwa yamewekwa barabarani.
Kutokana na
kushindwa kuendelea na safari, Salum aliamua kubaki ili kulinda
pikipiki hiyo,
lakini wanakijiji hao ambao walikuwa wameshikilia mapanga, magongo
na visu
walimkamata na kumpakia kwenye mkokoteni hadi porini ambako inasadikiwa
walimpiga hadi
kufa.
Askari mwenzake
ambaye alikuwa amempakia kwenye pikipiki hiyo alifanikiwa
kutoroka na kutoa
taarifa polisi kuhusu kutekwa kwake, lakini juhudi za kumpata
akiwa hai
zilishindikana kwani katika msako huo polisi walifanikiwa kuukuta
mkokoteni
uliotumika kumbeba ukiwa umetapakaa damu.
Hii ni mara ya
pili kwa wananchi kisiwani Pemba kumwua askari, ambapo mwaka 2001,
askari mwingine
Muslim Mussa alikufa kwa kupigwa panga kichwani katika maandamano
haramu ya CUF
Januari 26, 2001
CCM yakana
kuorodhesha shahada za wapigakura
Na Lilian Mamushu
wa PST, Shinyanga
CHAMA cha
Mapinduzi wilaya ya Shinyanga Mjini, kimesema wajumbe wake wa mashina
hawaorodheshi
shahada za wapiga kura wilayani humo.
Chama cha
Demokrasi na Maendeleo (CHADEMA), kimetoa shutuma hizo kikiwatuhumu
wajumbe hao wa CCM
kwa kudai wamekuwa wakipita nyumba hadi nyumba wakiorodhesha
shahada hizo.
Akizungumza na
waandishi wa habari mjini hapa, Katibu wa CCM wilaya, Kilumbe
Ngenda, alisema
madai hayo ya CHADEMA ni uongo mtupu na hayana ukweli wowote.
Alisema chama
chake hakina sababu zozote za kuwafanya wajumbe wake wa mashina
kupita nyumba hadi
nyumba kuorodhesha shahada za wapiga kura.
Pia, alikanusha
madai ya kuwashawishi wafuasi wa vyama vya upinzani kuuza shahada
zao kwa lengo la
kupunguza kura za wagombea kutoka katika kambi hiyo ya upinzani.
Alisema jimbo la
Shinyanga Mjini lina zaidi ya wapiga kura 70,000
walioandikishwa,
ambapo CCM katika jimbo hilo ina wanachama 18,000 na kuhoji ni
kiasi gani cha
fedha ambacho kitatumika kununua shahada hizo kutoka kwa
wapinzani.
Hata hivyo,
alisema chama kwa upande wake kiliwaagiza wenyeviti wake wa mashina
kufanya kampeni za
nyumba hadi nyumba kwa ajili ya kumtambulisha mgombea wao wa
ubunge, Dk.
Charles Mlingwa, ambaye hafahamiki kwa wakazi wengi wa jimbo hilo.
"Mimi
nafahamu kuwepo kwa zoezi la wenyeviti wetu wa mashina kupita nyumba hadi
nyumba
kumtambulisha mgombea ubunge wetu ambaye kwa kweli hafahamiki vizuri na
wapiga kura, hiyo
ndiyo kazi inayofanyika mitaani na si kuorodhesha shahada za
wapiga kura,"
alieleza Ngenda.
Kuhusu uzushi wa
kununua shahada, alisema CCM haiwezi kufanya upuuzi huo na kama
kweli CHADEMA ina
ushahidi, basi inapaswa kutoa taarifa polisi ili wahusika
wakamatwe na
kufikishwa mahakamani.
Alisema
malalamiko hayo ni dalili za kushindwa ambazo tayari CHADEMA imeshaziona,
hivyo inatafuta
visingizio ambavyo havina msingi.
"Sisi
hatuwezi kununua shahada za wapiga kura Tunanunua ili iweje? Tunao
wanachama wa
kutosha na mtandao wa uongozi kuanzia chini ambao unatuwezesha
kupata ushindi
bila shida. Labda wao CHADEMA ndiyo wanaonunua shahada, tunao
ushahidi, kwani
mmoja wa viongozi wao alikamatwa hivi karibuni na shahada za
wapiga kura,"
alisema Ngenda.
Mapema wiki
iliyopita, CHADEMA mjini hapa kiliandika barua kwa msimamizi wa
uchaguzi jimbo la
Shinyanga Mjini, kikilalamikia ilichodai wajumbe wa mashina wa
CCM kupita nyumba
hadi nyumba wakiorodhesha shahada za wapiga kura.
NLD Mara
yaiomba serikali iifute CUF
Na Joseph
Manyonyi, Bunda
KATIBU wa chama
cha NLD mkoani Mara, Ascetic Malagila, ameiomba serikali ikifute
chama cha CUF kwa
sababu kimepoteza sifa ya kuwa chama cha siasa kwa kuvunja
amani ya Tanzania.
Malagila alisema hayo
jana wakati akizungumza na waandishi wa habari nyumbani
kwake mtaa wa
Nyasura mjini hapa.
Alisema viongozi
na wanachama wa CUF wanataka kuiingiza Tanzania katika dimbwi la
damu, kutokana na
vitendo viovu vya chama hicho vya kuwapiga waandishi wa habari,
maandamano ya mara
kwa mara, fujo na jazba za kidini.
Malagila ambaye
ni mwanasiasa machachari, alieleza kuwa vitendo vya CUF ni kama
bomu linaloweza
kuiangamizi Tanzania ikiwa serikali haitakifuta chama hicho kwa
siasa za ubabe na
chuki.
Akizungumzia
uchaguzi wa Zanzibar uliomalizika hivi karibuni, alisema ulikuwa
huru na wa haki.
Amevitaka vyama
vya siasa visiingizwe katika serikali ya mseto, kwani kufanya
hivyo ni kupata
madaraka bila ridhaa ya wananchi.
Alipinga wazo la
kuwepo kwa mazungumzo kati ya CCM na CUF, kwani ni kupoteza muda
na fedha za
wananchi, ambazo zinatakiwa kuleta maendeleo hapa nchini.
Katika mkutano
huo, Malagila alijitangaza kugombea uspika wa Bunge la Jamhuri ya
Muungano wa
Tanzania kwa tiketi ya NLD, na kueleza kuwa tayari amekwishapata
baraka za Kamati
Kuu ya chama chake.
Wananchi
wainyime kura CUF kutokana na sera za mabavu
Na Prosper
Kulita, Morogoro
CHAMA cha
Mapinduzi wilaya ya Morogoro, kimewataka wakazi wa mkoa huo
kutowachagua wagombea wa chama cha CUF kwa kuwa chama hicho hakil