UHURU 17.11.2005
BAADA YA
UCHAGUZI MKUU KUAHIRISHWA:
Na Mwandishi Wetu
KITIMTIM cha kampeni za kugombea urais wa
Jamhuri ya Muungano wa
kitaanza tena mwishoni mwa wiki hii ambapo mgombea mwenza wa Chama Cha Mapinduzi,
Dk. Ali Mohamed Sheni atakuwa Lushoto, Jumapili.
Mgombea urais kwa tiketi ya CCM, Jakaya Kikwete katika awamu hii ataanzia kampeni
zake wilayani Rufiji Jumanne ijayo.
Tume ya Taifa ya
Uchaguzi (NEC), jana ilipitisha ratiba ya kampeni za uchaguzi za
wagombea Urais
utakaofanyika Desemba 14, mwaka huu.
Mkuu wa Idara ya
Elimu kwa Wapigakura wa Tume ya Uchaguzi, Eda Sanga, alisema
jana kuwa mgombea
wa Urais wa CCM, Jakaya Kikwete kwa upande wake ataanza
mzunguko wa
kampeni zake Jumanne ijayo wilayani Rufiji.
Ratiba hiyo
ilipitishwa baada ya kikao cha vyama vyote vyenye wagombea Urais,
isipokuwa
PPT-Maendeleo. Kampeni za wagombea Urais zitaanza Jumamosi kama
ilivyopangwa awali
na vyama vya CUF na CCM pekee ndivyo havitakuwa na mkutano
wowote siku hiyo.
CCM inatarajia
kuhitimisha kampeni zake Desemba 13, kwenye viwanja vya Jangwani,
wakati CUF
itahitimisha kampeni zake kwenye uwanja huo huo, Desemba l2.
Eda alisema CUF,
nayo itaanza kampeni zake Jumapili ijayo, ambapo mgombea Urais,
Profesa Ibrahim
Lipumba atakuwa mjini Mwanza na Mgombea Mwenza, Juma Haji Duni,
atakuwa Morogoro
Vijijini.
Ofisa wa CUF
anayeshughulikia masuala ya uchaguzi, Maole Kuchilungilo, alisema
kuwa mkutano wa
kampeni mjini Mwanza utarushwa moja kwa moja kupitia Radio Free
Africa na
itarekodiwa na kurushwa usiku kupitia televisheni ya Star.
Kwa mujibu wa
Kuchilungilo, mikutano kama hiyo huko Tabora, Mtwara na ule wa
kufunga kampeni wa
Dar es Salaam nayo itaonyeshwa kwa utaratibu kama huo wa
Mwanza.
Ratiba ya kampeni
ya vyama vingine ni DP itakayozindua awamu ya pili ya kampeni
jimboni Kilolo
Jumamosi na kumalizia huko Chake Chake, Desemba 13. Katika siku za
karibuni mgombea
Urais wa chama hicho, Mchungaji Christopher Mtikila alisema kuwa
chama chake
kinawania kuiteka CUF, ngome yake ya Pemba.
Mgombea Urais wa
TLP, Augustine Mrema na mgombea Mwenza wake, Rukia Kiota
wataanza Jumamosi
katika majimbo ya Moshi Vijijini na Vunjo na watamalizia mkoani
Dar es Salaam
siku ya mwisho wa kampeni.
Mgombea Urais wa
Chadema, Freeman Mbowe atazindua awamu hiyo ya pili ya kampeni
Jumamosi huko
Kinondoni na mgombea Mwenza atakuwa Visiwani Ukerewe. Kampeni hizo
zitahitimishwa kwa
mgombea Urais kuwa jimboni Hai na Moshi Mjini, huku Mgombea
Mwenza, Anna Komu
atakapokuwa mjini Kigoma.
Chama cha NCCR,
kitaanza na mikutano ya wagombea wake, Dk. Sengondo Mvungi na
Mgombea Mwenza
Naila Jiddawi Mtwara mjini na watamalizia Desemba 13 huko Ubungo,
Dar es Salaam.
Uchaguzi
utafanyika Desemba 14, mwaka huu, baada ya kuahirishwa mara mbili
tofauti, kutokana
na kifo cha aliyekuwa mgombea mwenza wa Chadema, Jumbe Rajab
Jumbe aliyefariki
usiku wa Oktoba 26, zikiwa ni siku tatu kabla ya uchaguzi mkuu
ambao ulikuwa
ufanyike Oktoba 30.
Mboma aomba
TRC ibinafsishwe haraka
Na Mwandishi Wetu
SHIRIKA la Reli
Tanzania (TRC) linasuasua katika uendeshaji na limeiomba serikali
kulinasua kwa
kuharakisha ubinafsishaji wake kutokana hali ngumu ya kiuchumi
linayolikabili
shirika hilo, imeelezwa.
Mkurugenzi Mkuu
wa TRC, Linford Mboma alitoa kilio hicho jana kwa wajumbe wa Bodi
ya Mamlaka ya
Usimamizi wa Vyombo vya Majini na Ardhini (SUMATRA), uliotembelea
vitengo mbalimbali
vya shirika hilo.
Ujumbe huo uliokuwa
ukiongozwa na Mwenyekiti wa Bodi ya SUMATRA, Peter Bakilana,
ulitembelea
vitengo kadhaa kikiwemo cha karakana ya TRC mjini Dar es Salaam.
Alisema kutokana
na hali hiyo, safari za treni kwa reli ya kati sasa zimepungua
kutoka kila siku
hadi tatu kwa wiki.
Mboma alisema
tangu TRC itangazwe kubinafsishwa mapema mwaka huu, utekelezaji
wake umekuwa
ukisuasua kutokana na sababu mbalimbali hatua aliyosema imekuwa
ikiathiri
uendeshaji wa TRC ambayo hapo awali ilikuwa ikitegemea wafadhili kutoka
Canada na
Uingereza.
Alisema kutokana
na kucheleweshwa huko TRC imekuwa ikiendelea kujiendesha katika
hali ya kusuasua
na kupata hasara ya wastani wa asilimia 20 kila mwaka.
Mapema mwaka huu, kampuni mbili za Great Lakes Railway Consortium (GLRC) na Rites
Consortium, zilijitokeza kuomba kukodisha miundo mbinu ya
shirika
katika hatua za
awali za uchambuzi wa mapendekezo ya masuala ya kifedha, Rites
ilishinda, lakini
iliingwa na GLRC.
Pia, GLRC
ilifungua kesi dhidi ya Tume ya Rais ya Kurekebisha Mashirika ya Umma
(PSRC) katika
Mahakama Kuu ya Tanzania, Kitengo cha Biashara, ikipinga kutupwa
kwa zabuni yao
hasa katika kipengele cha kiufundi. Hata hivyo, kesi hiyo
iliondolewa
mahakamani bila masharti Novemba 10, mwaka huu.
Akifafanua, Mboma
alisema kutokana na hali hiyo TRC imekuwa ikijiendesha katika
mazingira magumu
na hasa ikizingatiwa uchakavu wa injini za treni, mabehewa na
reli kwa jumla.
Kwa mujibu wa
Mboma, mbali na uchakavu, TRC pia imekuwa ikiwajibika moja kwa moja
katika kufanya
matengenezo ya reli pindi inapoharibika.
Pia, TRC imekuwa
ikiendelea kulipa kodi kutokana na mafuta inayonunua na
kuendelea
kusafirisha abiria wa daraja la tatu kwa bei ya chini licha ya matatizo
yaliyopo.
Kulingana na
Mboma, TRC imekuwa ikitoa wastani wa sh. bilioni 2 kwa
mwaka kwa
ajili ya kulipia
kodi ya mafuta na pia imekuwa ikipoteza mapato ya wastani wa sh.
bilioni 3 kwa
mwaka kwa ajili ya kuendelea kutoa huduma za usafiri wa daraja la
tatu.
Hata hivyo, Mboma
alisema pamoja na matatizo hayo, TRC imekuwa ikipiga hatua
katika baadhi ya
maeneo yakiwemo ya ufuatiliaji wa safari za treni ambapo kwa
sasa taarifa za
treni zilizoko safari zinakuwa zimefika makao makuu katika muda
wa saa mbili tangu
ilipoanza safari.
Chini ya
utaratibu huo unaendeshwa kwa kutumia mtandao wa kompyuta, taarifa za
treni
zinazohusiana na mizigo na abiria walioko safarini zinakuwa ziko kwenye
mtandao na hivyo
kurahisisha ufuatiliaji wa safari hizo.
Kuhusu suala la
ulinzi wa mizigo na miundombinu ya reli, Mboma alisema TRC
imeingia mkataba
na vijiji 55 katika baadhi ya maeneo ambavyo vimekuwa
vikishiriki katika
kutoa ulinzi.
Pia, alisema
shirika hilo limeanzisha utaratibu wa wateja kushirikishwa katika
kufuatilia mizigo
yao kutoka inapopakiwa hadi inaposhushwa, hatua aliyosema
imepunguza tatizo
la wizi wa mizigo.
Alisema hilo
lilikwenda sambamba na TRC kukabidhi vituo vyake vya mafuta kwa
kampuni ya GAPOIL
na kwamba TRC inawajibika tu pale mafuta yanapoingizwa kwenye
mabehewa na kwenye
injini.
Kimsingi, alisema
huduma za reli zina umuhimu wa pekee na hasa ikizingatiwa
kwamba zinachangia
katika kukuza uchumi sambamba na kufanikisha shughuli za
kilimo na
viwandani.
Alisema kuyumba
kwa TRC kwa kiwango kikubwa kutaathiri shughuli za Mamlaka ya
Bandari Tanzania
(THA) na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) ambazo zimekuwa
zikiitegemea
katika usafirishaji wa mizigo.
Pia, alisema
iwapo uwekezaji huo, utachelewa kuna uwezekano wa soko la TRC kwa
nchi ambazo hazina
mlango bahari likachukuliwa na nchi zingine za jirani.
Mboma alisema
injini kumi zilizoko Tabora zilizokodishwa kutoka India ziko
hatarini
kuchukiliwa kufuatia deni la sh. bilioni 3 ambazo TRC
inadaiwa. Alisema
fedha hizo ni hadi
kufikia Desemba, mwaka 2002.
Majambazi
yamtwanga mwanamke risasi kichwani na kupora gari
MWANAMKE mmoja
ameuawa kwa kupigwa risasi kichwani na watu wanaohisiwa kuwa ni
majambazi baada ya
kuvamia na kuliteka gari aina ya Hiace.
Shirika la habari
la PST mjini Shinyanga limemkariri Kamanda wa Polisi Mkoa
Abdalah Mssika
alisema tukio hilo lilitokea mwishoni mwa wiki iliyopita saa 12
jioni katika
kijiji cha Ibelambogo kwenye barabara itokayo Runzewe kwenda Bwanga
katika kata ya
Uyovu mpakani mwa wilaya za Bukombe na Biharamulo.
Mssika alimtaja
mama huyo aliyeuawa kwa jina la Imelda Francis (40) mkazi wa
kijiji cha
Nyakahala wilaya ya Biharamulo mkoa wa Kagera.
Alisema gari aina
ya Hiace lenye namba za usajili T 288 AMM likiwa linatoka
Runzewe kwenda
wilayani Biharamulo lilivamiwa na majambazi yenye silaha aina ya
SMG ambayo
haikuweza kufahamika namba zake kwa lengo la kutaka kufanya uporaji.
Alisema majambazi
hayo yalipoanza uporaji yalimfikia Imelda ambapo alikataa kutii
amri yao na ndipo
yalipomfyatulia risasi katika mkono wa kulia na kichwani na
kumpora sh.
50,000.
Alisema mara
baada ya uvamizi huo watu hao walitoweka na kukimbilia katika pori
la Bwanga.
Kamanda Mssika
alisema polisi bado inaendelea kuwasaka majambazi hao ili kuwaweka
katika mkono wa
sheria na kujibu shitaka la mauaji.
Katika tukio lingine,
mkazi wa kijiji cha Kitongo kata ya Igwamanoni wilayani
Kahama Sofia
Mpangala (55) alikutwa amekufa nyumbani kwake kwa kukatwakatwa
mapanga kichwani
na watu wasiofahamika.
Tukio hilo
lilitokea Jumatatu usiku kijijini humo baada ya watu wasiofahamika
kuvamia katika
nyumba hiyo na kumshambulia kwa kumkatakata mapanga hadi kumuua na
kwamba mauaji hayo
yanahusishwa imani za kichawi.
Katika tukio la
tatu mkazi wa kijiji cha Ibelasula kata ya Ushetu wilayani Kahama
aliyetambuliwa kwa
jina la Manyasura Bundala (60) amekutwa amekufa na mwili wake
kutupwa porini.
Mjini Morogoro
Latifa Ganzel anaripoti kuwa, Kamanda wa Polisi mkoa Steven Ngowi
aliwaambia
waandishi wa habari jana ofisini kwake kuwa Atanas Edward (20) mkazi
wa Ludewa Peapea
wilayani Kilosa alifariki dunia baada ya kupigwa na kundi la
watu wanane
akituhuhiwa kuiba baiskeli na radio.
Kamanda Ngowi
alisema kuwa tukio hilo lilitokea Jumanne jioni ambapo Edward
anadaiwa kuiba
baiskeli, radio na fedha taslimu sh. 5,000 mali ya Donald Kayombo.
Waliojiriwa
kinyemela kusimamishwa kazi
Na Mwandishi Wetu
TUME ya Utumishi
wa Umma itakagua taratibu za ajira ya wafanyakazi wa wizara nane na idara mbili
za umma ili kujua kama taratibu za ajira zinafuatwa na kwamba wakipatikana
walioajiriwa kinyemela, watasimamishwa kazi,.
Katibu wa Tume
hiyo, Thecla Shangali alisema hayo jana alipozungumza na wakaguzi watakaoanza
kazi Novemba 22 hadi Desemba 4 mwaka huu, wakati wa hafla ya uzinduzi wa mpango
huo iliyofanyika kwenye ofisi ya Tume hiyo barabara ya Samora jijini Dar es
Salaam.
Wizara
zitakazokaguliwa katika awamu hii ni Wizara ya Elimu na Utamaduni, Wizara ya
Mambo ya Ndani, Wizara ya Afya, Wizara ya Kilimo na Chakula, Wizara ya Maji na
maendeleo ya Mifugo, Wizara ya Sayansi, Teknolojia na Elimu ya juu, Wizara ya
Ardhi na maendeleo ya Makazi na Ofisi ya Rais Mipango na Ubinafsishaji.
Idara
zitakazokaguliwa ni Kamishna ya zimamoto na uokoaji na Idara ya uhamiaji.
Hata hivyo lengo
la Tume ya utumishi kwa mwaka 2005/2006 ni kukagua masuala ya ajira katika
wizara 20, Idara 10 halmashauri 40 na ofisi za makatibu wa mikoa 10.
Kwa kipindi
kirefu Tume ya ajira ilihusika katika kuajiri wafanyakazi wa umma, lakini
sheria namba nane ya mwaka 2002 iliiondolea mamlaka hayo na kutoa madaraka kwa
kila wizara au idara kutoa ajira kwa kufuata sheria na taratibu bila upendeleo.
Ukaguzi huo
unafanyika ili kujua kama mamlaka za ajira zinafuata taratibu na sheria za
ajira na kwamba kama watapatikana walioajiriwa kwa upendeleo au bila sifa watasimamishwa
kazi ili kupata ufafanuzi zaidi.
Thecla alisema
katika ukaguzi huo, fomu nane zitatumika ikiwemo fomu ya kwanza ambayo itahusu
kutaka kujua kada husika ya ajira, idadi ya wafanyakazi walioomba, idadi ya
walioitwa kwenye usaili na idadi ya waliochukuliwa kwa sifa.
Fomu ya pili
itahusu kujua idadi ya watumishi waliothibitishwa kazini, idadi ya
walioongezewa muda wa kuthibitishwa na idadi ya watumishi wasiothibitshwa
kazini na kwamba fomu ya tatu itahusu idadi ya wafanyakazi waliopandishwa vyeo.
Alisema ukaguzi
wa kutumia fomu ya nne utahusu masuala ya nidhamu kwa kuangalia idadi ya
mashauri, yaliyoshughulikiwa, barua za maamuzi wakati ukaguzi wa masuala ya
mafunzo ya watumishi utaangalia idadi ya wafanyakazi waliopata mafunzo, idadi
ya wanaoendelea kupata mafunzo na idadi ya waliokosa.
Katika ukaguzi
huo, fomu ya sita itajikita juu ya maslahi kwa kuangalia watumishi wanaoilipwa
mishahara, wasiokuwepo, watumishi waliorekebishiwa mishahara, wanaodai
malimbikizo ya mishahara, idadi ya watumishi walioshughulikiwa pensheni, idadi
ya miradi iliyoshughulikiwa na iliyokwama.
Pia alisema , wakaguzi wataangalia fomu ya saba inayohusu
upimaji na tathimini ya wazi kwa kila mfanyakazi ikiwa ni pamoja na kuangalia
kama upo mpango maalum wa malengo, kuwepo kwa mkataba wa huduma kwa mteja. Kuwepo
kwa mgawanyo wa kazi na kuwepo kwa mikakati ya utendaji kazi
Fomu ya nane
katika ukaguzi huo itahusu masuala ya takwimu muhimu zikiwemo za watumishi
wote, idadi ya watumishi waliostaafu kwa hiari, waliostaafu kwa ugonjwa,
waliostaafu kwa lazima na idadi ya watumishi waliofariki.
Akifafanua juu ya
umuhimu wa kukagua ajira za watumishi wa umma, Thecla alisema lengo
nikutekeleza sheria na kwamba ukaguzi lazima ufanyike kwa haki na kuzingatia
taratibu bila woga.
‘Fanyeni ukaguzi
kwa fedha zilizoidhinishwa, zingatieni muda, fanyeni kwa uwazi na ukaguzi huo
utoe matokeo bayana na kutoa ripoti ya kweli na sahihim,’’
alisema na kuongeza kwamba ni muhimu pia ripoti hizo zikaandikwa kwa wakati.
Mawaziri wapya
Z’bar waapishwa rasmi
Na Mwandishi Wetu
RAIS wa Zanzibar
na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Amani Abeid Karume jana aliwaapisha
mawaziri 12 ambao ni wajumbe wa baraza lake jipy alilolitangaza juzi.
Walioapishwa na
wizara zao kwenye mabano ni Ali Juma Shamhuna (Waziri wa Habari Utamaduni na
Michezo). Shamhuna pia ni Naibu Waziri Kiongozi wa Serikali ya Mapinduzi
Zanzibar.
Wengine
walioapishwa kushika nafasi za uongozi katika cha pili cha 2005-2010 cha
uongozi wa Rais Karume ni Amina Salum Ali (Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Kiongozi)
na Dk. Mwinyihaji Makame Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais anayeshughulikia Fedha na
Uchumi.
Zainab Omar
Mohammed (Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais kazi maalum), Burhan Saadat Haji (Waziri
wa Kilimo, Mifugo na Mazingira) na Sultan Mohammed Mugheir (Waziri wa Afya na
Ustawi wa Jamii).
Wengine ni Haroun
Ali Suleiman (Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amani), Brigedia Jenerali Mstaafu
Adam Mwakanjuki ( Waziri wa Mawasiliano na Uchukuzi)
na Suleiman Othman Nyanga (Waziri na Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Vikosi
vya SMZ).
Mansour Yussuf
Himid (Waziri wa Maji, Ujenzi, Nishati na Ardhi), Ramadhan Abdallah Shaaban
(Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Katiba na Utawala Bora), Samia Suluhu Hassan
(Waziri wa Utalii, Biashara na Uwekezaji ) na Asha
Abdallah Juma (Waziri wa Vijana, Wanawake na Watoto.
Hafla hiyo fupi
iliyofanyika Ikulu mjini Zanzibar na ilihudhuriwa na Waziri Kiongozi, Shamsi
Vuai Nahodha, Jaji Mkuu Hamid Mahmood, Spika wa Baraza la Wawakilishi, Pandu
Ameir Kificho pamoja na Kadhi Mkuu wa Zanzibar, Sheikh Mussa Makungu.
Wanafunzi 28
hatimaye watoka hospitali
Na El-hadji
Yuusuf, Tabora
WANAFUNZI 28
waliokuwa wamelazwa katika hospitali ya mkoa wa Tabora, kupatiwa matibabu baada
ya kuanguka kutokana na kupatiwa tiba ya minyoo na kichocho, wametolewa
hospitalini huku hali zao zikiendelea vizuri.
Pamoja na
kutolewa hospitalini hapo jana, wanafunzi waliokuwa darasa la nne wameshindwa
kufanya mtihani wa taifa baada ya kukumbwa na athari za dawa hizo.
Wanafunzi hao
walilazwa kutokana na kuanguka huku wengi wao wakiwa wamekumbwa na matatizo ya
kuumwa sana kichwa, kizunguzungu, kutapitika na kuharisha kiasi cha kufikia
hatua ya kupoteza fahamu.
Kaimu Mganga mkuu
wa hospitali ya mkoa wa Tabora, Dk. Amos Nsheha, aliwataja wanafunzi
walioruhusiwa hadi kufikia jana mchana kuwa ni Fatuma Shaaban, Lucy Fussi,
Johari Rajab, Tea Juma, Pili Mussa, Mwajuma Ramadhani, Tausi Ramadhani, na
Gulamali Selemani.
Wengine ni Habiba
Nasib, Asha mohamed, Hussein Selemani, Rashid Hamina, Mohamed Mustafa, Sudi
Mussa, Cecilia Vincent,Christina Paul, Asha Mashaka,
Bakari Omari, Mwanahamis Juma, na Michael Mziku.
Dk. Nsheha,
aliwataja wanafunzi wengine waliotolewa jana kuwa ni Sabina Evans, Asha
Athumani, Nassibu Athumani, Tausi juma, Juma Mashaka, Christopher Melkior na
Athumani Mussa.
Alisema watoto
hao walipatwa matibabu na kuwa hali hiyo nikutokana na sababu mbalimbali ikiwa
pamoja na kushindwa kupatiwa chakula chenye lishe ya kutosha muda mfupi kabla
ya kupewa dawa hizo ambazo ina nguvu kubwa ya kukabiliana na ugonjwa wa
kichocho.
Alisema kuwa
wanafunzi waliopatwa na mkasa huo, wanatoka katika shule 11 za manispaa hiyo
kati ya shule 20.
Aliongeza kuwa
wanafunzi waliokumbwa na mkasa huo wanaweza pia kuwa walikuwa na matatizo
mengine ya kiafya kama kuwa na vijidudu vya malaria, kuwa dhaifu kiafya na
sababu nyinginezo.
Hata hivyo, Dk
Nsheha, alisema kuwa watoto hao walipatiwa tiba bure hospitalini hapo na kwamba
kulikuwa na uangalizi maalum, kitu ambacho kimesaidia kuwapatia huduma bora na
nzuri na hivyo kuokoa maisha yao.
Mkuu wa wilaya ya
Tabora, Alhaji Mussa Samizi, alisema dawa hizo hazina madhara, lakini kuna
uzembe uliofanywa na walimu baada ya kuwapa bila ya kuwapa chakula cha kutosha,
tatizo ambalo alisema limetokana na walimu hao kushindwa kufuata muongozo
waliopewa.
DAWASCO:
Watakaounganisha maji kinyemela kukiona
Na Mwandishi
Wetu.
SHIRIKA la
Uendeshaji la majisafi na maji taka Dar es Salaam (DAWASCO)limetangaza
kuwafuta uteja na kuwang'olea mabomba wateja wote ambao watabainika kwenda
kinyume na taratibu za kuunganisha maji ikiwa ni pamoja na uchepushaji wa mita.
Hatua hiyo ya
kuwafuta wateja katika orodha yake imewakumba wateja kadhaa waliokuwa wameingia
mkataba na DAWASCO kama wateja wa majumbani, lakini wakakiuka taratibu na
badala yake kufanya biashara ya kuuza maji.
Baadhi ya wateja
wanaotuhumiwa kwa madai ya kuhusika na utaratibu huo mpya wa DAWASCO ni pamoja
na Dismas Njau, Izadin Kazokola na Oliverturist Mwakaikamu wakazi wa Mbezi
Luois.
Meneja Uhusiano
wa DAWASCO, Shy-Rose Bhanji aliwaambia waandishi wa habari kwamba pamoja wateja
hao kufutiwa uteja na mabomba yao kung'olewa, vilevile watatozwa faini ya
malipo ya matumizi ya maji kwa miezi 24.
Shy-Rose alisema
kila mteja aliyebainika kuchepusha mita na kuuza maji kwa wenye magari atatozwa
faini ya sh. milioni 11.8 na sh. milioni
4.3 kwa kuuza maji kwa wenye mikokoteni la sivyo atapelekwa mahakamani.
Kwa sasa wateja
wa majumbani wanatozwa kiasi cha sh. 359 kwa mita za ujazo tano za mwanzo na
iwapo zitazidi basi mteja atatozwa sh. 506 kwa kila mita moja ya ujazo. Wateja
wa biashara wanatozwa kiasi cha sh. 725 kwa mita ya ujazo.
Shy-Rose ametoa
wito kwa wateja wote kuheshimu taratibu zote za kuunganishiwa maji kwani
kuanzia sasa DAWASCO haitamvumilia mteja ambaye atakiuka taratibu.
"DAWASCO
inatoa wito kwa wateja wake wote kufuata taratibu zilizowekwa kwa kweli sasa
kila tukibaini kwamba mteja amechepua mita tunachofanya ni kuondoa uteja wa
mteja husika na zaidi ya hapo ni kung'oa bomba na mteja huyo hatapatiwa tena
huduma ya DAWASCO, " alisema meneja huyo wa uhusiano.
DAWASCO ambayo imeingia
madarakani kwa takriban miezi mitano sasa, imemaliza mkakati wake wa siku 100
ulioanza mwezi Julai hadi Oktoba ambapo imeweza kufanikisha malengo
iliyojiwekea chini ya mkakati uliojulikana ‘siku 100 za utekelezaji’.
Juzi Waziri wa
Maji na Maendeleo ya Mifugo, Edward Lowassa alitembelea maeneo kadhaa ya jiji
kujionea hatua iliyofikiwa na DAWASCO.
Baadhi ya wakazi
walikiri kuboreshwa kwa huduma ya maji katika maeneo ya Sinza, Mikocheni,
Kigogo, Kijitonyama Block 46/47, Mwananyamala kisiwani na Tabata. Wakazi wa
Mburahati hata hivyo walisema bado huduma ya maji inahitaji kuboreshwa zaidi.
Walemavu
waliogawa vibanda kwa wengine kunyang’anywa
Na Mwandishi Wetu
WALEMAVU
waliopangisha vibanda vya biashara walivyogawiwa na Halmashauri ya Jiji
la Dar es Salaam
watanyang’anywa na kugawiwa kwa wengine.
Mkuu wa mkoa wa
Dar es Salaam, Luteni Yusuf Makamba alitangaza azma hiyo jana
alipokuwa
akizungumza wakati wa hafla ya kuwakabidhi walemavu baiskeli.
“Nataka niwahakikishie
kuwa serikali hii na hata hiyo ijayo inawapenda na ndiyo
sababu imefanya
juhudi kadhaa za kuwasaidia, ikiwemo ya kuwapatia vibanda vya
biashara ingawa
wengi wenu mmevipangisha badala ya kuvitumia kujiendeleza,”
alisema.
Alisema uamuzi wa
walemavu hao kupangisha vibanda hivyo kwa wafanyabiashara
wengine ni
ukiukwaji wa mikataba ya umilikaji ambayo lengo lake ni kuwahudumia
watu wenye ulemavu
kwa kuwapatia nafasi za uhakika za kufanya biashara katika
maeneo
yanayokubalika kisheria.
Luteni Makamba
alibainisha kuwa uchunguzi wake kuhusu umilikaji wa vibanda hivyo
umebaini kuwa kwa
sasa asilimia kubwa vinatumiwa na wafanyabiashara wengine na
walemavu wamebakia
kuwa ‘maboya’ tu.
“Unapotembelea
vibanda hivyo, kweli utaona vinamilikiwa na walemavu kwa vile vina
maandishi
yanayoonyesha hivyo, lakini ukivisogelea utapokewa na kukaribishwa na
wafanyabiashara
ambao sio walemavu na unapohoji zaidi, wanakosa hata jibu,”
alisema na
kuongeza kuwa hali hiyo inatia shaka kuhusu wamilikaji halali wa
vibanda hivyo.
Utaratibu wa
kuhakikisha vibanda hivyo vinarejea na kumilikiwa kwa walengwa
unaanza mara moja
ambapo Makamba amewaagiza walemavu waliovipangisha kuwaondoa
wapangaji wao.
Sambamba na hatua
hiyo, pia ameiagiza Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam
kufanya tathmini
ili kupata takwimu sahihi kuhusu idadi kamili ya vibanda
vilivyokodishwa
kinyume cha sheria ili waliokodisha waweze kuchukuliwa hatua
ambazo ni pamoja
na kunyang’anywa.
Uamuzi wa
kuwanyang’anya walemavu vibanda hivyo umekuja kutokana na wengi wao
kuingia mitaani na
kuwa omba omba baada ya kukodisha vibanda hivyo, kazi ambayo
Makamba alisema
ni aibu kwao, familia zao pamoja na taifa.
Akizungumza
katika halfa hiyo, Askofu Mkuu wa Kanisa la International Evangelism,
Eliud Issangya
aliwashauri walengwa waliopatiwa baiskeli hizo kuzitumia kwa
shuhguli za
kimaendeleo zaidi ili ziweze kuwanufaisha.
“Ni vema mkatumia
msaada huu kama nyenzo ya kuwapeleka kwenye nyumba za ibada,
sambamba na katika
shughuli za kibiashara badala ya kwenda kwenye vilabu vya
pombe,” alisema.
Baiskeli hizo 100
zenye thamani ya sh. milioni 35 zimetolewa na kanisa
hilo baada
ya kuzipokea
kutoka kwa wasamaria wema nchini Marekani.
Viongozi wa
TLP wilayani Arusha wafikishana kortini
Na Omari Shaaban,
Arusha
CHAMA cha
Tanzania Labour (TLP) wilayani Arusha kipo katika mgogoro mzito
kufuatia
kutofautiana kwa viongozi wake na hivyo kukifanya kishindwe kuendesha
kampeni zake.
Mgogoro huo
umezidi kuota mizizi ambapo hivi sasa mwenyekiti wa wilaya wa chama
hicho, Calist
Lazaro, anadaiwa kumshtaki mgombea udiwani wa kata ya Ngarenaro
kupitia TLP,
Raphael Mwaisambule, kwa tuhuma za wizi wa kuaminiwa.
Katika tuhuma
hizo, mwenyekiti huyo wa wilaya, anamtuhumu mgombea huyo, kuiba
vifaa vya umeme
vyenye thamani ya sh. milioni moja ambavyo ni seti
nzima ya vifaa
vya kutangazia vya
kampeni, spika, vipaza sauti na vinginevyo.
Mgombea udiwani
huyo, anashatakiwa kwa wizi wa kuaminiwa wa vifaa hivyo ambavyo
ni mali ta TLP.
Imeelezwa na watu
kutoka ndani ya TLP Arusha, kwamba kufunguliwa kwa mashataka
kwa mgombea
udiwani huyo ni maagizo kutoka ngazi za juu za chama hicho, ingawa
hawakuwa tayari
kuelezea suala hilo.
Hata hivyo, hadi
kufikia jana asubuhi mgombea udiwani huyo alikuwa bado
hajafikishwa
mahakamani kutokana na tuhuma hizo, na hakuwa amepatiwa dhamana kwa
siku mbili tangu
awekwe rumande ya polisi kwa uchunguzi wa tuhuma hizo.
Akithibitisha
tukio hilo, Kamanda wa Polisi mkoa, James Kombe alisema kuwa
mgombea udiwani
huyo anatuhumiwa kuiba spika, kipaza sauti na kifaa maalumu cha
kuongeza mwangwi
wa sauti, ambavyo vyote ni mali ya TLP.
Alisema kuwa
uchunguzi wa madai hayo unaendelea vizuri na kwamba mtuhumiwa huyo
ambaye
amefunguliwa mashtaka hayo na mwenyekiti wake wa wilaya atafikishwa
mahakamani leo.
Habari za uhakika
kutoka TLP zimeeleza pia kuwa, tangu kukamatwa na kuweka ‘selo’
kwa mgombea huyo,
inadaiwa kuwa mgombea ubunge wake, kupitia chama hicho,
Godbless Lema
hajawahi hata kukanyaga eneo hilo la polisi ambalo kwake lilikuwa
kama mazoea kabla
ya tukio hilo na wananchi kujiuliza maswali mengi kuhusiana na
tukio hilo.
CCM Moro
yateua kaimu katibu wa wilaya K’mbero
Na Igamba
Libonge, Kilombero
CHAMA cha
Mapinduzi mkoani Morogoro kimemteua Juma Ndekanye (52) kuwa kaimu
katibu wa wilaya
ya Kilombero kukaimu nafasi ya katibu ambaye hivi sasa
anakabiliwa na
matatizo ya kuumwa.
Taarifa
iliyotolewa jana na Katibu wa CCM Mkoa wa Morogoro Catherine Ndahani
katika kikao cha
kamati ya siasa wilaya kilichofanyika makao makuu ya chama
wilaya mjini
Ifakara.
Ndekanye ambaye
pia ni Katibu wa Wazazi wilaya Kilombero amekaimu nafasi hiyo
baada ya katibu wa
wilaya, Luteni Makame Makame kuugua na kulazwa katika
Hospitali ya
Taifa Muhimbili jijini Dar es Salaam.
Catherine alisema
Sekretarieti ya CCM mkoa Morogoro imeamua kumteua Ndekanye
baada ya kuona
wilaya haina kiongozi mkuu, hasa katika kipindi hiki kigumu cha
uchaguzi.
Alisema kwa sasa
wilaya ilikuwa inaongozwa na wasaidizi, kwani mapema mwezi
uliopita
mwenyekiti wa Chama, Kassimu Kulolela alifariki dunia ghafla nyumbani
kwake huko
Mang’ula na sasa katibu wake anaumwa hivyo ofisi iko wazi.
Katibu huyo wa
mkoa alisema Ndekanye atashikilia wadhifa huo hadi hapo hali ya
Makame itakapokuwa
njema au makao makuu ya Chama kumteua katibu mwingine.
Maregesi
achangia sh. milioni 3.6 sekondari za WAZAZI
Na Mussa Homera,
Songea
MWENYEKITI wa
Jumuia ya Wazazi Tanzania, Abiud Maregesi amechangia jumla ya sh.
milioni 3.6
kuimarisha shule za sekondari za Wazazi mkoani Ruvuma.
Alitoa mchango
huo mwanzoni mwa wiki alipokuwa ziarani mkoani Ruvuma kukagua
maendeleo ya elimu
na malezi, majukumu yanayosimamiwa na Jumuia hiyo ya CCM.
Katika Shule ya
Sekondari Mkinga iliyoko wilayani Mbinga Maregesi aliipatia shule
hiyo sh. 600,000
ili kukarabati majengo ya shule yaliyopo, wakati katika Shule ya
Sekondari
Namtumbo aliipa sh. milioni moja ili kuanzisha ujenzi
wa madarasa ya
kidato cha tano na
sita.
Mchango wa aina
hiyo aliutoa wilayani Tunduru ambako jumla ya sh. milioni
mbili
alizitoa kwa ajili
ya kusaidia kuokoa matofali laki tatu yaliyofyatuliwa na
wananchi ili
kuanzisha ujenzi wa shule ya sekondari Muhuwesi, itakayomilikiwa na
Jumuia ya Wazazi.
Mbali ya kukagua
maendeleo ya elimu na malezi, mwenyekiti huyo pia alihutubia
mikutano ya
hadhara iliyoambatana na kampeni za uchaguzi mkuu wa taifa ambapo
aliwataka wananchi
kuipa ridhaa CCM kuunda serikali kwa mara nyingine tena ili
kuendeleza
mafanikio yaliyopo.
Aliwaonya
wananchi kutofanya majaribio katika kuweka viongozi ndani ya dola kwa
kuwakumbusha kuwa
vyama vya upinzani havijajenga mwelekeo wa kuweza kuiongoza
nchi.
Alitoa mfano wa
baadhi ya vyama kuwa vimekuwa vikigombania ruzuku kila kukicha na
kushangaa iwapo
vitapewa kasiki la umma watafanyaje kama siyo kuuvuruga uchumi
uliojengeka na
serikali ya CCM katika kipindi cha miaka mitano iliyopita.
Katika ziara
hiyo, Maregesi pia alitoa baiskeli nane kwa Jumuia za Wazazi na
mbili kwa UWT
wilaya ya Tunduru ili zisaidie kurahisisha utendaji kazi katika
matawi ya jirani.
Watakiwa
kujitokeza kuchukua mafunzo ya ufundi
Na Hussein
Semdoe, Handeni
WANANCHI wilayani
Handeni wametakiwa kujitokeza kwa wingi kujifunza ufundi katika
fani mbali mbali
katika Chuo cha maendeleo ya wananchi FDC kilichopo mjini
Chanika.
Wito huo
umetolewa na Mkuu wa Chuo hicho Barnaba Majili alipokuwa akiongea na
mwaandishi wa
habari hii Ofisini kwake.
''Natoa wito kwa
wananchi kujitokeza kwa wingi kwa kusoma ufundi katika chuo chao
hiki ili waweze
kujiajiri wenyewe na kuacha tabia iliojengeka kwa vijana ya kukaa
vijiweni,
''alisema.
Majili alsema
mafunzo yanayotolewa na chuo ni pamoja na
ufundi
magari,umeme,ushonaji,uselemara,upishi na kompyuta biashara,kilimo na
mifugo .
Alisema hivi sasa
kuna wanafunzi 80 wakiwemo wanawake 30wanaofanya mitihani ya
kitaifa ya VETA
iliyoanza juzi katika masomo ya ufundi mbalimbali.
Majili aliwaomba
wafadhili kama Halmashauri ya Wilaya, Serikali,mashirika
ya
Serikali na
yasiyo ya kiserikali kuwadhamini walemavu kwa kuwalipia ada za masomo
ambazo alizitaja
kuwa ni kati ya Sh.70,000 na sh 130,000 kutegemea na fani ya
ufundi mwanafunzi
atakayochukua.
China yatoa
misaada ya vifaa vya kilimo
Na Furaha Omary
na Njumai Ngota
UBALOZI wa China
umeipatia Wizara ya Kilimo na Chakula, vifaa vya kilimo vyenye
thamani ya sh. 141,119,813 (Dola za Marekani 123,615).
Vifaa hivyo
ambavyo ni pamoja na pampu za umwagiliaji (2), mashine za kusaga (3),
mashine kulimia
(7) na trekta (3) zilikabidhiwa na Balozi wa China nchini, Yu
Quing Tai, kwa
Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Wilfred Ngirwa.
Sherehe za
makabidhano zilifanyika juzi kwenye maghala ya wizara Chang'ombe, Dar
es Salaam ambapo
katibu mkuu huyo alisema itasaidia nchi kuingia katika kilimo
cha kisasa.
"Msaada huo
umekuja katika wakati mwafaka, ambapo wananchi wetu wanauhitaji kwa
kiasi kikubwa
teknolojia ya kisasa katika uzalishaji wa kilimo," alisema Ngirwa.
Alisema Serikali
imejitahidi kuwa na uzalishaji wa kisasa na wa kibiashara katika
sekta ya kilimo na
hivyo pampu hizo zitatumika kwenye miradi iliyoanzishwa ya
umwagiliaji.
Kwa mujibu
Ngirwa, katika siku za karibuni kulikuwa na vituo 55 vya maksai
kusaidia kilimo na
wananchi sasa wameanza kubadilishwa, ili waondokane na jembe
la mkono na
kuingia kwenye kilimo cha maksai.
Alisema, mauzo ya
trekta kitaifa yameongezeka maradufu, akitroa mfano wa mwaka
1996 kulikuwepo
na trekta 49 mwaka 1996 na sasa kiwango hicho kimefikia 350 kwa
mwaka, ilipofika
mwaka jana.
Ngirwa alisema,
hali hiyo imewezekana zaidi pia kutokana na msamaha wa kodi
katiia ununzi wa
nyenzo hizo za kilimo.
Pia kumekuwepo na
mfuko wa kuendeleza kilimo ambacho kimewezesha kukarabati
matrekta
yaliyoharibika, kununua mapya na wananchi kukodi, yote hiyo ikiwa na
maana kubwa kwa
maendeleo ya kilimo.
Ngirwa alisema,
licha msaada katika sekta hiyo ya kilimo na chakula, pia nchi
hiyo imekuwa
ikiisaidia Tanzania katika sekta za afya, pia usafiri na
mawasiliano.
Kwa upande wake
Balozi Tai, alisema lengo la msaada huo ni kuwafanya wafikie
lengo la
kujitegemea kwa chakula, na kuwa na uhakika wa upatikanaji wa chakula.
Mafunzo
yatolewa kuuelewa Mkukuta
Na Rodrick
Makundi,Moshi
SERIKALI imesema
mafanikio ya uelewa wa kutosha juu ya mkakati wa kukuza uchumi
na kupunguza
umaskini, Mkukuta, utafanikisha kutoa elimu kwa Watanzania ambao
watakuwa na mbinu
za kutosha juu ya kukuza uchumi wao hususani uchumi wa
mwananchi moja
mmoja.
Hayo yamesemwa na
Katibu Mkuu wa Ofisi ya Makamu wa Rais, Mary Mushi, wakati
alipokuwa
akifungua juzi mafunzo ya Mkukuta ambayo yamewashirikisha wadau wa
mpango huo kutoka
mikoa ya Arusha,Tanga na Kilimanjaro.
Washiriki wa
mafunzo hayo ni wataalamu wa sekretarieti za mikoa na mamlaka za
serikali za
mitaa,ambapo pia mafunzo yanatolewa katika kanda sita,zinazojumuisha
mikoa yote nchini.
Katika hotuba
yake katibu huyo alisema matarajio makubwa ni kwamba iwapo
wataalamu
wataufahamu Mkukuta watakuwa na nafasi kubwa ya kuelimisha wengine
katika ngazi ya
mikoa, halmashauri hadi kufikia ngazi za jamii.
"Ili kufikia
malengo ni jukumu la kila mmoja kusimamia na kufuatilia utekelezaji
wa mikakati ya
kisekta ya kupambana na umaskini na kutumia vizuri fedha za
serikali na
rasilimali katika kuandaa mipango bora," alisema katibu huyo.
Pia aliongeza
kuwa mafunzo juu ya Mkukuta kwa wataalamu kutoka katika ngazi zote
za utawala ndani
ya serikali yamelenga kuzifahamisha sekretarieti za mikoa na
mamlaka za
serikali za mitaa juu ya mfumo wa ufuatiliaji unaofanywa katika
kuboresha ili
kufuatilia utekelezaji wa mpango huo.
Akitoa maelezo
mafupi juu ya mafunzo hayo Mkurugenzi Msaidizi wa mpango huo,
Marry Mwasha,
alisema kuwa serikali imeweka mkazo mkubwa katika kuhakikisha kuwa
bajeti ya serikali
inalenga kuutekeleza mpango huo kulingana na bajeti ya mwaka
wa fedha 2005/06.
Alisema kuwa hivi
sasa mtazamo wa serikali ni kuhakikisha kuwa utekelezaji wa
mpango huo
unafanywa kama ilivyopangwa, ili kufikia malengo ya uanzishwaji
wake,ambapo Ofisi
ya Makamu wa Rais imepewa jukumu la kutoa elimu kwa
sekretarieti za
mikoa na mamlaka za serikali za mitaa kuhusu mpango huo.
Mpango wa kukuza
uchumi na kupunguza umaskini Mkukuta,ni awamu ya pili
ya
utekelezaji wa
mkakati wa kupunguza umaskini ulioandaliwa mwaka 2000,chini ya
mpango wa msamaha
wa madeni kwa nchi masikini sana duniani.
Mkakati huo
umefanyiwa mapitio,kufuatia utekelezaji wake katika
kipindi cha miaka
mitatu,lengo la
mapitio hayo likiwa ni kubaini mapungufu na kuboresha mkakati ili
uweze kuleta
mafanikio zaidi kwa wananchi na kuhakikisha kuwa uchumi unakuwa
zaidi kwa kasi na
hivyo kuiwezesha Tanzania kufikia malengo yaliyobainishwa
kwenye dira ya
taifa ya maendeleo ya 2025.
Mapitio hayo
yalifanywa kwa ushirikiano kati ya serikali na wadau katika ngazi
mbali mbali kwa
njia ya mahojiano,ukusanyaji wa maoni na majadiliano,maoni
yaliyokusanywa na
uzoefu uliopatikana katika utekelezaji wa awamu ya kwanza
ulifanyiwa
uchambuzi wa kina na kufanikisha maandalizi ya MKUKUTA.
Tofauti na
mkakati Mkukuta unatambua mchango wa sekta zote katika kukuza uchumi
na kuondoa
umaskini wakati mkakati ulitoa kipaumbele kwa sekta sita ambazo ni
kilimo,elimu,afya,maji
na barabara vijijini.
Plan International kutumia sh. milioni 300 mpango wa HISA
SHIRIKA la Plan
International la hapa nchini limesema litatumia jumla ya sh.
milioni 300
kusambaza mpango wa akiba ya kuweka na kukopa vijijini maarufu kama
HISA katika
wilaya tatu nchini, inaripoti PST mjini Mwanza.
Wilaya ambazo
zinatarajiwa kufikishiwa huduma ya mpango huo hivi karibuni na
shirika hilo ni
pamoja na Geita mkoani Mwanza, Ifakara mkoani Morogoro na Kibaha
mkoani Pwani.
Hayo yalielezwa
na Mkurugenzi wa Plan Internation nchini Heather Borquez wakati
wa ufunguzi wa
warsha ya kuutangaza mpango huo kwa wadau wake kutoka katika nchi
mbalimbali za kusini
na mashariki mwa bara la Afrika.
Alisema hatua
hiyo inatokana na mafanikia makubwa yaliyopatikana katika mradi wa
majaribio wa
wilayani Kisarawe mkoani Pwani, ambao walifanya kwa kushirikiana na
Shirika la Care
International.
Borquez alisema
mpango wa HISA ni rahisi kuuendesha, hauhitaji mtaji, unamilikiwa
na wananchi
wenyewe ambao wanaweka mitaji yao kwa kuweka fedha na baadaye
kuzikopa.
Alisema HISA
inamnufaisha mwanajamii moja kwa moja kwa kuwa anao uwezo wa kukopa
fedha bila ya
masharti magumu na urasimu, ili mradi awe mwanakikundi na
alishaweka akiba
kupitia katika mpango huo.
Warsha hiyo
imehudhuriwa na washiriki kutoka Sudan, Burkina Faso, Kenya, Uganda,
Niger, Zambia,
Zimbabwe, Ujerumani, Marekani na Uingereza ambayo ni makao makuu
ya Shirika hilo na
wenyeji Tanzania.
TOUCH laokoa
waliojiingiza kwenye ukahaba
WASICHANA kadhaa
waliokuwa wakifanya biashara ya ukahaba katika mji wa Kigoma
wameokolewa na
kurudishwa kwao na shirika linashughulika na kutetea haki za
watoto la Tanzania Outreach For Children (TOUCH) lenye makao yake makuu mjini
Kigoma.
Kwa mujibu wa PST hayo yalisemwa
juzi na Mkurugenzi wa shirika
Filbert wakati wa tamasha la watoto lililofanyika kwenye uwanja wa Jamhuri mjini
manispaa ya
Filbert alisema watoto hao waliwaokoa katika kipindi cha mwaka huu na wengi wao
walikuwa na umri wa chini ya miaka 15 ambapo baada ya kuwaokoa waliwauliza
wanatoka wapi na wote waliwasafirisha hadi kwenye maeneo wanayotoka.
Alisema watoto hao walikuwa wakifanya biashara ya ukahaba katika maeneo
mbalimbali ya mji wa Kigoma na wateja wao wakubwa wanadaiwa kuwa ni wavuvi wa
dagaa na samaki.
Filbert alisema kuwa shirika
ukahaba katika mji wa Kigoma inafanywa na watoto wadogo, ndipo walipoamua
kuwakusanya na kuwarudisha kwao.
Alisema japo ilikuwa ni kazi ngumu kuwashawishi ili warudi kwao lakini kwa juhudi
walizozifanya walifanikiwa kuwarudisha na hadi sasa wanafuatilia kuhakikisha kuwa
hawarudi tena mjini.
TOUCH bado linaendelea na kazi ya kuwakusanya watoto ambao wapo katika ajira
mbaya na kuwarudisha kwao na vilevile kuwatetea watoto.
Williamson Diamonds yawapa tuzo mameneja wastaafu
KAMPUNI ya mgodi wa machimbo ya almasi ya Williamson Diamonds Limited ya Mwadui
mkoani Shinyanga imewatunuku mameneja wake wastaafu sita tuzo ya utumishi bora
ikiwa ni moja ya
maadhimisho ya kutimiza miaka 65 ya mgodi, inaripoti PST.
Tuzo hizo
zilikabidhiwa kwa wastaafu hao juzi katika sherehe za maadhimisho ya
kutimiza miaka 65
tangu mgodi huo ulipoasisiwa nchini katika sherehe
zilizofanyika
ukumbi wa Recreation Club uliopo mgodini humo na kuhudhuriwa na
viongozi
mbalimbali wakiwemo wajumbe wa bodi ya wakurugenzi kutoka Afrika ya
kusini.
Mameneja wastaafu
waliotunukiwa tuzo hizo hiyo juzi ni pamoja na William Manning
(1976-1979), John
Kiwia (1979 - 1982), Erasto Ndanguzi (1982 - 1983) Samwel
Lwakatare (1973 -
1976) Robin Crawford (1958 - 1973) na Sylivanus Mipawa (1984 -
1994).
Pia tuzo hiyo ya
utumishi bora ilitolewa kwa wafanyakazi wengine walioonyesha
juhudi katika
utendaji kazi wao akiwemo mshauri wa kampuni kuhusu masuala ya
mazingira Bertus
Stoker.
Akikabidhi tuzo
hizo kwa mameneja hao, Mwenyekiti wa kampuni tanzu inayomiliki
mgodi huo ya De
Beers yenye makao yake nchini Afrika Kusini Jonathan Oppenheimer
alisema utendaji
kazi wa wastaafu hao ndio uliochangia kwa kiasi kikubwa
kuendelea kuwepo
kwa mgodi huo hadi hivi leo.
Oppenheimer
aliwapongeza mameneja hao kwa uhodari wao na uvumilivu waliouonyesha
wakati wa utendaji
kazi licha ya kufanya hivyo katika mazingira magumu.
Hata hivyo,
alisema changamoto ilinayoukabili mgodi huo kwa sasa ni kuongeza
uboreshaji pamoja
na tija, hali bora ya maslahi ya watumishi na familia ili nao
wapate mafanikio
sambamba na kampuni yenyewe.
Alisema pamoja na
mafanikio ambayo mgodi umepata kwa bado wafanyakazi
wanalojukumu la
kuhakikisha hali hiyo inaendelea katika kipindi cha miaka 35
ijayo ambapo mgodi
utatimiza miaka 100.
"Ni nadra
mno kampuni kufikisha umri wa miaka 65 bila kuanguka mfano barani
Amerika kampuni
nyingi huishia miaka 13 au zaidi kidogo kwetu sisi huo ni fahari
na tunajivunia kwa
hilo," alisema Oppenheimer.
Mgodi wa Williamson Diamonds Limited ulianzishwa na mtaalamu wa madini kutoka
Canada John Williamson mwaka 1940 ambao umeendelea kuchimba almasi katika eneo
Mashariki.
Morogoro yateuliwa mfano wa
kuboresha maduka ya dawa baridi
Na Mwandishi Wetu
MKOA wa Morogoro umeteuliwa kuwa miongoni mwa mikoa mitatu nchini itakayoshiriki
awamu ya kwanza ya
usambazaji wa mpango wa kuboresha maduka ya dawa baridi, mikoa
mingine ikiwa ni
Rukwa na Mtwara.
Mkurugenzi Mkuu
wa Mamlaka ya Chakula na Dawa Magreth Ndomondo juzi wakati wa
warsha ya
uhamasishaji kwa wadau wa ngazi ya mkoa kuhusu mpango huo ambao mara
baada ya
kuboreshwa kwa maduka hayo yataitwa maduka ya dawa muhimu.
Alisema mpango hu