UHURU 18.11.2005
Nimekwenda Kyela
kuwakabili maadui watatu, asema Dk. Mwakyembe
Na Bashir Nkoromo, Kyela
MGOMBEA wa Ubunge wa jimbo la Kyela, Dk. Harrison Mwakyembe amesema hakwenda katika jimbo hilo kupambana na mbunge wa zamani, John Mwakipesile ila kupambana
na maadui watatu wa taifa, yaani ujinga, maradhi na umasikini.
Dk. Mwakyembe alitamka hayo alipokuwa akisalimia wananchi kwenye mkutano wa
hadhara uliohutubiwa na Katibu Mkuu wa CCM, Philip Mangula katika Kata ya
Ipinda, Kyela juzi.
“Ndugu wananchi mimi nilikuja Kyela si kwa nia ya kupambana na Mwakipesile.
Hapana. Nilikuja kwa ajili nisaidiane nanyi katika kupambana na ujinga, umasikini
na maradhi,” alisema Dk. Mwakyembe na
kumtaka Mwakipesile ampatie ushirikiano kila mahali katika kampeni.
Dk. Mwakyembe aliwaambia wananchi wa
jimbo
miaka mitano ya uongozi wake
akiwa Mbunge, itakuwa si ya starehe ila ya kila mwanajimbo kufunga kibwebwe na
kuchapa kazi kwa uwezo wake ili kutekeleza Ilani ya Uchaguzi ya 2005.
Akihutubia mkutano huo, Mangula alisema, baada ya kura za maoni na baadaye
kuteuliwa kwa mgombea katika jimbo
sasa kazi iliyobaki kwa kila mwana-CCM ni kuungana na wenzake kumpigia kura
mgombea wa Chama bila kujali tofauti zilizojitokeza wakati wa kura za maoni.
Mangula alisema, wale wote walioshiriki katika mchakato ili kupitishwa kugombea
majimboni, lakini kwa mapendekezo ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM wakaachwa
hawana sababu ya kuingiwa na kwikwi
isiyoisha kwa sababu ikiwa ni wanachama
wa CCM ni lazima wazingatie nidhamu ya Chama ambayo ni pamoja na kukubali na
kutekeleza maamuzi ya juu ya Chama.
Alimpongeza mbunge za zamani wa jimbo la Kyela, Mwakipesile kwa kutotetereka
baada ya kuachwa katika kura za maoni na badala yake akaendelea kumpa ushirikiano
Mwakyembe ambaye alipitishwa.
Mangula akishangiliwa na wananchi katika mkutano huo aliwaita jukwaani Dk.
Mwakyembe na Mwakipesile na kuwataka wakumbatiane mbele ya hadhara kudhihirisha
mshikamano wao ambapo walipanda jukwaani na kufanya hivyo.
Alizungumzia haja ya wananchi kuchagua wagombea wa CCM katika ngazi zote ikiwemo
ya Urais, Mangula alisema,
watanzania hawana budi kuwachagua wagombea hao kwa tiketi ya CCM kwa kuwa ni
wagombea wa Chama kinachoaminika na chenye sera inayotekelezeka.
Umeme katikati ya
Jiji kuwa ahueni J’tatu
Na Mwandishi Wetu
HALI ya upatikanaji umeme katika maeneo ya katikati ya jiji na wilaya ya Ilala
kwa jumla itakuwa ahueni kuanzia Jumatatu baada ya kukamilika ujenzi wa njia mpya
kutoka Ubungo.
Meneja wa Usambazaji Umeme Hans Lotterine aliyosema hayo mbele ya Naibu Waziri wa
Nishati na Madini, Dk.Ibrahim Msabaha kwamba ujenzi wa njia nyingine ya umeme
kwenye njia kuu kati ya Ubungo na Ilala unatarajiwa kumalizika Jumatatu na kwamba
umeme katika wilaya ya Ilala utarejea katika hali ya kawaida, lakini Temeke
itaendelea kuwa na matatizo sehemu chache.
Lotterine alisema uwekaji nyaya za umeme kwenye njia kuu yenye urefu wa kilometa
10 kati ya Ubungo na Ilala, ulianza Novemba 8, na ulitarajiwa kukamilika Novemba
26, lakini sasa utakamilika Jumatatu ijayo kwa gharama ya karibu sh. milioni 200
na kwamba msongo wa umeme huo ni 132 Kv.
Katika hatua nyingine, Meneja huyo alimweleza Naibu Waziri kwamba Shirika lake
linao mpango wa kununua transfoma
mpya kutoka
bilioni 1.5 na kwamba watalaamu
walitarajiwa kuondoka jana kwenda
kupanga zaidi juu manunuzi hayo.
Alisema transfoma hiyo itasaidia kupunguza matatizo ya umeme maeneo ya katikati
ya jiji yakiwemo Kariakoo, Sokoine, Temeke na baadhi ya maeneo ya Kipawa.
Hata hivyo, Naibu Waziri alishauri kwamba pamoja na mipango hiyo, Shirika halina
budi kuweka utaratibu maalum wa kuhakikisha mitambo yake haiharibiki ovyo.
Alisema serikali kwa upande wake itaendelea kutekeleza majukumu yake ikiwa ni
pamoja na kuhakikisha uzalishaji wa
umeme wa Megawati 510 unaendelea
kutoka vyanzo vya IPTL, Songas na kwenye mabwawa
Matatizo ya umeme wilayani Ilala na Temeke yanasababisha hasara ya wastani wa sh.
milioni 50 kila siku.
Dk. Msabaha amewataka wafanyakazi wa TANESCO kuongeza kasi ya kuzuia mapema
uharibifu wa miundombinu iliyopo ili kuepusha tatizo la kuwakosesha umeme wateja
kwa muda mrefu.
Naibu Waziri alitoa wito huo baada ya kumaliza ziara yake ya kujionea jitihada za
Tanesco katika kutengeneza nyaya za umeme zitakazotoa umeme Ubungo hadi Ilala ili
kupunguza matatizo ya umeme katika wilaya za Ilala na Temeke.
Machi, mwaka huu, Transfoma moja iliyopo Ilala iliharibika, lakini TANESCO
hawakushtuka hadi Oktoba 18, zilipoharibika Transfoma zingine mbili kwa mpigo na
kusababisha upungufu mkubwa wa umeme katika wilaya hizo.
Baada ya kuharibika kwa transfoma hizo, Wilaya ya Ilala inayohitaji Megawati kati
ya 80 na 100 iliweza kupata megawati 40 tu, wakati Temeke inayotumia megawati 50
ilifanikiwa kubaki na megawati 26 tu.
Na Mwandishi Maalum,
RAIS Hosni Mubarak wa Misri, Makamu
wa Rais wa
Serikali ya
wa Baraza la Mapinduzi, Amani Abeid Karume, kwa kuchaguliwa kuendelea tena
kuiongoza
Pongezi kutoka kwa viongozi hao ziliwasilishwa kwa njia ya maandishi kupitia
ofisi za balozi zao nchini
Katika salamu kutoka kwa Rais Mubarak ambazo ziliwasilishwa na Balozi Mdogo wa
Misri nchini
matokeo ya uchaguzi mkuu wa
Taarifa hizo zilimpongeza Rais Karume kwa ushindi mkubwa alioupata kufuatia
mafanikio makubwa ya uchaguzi mkuu
wa
amani na utulivu jambo ambalo lilitoa fursa kwa wananchi kupiga kura kuchagua
viongozi wanaowataka.
Rais Mubarak alimtakia heri na mafanikio Rais Karume katika juhudi zake za
kuwapatia maendeleo wananchi wa
Salamu za Makamu wa Rais wa
serikali na wananchi wa
na
Alisema ana imani kuwa uhusiano huo utaendelezwa zaidi katika kipindi chote cha
uongozi wa Rais Karume, ambaye
ameshinda uchaguzi mkuu wa
ridhaa ya wananchi wa
Salamu kutoka
pili, kunaashiria heshima na imani
kubwa waliyonayo wananchi wa
kukubalika kwa juhudi na sera zake za maendeleo.
Pia taarifa hiyo ilielezea juu ya matarajio makubwa ya
Serikali ya
kuendeleza ushirikiano kati ya wananchi wa nchi hizo mbili.
Wakati huo huo, Balozi mdogo wa Misri, Kamel alifanya mazungumzo na Rais Karume
na katika mazungumzo
Rais Karume alieleza kuwa
demokrasia kwa lengo la kudumisha umoja, amani, utulivu na mshikamano nchini.
Alisema Zanzibar ina dhamira ya kujenga mfumo wa utawala wa demokrasia na
maandalizi ya uchaguzi pamoja na juhudi za kujenga misingi ya amani na utulivu
nchini ikiwemo utekelezaji wa muafaka wa pili ni uthibitisho wa dhamira ya
Serikali ya Mapinduzi katika kuimarisha utawala wa demokrasia nchini.
Rais Karume alichaguliwa tena kuiongoza
mitano katika uchaguzi uliyofanyika Oktoba 30, mwaka huu.
Wastaafu wa EAC wakana kutayarisha maandamano
Na Mwandishi Wetu
CHAMA cha wastaafu wa iliyokuwa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) kimesema hakina
habari na maandamano ya wastaafu hao yaliyopangwa kufanyika kushinikiza malipo
Katibu Mkuu wa Jumuiya hiyo, Vitus Lyamkuyu, alisisitiza chama chake hakiwezi
kushawishi wastaafu waandamane kwa lolote, kwani licha ya kukiuka sheria, pia ni
ukiukwaji wa maadili kutokana na ukweli kwamba serikali tayari imeshaonyesha
dhamira ya kutekekeza matakwa
Mapema wiki hii, kundi moja la wastaafu hao walitamka wataenda Ikulu kuonana na
Rais Benjamin Mkapa kushinikiza malipo
kinachostahili na wengine hawajalipwa kabisa.
Pia kundi
mwenyekiti kuwa amewapotosha kisheria.
Hata hivyo, Lyamkuyu alikiri kiasi walicholipwa hivi karibuni kipo kwa wastani wa
asilimia 10 ya kile wanachokidai,
lakini hawatatumia njia ya mabavu
maandamano kudai haki hiyo pia kwa mujibu wa makubaliano ya kisheria waliongia na
serikalini.
Alisema kauli rasmi ya wastaafu inatoka katika chama hicho ambacho hakijawahi
kufikiria hata siku moja kushurutisha serikali, ikiwa ni pamoja na kupanga
maandamano, kauli hizo zimekuwa zikitolewa na baadhi ya wastaafu walio nje ya
uongozi wake.
Lyamkuyu alionyesha nakala ya makubaliano ya kisheria baina ya wastaafu na
serikali kattika kesi ya madai namba 95 ya mwaka 2005, ambapo ilikubaliwa
serikali baada ya kuwalipa wastaafu
itayafanyia kazi ndani ya miezi sita, kuanzia Oktoba 28 mwaka huu na kwa maana
hiyo kipindi hicho kinaishia Aprili 28 mwakani.
Alisema ofisi yake inaendelea kupokea madai na malalamiko mbalimbali ya
wasioridhika na malipo au
kusahauliwa katika ili wahakikishe haki
inapatikana, vivyo hivyo kwa warithi wa wastaafu waliofariki dunia.
Lyakumyu alitupia lawama Hazina na mashrikia yaliyorithi shughuli za iliyokuwa
Jumuiya ya Afrika Mashariki, kwamba wamepotosha kumbukumbu na wapo ambao baadhi
ya nyaraka katika majalada
Pia ameshangazwa na hatua ya Hazina kuchukua mafaili ya wastaafu kutoka mashirika
waliokuwa na kuyalundika katika ofisi zake, kitu kitakacholeta ugumu katika
kushughulikia madai ya wastaafu husika.
Katibu Mkuu huyo, alisema licha ya hazina kulipa kiasi cha sh. bilioni 117 lakini
wana imani watalipwa kiasi kingine
kumalizia madai
lakini ilitamka kuwa uwezo wake ni mdogo hivyo itafanya kwa awamu.
Alisema kwa mujibu wa makubaliano
yaliyofikiwa ya mgawanyo wa
wastaafu hao walitakiwa kulipwa kwa thamani ya dola ya Marekani tarehe hiyo ya
mwaka 1977, ambapo dola moja ilikuwa na thamani ya sh. nane na riba ya asilimia
saba kwa mwaka kila zitakapochelewa.
Licha ya kanuni hiyo, serikali iliwalipa kwa kanuni ya riba ya asilimia 17.5 ya
sh. ya Kitanzania kwa mwaka jambo linaloleta tofauti, juu ya kiasi halisi
wanachokidai.
Kuhusu mkanganyiko ulioibuka kuhusiana na uongozi wa chama hichi cha wastaafu wa
EAC, alisema hadi sasa Mwenyekiti wao ni Bishota na amekuwa akishikilia wadhifa
huo tangu mwaka 2000, lakini mwaka juzi aliugua na kufanya nafasi yake ishikiliwe
na viongozi wengine kwa muda.
Lyamuya, aliwataja waliokuwa wakikaimu nafasi hiyo tangu Bishota augue ni
wafuatao na miaka husika katika mabano: Jafari Kibwana (2003), Nicolas Kimaro
(2003), Vitus Lyamuya (2003), Curthbert Zuberi (2004), Afree Kinyondo (2004) na
Alfred Karere ambaye ndiye kiongozi hadi sasa.
Alisema wakati wanaingia katika vikao vya mwafaka mnamo Juni mwaka jana,
mwenyekiti wao alikuwa Kinyondo ambaye aliondoka madarakani mapema mwaka huu.
Ngawaiya: Kukumbatia
upinzani ni kurudisha nyuma kimaendele
Na Rodrick Makundi, Vunjo
MPIGA debe maarufu wa CCM, Thomas Ngawaiya amewaambia wananchi wa jimbo la Vunjo
kuwa kuendelea kukumbatia upinzani kutachelewesha shughuli za maendeleo na
kuwasababishia kuendelea kuishi katika mazingira magumu kwa kukosa huduma muhimu.
Akitolea mfano, Ngawaiya alisema wakati akiwa TLP alishindwa kutekeleza majukumu
yake ya kuwatumikia wananchi kwani alitofautina na mwenyekiti wake wakati wa
kufanya mipango ya kuhudumia waliompigia kura.
Akaongeza kuwa yeye na Mrema walipanga mambo mengi ambayo utekelezaji wake
ulikuwa mgumu kwani hawakuwa na serikali, huku kukiwa na mikingamo mingi
iliyojitokeza baina ya viongozi hao wawili hivyo kuishia kwenye migogoro huku
wananchi waliomchagua wakisahaulika.
Alisema wanaong'ang'ania upinzani ni
kwa maslahi
ya wananchi: "Mimi nilipokuwa
mbunge nasema kabisa mshahara wangu nilikuwa
lakini linapofika suala la kuwahudumia wananchi niliambiwa nenda kwa baba yako
Mrema akakupe msaada huo."
"Nataka mjue huwezi kuwa mpinzani ukaleta maendeleo jimboni unapoona Serikali ni
ya CCM na
za kijamii limo katika ilani yake," alisema Ngawaiya.
Hivyo aliwataka wananchi wa jimbo la Vunjo kuhakikisha kuwa wanampa kura mgombea
wa eneo
vijijini Dk. Cyril Chami waweze kusukumu mbele maendeleo yaliyokosekana katika
majimbo hayo kwa muda mrefu.
CCM Chunya wapongezwa
kuwezesha wabunge kupita bila kupingwa
Na Bashir Nkoromo, Chunya
CHAMA Cha Mapinduzi kimeupongeza uongozi wa Chama wilayani Chunya kwa wagombea wa
majimbo yote mawili wanaowania ubunge kwa tiketi ya CCM wilayani humo, kupita
bila kupingwa.
Pongezi hizo zilitolewa kwa nyakati tofauti na Katibu Mkuu wa CCM, Philip Mangula
akihutubia mikutano ya kampeni kwa ajili ya wabunge hao waliopita bila kupingwa
katika majimbo ya Songwe na Lupa.
Victor Mwambalasa amepita bila kupingwa katika jimbo la Songwe na Dk. Gido
Singonda amepita Lupa lililokuwa la mbunge wa zamani, Njelu Kasaka ambaye baada
ya kutoteuliwa kugombea tena ametimkia CUF.
"Hii imetokana na mikakati yenu mizuri mliyoonyesha, ujenzi wa Chama na
utekelezaji wa dhati wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2000 ndiyo sababu hata
vyama vya upinzani vikaridhika kuwa havina sababu ya kuweka wagombea katika
majimbo yenu," alisema Mangula na kuongeza kwamba huo ni mtaji mwingine ambao CCM
itaingia nao katika uchaguzi.
Alivipongeza na kuvishukuru vyama vya upinzani kwa busara ya kuikubali CCM na
kuamua kuipa nafasi ya kuweka wabunge wake ili iweze kuendeleza uletaji wa
maendeleo ya nchi wakati katika awamu nyingine.
Pia Mangula alimpongeza Njelu Kasaka kwa uamuzi wake wa kutangaza kujitoa CCM
baada ya kudhani ameonewa kutopewa kugombea tena jimbo la Lupa.
"Kwa hakika nampongeza Kasaka kwa uamuzi wake maana amekuwa muwazi. Maana wapo
wengine wasiporidhika na maamuzi ya ngazi za juu ya Chama huendelea kujifanya
wako nasi huku wakitusaliti ili tukose ushindi. Wanakuwa CCM mchana kumbe usiku
wapinzani," alisema.
Mangula ambaye alihutubia katika maeneo ya Tewe, Makongolosi na Mkwajuni, alisema
ni wale tu wasio na macho ndio bado wana hamu ya kuipinga CCM isiendelee kushika
dola kwa sababu tangu TANU imekwishafanya mengi katika kipindi chake cha miaka 43
ya utawala.
Alisema wananchi wasibabaike na vyama vya upinzani kwa kuwa ni timu zilizoingia
uwanjani zikiwa hazina kocha tofauti za CCM ambayo kocha wake yupo ambaye ni
Ilani ya Uchaguzi ya 2005 ambayo imeandikwa kwa makini na inatekelezeka.
Mangula aliwataka wananchi kutochoka baada ya uchaguzi kusimamishwa kwa mujibu wa
sheria kutokana na kufariki dunia aliyekuwa mgombea mwenza wa Chadema, badala
yake waendeleze mshikamano na kujitokeza kwa wingi kuipigia kura CCM wakati wa
uchaguzi utakaofanyika Desemba 14 mwaka huu.
Mpiganaji wa JKU aliyeuawa
Na Mwandishi Wetu
MPIGANAJI wa Jeshi la Kujenga Uchumi (JKU), Shariff Salim, aliyeuawa baada ya
kutekwa na wanakijiji cha Piki
kisiwani
Kwa mujibu wa kipindi cha mawio
kilichorushwa jana asubuhi na Sauti ya
mchana kijijini kwao, Chambani, mkoa Kusini Pemba.
Mwili wake ulikutwa eneo la Penjewani, Piki ukiwa umefukiwa kwenye tope na kisha
kufunikwa makuti juu yake huku kofia yake ikiwa imewekwa mfukoni mwa suruali yake
ya kijani ambayo ilikuwa sare ya
jeshi
Kuhusu kifo hicho, uchunguzi uliofanywa kwa ushirikiano kati ya madaktari wa
hopsitali ya Wete na wenzao kutoka Tanzania Bara umebainisha askari huyo alikufa
baada ya ubongo wake kuchanganyika na damu.
Taarifa ya kipindi hicho pia ilieleza kuwa, damu hiyo ilitokana na Salum kuvunjwa
fuvu la kichwa baada ya kupigwa kwa kutumia kitu kizito kichwani. Pia alivunjika
mbavu. Marehemu ameacha mjane na watoto watano.
Salim alikufa kutokana na kipigo baada ya kutekwa na wananchi wa kijiji hicho
Novemba Mosi mwaka huu kutokana na kushindwa kukwepa vizuizi vilivyowekwa
barabarani wakati akitokea kambi ya JKU, Msaani kwenda kambi ya Chambani.
Akizungumza baada ya mazishi hayo, Mkuu wa
Mkoa wa Kaskazini
Fakih alilaani mauaji hayo na kuahidi Jeshi la Polisi litaendelea kuwasaka
wahalifu waliohusika na kifo hicho.
Sumaye awanadi
wagombea wa CCM Moshi Vijijini na Vunjo
Na Rodrick Makundi, Moshi
WAZIRI Mkuu Fredrick Sumaye, amekutana na wananchi wa majimbo ya Moshi Vijijini
na Vunjo, katika ziara yake ya siku mbili mkoani hapa, ambapo alitumia nafasi
hiyo kuwanadi wagombea ubunge na udiwani kwenye kata zao alizotembelea wilayani
Moshi Vijijini.
Katika jimbo la Moshi Vijijini Sumaye ambaye pia ni mlezi wa chama mkoa wa
Kilimanjaro, aliwahutubia wananchi wa kata ya Kibosho Magharibi,eneo la Mlama,na
aliwataka wananchi wa eneo
maendeleo ambayo yamo katika ilani ya uchaguzi ya Chama.
Alisema kuwa pamoja na kuwa na mfumo wa vyama vingi, asilimia kubwa ya Watanzania
wanaamini kuwa CCM itashinda katika nafasi ya urais kwa asilimia kubwa wakati
nafasi za wabunge na madiwani zitachukuliwa na chama hicho pia kwa asilimia kubwa
katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu.
Katika kauli yake hiyo Waziri Mkuu Sumaye alidai kuwa wapinzani wenyewe wanaamini
kuwa rais ajaye ni wa CCM,na kwamba serikali itakayofuata itakuwa ni ya CCM,na
kwamba ilani itakayotekelezwa kwa kipindi chote hicho ni ya CCM.
“Yeyote yule
Kikwete, na anafahamu wapinzani hawawezi kuwapata urais, hata wao wenyewe
wanaogombea wanatambua
CCM,maana Kikwete atakuwa rais tu,” alisema Sumaye.
Aliongeza kuwa kutokana na hali hiyo viongozi wa serikali na Chama watatekeleza
ilani ya chama tawala, huku watendaji wake wakuu wakiwa ni viongozi kutoka ndani
ya chama kwani kwa kuweka kiongozi wa upinzani atapingana na ilani.
Hivyo akawataka wanachama wa Moshi Vijijini kumpigia kura mgombea wa CCM katika
nafasi ya ubunge ambaye atashirikiana na rais katika kuwaletea mandeleo wananchi
wa jimbo
mtusute”.
Alisema kuwa anaamini kuwa Dk. Chami atakuwa mbunge atakayetekeleza ilani ya
Chama katika jimbo
unaohusu masula ya kiuchumi kwenye serikali ya Rais Mkapa, ushauri ambao
umeonyesha mafanikio makubwa katika kukua kwake.
Pia aliwaambia wananchi hao kuwa madai ambayo yanatolewa dhidi ya Dk. Chami sio
ya kweli bali yamelenga kumchafua kwa lengo la kumkosesha kura wakati wa
uchaguzi.
"Hawa wanaosema kuwa Dk.Chami ni
mfagiaji wa ofisi ya rais wana
kukosa sera, mimi nawathibitishia kuwa ni mtu mwenye digirii mbili za uchumi na
serikali inalitambua
Waziri Mkuu.
Akatoa takwimu katika uchaguzi wa mwaka 2000,kuwa CCM ilishinda viti 202,wakati
upinzani walishinda viti 14,ushindi ambao ni wa asilimia zaidi ya 96,na
kutahadharisha kuwa huenda idadi ya viti vya upinzani bungeni ikapungua kwa mwaka
huu.
“Haya makelele yote wanayopiga hawa wapinzani na hata kufanya maandamano na fujo
ni katika kutetea viti hivyo kumi na vinne tu,na nina wasiwasi mwaka huu huenda
hata viti vitano wasipate,” aliongeza Sumaye.
Alipozungumza mara baada ya utambulisho, Dk. Chami alimhakikishia Waziri Mkuu
kuwa CCM katika jimbo la Moshi Vijijini linafanya kampeni za utulivu pamoja na
kuwa na maneno ya kashfa na kejeli yanayotolewa na wapinzani jimboni humo.
Akasema kuwa maneno
kuamua kuvihama vyama hivyo kwena CCM,kutokana na kejeli hizo badala ya kueleza
sera za vyama vyao wakati wa kampeni.
Hata hivyo,aliwataka wanachama wa CCM,kuendeleza ushirikiano uliofanywa wakati wa
kampeni kabla ya kuahirishwa kwake,kwa kutofanya fujo,au kujibu tuhuma za
wapinzani kwani hali hiyo inaweza kutia doa chama,hivyo kupoteza sifa kwa wapiga
kura wake.
Kwa upande wa mgombea wa Vunjo Aloyce Kimaro aliwataka wananchi na wanachama wa
CCM jimboni humo kuipigia kura CCM,ili iweze kutekeleza ahadi zake za maendeleo
na ambazo zimo kwenye ilani ya uchaguzi wa mwaka huu.
Alisema tangu upinzani kulishikilia jimbo la Vunjo kumekuwa mahitaji duni ambapo
miundombinu
kiwango cha kumtosheleza kila mwananchi.
Alisema kuwa CCM ina nia thabiti katika kuyatekeleza mambo hayo,ambapo wananchi
wanalo jukumu kubwa la kuipigia kura ili iwe na nafasi ya kuonyesha hayo.
UVCCM Shinyanga
Vijijini wampongeza Karume
Na Anthony Komanya, Shinyanga
UMOJA wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi, wilaya ya Shinyanga Vijijini wamempongeza
Rais Amani Abeid Karume, kwa ushindi wake mnono uliomwezesha kuendelea kushika
kiti cha Urais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.
Katibu wa UVCCM Shinyanga Vijijini, Richard Pambe, alisema ushindi huo wa Rais
Karume, unadhihirisha jinsi wananchi wa
uongozi wa CCM.
Umoja huo pia umelaani kitendo cha wafuasi wa chama cha Cuvic United Front (CUF),
kuwashambulia na kuwadhuru waandishi wa habari mapema mwezi huu.
Novemba 5 kwenye Makao Makuu ya CUF, eneo la Buguruni,
jijini
waandishi wa ITV, Chanel Ten, na Star tv, walishambuliwa na vitendea kazi vyao
kuharibiwa na watu wanaodhaniwa kuwa wafuasi wa CUF.
Ujenzi wa benki ya damu waanza Tabora
Na El-hadji Yuusuf, Tabora
UJENZI wa kituo cha utunzaji wa damu salama umeanza kufanyika katika hospitali ya
mkoa wa Tabora ya Kitete, ambao unatarajia kukamilika katika kipindi cha miezi
mitatu ijayo.
Kaimu Mganga Mkuu wa mkoa wa Tabora, Dk. Amos Nsheha, alisema ujenzi huo
unaofanywa na Shirika la Msalaba Mwekundu Duniani utasaidia wagonjwa wanaohitaji
kupatiwa damu katika hospitali hiyo kupata damu salama.
Alisema damu itakayokuwa ikihifadhiwa katika kituo hicho, itakuwa salama kwa
sababu itaangaliwa
kusababbisha madhara kwa mgonjwa.
Dk. Nsheha alisema katika kituo hicho kutakuwa na mashine ya kisasa za kupima
damu ili kuifanya iwe salama na kuzuia maambukizi ya magonjwa yanayoweza kutokana
na mtu kuongezewa damu.
Alisema hata hivyo benki hiyo ya damu katika siku za mwanzo itakuwa ikipokea damu
inayochunguzwa katika hospitali ya Bugando, ambayo kwa sasa ndiyo yenye kituo cha
kisasa cha uchunguzi wa magonjwa katika mikoa ya kanda ya kati, ziwa na
magharibi.
Alisema kuwa kituo hicho kinatarajia kuwahudumia wakazi wa mikoa ya Tabora,
Rukwa, Singida, Shinyanga, Kigoma na
Hata hivyo, Dk Nsheha, hakuweza kueleza gharama halisi zinazotumika katika ujenzi
wa kituo hicho, lakini alisema mkandarasi kwa ajili ya kuanza kazi hiyo
amekwishafika mkoani Tabora.
Wakati huo huo, hospitali ya Kalunde inatarajia kuanza kazi ya utoaji wa huduma
kwa wagonjwa Jumatatu wiki ijayo, baada ya ukarabati uliokuwa ukifanyika katika
hospitali hiyo kukamilika.
Dk. Nsheha, alisema ukarabati huo umefanyika kwa kipindi cha miezi sita,
ulifanywa baada ya hospitali hiyo kuwa katika hali mbaya, kutokana na kuwa na
majengo chakavu na kutokuwa na vifaa vya kisasa kwa ajili ya utoaji wa tiba.
"Hamasisheni
kupata ushindi wa kishindo'
Na Eva Musiba, Mwanza
KATIBU Umoja wa Vijana Mkoa wa Mwanza Ghati Abubakar amewataka vijana wasibweteke
kwa kudhani kuwa CCM tayari imeshinda na kuwa wafanye uhamashishaji ifikapo
Desemba 14 kuhakikisha Chama kinashinda kwa kishindo.
Aliyasema hayo alipokuwa akizungumza na viongozi mbalimbali wa umoja huo katika
ofisi za Chama, zilizoko uwanja ya CCM Kirumba jijini hapa.
Ghati amewaasa vijana kudumisha amani iliyoachwa na wasisi wa Taifa hili, kwani
nchi mbalimbali zinazipigana, vijana ambao ndiyo wenye nguvu wanaathirika zaidi
ikiwemo pia na wanawake, watoto na wazee.
Aliwataka vijana kuwa wadadisi na kutekeleza majukumu ya kufanya kazi za Chama
kwa uaminifu na kuhakikisha wapinzani wanarejea CCM katika hali ya utulivu na
amani.
Akizungumzia kuhusu chipukizi aliwataka viongozi kuahakikisha wanapata mafunzo ya
malezi bora, usafi na tabia njema ili kuwaandaa kuwa viongozi wema na waadilifu.
Kanisa Anglikana sasa kuongeza idadi ya watoto yatima inaowasomesha
Ni kutoka 92 hadi 250
Na Solomon Mwansele, Mbeya
ASKOFU wa Kanisa la Anglikana Dayosisi ya Kusini, John Mwela amesema kanisa lina
mpango wa kuongeza idadi ya watoto yatima linaowasomesha kutoka 92 hadi kufikia
250 ifikapo mwaka 2007.
Aliyasema hayo jana wakati akikabidhi msaada wa sare za shule na vyakula kwa
watoto yatima katika kata ya
Askofu Mwela alisema kwa sasa
kanisa
elimu ya msingi na kwamba wanafunzi watatu wanasomeshwa chuo kikuu na chuo cha
mipango na kwamba kanisa limeanzisha miradi ili liweze kuwahudumia yatima wengi
zaidi.
Naye Mkuu wa wilaya ya Mbeya, Moshi Chang'a akizungumza katika hafla hiyo,
alikemea tabia ya baadhi ya wanawake wasiotaka kuwajibika na waliokata tamaa na
kuwaacha watoto wao wawe ombaomba mitaani wakati wanao uwezo wa kuwalea.
Alisema Mkoa wa Mbeya unaoonekana kuwa una idadi kubwa ya watoto yatima kutokana
na kutofanyika kwa utafiti kubaini
wapi kati
msaada na ambao wanao walezi wenye uwezo lakini wamewatelekeza.
"Watu wengi wamewekeza katika kuchangia sherehe na mashindano yasiyo na na
manufaa kwa jamii huku wakiwaacha watoto wao wakizurura mitaani na kukosa haki
zao za msingi," alisema Chang'a.
Mkuu huyo wa wilaya alisema ni aibu kuona baadhi ya watu wanaona ni heshima kuwa
na watoto yatima na kutafuta misaada, wakati uwezo wa kuwalea wanao na kuwa
misaada kwa yatima itolewe baada ya kufanyika utafiti wa kina ili wenye shida
wasaidiwe.
Wito kwa wana-Korogwe kuungana na kuunda klabu
Na Esther Katua
WANANCHI wa Wilaya ya Korogwe waishio maeneo mengine ya nchi wametakiwa kuungana
na kuunda klabu kwa lengo la kuchangia maendeleo ya wilaya hiyo.
Hayo yalisemwa jana na Makamu Mwenyekiti wa Klabu ya wanananchi wa Korogwe
waishio Dar es Salaam Luteni Kanali Iddi Kipingu alipokuwa akizungumza na
waandishi wa habari kwenye ukumbi wa Idara ya Habari (MAELEZO) mjini Dar es
Salaam
Kipingu ambaye alizungumza kwa niaba ya mlezi wa klabu hiyo, Luteni mstaafu Yusuf
Makamba alisema wanachama waliokutana hivi karibuni wamechagua viongozi wa muda
kwa ajili ya kuongoza klabu hiyo.
Aliwataja viongozi wa muda waliochaguliwa na nafasi zao kwenye makano kuwa ni
Makamba (Mlezi), Martin Mvaa (Mwenyekiti), Kipingu ( Makamu Mwenyekiti), Nicholas
Kingazi ( Katibu) na Issa Lupatu (Mhazini).
Wengine ni wajumbe watano, Profesa Maurice Mbago, Christopher Shekiondo, Ayubu
Mbegha, Hemed Kimea na Maurice Sapanjo.
Alisema kuwa klabu inaandaa katiba rasmi kwa ajili kuisajili kwa mujibu wa
taratibu za kisheria.
Kipingu alisema wanananchi wa Korogwe waishio mikoa mbalimbali nchini hawana budi
kuanzisha klabu kama iliyoanzishwa
kuchangisha fedha kwa ajili ya kuchangia maendeleo ya wilaya ikiwa ni pamoja na
ujenzi wa shule na hospitali.
Alisema wana-Korogwe waishio
lengo la kuendeleza vitu mbalimbali vilivyokufa wilayani humo ikiwemo mazao ya
biashara.
"Kwenye klabu hii iliyoanzishwa juzi, tumeazimia kumalizia ujenzi wa madarasa
manne kwenye shule ya Sekondari ya Chifu Kimweri ili kuokoa wanafunzi wanaokosa
nafasi ya kujiunga na sekondari pamoja kuwa wamefaulu," alisema Kipingu.
Alisema mbali na ujenzi wa madarasa hayo manne, wanachama waliazimia kukarabati
jiko la hospitali ya wilaya ya Magunga ambalo ni bovu.
" Pamoja na uchache tuliokuwa nao lakini kwa kuwa tulikuwa na malengo,
tulifanikiwa kuchangishana sh. 5,580,000 na hii ni kwa ajili ya kumalizia ujenzi
wa madarasa manne na tunawaomba wenzetu wengine wajitokeze hasa wa mikoa mingine
kwa ajili ya kufanikisha lengo letu," alisema Kipingu.
Alisema shule hiyo ya Chifu Kimweri, iliyoanza kujengwa mwaka jana ina madarasa
mawili ambayo yana wanafunzi wanaopaswa kuingia kidato cha pili mwakani, hivyo
inawalazimu kujengwa madarasa mengine mawili ili wanafunzi hao wapate madarasa ya
kuhamia na kuwapisha wanafunzi wapya wa kidato cha kwanza mwakani.
Kipingu alisema ili shule ikamilike zinahitajika jumla ya sh. milioni 25.
Mgodi wa Kiwira mfano bora wa uwekezaji - Mangula
Na Bashir Nkoromo, Mbeya
KATIBU Mkuu wa CCM, Philip Mangula amesema mgodi wa Mawe wa Kiwira mkoani Mbeya
hapa ni kielelezo cha mfano bora wa uwekezaji.
Mangula alisema hayo juzi alipotembelea mgodi huo wakati akielekea wilaya ya
Rungwe kuhutubia mikutano ya kampeni katika majimbo ya Rungwe Magharibi na Rungwe
Mashariki .
Alisema tangu mgodi huo uwe chini ya mwekezaji kampuni ya Tanpower Resources
Limited, umekuwa na mafanikio.
Akipatiwa maelezo kuhusu mgodi huo, Mkurugenzi wa Kampuni hiyo, Evans Mapundi
alisema sasa una wafanyakazi zaidi ya 4,000 na ndio unaoipatia gridi ya Taifa
umeme unaokwenda Tukuyu, Mbeya na Kyela.
Akieleza mipango ya baadaye Mapundi alisema, mgodi una mpango wa kuanzisha
uzalishaji wa gesi mwakani au mwaka 2007.
Alisema, awali mgodi ulikuwa ukimilikiwa na
STAMICO lakini baadaye ukabinafsishwa kwa Wachina ambao nao wameuza hisa na
kujindoa na sasa unaendeshwa na kampuni yake kwa ushirikiano wa kampuni nyingine
tatu.
Alisema, binafsi anaona fahari mgodi huo kupiga hatua kwa sababu ni sehemu ya
utekelezaji wa Ilani ya CCM ambapo sehemu kubwa ya hisa na wafanyakazi ni
wazalendo wa hapa nchini.