UHURU 19.11.2005
Wakulima Mtwara
wafungia korosho ndani
Na Rashid Mussa, Masasi
WAKULIMA wa korosho nchini, msimu huu wamekataa kuwauzia wafanyabiashara kwa
sababu wamekiuka makubaliano yaliyokuwa yamefikiwa ya kwamba bei ya kilo moja
isiwe chini ya sh. 600.
Makubaliano ya bei hiyo ya sh. 600 kwa kilo yalifikiwa katika mkutano wa pamoja
uliofanyika Septemba 18, mwaka huu mjini Mtwara.
Uamuzi huo wakulima kugoma kuuza korosho zao kwa wafanyabiashara ulifikiwa jana
katika mkutano wa wadau wa korosho nchini uliyofanyika mjini Masasi ambapo
wakulima hao kutoka wilaya mbalimbali walitaka matatizo yaliyojitokeza katika
ununuzi msimu huu yasihushwe na uchaguzi kwa kuishutumu serikali ama chama
chochote cha kisiasa.
Kufuatia uamuzi huo ambao ulikuja baada ya upande wa wafanyabiashara kuweka
msimamo mkali ulioonekana kuwadhalilisha wakulima wa kutotaka kujadiliana kiwango
cha bei mpya waliyoweka wao cha sh. 400 kwa kilo moja, wakulima wameiomba
serikali kupitia wizara yake ya ushirika na masoko kushughulikia tatizo hili ili
kupata ufumbuzi wa haki.
Mkutano huo uliwalaani wafanyabiashara hao kwa kutaka kuwachonganisha wananchi na
serikali ili ionekane haimjali mkulima na kutaka kutumia uwezo wao kuvuruga
uchaguzi ama kusaidia baadhi ya vyama vya siasa kwa kuwapa hoja ya kushuka kwa
bei itumike katika kampeni.
Mkulima mmoja kutoka Ruangwa, alishangiliwa na umati mkubwa wa wakulima hao
alipochangia kuwa wao watabaki na korosho zao na kwamba wanatambua kuwa suala
kura katika uchaguzi ujao.
Mkutano huo uliokuwa chini ya uenyekiti wa mkulima kutoka Tandahimba, Adinani
Bakari Mbwana na mwenza wake mfanyabiashara Arom Amar wa Kampuni ya Olam
kuuza kwa bei hiyo wanayotaka wanunuzi.
Nao wafanyabiashara wakizungumza na mwandishi wa habari hii mara baada ya mkutano
kuvunjika, walisema wamefadhaishwa na msimamo mkali wa wakulima katika mkutano
huo na kwamba hawana la kufanya na kwamba wamekwishawasiliana na wanunuzi wao
waliyo kwenye vituo vya ununuzi kusimamisha na kuondoka.
Hali hii ikiwa na maana kuwa msimu wa ununuzi wa korosho mwaka huu umevurugika,
ambapo habari kutoka vijijini zinasemekana kuwa wapo baadhi ya wakulima wanaouza
korosho zao kwa kati ya sh. 150 kwa kilo hadi 400 kutokana na dhiki na matatizo
makubwa yanayowakabili wakati huu.
Wakulima waliwakilishwa katika mkutano huu na viongozi wao wa vyama vya ushirika,
na wengine binafsi waliokuja kwa malori, mabasi kutoka wilaya mbalimbali za mikoa
ya Mtwara,
waliwashtumu wafanyabiashara hao kwa kushusha bei kiholela bila kufuata taratibu
walizojiwekea.
Karibu wazungumzaji wote kutoka wilaya mbalimbali waliokuja kwa gharama zao
walidai kuwa wamechoka kudhalilishwa na wafanyabiashara hao kila mwaka bila
kujali shida na matatizo yanayomkabili mkulima wa korosho miaka hii ambapo
gharama za uzalishaji zinapanda kila mwaka.
Wafanyabiashara hao ambao nao kampuni zao karibu zote zilituma wawakilishi katika
mkutano huu kwa mujibu wa barua waliyoiandikia CBT na kutolewa maelezo katika
mkutano huu na mwenyekiti mwenza Amar wameshusha bei kutoka sh. 600 kwa kilo moja
hadi sh. 400 kwa madai ya bei soko
la nje imeporomoka
Hata hivyo, madai hayo yalishindwa kuthibitishwa katika mkutano huo kwa kukosa
vielelezo ambapo bodi ya korosho nchini CBT ilitoa vielelezo vya kuonyesha bei ya
nje ya zao hili kwa sasa imethibitika kuwa haijashuka kwa kiwango hicho
lilichokuwa kinadaiwa cha dola za Kimarekani 200 kwa tani.
Bodi ya Korosho iliwasilisha vielelezo vinavyoonyesha kuwa tani moja katika soko
la
wafanyabiashara hao walidai kuwa
wameambiwa na wanunuzi wao huko
dola za Marekani 700.
Kufuatia malumbano hayo yalifanya kikao hicho kuvunjika kabla ya kufikia mwafaka
wa bei mpya baada ya mwenyekiti mwenza ambaye anatoka upande wa wafanyabiashara
kukataa kujadiliana ili kupata bei mpya badala hiyo ya sh. 400 ambayo wakulima
wanadai kuwa ni ya chini mno itakayoua kilimo cha zao hili kwa kulinganisha na
gharama.
Anayedaiwa jambazi
sugu ajisalimisha polisi Dar
MMOJA wa watuhumiwa wa matukio ya ujambazi na uporaji kwenye mabenki, Sixtus
Alfred Ngowi (42) mkazi wa
kujisalimisha jana kwenye Kituo
Kikuu cha Polisi mjini
Kamanda wa Polisi Mkoa wa
alijisalimisha jana mchana na alikuwa anahojiwa na polisi kuhusiana na matukio
mbalimbali ya ujambazi.
“Amejisalimisha leo (jana) mchana na tunaendelea kumhoji kutokana na matukio
mbalimbali ya ujambazi kwenye benki mbalimbali jijini,” alisema Tibaigana.
Novemba 11, mwaka huu, Kamanda Tibaigana alitangaza kuwatafuta watu watatu
wanaodaiwa kuwa watuhumiwa sugu wa matukio ya ujambazi ikiwemo uporaji kwenye
mabenki.
Watuhumiwa wengine waliotangazwa kutafutwa pamoja na Sixtus ni mkewe ambaye jina
hayajulikani na Sadiki Fatee mkazi wa Muheza mkoani Tanga ambaye umri wake
haukufahamika.
Alisema kuwa watuhumiwa wote wanaonekana mara kwa mara
1.6 kutoka Kampuni ya Security Group ambayo wafanyakazi wake na watuhumiwa
wengine 18 wana kesi inayoendelea katika Mahakama ya Kisutu.
Ngowi anamiliki kituo cha vinywaji baridi kiitwacho Cold Cap kilichopo jijini Dar
es Salaam, ambapo mkewe ambaye hadi sasa amejificha, anatafutwa kwa tuhuma za
kushirikiana na mumewe baada ya nyumbani kwake kukutwa kasha la fedha lililoibwa
kwenye Kampuni ya Security Group.
Polisi inaendelea kuwatafuta Fatee na Mongi.
DC Chunya atoa
changamoto CHUTCU kujenga sekondari
Na Mwandishi Wetu, Chunya
MKUU wa Wilaya ya Chunya, Frank Uhahula, ametoa changamoto kwa Chama Kikuu cha
Wakulima wa Tumbaku wilayani humo (CHUTCU), kujenga shule za sekondari kwa ajili
ya kuwapatia watoto wao nafasi za kuendelea na masomo ya sekondari.
Alisema hayo jana alipokuwa akifungua mkutano mkuu wa mwaka wa chama hicho chenye
jumla ya muungano wa vyama 18.
Uhahula alisema inasikitisha kuona wakulima wamekuwa wakiuza tumbaku vizuri na
kupata fedha lakini wilaya hiyo ina shule nne tu za sekondari na watoto wamekuwa
wakihangaika kutafuta shule katika maeneo mengine au kukosa kabisa na kuwa
wazururaji.
"Katika jimbo hili la Lupa kuna shule moja tu ya sekondari... pesa tunapata
lakini hatujui kuzitumia, ni vizuri tukawekeza katika elimu kwa watoto wetu ambao
ndiyo watakuwa viongozi na wakulima wenye elimu hapo baadaye," alisema.
Alliwataka wakulima hao kuongeza mchango wao katika elimu na kuachana na sh. 10
wanayotoa katika mfuko wa maendeleo
ya elimu wauzapo mazao
kiwango hicho cha pesa ni kidogo
"Mfikirie kuongeza ili kwa kusaidiana... tutakwenda haraka, kwani bado tunatambaa
hata kutembea hatujaanza," alisisizia na kusema kuwa kipato cha mauzo ya tumbaku
hivi sasa kimeongezeka lakini hakilingani na maisha halisi ya wakulima na familia
zao.
Aliwataka viongozi wa vyama hivyo kushirikiana na serikali katika kutoa elimu kwa
wakulima kwa ajili ya matumizi mazuri ya fedha wanazozipata badala ya kuishia
vilabuni huku watoto na familia zao zikikosa huduma muhimu.
Alisema siyo tu masuala ya elimu, wakulima wanapaswa kufikiria pia huduma
wanazozihitaji wilayani humo badala ya kuitegemea serikali peke yake.
Alivitaka vyama hivyo pia kuanzisha mpango na mafunzo ya utunzaji mazingira,
kwani kilimo cha tumbaku kimekuwa ni adui mkubwa wa Mazingira. Aliwataka wakulima
wa tumbaku kupanua mashamba
ajili ya ukakushaji wa tumbaku.
"Ni muhimu mkasimamia program ya hifadhi ya mazingira ili tusiendelee kukata
misitu yetu ovyo na kusababisha ukame hapo baadaye," alisema Uhahula na kuwataka
wakulima hao sasa kuanza kutumia teknolojia ya kisasa ya ukaushaji tumbaku badala
ya kutumia magogo ya miti.
Kanisa Katoliki
Songea ‘laiangukia’ serikali
Na Mwandishi Wetu
Kanisa Katoliki jimbo la Songea, limeiangukia serikali ya
mkoa wa
kuomba radhi kufuatia kujiingiza kwenye siasa, kwa kuonekana likimfanyia kampeni
waziwazi mmoja wa wagombea wa vyama vya upinzani.
Hali hiyo ilionekana hapa kuhatarisha amani katika kanisa
waumini kuwazomea viongozi wake, hususan mapadre wakati wa ibada.
Akiomba radhi kwa Mkuu wa Mkoa wa
ofisini kwake jana, Mwenyekiti wa
Baraza la Walei la Kanisa
alisema Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Songea, halitarudia tena kuhubiri siasa
kanisani na kwamba litaendelea na mahubiri ya kiroho kwa misingi ya haki na
kulinda heshima ya kanisa
Mwenyekiti wa baraza
wajumbe wawili, alikutana na mkuu wa mkoa na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya mkoa
wa Ruvuma, ambao kwa pamoja
walisisitiza kanisa
wanasiasa wenyewe huku kanisa likiwa katikati ya wote.
Jumapili iliyopita kanisa
waumini wake kutokana na mtafaruku uliolikumba kwa muda wote tangu kampeni zianze
kutokana na kanisa kujitumbukiza kwenye mahubiri ya kisiasa hali iliyosababisha
amani kanisani hapo ivunjike.
Pia, hali hiyo ilisababisha katika ibada zote waumini kusali chini ya ulinzi
mkali wa polisi wa sare na wasiovaa sare.
Akijibu, Mkuu wa Mkoa, Jenerali mstaafu Kalembo alisema Kamati ya Ulinzi na
Usalama ya Mkoa imefurahishwa na hatua hiyo ya Baraza la Walei kupiga marufuku
mahubiri ya kisiasa katika makanisa yote ya katoliki ambayo ndiyo yanalalamikiwa
na wananchi na waumini na kwamba serikali haina tatizo na madhehebu yoyote ya
dini ilimradi yafuate sheria.
Alionya kuwa serikali haitavumilia kuona amani
Inavunjika, hasa kutokana na wanaosababisha ni viongozi wa dini, badala yake
hatua kali zitachukuliwa endapo hali hiyo itaendelea tena kwa vile madhara yake
ni makubwa
Jumapili iliyopita waumini wa
kanisa
Polisi huku wengine wasiovaa sare waliingia ndani ya kanisa na wale waliovaa sare
walikaa nje ya kanisa na waliondoka baada ya ibada kumalizika.
Waumini wa kanisa
kumfanyia kampeni mgombea ubunge wa CHADEMA, Edson Mbogoro, dhidi ya wagombea wa
vyama vingine vikiwemo CCM, TLP, CUF na NCCR-Mageuzi.
Ujumbe wa kanisa
kuomba radhi Chama cha Mapinduzi, ambapo walipokewa na Katibu wa CCM mkoa wa
hapa.
Viongozi wa dini ya Kiislamu wampongeza Rais Karume
Na Mwandishi Maalum,
Kadhi Mkuu, Mufti Mkuu na Makadhi
wa wilaya za
kuchaguliwa tena kuendelea
kuiongoza
mitano.
Pongezi za viongozi hao wakuu wa dini nchini zilitolewa jana wakati walipofanya
mazungumzo na Rais Karume, Ikulu mjini hapa.
Viongozi hao wa dini walieleza kuwa wameridhishwa na kufarajika kutokana na
matokeo ya uchaguzi mkuu wa
na utulivu jambo ambalo wamesema ni kiini cha maadili mema ya dini.
“Katika kipindi hiki kinachofuatia uchaguzi mkuu wa Oktoba 30, wananchi hawana
budi kuzingatia umuhimu wa amani na kutokana na msingi imara wa maelewano na
ushirikiano uliotandikwa kwa kushirikiano na serikali iliyopo madarakani, ni
hatua njema itakayowahakikishia wananchi kuishi kwa maendeleo na mafanikio
makubwa zaidi,” walieleza viongozi hao wa dini katika salamu zao za pongezi.
Ujumbe huo wa watu wanane, uliyoongozwa na Kadhi Mkuu ulimtakia heri na mafanikio
Rais Karume katika juhudi zake za kuwapatia maendeleo
wananchi wa
Rais Karume aliwaeleza viongozi hao wa dini kuwa Serikali ya Mapinduzi ya
na utulivu.
“Serikali itaendelea kwa hali na
dini ili kuiwezesha jamii kuishi katika maadili mema katika azma yake ya
kuiendeleza kimaisha,” alisisitiza Rais Karume.
Rais Karume aliwapongeza viongozi wote wa kidini nchini kwa kazi kubwa
waliyoifanya na wanayoendelea kuitekeleza katika kuisaidia jamii kuishi kwa
maelewano.
“Mafanikio makubwa yameonekana kutokana na uwezo wenu mkubwa na nia zenu njema
katika kuiongoza jamii kufuata maadili mema, na kusaidia kupata suluhu ya
matatizo mengi ya wananchi katika jamii,” alisema.
Aliendelea kusema kuwa serikali imeridhishwa na kazi inayofanywa na viongozi hao
wa dini na aliwashauri waendele kwa moyo huo huo katika kuwasaidia wananchi
kutatua matatizo
mema katika jamii, kwani jambo jema siku zote huzaa mafanikio,” alisema Rais
Karume.
Ujumbe huo uliwakilishwa na Kadhi
Mkuu wa
Mufti Mkuu Sheikh Harith Bin Khelef Bin Khamis, Naibu Kadhi wa
Ali Khatib Mranzi, na Makadhi wa wilaya ambao ni Sheikh Omar Said Omar, Sheikh
Said Mahmood Abdulrahman, Sheikh Omar Mussa Makungu, Sheikh Nyange Omar Ali na
Sheikh Ali Zubeir.
Mahitaji ya wananchi
muhimu katika kutekeleza MKUKUTA
Na Pendo Mangala,
SERIKALI imeshauriwa kwamba ili iweze kutekeleza mkakati wa kukuza uchumi na
kupunguza umaskini nchini (MKUKUTA) kwa wananchi ni lazima ijue mahitaji husika
ya wananchi na namna ya kuyatekeleza.
Ushauri huo ulitolewa jana na Mwenyekiti Mtendaji wa TACAIDS, Meja Jenerali
mstaafu Herman Lupogo, alipokuwa akizungumza na kamati shirikishi za kudhibiti
ukimwi mjini hapa.
Lupogo alisema ni lazima serikali itambue mahitaji muhimu ya wananchi pamoja na
jinsi ya kuyatekeleza ndipo itaweza kwenda sawa na mkakati huo.
Alisema Serikali kupitia viongozi husika ndiyo yenye jukumu la kuyatambua
mahitaji ya wanachi hivyo haina budi kufanya hivyo.
Alisema endapo Serikali itafanya hivyo itaweza pia kutekeleza masuala mbalimbali
ya wananchi ikiwa ni pamoja na kuleta maendeleo ya nchi kwa ujumla.
Alisema viongozi wanatakiwa kujua mahitaji ya jamii kwanza ndipo waanze
kuwaelezea masuala mengine yaliyopo katika jamii husika.
Alisema kiongozi ama mtu yeyote mwenye madaraka ya uongozi anapokwenda kwa
wanachi na kuwakuta hawana mahitaji muhimu ya kijamii ambayo ni maji,afya na
nyinginezo inabidi awasikilize na kujua namna ya kutekeleza matatizo hayo na si
kuanza kuelezea masuala yake ambayo yatawafanya wasiyazingatie.
Aliipongeza Serikali kwakuanzisha mkakati huo wa kukuza uchumi na kupunguza
umaskini (MKUKUTA), kwani ukitumiwa vizuri utasaidia kupunguza umaskini miongoni
mwa jamii na nchi kwa ujumla hasa katika dunia iliyopo ambayo ni ya utandawazi.
Makamba akemea
umwagiliaji wa matofali kwa maji
Na Mwandishi Wetu
MKUU wa Mkoa wa
wakazi wa jiji
kubwa ya watu wanaokosa huduma hiyo.
Makamba aliyasema hayo jana wakati akifunga mkutano wa Umoja wa Uelimishaji na
Uhamasishaji Umma Sekta ya Maji Tanzania (WEMMA), uliofanyika katika ukumbi wa
mikutano wa Shirika la Majisafi na
Majitaka
Salaam.
Alisema mbali ya kitendo hicho kuwa si cha kiungwana, lakini pia kinakwenda
kinyume na sheria zinazosimamia
utoaji wa huduma za maji
Kwa mujibu wa Makamba tabia hiyo haipaswi kufumbiwa macho, hasa ikizingatiwa
kwamba maji hayo yanazalishwa kwa gharama kubwa na hivyo ni vyema yangetumika
Alisema gharama za uwekaji wa dawa katika maji na usambazaji wake ni kubwa na
kiwango kidogo kilichopo kinapaswa kutumiwa vyema badala ya kumwagilia matofali
na bustani.
Makamba alisema maji yana umuhimu mkubwa katika maisha ya binadamu na amewataka
wanachama wa WEMMA ambao ni Maofisa Uhusiano wa Mamlaka za Majisafi na Majitaka
Mijini
Alisema kutokana na umuhimu huo, serikali kupitia Chama Tawala imekuwa ikitoa
kipaumbele katika kuhakikisha huduma za maji zinaboreshwa siku hadi siku, juhudi
ambazo alisema zinapaswa kuungwa mkono.
Mapema akitoa maelezo ya umoja huo, Mwenyekiti wa WEMMA, Sebastian Warioba,
alisema ili kutimiza malengo ya umoja huo, WEMMA itaanzisha programu za pamoja za
elimu na uhamasishaji umma katika sekta ya maji katika masuala ya sera na sheria
zinazosimamia sekta hiyo.
Pia, WEMMA imelenga katika kuimarisha ushirikishwaji wa kinamama katika maendeleo
ya sekta ya maji nchini.
Tume yamthibitisha
Anna Komu kuwa mwenza
Na Mwandishi Wetu
TUME ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imemtangaza Anna Komu kuwa mgombea mwenza wa
Freeman Mbowe, katika kusaka urais wa Jamhuri ya Muungano kwa tiketi ya CHADEMA.
Mwenyekiti wa Tume hiyo, Jaji Lewis Makame, aliwaambia waandishi wa habari jana
kwamba Tume yake imepitia vielelezo vyote vinavyomuhusu Anna na kuridhika navyo,
na kwamba ametimiza taratibu za kisheria.
Alisema pamoja na Tume yake kumtangaza jana, mtu yeyote anayo nafasi ya kupinga
uteuzi huo kisheria katika muda wa saa 24 kuanzia jana hadi leo saa 10 alasiri.
Anna anakuwa mgombea mwenza wa Mbowe kufuatia kifo cha aliyekuwa mgombea mwenza
wake wa awali, Jumbe Rajabu Jumbe, aliyefariki dunia mwishoni mwa mwezi uliopita
na kusababisha uchaguzi uahirishwe kutoka Novemba 30 hadi Desemba 14, mwaka
huu.
Kuhusu hasara iliyotokea kutokana na kuahirishwa uchaguzi huko, Jaji Makame
alisema Tume yake imehitaji fedha zaidi za nyongeza.
Akifafanua zaidi Mkurugenzi wa Uchaguzi, Rajabu Kiravu, alisema gharama ya ziada
sasa itakuwa sh. bilioni 5.3 na kwamba sh. bilioni 2.1 kati ya hizo ni kwa ajili
ya kuchapisha karatasi za kupiga kura ya Rais, wakati sh. bilioni 3.2 zitatumika
kwa mafunzo yatakayotolewa kwa wasimamizi wa uchaguzi kwa muda wa siku moja.
Wakati huo huo, kampeni za uchaguzi mkuu kwa wagombea urais zinaanza tena leo
ambapo vyama vinne vyenye wagombea wa urais vitajitupa kwenye viwanja mbalimbali
kuomba kura.
Chama cha NCCR-Mageuzi leo kitatumia siku nzima kuomba kura katika mkoa wa
Mtwara, CHADEMA itahangaika kusaka kura Ukerewe na Ilala na Kinondoni mkoani Dar
es Salaam, wakati TLP kitaomba kura mkoani Kilimanjaro, na chama cha DP kitaomba
kura wilaya ya Kilolo mkoani Iringa.
Ratiba ya kampeni iliyotolewa na Tume inaonyesha kwamba kesho, CCM itanguruma
wilayani Lushoto mkoani Tanga, wakati CUF itakuwa ikihaha mkoani Mwanza na
Morogoro, huku CHADEMA ikiendelea na kampeni wilaya za Ilala na Temeke. Chama cha
SAU kitakuwa jimbo la Ukonga.
Ushindi wa CCM unategemea mchango wa wazee - Mapuri
Na Dunstan Bahai, Kondoa
CHAMA Cha Mapinduzi kimesema ushindi mkubwa kinaoutarajia kuupata katika uchaguzi
mkuu utategemea ushiriki na mchango wa wazee.
Kauli hiyo ilitolewa na Katibu wa Itikati na Uenezi wa CCM Taifa Omar Ramadhan
Mapuri kwenye ziara yake ya siku tatu aliyoifanya wilayani Kondoa. Ziara hiyo
imemalizika jana.
"Wazee kama mnaitakia mema
kuongeza kuwa misingi mizuri
iliyopo
Cha Mapinduzi.
Mapuri ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM
alisemna wazee ni dawa na kwamba kila jambo linalofanikiwa lazima wazee wametie
busara zao na kwamba CCM na serikali yake inathamini michango inayotolewa na
wazee.
Alisema endapo Watanzania watafanya makosa ya kuchagua vyama vya upinzani,
watazorotesha maendeleo ya kijamii yaliyokwishaanza kutekelezwa na CCM na kwamba
hata mipango ya baadaye ya utekelezaji iliyoandaliwa itazorota.
Mapuri alisema ushindi wa kishindo unaotarajiwa utafanikisha kuendeleza yale yote
mazuri yaliyokwisha anzishwa na serikali ya awamu ya tatu.
Kwa mujibu wa Mapuri, CUF inayolilia kushika dola itaipeleka pabaya nchi hii
kwani sera zao ni za visasi na chuki na kwamba CCM itaendelea kudumisha amani,
utulivu, mshikamo wa kijamii na kitaifa na Muungano ambao vyama vingine sera yake
ni kuvuruga hayo.
Hata hivyo alisema kwa uhakika CCM itapata ushindi mkubwa na kwamba imeanza
"Kule Zanzibar tumewanyoa na wembe mkali
ni kuficha vipara hivyo kwa kofia," alisema na kufafanua kuwa uchaguazi ulikuwa
wa huru na wa haki.
Japan yatoa msaada kwa sekondari tano za wasichana
Na Mwandishi Wetu
JAPAN imetoa msaada wa sh. milioni 292 kwa shule tano za sekondari za wasichana
kwa ajili ya ujenzi wa mabweni, madarasa na tangi la kuvunia maji ya mvua.
Msaada huo umelenga kupunguza adha wanayoipata wanafunzi katika shule hizo
likiwemo la kupata mimba kutokana na wengi wao kupanga kwenye nyumba za watu
binafsi na wengine wanapokwenda kutafuta maji.
Hati za makubaliano ya msaada huo zilitiwa saini jana mjini
nyumbani kwa Balozi wa Japan hapa nchini, kati ya Balozi wa nchi hiyo, Katsuya
Ikeda na wawakilishi wa shule hizo.
Shule zilizonufaika na msaada huo ni za Masasi, iliyopo mjini Masasi mkoani
Mtwara, Songea iliyopo mkoani
zilizopo mkoani Kigoma.
Shule ya sekondari ya wasichana Masasi imepata sh. milioni 53 kwa ajili ya
ununuzi wa samani, ujenzi wa tangi la kuvunia maji ya mvua na madarasa. Shule
hiyo iliwakilishwa na mkuu wake, Paulina Ndigeza.
Ismani ambayo katika hafla hiyo iliwakilishwa na mkuu wa shule, Dainess Myalla
akifuatana na Mjumbe wa Bodi ya shule hiyo, mbunge wa Ismani na Waziri wa nchi
Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera), William Lukuvi imepata sh. milioni 75.3 kwa ajili ya
ujenzi wa bweni na ununuzi wa samani.
Mkuu wa shule ya sekondari ya wasichana, Songea Mary Kisanji aliiwakilisha shule
hiyo iliyopata msaada wa sh.milioni 66.8 kwa ajili ya ujenzi wa bweni na ununuzi
wa samani
Shule za sekondari Myatazo na Nyarubanda ambazo ziliwakilishwa na Mkurugenzi wa
Shirika la Maendeleo la Kigoma (KDPA), Leonard Soza, mjumbe wa Bodi ya shule ya
Nyarubanda, Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira), Arcado Ntagazwa
zimepata sh.milioni 53.2 kwa ajili ya ujenzi wa bweni moja kila shule.
Katika hali isiyokuwa ya kawaida mwalimu wa
kujitolea kutoka
anayefundisha katika shule ya sekondari ya Wasichana Masasi alibubujikwa na
machozi ya furaha baada ya kutiwa saini hati za makubaliano ya msaada huo.
Satomi mara baada ya kutiwa saini hati hizo alimfuata Mkuu wa shule hiyo, Paulina
na kumbatia kwa takriban dakika moja huku akibubujikwa machozi ya furaha.
Alipoulizwa na mwandishi wetu sababu iliyomfanya ububujikwe machozi, Satomi
alisema amepata matumaini mapya ya kupatikana maji kwa uhakika shuleni hapo kwa
kuwa tatizo
wafanyakazi na wanafunzi.
Naye Mkuu wa shule ya sekondari Isman, Dainess alisema msaada huo ni ukombozi kwa
shule yake kwa kuwa utasaidia kupunguza tatizo la kupata mimba wanafunzi wake.
Alisema kwa wastani wanafunzi 12 hupata mimba kwa mwaka.
Dainess alisema hali ya taaluma katika shule hiyo ni mbaya kutokana na wanafunzi
kuishi katika nyumba za kupanga za watu binafsi hivyo imekuwa rahisi kupata
vishawishi vya kufanya ngono na kupata mamba.
Mgombea udiwani wa CHADEMA amfikisha mahakamani wa CUF
Ni kwa madai ya kumuita mchawi
Na Angela Sebastian, Bukoba
MGOMBEA udiwani kwa tiketi ya CHADEMA kata ya Kashai, Conchester Lwamulaza,
amemfikisha polisi mgombea mwenzake wa udiwani kwa tiketi ya CUF, Ramadhan
Bahati, akimlalamikia kuwa amemtukana.
Bahati alifikishwa kituo ha polisi cha mjini hapa jana, akidaiwa kumtuhumu
Conchester katika mikutano yake ya kampeni kwa kudai kuwa mgombea huyo ni mchawi.
Conchester ambaye pia alikuwa diwani wa viti maalum kupitia CHADEMA katika
kipindi kilichopita, anamlalamikia Bahati kuwa alimtuhumu hadharani katika
mkutano kuwa mama huyo ni mchawi kitendo ambacho alisema kimemdhalilisha mbele ya
watu.
Mlalamikiwa Bahati alipozungumza na mwandishi wa habari hizi jana, alikana
kutumia lugha za matusi katika mikutano yake na kudai mgombea mwenzake huyo
amefanya hivyo makusudi kwa lengo la kutaka kumharibia.
Bahati alisema anapanda jukwaani kunadi sera za chama chake na kuelezea yale
atakayowafanyia wananchi pindi akichaguliwa kuwa diwani wa kata hiyo, na kuwa
hawezi kupanda jukwaani kutoa lugha za matusi.
Alisema hakuwahi kutumia lugha za matusi katika mikutano yake na kuwa anazo kanda
zinazorekodiwa katika kila mkutano
anaoufanya na akataka zisikilizwe
lugha yoyote ya matusi.
Alidai mama huyo alifanya hivyo kwa sababu zake binafsi ili yeye akamatwe awekwe
ndani na kupelekwa mahakamani kwa lengo la kumdhalilisha.
Alidai pia mgombea mwenzake huyo alimlalamikia kuwa aliwahi kumkaribisha chakula
akakikataa na kudai haoni sababu ya yeye kumwandalia chakula kwa kuwa hata katika
kumbukumbu zake hajui
hatua ya kumwandalia chakula.
Polisi mkoani hapa imethibitisha wagombea hao kufikishana kituoni hapo na kuwa
walihojiwa na kuachiwa.
Sumaye awataka Moshi
mjini kubadilika
Na Rodrick Makundi, Moshi
WANANCHI wa jimbo la Moshi mjini wametakiwa kuondokana na dhana potofu ya
kutotaka kuongozwa na wanawake na badala yake wawaone ni viongozi wanaoweza
kuleta mabadiliko makubwa ya
kiuchumi katika kuboresha maisha
Kauli hiyo ilitolewa hapa na Waziri mkuu Fredrick Sumaye, alipohutubia mkutano wa
hadhara wa kumnadi mgombea ubunge
kwa tiketi ya CCM katika jimbo
Minde.
Sumaye ambaye ni mlezi wa chama mkoa wa Kilimanjaro alitoa kauli hiyo kwa kile
alichoeleza kumekuwa na dhana kuwa mwanamke hafai kuwa kiongozi bora na anayeweza
kuongoza wananchi.
Kutokana na hali hiyo alisema dhana hiyo inapaswa kufutiliwa mbali, kwani hata
sera ya CCM kwa serikali ijayo imetoa kipaumbele kwa wanawake kushika nyadhifa
mbalimbali serikalini na katika chama.
Akimnadi mgombea huyo wa ubunge jimboni humo, Waziri Mkuu alisema kutokana na
uzoefu alionao katika masuala ya
sheria, anaamini
wananchi wa Moshi mjini ipasavyo kwa kuzipanga hoja zenye ushawishi wa kutekeleza
sera na ilani ya CCM katika jimbo
"Mtu asiwadanganye eti mwanamke hawezi kuwaongoza, eleweni kuwa Minde (Elizabeth)
ni mwanasheria anayepanga hoja, sasa sisi tunaamini atakuwa mwakilishi imara na
mbunge atakayetetea wananchi watakaomchagua," alisema.
Akaongeza kuwa pamoja na kelele zinazopigwa na wagombea wa vyama vya upinzani,
hazitasaidia kumpata rais wa upinzani atakayeingia ikulu, hivyo iwapo serikali
ijayo itakuwa ya CCM sera zitakazotekelezwa zitakuwa za CCM.
Pia alisema hata wabunge wengi watatoka CCM na ndio watakaokuwa na nafasi ya
kupendekeza utekelezaji wa ilani kwa kupitisha hoja nyingi zinazotolewa na
wabunge hao wa CCM.
Sumaye aliongeza kuwa ili kutekeleza malengo hayo wananchi wanapaswa kumpigia
kura wagombea wote wa CCM kuanzia ngazi ya urais, wabunge na madiwani ili kuwa na
mzunguko wa viongozi bora wenye msukumo wa kutekeleza ahadi zinazotolewa.
"Ninyi wakazi wa Moshi mjini,napenda mfahamu iwapo mtakuwa na mbunge wa CCM, bado
pia mnalo jukumu la kuwa na madiwani wa CCM kwani hatutakiwi kuwa na halmashauri
inayoendeshwa na wapinzani, huku mbunge wake ni wa CCM," alisema na kuongeza kuwa
hiyo itapelekea kupingwa kwa kila kinachojadiliwa wakati wa vikao.
Kwa upande wake, mpiga debe wa CCM, Thomas Ngawaiya aliwaambia wananchi hao kuwa
iwapo watachagua kambi ya upinzani bado watakuwa katika wakati mgumu wa kupata
huduma zinazohitajika.
Alisema idadi kubwa ya wabunge wa chama kimoja ndiyo inayowezeshwa kupitishwa
hoja za kutekeleza ujenzi wa miundombinu katika majimbo na akaongeza kuwa
wapinzani wamekuwa wakishindwa
kutekeleza majukumu
bungeni.
Hivyo alidai wapinzani wataendelea kuwa wasindikizaji, bungeni huku CCM
ikiendelea kutekeleza majukumu yake na akatoa wito kwa wananchi wa jimbo la Moshi
mjini kuipa kura CCM.
Akizungumzia suala la jinsia katika uongozi Ngawaiya aliwataka wananchi kutambua
mchango mkubwa,wa aliyekuwa mbunge wa zamani Moshi Lucy Lamecki ambaye alileta
maendeleo makubwa na ambayo hakuna kiongozi yeyote aliyefikia hatua ya mbunge
huyo.
Aliainisha baadhi ya miundo mbinu hioyo kuwa ni pamoja na barabara, huduma za
afya, upatikanaji wa maji
kubwa na uwezo wa kuweza kuleta maendeleo kinyume na mtazmo wa watu wanaodai
mwanamke hawezi kuongoza.
Mgombea ubunge wa jimbo
huo kuwa iwapo watamchagua kuwa mbunge wao atahakikisha utekelezaji wa sera
zinazoelezwa na CCM unafanikishwa
katika jimbo
inao uwezo mkubwa wa kuwaangalia wananchi wake.
Mgodi wa Kiwira Mbeya kuongeza uzalishaji
Na Nico Mwaibale wa PST, Mbeya
MGODI wa makaa ya mawe Kiwira (KCM) mkoani Mbeya, unatarajia kuongeza uzalishaji
wa makaa kutoka wastani wa tani 150,000 kwa mwaka hadi zaidi ya tani 500,000
kuanzia mwaka ujao baada ya kupata mwekezaji mzalendo.
Mwekezaji huyo amekwisha tenga zaidi ya sh. bilioni mbili kwa ajili ya kufanyia
matengenezo na ukarabati wa mitambo, miundombinu na kununua vifaa vipya vya
kisasa vya mgodi huo.
Meneja mkuu wa mgodi huo, Abdul Adam, alisema jana kuwa mwekezaji huyo ameingia
ubia na serikali tangu Agosti mwaka huu, ambapo amechukua asilimia 88 ya umiliki
na serikali imebakiwa na asilimia 12, na kuwa tayari amekwishaanza kazi ya
ukarabati na matengenezo katika mgodi huo.
Hata hivyo, Meneja Mkuu huyo hakuwa tayari kutaja kiasi cha fedha kilichowekezwa
na mwekezaji huyo, lakini habari zilizopatikana mgodini hapo zilieleza kuwa mbia
huyo amenunua mgodi huo kwa kiasi cha sh. bilioni tano.
Mkurugenzi Mtendaji huyo, Balozi Evans Mapundi ambaye ndiye mwekezaji, alisema
baada ya kukamilisha matengenezo na ukarabati unaoendelea hivi sasa, mgodi
utakuwa na uwezo wa kuzalisha zaidi ya tani 500,000 za makaa ya mawe kwa mwaka
kutoka wastani wa tani 150,000 zilizokuwa zinazalishwa.
Mapundi alisema lengo ni kuuwezesha mgodi huo kuzalisha wastani wa tani milioni
moja ya nishati hiyo kwa mwaka na
kwamba
kijacho kutokana na kuweka vifaa vya kisasa na kufanyiwa ukarabati na matengenezo
ya mitambo iliyopo.
Alisema kampuni hiyo ya makaa ya mawe Kiwira hivi sasa inazalisha umeme wa
megawati sita ambao megawati moja inatumika mgodini hapo, 0.5 zinatumika katika
wilaya ya Kyela, na megawati mbili zinatumika wilaya ya Rungwe kupitia gridi ya
Taifa kwa mkataba na Shirika la
Umeme
Aliongeza kuwa hata hivyo, kampuni hiyo inakifanyia matengenezo kituo cha
kuzalisha umeme ili kuongeza uzalishaji kutoka megawati sita zinazozalishwa sasa
hadi megawati 50 ifikapo Januari 2007, kiwango ambacho kitazidi mahitaji kwani
mkoa wote wa Mbeya unatumia megawati 20 sasa.
Alisema umeme unaozalishwa mgodini hapo ni wa uhakika katika kipindi chote, kwani
hauathiriwi na hali ya hewa
hali ya hewa na ujazo wa maji katika mabwawa ya Mtera na Kidatu.
Balozi Mapundi alisema ana uhakika wa soko la makaa ya mawe katika kiwanda cha
Saruji cha Songwe Mbeya, Wazo Tanga, kiwanda cha SPM, viwanda vya chai, kiwanda
cha nguo cha New Mbeya Textile na
wateja wengine wadogo
na vyuoni, na kwamba wanatarajia pia kutengeneza makaa ya kiwango cha chini
kitakachowezesha kutumika majumbani.
Habari zaidi zimeeleza kuwa uboreshaji wa mgodi huo unakwenda sambamba na maslahi
ya wafanyakazi, ambapo kuanzia Januari mwaka ujao kiwango cha mshahara
kinatarajia kuongezwa kutoka sh. 50,000 hadi sh. 100,000 kwa mwezi kulingana na
mfanyakazi anavyozalisha.
Alisema katika kuboresha maslahi pia watoto watatu wa kila mfanyakazi
watagharamiwa masomo hadi ngazi ya chuo kikuu.
Mgodi huo una wafanyakazi 500 kutoka zaidi ya 1,500 waliokuwepo zamani, ambapo
wafanyakazi 300 kati