UHURU 20.10.2005

Kikwete abubujikwa na machozi ya furaha akihutubia Chalinze

MGOMBEA Urais wa Tanzania kwa tiketi ya CCM, Jakaya Kikwete jana alibubujikwa na machozi ya furaha aliwapowahutubia mamia kwa mamia ya wakazi wa Chalinze ambalo lilikuwa jimbo lake la uchaguzi wa bunge.

Hata hivyo kabla ya kwenda Chalinze kampeni yake alianzia Maili Kibaha Moja, ambako alisema akichaguliwa atabadili sura ya mji wa Kibaha kwa kuupatia viwanda badala kuendelea kuwa kivuli cha Dar es Salaam.

Akiwa Kibaha Maili Moja Kikwete alihutubia mkutano mkubwa wa kampeni mwanzoni mwa kampeni zake alizoanza jana katika mkoa wa Pwani na kusema hakuna njia nyingine itakayoweza kuubadili mji huo mdogo lakini mkongwe, kujikwamua mahali ulipo sasa kwa kuupatia viwanda ambapo alisema bado unategemea Dar es Salaam.

"Kibaha haina matumaini ya kubadilika kama haukufanyika mkakati huo ...isipofanyika hivyo utaendelea kuwa kivuli cha Dar es Salaam...hakuna shughuli muhimu zaidi ya viwanda itakayoweza kuleta mageuzi ya haraka ya kiuchumi katika mji huu", alisema Kikwete.

Aliwahakikishia wananchi wa mji huo kwamba hiyo si ahadi tu lakini ni suala ambalo tayari limo katika mikakati ya CCM iliyopangwa kutekelezwa iwapo itapewa tena ridhaa ya kuongoza kwa awamu ya nne.

Kikwete alisema kuwepo viwanda katika mji huu kutawezesha wananchi hasa vijana kupata ajira za kuajiriwa tofauti na zile za kujiajiri ambazo kwa upande waake pia alisema uongozi wake utazifanyia kazi.

Akiwa Chalinze Kikwete alibubujikwa na machozi jukwaani kwa furaha baada ya kukumbana na umati mkubwa wa watu katika mkutano wake wa kampeni aliofanya katika jimbo la Chalinze ambalo kabla ya kuteuliwa kugombea nafasi hiyo alikuwa mbunge wake.

'Kilio' hicho cha muda kilimfanya kutoendelea kuhutubia mkutano huo na kumwachia mgombea wa sasa wa ubunge katika jimbo hilo, Ramadhani Maneno.

Kabla ya kumkabidhi kuzungumza na wananchi, Kikwete alimpa wosia Maneno, akimweleza kwamba ili aweze kupata mafanikio katika jimbo hilo ni lazima aweke uungwana mbele.

Akamweleza kwamba ni lazima ahakikishe habezi wapigakura wake; anawasikiliza

na kuwa nao mara kwa mara katika kutatua matatizo mbalimbali kwa kadri ya uwezo wake.

Kikwete alimuusia kwamba mambo hayo na mengine mengi ikiwa ni pamoja na jitihada za kuwaletea maendeleo wana-Chalinze ndiyo sababu amefika alipo sasa.

Mapema kwenye mkutano huo aliweza kufanikisha kuzoa wanachama wapya 6446 kujiunga na CCM kati yao wakiwemo 1220 waliokimbia kutoka vyama vya upinzani.

Akiwa Mlandizi, Kikwete pia alizoa wanachama wapya 4117 waliojiunga na CCM kati yao 117 wakiwa ni waliotoka CUF wakiongozwa na Katibu wa chama hicho Wilaya ya Kibaha, Mohamed Pongwe.

Mgombea huyo wa CCM, akizungumza katika mkutano wa hadhara, aliwaahidi wananchi kuwa Mlandizi karibu itapata maji ya uhakika hivi karibuni, kwa kuwa sasa awamu ya pili ya mradi wa maji unaofadhiliwa na Benki ya BADEA inakaribia kuanza.

Kikwete leo anaendelea na ziara yake ya kampeni mkoa wa Pwani.

UDHAIFU WA WAPINZANI

Kukosoa serikali iliyoko madarakani ni wajibu wa vyama vya upinzani. Aidha kujikosoa na kukosoana ni sera ya msingi ndani ya CCM. Suala la kukosoa, kujikosoa na kukosoana ndani ya CCM kwanza nikusemana au kuambizana ukweli, pili ni kuwa tayari kukosolewa bila kuhamaki, na tatu ni kuwa tayari kujirekebisha.

Lakini kukosoa kwa mambo ambayo hayasaidii kuimarisha demokrasia au hayana maslahi kwa taifa ni kupoteza muda. Kiongozi kuwaahidi wananchi kwamba akiingia Ikulu atauza ndege ya Rais, ukweli ni kwamba hata ndege ya Rais ikiuzwa bado Rais huyo atasafiri na fedha nyingi zitatumika au si ajabu hata kulazimika tena kununua ndege nyingine. Viongozi wa aina hiyo wanaonekana kukazania zaidi mambo yenye maslahi kwao binafsi kuliko yale ya wananchi.

Mwelekeo wa sera za Wapinzani hapa nchini hauwezi kuwapeleka Ikulu kwa sababu zinaashiria shari au mfarakano. Tangu nchi yetu iingie katika mfumo wa vyama vingi vya siasa sera za wapinzani zimeendelea kutawaliwa na matusi, kashfa, kejeli na vitisho kadha wa kadha.

Vipo vyama vya siasa ambavyo msingi na itikadi zao ni dini au kabila. Nani hajui madhara ya chama ambacho msingi wake ni dini au ukabila kwamba kitaleta mfarakano katika jamii? Vitendo vya kuwagawa wananchi kwa misingi ya dini au ukabila vimejipenyeza katika siasa na kugawa wananchi.

Ukabila pia umeanza kuenea katika baadhi ya vyama vya siasa kama mkakati wa vyama hivyo kuingia Ikulu. Baadhi ya viongozi wa vyama vya upinzani wamekithiri kwa kueneza uongo. Mara nyingi wakiwa wanahutubia mikutano ya hadhara wanajazwa na jazba, hasira na kuwaandama viongozi wa CCM kwa kuporomosha matusi hata ya nguoni, kashfa, kejeli na kadha wa kadha.

Kwa mfano katika mkutano mmoja wa hadhara nilimsikia kiongozi mmoja wa chama cha siasa cha upinzani akiwahutubia wananchi na kuwaambia kwamba mwisho wa elimu ya msingi ni darasa la nne. Hebu tujiulize hivi ni kweli hapa Tanzania mwisho wa elimu ya msingi ni darasa la nne? Je, nani hajui kwamba elimu ya msingi (std. 1-VII) ni ya lazima kwa watoto wote waliofikia umri wa kwenda shule?

Aidha nani hajui kwamba sasa hivi kuna mpango kabambe wa kupanua elimu ya Sekondari? Akiendelea kuhutubia idadi ya watu 60 waliohudhuria mkutano wake, alitaja mambo mengi ya uongo na kubwa kuliko yote ni kwamba CCM imekumbatia madaraka kwa zaidi ya miaka 40 na katika kipindi hicho hakuna chochote kilichofanyika na huku akijua wazi kwamba amesomeshwa na serikali za CCM na kabla yake TANU na ASP.

Wahenga wanatukumbusha kwamba”akutakanaye hakuchagulii tusi”. Hebu tujiulize hivi ni kweli katika kipindi chote cha zaidi ya miaka 40 CCM au kabla yake, hakuna chochote kilichofanyika? Je, hoja kama hizi ni nini kama si kukufuru?

Kama haitoshi bwana mkubwa aliendela kuwapotosha wananchi waliohudhuria katika mkutano kwa madai kwamba chama tawala kina mpango wa kuwafanya watoto wote waishie darasa la VII. Ati ili iwe rahisi kuwatawala wananchi wa Tanzania.

Leo hii nani hajui kwamba jitihada za serikali za sasa ni kuona kuwa kila kata ina jenga sekondari yake? Je, kwa viongozi wanaopotosha ukweli wa mambo, kweli wanastahili kupewa madaraka ya kuongoza nchi hii ifikapo Oktoba 2005?

HAWAKI AMANI

Watanzania wengi bado wanataka umoja wa taifa hili uendelee kuimarika na kwamba kazi hii iwe ni ya kudumu. Kadhalika Watanzania wanataka hali ya amani na utulivu nchini iendelee kuimarika na kudumishwa.

Kati ya vyama vyote vya siasa vilivyopo hapa nchini ni chama cha Mapinduzi peke yake ndicho chama ambacho kinaweza kuwahakikishia Watanzania kuwa kikishinda katika uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2005, basi umoja wa taifa na hali ya amani na utulivu nchini ni mambo yatakayoimarika na kuendelezwa.

Na kwa msingi huo lazima Watanzania watambue kwamba kauli za baadhi ya viongozi wa vyama vya upinzani, ni ushahidi tosha kwamba wenzetu hawana nia ya kuimarisha umoja wa taifa wala kuendeleza mazingira ya amani na utulivu nchini katika ajenda zao za kisiasa . Kauli na vitendo vyao vinaashiria mfarakano katika taifa, vurugu, uhasama na chuki.

Lakini ikumbukwe pia kwamba kuchochea vurugu kwa visingizio mbalimbali ili amani na utulivu uliopo nchini vitoweke ni kosa la jinai. Hali kadhalika matamshi ya baadhi ya viongozi wa vyama vya upinzai dhidi ya CCM na viongozi wake ni ishara tosha kwamba wapinzani hawana chochote cha kuwafanyia wananchi wa Tanzania.

Malengo yao ya kutaka Watanzania wafarakane ndipo waingie Ikulu, dawa pekee ya kuondokana na balaa hilo ni kutowapigia kura itakapofika Oktoba 2005 na hiyo ndiyo itakayowahakikishia Watanzania kuendelea kudumisha umoja wao wa kitaifa na nchi yetu kuendelea kuwa ya amani na utulivu.

Na kwa msingi huo, CCM ndicho chama pekee kitakachowahakikishia Watanzania wote kuwepo kwa umoja wa kitaifa, mshikamano, upendo, undugu na hali ya amani na utulivu. Chonde chonde Oktoba 30, 2005 twende tena tukakichague Chama cha Mapinduzi kwa manufaa ya nchi na vizazi vijavyo!

Tanzania ni ya Watanzania wote, na ujenzi wa taifa hili ni wa kila mwananchi hasa kila mzalendo bila kujali tofauti za kisiasa, kiuchumi, kabila, dini, jinsia au umajimbo.

Makundi mbalimbali katika nchi yetu yamekuwa yakiombea uchaguzi wa mwaka huu uwe wa amani na utulivu. Mimi nafikiri kuombea peke yake haitoshi. Ila kinachotakiwa kwa upande wa pili wa sarafu ya shilingi ni wananchi kukichagua Chama cha Mapinduzi, ambacho mwelekeo wa sera zake ni kujenga umoja wa kitaifa ili wananchi waendelee kujisikia kama ni taifa moja na chenye sera zinazounda mazingira ya amani na utulivu katika jamii na nchi.

Vyama vyote vya upinzani ambavyo sera zake zina mwelekeo wa itikadi za ukabila, udini, uzawa na kadhalika tuviogope kama Ukimwi au Ukoma. Lakini inapofika mahala Chama katika kunadi sera zake kinatamka wazi kwamba kama hakikushinda uchaguzi mwaka huu , damu itamwagika au nchi haitatawalika na sisi tunakipigia kura, hapo tunajitakia makubwa sisi wenyewe na wala tusije tukathubutu kumlaumu mtu. Kwa hiyo kama Watanzania wapenda amani na maendeleo tusifanye makosa ya kuviweka madarakani vyama ambavyo havitutakii mema.

Tanzania ni ya Watanzania wote, na ujenzi wa nchi ni wa kila Mtanzania na hasa kila mzalendo. Hivyo ukitaka maendeleo endelevu yaliyokwisha fikiwa hadi sasa Oktoba 30, 2005 , kila Mtanzania mpenda amani , aliyejiandikisha katika daftari la kudumu la wapiga kura, piga kura yako kwa CCM.

Mtazamo wa kulaumu na kushutumu kufumbia macho kila jema lililofanywa na chama Tawala (CCM) kwa kipindi kilichopita si kitendo cha uungwana hata kidogo. Wachina wana msemo unaosema “Ni heri kuwasha mshumaa kuliko kutukana giza”.

Katika nchi ya waungwana kama Tanzania , kila mwananchi anatakiwa kujihisi kama ni sehemu ya ufumbuzi wa matatizo na wala si mtazamaji au mtu wa kuelekeza tu au kuzua matatizo kila kunapokucha . Katika nchi kama Tanzania kila mwananchi ajione ni mdau wa ulinzi, usalama, amani na uhai wa maendeleo ya Taifa letu.

Aidha kila mwananchi akikubali kwamba yeye ni mdau wa taifa hili, akubali pia kushiriki katika kutafuta ufumbuzi wa matatizo yake binafsi na ya taifa kwa ujumla.

Viongozi hasa walioko katika kambi ya upinzani ni lazima wafike mahali na kutambua kwamba, maendeleo katika nchi maskini kama ya kwetu hayana budi kusimamiwa na watu wanaoona mbali, ambao uzalendo wao hautiliwi mashaka, viongozi wasioogopa kuwa wa wazi na wa kweli na wanaoweka mbele maslahi ya umma kwanza.

Tusipandikize chuki na kushamirisha mfarakano kwa kudhani nchi yetu itajengwa kwa siku moja tu. Kwa sababu katika nchi maskini kama ya kwetu ni vigumu kuweka vipaumbele. Kila kitu kinaonekana ni muhimu. Ni jambo la msingi kujua kipi kitangulie na kipi kifuate. Kupanga ni kuchagua.

Kipaumbele cha kwanza ni kuendelea kuboresha mazingira ya kisiasa na kiuchumi ili nchi yetu iendelee kuwa ya umoja na amani na wananchi waendelee kuishi bila hofu na wasi wasi. Na hiyo itawezekana tu kama Chama Tawala (CCM) kitapewa tena ridhaa ya kuwaongoza Watanzania kwa miaka 10 mingine ijayo.

KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI.

NA MAPINDUZI DAIMA.

Kampeni za kisiasa Arusha ni shwari – RC

Na Omari Shaaban, Arusha

MKUU wa mkoa wa Arusha, Mohamed Babu, amesema hali ya kampeni mkoani hapa ni nzuri na hakuna malalamiko yoyote katika harakati za kampeni za udiwani na ubunge kutoka kwa wagombea na wafuasi wao.

Babu aliyasema hayo jana wakati akifungua mkutano wa 15, wa mwaka wa Mfuko wa Hifadhi wa Mashirika ya Umma (PPF), kwenye ukumbi wa mikutano wa AICC, jijini hapa.

Alisema vyama vyote vinaendelea kufanya kampeni zake kwa nguvu bila ya kujaribu kuhatarisha amani katika mikutano yao.

"Tunashukuru Mungu kwamba mkoani hapa, hakuna lolote la kuhatarisha amani ambalo limetokea mpaka sasa katika kipindi hiki cha kampeni za Uchaguzi Mkuu wa Oktoba...na tuhakika hali itakuwa hivi hivi katika kipindi chote cha uchaguzi," alisema Babu.

Mkuu huyo wa mkoa alisema hakuna mgombea wala mwanachama wa chama chochote ambaye amekwisha lalamika kupigwa na wafuasi wa vyama vingine.

Kuhusu suala la ulinzi katika mikutano, alisema jeshi la polisi limekuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha usalama unakuwepo kwenye maeneo ya mikutano ya kampeni bila ya upendeleo.

Akizungumzia mkutano huo, alisema wadau wa PPF wanaohudhuria mkutano huo, watoe michango ambayo itakuwa ni ya kuimarisha mfuko huo na wawe wasikivu wa mada zitakazotolewa na wawezeshaji.

Katika mkutano huo wa siku tatu, mkuu huyo wa mkoa aliwakabidhi vyeti maalumu waajiri wa asasi binafsi na za serikali kutokana na kuwachangia vizuri wafanyakazi wao kwa wakati unaotakiwa kwenye mfuko huo.

Wajitokeza kushangaa helikopta ya Mbowe badala ya kusikiliza hotuba

Na Dunstan Bahai, Dodoma

MGOMBEA urais kwa tiketi ya CHADEMA Freeman Mbowe

UMATI wa wananchi wa Dodoma juzi na jana ulifurika katika viwanja vya barafu mkoani hapa kushuhudia helikopta inayotumiwa na mgombea urais kwa tiketi ya CHADEMA Freeman Mbowe.

Mgombea urais huyo, alifika juzi mjini hapa jioni na kuanza kuhutubia mkutano wa hadhara saa 12.25 jioni, ambapo umati wa watu ulikurupuka kutoka maeneo mbalimbali baada ya kuona helikopta hiyo inatua katika viwanja hivyo.

Eneo la mkutano ni maarufu kwa gereji, wauza mbao, maduka ya vifaa vya ujenzi na magari na wafanyabiashara hao na maeneo ya jirani walikurupuka na kuacha shughuli zao kwenda kushuhudia helikopta hiyo.

Mbowe ambaye alihutubia kwa takriban dakika 20, aliwapa wakati mgumu polisi waliokuwa wakilinda usalama eneo hilo, kwani muda wa kuhutubia ilikuwa uishe saa 12.30 lakini pamoja na jitihada za polisi kutaka asitishe aliendelea hadi saa 12.45.

Katika mkutano huo, aliwadhihaki polisi kwa kusema hawajui hatima yao kwani anachokifanya ni kuweka mazingira mazuri kwao na Watanzania kwa ujumla.

Baada ya kuahirisha mkutano wake huo, aliendelea nao jana mchana ambapo watu walifurika kwa kuizunguka helikopta hiyo.

Katika kuweka mambo sawa, Mbowe alisema wananchi wakimpa ridhaa ya kuongoza ataendeleza msimamo wake wa kuigawa nchi kwenye majimbo na kwamba kila jimbo litakuwa linaendesha shughuli zake za maendeleo kulingana na mapato yake, na kwamba serikali itakuwa inapata asilimia kadhaa.

Mbowe alisema wananchi wakimpa ridhaa ya kutawala, ataubadili mkoa wa Dodoma na kuwa mkoa wa elimu kwa kuweka idadi kubwa ya vyuo vikuu hali itakayobadilisha na hali ya kiuchumi wa mkoa na wananchi wake kwa ujumla.

Alisema azma ya Serikali ya kuhamia Dodoma haiwezekani na kwamba akiingia madarakani atafuta uamuzi huo, na badala yake ataifanya Dodoma kuwa makao makuu ya elimu kwa kuwa na idadi kubwa ya vyuo vikuu na taasisi nyingine za kielimu.

CCM Mtwara watakiwa kufuta kabisa tofauti zao

Na Rashid Mussa, Tandahimba

VIONGOZI na wanachama wa CCM wametakiwa kushirikiana na kufuta kabisa tofauti zao kipindi hiki cha kampeni ili kuepuka kuwayumbisha wapenzi na wananchi walio na imani na wanaotarajiwa kukipigia chama katika uchaguzi huu.

Wito huo ulitolewa na Katibu wa CCM Mkoa wa Mtwara Anna Magowa katika vikao vyake na viongozi wa wanachama wa wilaya na kata wilayani Tandahimba ambapo alisema kuendeleza malumbano kunaweza kuwachanganya watu na kupunguza imani yao.

Alisisitiza haja ya wana CCM kukubaliana na kuvumiliana katika tofauti zao ili kukomesha tabia ya kushutumiana na kutambiana, kukomoana kupitia uchaguzi unaotarajiwa kufanyika mwishoni mwa mwezi huu.

Alisema tatizo lililopo sasa katika baadhi ya kata ni la wana CCM wenyewe kutokubaliana katika uteuzi wa wagombea hasa nafasi ya udiwani kwa madai kuwa wapo walioteuliwa ama kuachwa kwa shinikizo la watu fulani pamoja na sababu zingine za kiutendaji.

Anna aliwaagiza viongozi wa chama wilaya hiyo kushughulikia upesi tofauti zilizopo katika kata chache kwa kutumia hekima na busara na kuzingatia taratibu za chama na endapo kuna malalamiko ya msingi chama kinaahidi kuyashughulikia baada ya uchaguzi.

Akihutubia mikutano ya kampeni katika vijiji vya Namikupa, Milidu, Kitama na Mluta wilayani humo Anna aliwataka vijana wa CCM kuwa macho na watu wanaodaiwa kupandikizwa kufanya fujo siku ya kupiga kura kwa lengo la kuwazuia wanawake wasijitokeze kwa wingi kuhofia fujo hizo.

Alisema ingawa ana uhakika kuwa serikali imejiandaa kikamilifu lakini pia vijana wa CCM pia wanatakiwa kutoa ushirikiano mzuri utakaoviwezesha vyombo vya dola kudhibiti vitendo vyote vya hovyo vinavyoandaliwa na watu waliokata tamaa.

Taarifa ya kampeni zilizopatikana katika wilaya hiyo zinadai kumekuwa na kufanyiwa fujo kwa wana CCM katika mikutano yake zikiwemo kuchomewa moto mabanda na kutishiwa maisha hasa katika kijiji cha Nanyanga.

Hadi sasa, Anna alisema ana imani ya ushindi wa asilimia mia katika ubunge kufuatia kumalizika malumbano ya wana CCM wenyewe katika jimbo la Mtwara mjini

Tendwa: Kauli za viongozi wa CUF sasa zinaashiria vurugu

Ni za wafuasi kubaki vituoni baada ya kupiga kura

Na Fadhili Abdallah, Kigoma

MSAJILI wa vyama vya siasa nchini, John Tendwa, amesema kuwa kauli ya viongozi wa chama cha CUF kuwataka wanachama na wafuasi kubaki kwenye vituo vya kupigia kura baada ya kupiga kura ni mwanzo wa vurugu.

Akizungumza na waandishi wa habari katika hoteli ya Lake Tanganyika Beach mjini hapa jana, Tendwa alisema kuwahimiza watu ambao hawahusiki na hawana kazi yoyote kwenye vituo vya kupigia kura ni mwanzo wa kuzusha vurugu.

Alisema kimsingi mtu ambaye ameshamaliza kupiga kura yake na hana kazi yoyote kituoni, anapaswa kuondoka na kuendelea na shughuli zake nyingine badala ya kuendelea kukaa kituoni kwa madai ya kulinda.

Alisema anashangazwa na kauli hiyo ambayo inaweza kuwa mwanzo wa uchochezi wakati kila chama kinaweka wakala wake katika kila kituo kuhakikisha hakuna udanganyifu wowote.

Msajili huyo wa vyama vya siasa alisema ana imani mawakala wa kila vyama wanajua jukumu lao linalowaweka vituoni, na watafanya wanachopaswa kufanya badala ya kuanza kupandikiza chuki kwa watu wasiohusika ambazo zinaweza kuzaa vurugu.

"Kuwaambia watu wabaki vituoni baada ya kupiga kura kwa nia ya kulinda kura za chama fulani zisiibwe, jambo hilo halikubaliki kwa sababu linaweza kupandikiza chuki na kuanzisha vurugu kwa watu hao ambao kimsingi hawana kazi yoyote katika kituo cha kupigia kura," alisisitiza Tendwa.

Akizungumzia kuvamiwa kwa mgombea uraisi wa CCM mkoani Mwanza mwishoni mwa wiki iliyopita, Tendwa alisema huo ni ugaidi wa kisiasa ambao umeanza kungia nchini, ambao ni matokeo ya kukua kwa uchumi.

Alisema kwa kadri siku zinavyokwenda yapo mambo ambayo yanaweza kuibuka zaidi ya hilo, ambapo ametanabahisha kuwa ni muhimu wagombea uraisi kuwekewa ulinzi wa kutosha ili wasiweze kudhuriwa Alitahaharisha vyama vya siasa kuwa makini wakati vinapofanya matukio ambayo si ya lazima kama hilo, ambapo kamati inayohusika na jukwaa inapaswa kutoa taarifa kwa polisi na watu wanaohusika na ulinzi ili

kubainisha watu wanaopaswa kuwepo.

Upotoshaji wa vyombo vya habari hausaidii katika uchaguzi huru

Na Mwandishi Maalum, Zanzibar

MABALOZI wa nchi za Afrika wanaowakilisha nchi zao nchini Tanzania wameeleza kuwa tabia ya baadhi ya vyombo vya habari kupotosha taarifa na viongozi wa vyama vya siasa na kuchochea vurugu haisaidii kuwepo uchaguzi huru na haki.

Mabalozi hao walitoa kauli hiyo jana walipofanya mazungumzo na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Amani Abeid Karume, Ikulu mjini hapa.

Mabalozi walimueleza Rais Karume kuwa wamesikitishwa na baadhi ya vyombo vya habari kutoa taarifa za upotofu kuhusu hali ya kisiasa Zanzibar, jambo ambalo limezidisha hisia za uhasama miongoni mwa makundi ya wafuasi mbali mbali wa siasa.

Ujumbe huo ulisema taarifa za uchochezi huamsha uhasama na vurugu na hatimaye kusababisha wananchi kushindwa kushiriki kikamilifu katika harakati za uchaguzi.

"Zanzibar iko katika kipindi cha harakati kuelekea kwenye uchaguzi, si vyema kwa vyombo vya habari kushabikia taarifa za uchochezi. Kinachotakiwa hivi sasa ni kuisaidia Zanzibar kudumisha amani na utulivu ili wananchi waweze kupiga kura kwa amani," alisema Balozi wa Zimbabwe, Chipo Zindonga, ambaye aliongoza ujumbe huo wa mabalozi kutoka nchi za Afrika.

Mabalozi hao walieleza wasiwasi wao kwa baadhi ya waangalizi wa uchaguzi kwa kusema kuwa uzoefu katika nchi nyingi za Afrika ni kuwa waangalizi hao huonyesha tabia ya kuhodhi maoni yao na kushikilia msimamo wao ambao huujenga kabla ya kuwasili katika nchi husika.

"Hivi sasa wachunguzi wameshaanza kuingia Tanzania kupitia jumuiya mbalimbali za kimataifa, hivyo tatizo hilo linaweza kujitokeza Zanzibar, na jambo la busara ni kuwa waangalifu na wachunguzi hao na taarifa zao," walisema mabalozi hao.

Mabalozi hao wamempongeza Rais Karume kwa juhudi kubwa anayoichukua kuhakikisha amani, ambayo walisema ni msingi wa maendeleo ya wananchi wa Zanzibar katika sekta mbalimbali kuanzia uchumi, biashara na uwekezaji.

Katika mazungumzo hayo, Rais Karume alisema tabia ya kuongeza ‘chumvi’ na kushabikia utashi wa kisiasa kwenye taarifa muhimu katika kipindi hiki cha uchaguzi ni kwenda kinyume na maadili ya uandishi.

Rais Karume alisema kuwa ni vigumu kuelewa dhamira ya baadhi ya vyombo hivyo, lakini inafaa vyombo hivyo vikaelewa kuwa moja ya haki za wananchi katika mfumo wa demokrasia ni kupata taarifa sahihi ya matukio yanayowahusu katika jamii.

"Ni wajibu wa vyombo vya habari kufuatilia na kutoa taarifa zitakazosaidia wananchi kutumia haki ya demokrasia ya kupiga kura kwa manufaa ya taifa kwa jumla," alisema Rais Karume.

Rais Karume ambaye pia ni mgombea wa urais Zanzibar kupitia tiketi ya CCM na ni Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar, aliwaeleza mabalozi hao juu ya hali halisi ya kisiasa nchini kufuatia kampeni zinazoendelea, ambapo Oktoba 30, 2005 wananchi wa Zanzibar wanatarajiwa kupiga kura kuchagua viongozi watakaoshika madaraka kwa kipindi cha miaka mitano ijayo.

Katika mazungumzo hayo walishiriki mabalozi kutoka Zimbabwe, Afrika Kusini, Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo, Burundi, Uganda, Msumbiji na Rwanda.

Motisha kutolewa kwa wanaofanya kazi kwenye mazingira magumu

Na Prosper Kulita, Mahenge

SERIKALI kupitia Wizara ya Afya inakusudia kuongeza motisha kwa wafanyakazi wake waliopo katika maeneo

yenye mazingira magumu ili kuwawezesha kupenda kazi katika mazingira hayo.

Mpango huo ambao utawanufaisha wafanyakazi kuanzia ngazi ya chini, unatarajiwa kuanza mapemamwakani.

Hayo yalielezwa na Waziri wa Afya, Anna Abdalla, alipokuwa akizungumza na wafanyakazi wa hospitali yaWilaya ya Ulanga iliyopo katika mji wa Mahenge.

Alisema kuanzishwa kwa mpango huo kutasaidia watumishi wa wizara hiyo kutokimbilia sehemu nyinginekutokana na maslahi duni na mazingira mabaya.

Alitoa ufafanuzi huo baada ya kujibu maswali ya wafanyakazi mbalimbali wa hospitali hiyo waliokuwa wakitaka kujua serikali ina mpango gani kuhusu wafanyakazi wanaishi katika mazingira magumu.

Katika maswali yao, wafanyakazi hao walidai baadhi ya watumishi wanaopangiwa kufanya kazi katika hospitali hiyo wamekuwa wakiacha na wengine kuhama kutokana na mazingira magumu ya kazi yaliyopo wilayani

humo.

Akijibu maswali hayo, Waziri Anna alisema serikali tayari imeshapanga mikakati kuhakikisha wafanayakzi wa wizara hiyo waliopo katika mazingira hayo wanaboreshewa maslahi zaidi ili kuwa kichocheo cha kuwavuta wengine kwenda kufanya kazi sehemu hizo.

Kwa mujibu wa waziri, wizara ya afya sasa haitakubaliana na mtumishi yoyote kumuamisha kwa kigezo cha mazingira magumu. "Kuna madaktari wanapopangiwa vituo vyao, wanakwenda kuripoti halafu wanarudi wizarani kuomba

kuhamishwa kwa kisingizio kuwa mazingira magumu. Sasa nasema wazi, kuanzia sasa hatutahamisha mfanyakazi yoyote, tunataka afanye kazi hapohapo," alisema.

Alisema kutokana na hali hiyom kumesababisha kushusha takwimu za huduma ya afya, ambapo hadi sasa daktari mmoja anatibu wagonjwa 24,000 kwa mwaka, kiwango ambacho ni kikubwa sana ukilinganisha na nchi nyingine za Afrika.

Alisema ili kumaliza tatizo hilo wizara yake imeweka mikakati ya kuhakikisha inawaajiri haraka iwezekanavyo madaktari wanaotoka masomoni na kuwapangia katika vituo vyao vya kazi.

Alibainisha kuwa mbali na kutatua tatizo hilo pia wizara hiyo itaboresha huduma zake kwa kuhakikisha kila hospitali ya wilaya inakuwa na dawa pamoja na vitendea kazi vya kisasa.

Mtunza fedha 'asekwa Lupango' kwa wizi Babati

Na Serafina Sungusia, Babati

MTUNZA fedha wa shirika lisilo la kiserikali la Farm Africa Tanzania Limited la wilayani Babati, mkoani Manyara, Peter Tlaghasi (50), amehukumiwa kifungo cha miaka mitano jela baada ya kupatikana na hatia ya kuiba sh. 6,580,000 mali ya shirika hilo.

Hukumu hiyo ilitolewa jana na Hakimu Mkazi Mfawidhi, Huruma Shaidi wa Mahakama ya mkoa, baada ya kuridhika na ushahidi ulitolewa na mashahidi watano wa upande wa mashitaka na kusema ulionyesha kweli mtuhumiwa alitenda kosa hilo.

Kabla ya hukumu hiyo kutolewa, Mwendesha Mashitaka Mkaguzi wa Polisi Ralph Meela, alidai mtuhumiwa alitenda kosa hilo Julai 15 mwaka jana, kwa kuchukua kiasi hicho cha fedha na kuzitumia kwa matumizi binafsi.

Meela alidai mtuhumiwa alijipatia fedha hizo katika Benki ya NMB tawi la Babati mjini kwa kutumia hundi namba A 002455280 iliyokuwa imesainiwa na mwajiri wake.

Iliendelea kudaiwa kuwa alitumwa kuzihamisha kutoka kwenye akaunti ya shirika hilo kuziingiza kwenye akaunti ya Mkurugenzi wa Halmashari wilayani hapa kwa ajili ya malipo ya wakulima wa vijijini ambao shirika hilo lilitakiwa kuwalipa.

Julai 22 mwaka jana, ndipo taarifa kutoka kwa Mkurugenzi zilimfikia mwajiri wa mtuhumiwa, Farm Africa kuwa hakuna fedha zozote zilizoingizwa kwenye akaunti, ndipo alipoitwa na kumtaka kutoa maelezo, ambapo alikiri kuchukua fedha hizo na kuahidi kuzirejesha siku iliyofuata.

Akijitetea mahakamani kabla ya hukumu kutolewa, mshitakiwa alidai hakuwa na tabia ya wizi ila alidanganywa na vijana waliojifanya wafanyabiashara wa madini kutoka Musoma.

Aliimbia mahakama kuwa vijana hao pasipo kujua kuwa walikuwa matapeli, walimwambia akiwapatia kiasi hicho cha fedha wataenda kuzifanyia biashara na baada ya muda mfupi atarudishiwa mara mbili ya fedha hizo.

Mahakama ilitupilia mbali utetezi huo na kumpa adhabu ya kifungo hicho sambamba na kulipa fedha hizo, ili iwe fundisho kwa watumishi wengine wanaojali maslahi yao binafsi na kusahau nidhamu na uwajibikaji kazini.

VETA Rukwa watakiwa kuwa wabunifu

Na Prosper Mgimwa

WANAFUNZI wanaosoma vyuo vya ufundi stadi (VETA) Mkoa wa Rukwa wametakiwa kuwa wabunifu wakati wanapotengeneze bidhaa mbalimbali ili waweze kukidhi mahitaji ya soko katika ulimwengu huu wa utandawazi.

Kaimu Mkuu wa mkoa wa Rukwa, ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Sumbawanga, Evance Balama, alisema hayo wakati wa hafla ya kukabidhi vifaa mbalimbali vya kufundishia kwa vyuo vya ufundi stadi vyenye thamani ya sh. milioni 8.5 vilivyotolewa na VETA Nyanda za Juu Kusini kwa ajili ya kusaidia vyuo hivyo.

Alisema wanafunzi wanaosoma katika vyuo vilivyo chini ya usimamizi wa VETA wanapaswa kuwa wabunifu wakati watakapomaliza masomo yao na kuanza kazi ya kutengeneza bidhaa ili iwasaidie kupata soko bila wasiwasi katika kipindi hiki cha ushindani wa kibiashara.

Balama alisema inasikitisha kuona watu wanaomaliza katika vyuo vya ufundi wanakuwa watengeneza bidhaa za aina moja hali inayopelekea kutokuwepo ushindani wa bidhaa za aina tofauti na kusababisha kutokuwa na soko kubwa kwasababu wote wanakuwa na bidhaa zilizo sawa.

Kaimu Mkuu wa mkoa huyo alisema mafundi wanaoamua kujiajiri wanapaswa kuanzisha vikundi ambavyo vitawawezesha kupata mikopo iliwaweze kupata mitaji itakayo wasaidia katika kununua malighafi mbalimbali zitakazo wawezesha kutengeneza bidhaa bora.

Alisema vijana wanaweza kupambana na umaskini iwapo watajiunga kwenye vikundi ambavyo vitawasaidia kuweza kupata mikopo kutoka serikalini na kwenye taasisi mbalimbali itawawezesha kuongeza mitaji yao na kuweza kupambana na umaskini.

Awali akitoa taarifa kwa mgeni rasmi, Mkurugenzi wa VETA Nyanda za Juu Kusini, Steven Lazaro, alisema wanajitahidi kutoa vifaa mara kwa mara kwa vyuo vilivyosajiliwa, na mafunzo kwa walimu ili vyuo hivyo vitoe elimu yenye ubora kulingana na mahitaji la soko la kimataifa.

Sera za shari, vitisho udanganyifu na matusi kamwe haziwezi kuwapeleka wapinzani Ikulu

RAIS Benjamin Mkapa, Mwenyekiti wa CCM

MUONGO mmoja karibu umepita tangu nchi yetu iingie katika mfumo wa demokrasia ya vyama vingi vya siasa. Katika kipindi hicho umekwisha fanyika takribani uchaguzi mara mbili ndani ya mazingira ya ushindani wa mfumo wa vyama vingi vya siasa. Mwandishi ARON MWASAMALE katika makala hii, anachambua udhaifu wa wapinzani na umuhimu wa kuendelea kuipa CCM ridhaa ya kuongoza nchi ili iendelee kudumisha amani.

Uchaguzi wa kwanza katika mazingira ya ushindani wa kisiasa ulifanyika Oktoba 1995, Uchaguzi Mkuu wa Pili ulifanyika mwaka 2000. Mwishoni mwa mwaka huu (Oktoba 2005) utafanyika uchaguzi mkuu wa tatu tangu kuasisiwa kwa mfumo wa Vyama vingi vya siasa hapa nchini.

Katika vipindi vyote hivyo , (1995/2000) Chama Tawala (CCM) kimeendelea kupeta. Aidha utafiti uliofanywa Septemba 2004/55 na Redet umebaini kwamba CCM mwaka huu (Oktoba 2005) itaibuka na ushindi mkubwa wa zaidi ya asilimia 70 kwa kiti cha urais na ubunge kwa zaidi ya asilimia 65.

Katika uchaguzi wa Serikali za mitaa uliofanyika Novemba 2004, CCM ilishinda kwa zaidi ya asilimia 96. Wahenga walisema “Nyota njema huonekana asubuhi”.

Kinachoshangaza ni kwa wenzetu walioko kambi ya upinzani kutotaka kuona ukweli huo, au kuendelea kujipa matumaini ya kuingia Ikulu mwaka huu; na kujigamba mara kwa mara huku wakiwaahidi Watanzania kwamba wakiingia Ikulu ati watakomesha rushwa, wataimarisha uchumi wakati baadhi ya viongozi hao wa kambi ya upinzani waliwahi kushika nyadhifa za kuwa washauri waandamizi wakubwa wa masuala ya uchumi katika ofisi ya Rais huko Ikulu. Je, hizo ni ahadi za ukweli au ni ahadi za danganya toto? Kipi cha maajabu zaidi watakifanya wakiwa Ikulu wakati huko nyuma walishindwa kushauri uongozi uliokuwepo.

Labda wakati kama huu tunapojiandaa kuelekea uchaguzi Mkuu wa Rais, wabunge na madiwani Oktoba 30, 2005 ni vizuri kuendelea kukumbushana kwamba Chama Tawala (CCM) ni Chama chenye historia kilichotokana na TANU na ASP, ambacho hadi sasa kimekuwa madarakani tangu Uhuru upatikane katika nchi hii.

Katika kipindi chote cha utawala wake, Chama Cha Mapinduzi kimefanikiwa kuliko vyama vingine vya siasa katika bara la Afrika katika kutekeleza majukumu yake ya kihistoria ya kujenga umoja wa taifa na mazingira ya amani na utulivu nchini.

KWA NINI CCM IMEFANIKIWA

Kazi ya kujenga Umoja wa Taifa ili wananhci wajisikie wako huru na watu wa taifa moja, inafanyika kwa misingi ya sera. Ziko sera za vyama vya siasa na serikali ambazo husababisha kujengeka kwa umoja wa taifa huru na zipo sera ambazo hujenga mfarakano, chuki, uhasama au kutominiani katika nchi.

Sera za Chama Tawala (CCM) na kabla yake TANU na ASP , zimekuwa ni sera zinazojenga umoja , upendo , mshikamano, amani, utulivu na kuaminiana miongoni mwa wananchi wa Tanzania.

Sera kama hizo ni pamoja na sera ya msingi ya ujamaa na kujitegemea, ingawa wapo walio na mtazamo finyu ambao hawazingatii kanuni ya wakati na mahali katika kutafsiri sera hiyo katika mazingira ya sasa yanayotawaliwa na uchumi wa soko huru.

Katika mazingira ya sasa, upo umuhimu mkubwa kwa wana_CCM na viongozi wetu kuelewa vizuri dhana nzima ya kujenga ujamaa katika mazingira ya sasa, kwa sababu yapo mawazo kwamba CCM imeachana na falsafa ya ujamaa au ujamaa umekufa.

Chama Cha Mapinduzi kimekuwa na sera zinazounda mazingira ya amani na utulivu katika jamii na nchi. Sera hizo ni zile zinazopiga vita ukabila, udini, ubaguzi wa rangi (uzawa), jinsia na umajimbo.

Nyingine ni sera zinazojali na kuheshimu utawala wa sheria, sera zinazozingatia maslahi ya wanyonge na wavuja jasho katika jamii, sera zinazowashirikisha (ulinzi wa umma) wananchi wake katika kulinda nchi yao, sera zinazojenga mazingira ya ujirani mwema na sera ya demokrasia na uwazi na ukweli katika kuendesha shughuli za nchi na za taasisi kuanzia ngazi ya kitongoji au kijiji hadi Taifa.

Nchi nyingi za Afrika ambazo vyama na serikali zake zimekuwa na sera kinyume na sera hizi za CCM , zinashindwa hadi sasa kuwa nchi zenye umoja wa kitaifa. Wananchi katika nchi hizo bado wanakabiliwa na mfarakano ulioota mizizi katika misingi ya ukabila, udini, jinsia, ubaguzi wa rangi, umajimbo na kadhalika.

Kauli za baadhi ya viongozi wa vyama vya Upinzani hapa nchini na aina ya viongozi wenyewe wa vyama hivyo, ni ushahidi tosha kwamba hawana nia ya kuimarisha umoja wa taifa letu wala kuendeleza mazingira ya amani na utulivu nchini katika ajenda zao za kisiasa. Badala yake, kauli au matamshi yao na vitendo vyao vinaashiria utengano katika taifa, vurugu na uhasama.

MFUMO WA VYAMA VINGI

Kuanzishwa kwa mfumo wa demokrasia ya vyama vingi hapa nchini, hakukuwa na maana ya kuendeleza visasi baina ya chama na chama, kujenga chuki na uhasama, kutoa vitisho, kuvuruga amani na utulivu uliopo nchini, kukashifu au kubeza kila kitu kinachofanywa na serikali zilioko madarakani, na kadhalika.

Lengo na madhumuni ya kuanzishwa kwa mfumo wa demokrasia ya vyama vingi vya siasa hapa nchini yalikuwa :-

Vyama kushindana kwa sera au kushindanisha sera za chama na chama na wala si kuporomosha matusi, kutoa vitisho, kukashifu au kukejeli jitihada zinazofanywa na serikali kuwaondolea wananchi kero zinazowasibu.

Kupanua demokrasia ndani ya jamii ili kuwapa wananchi fursa kubwa zaidi ya kuchagua viongozi wanaowataka. Kwa sababu ndani ya mfumo wa chama kimoja cha siasa wapo watu walioamini kwamba demokrasia ilikuwa finyu.

Kuchochea maendeleo kwa kuzikosoa serikali zilizoko madarakani kwa ustaarabu na wala sio kupinga kila kitu kinachofanywa na serikali. Tangu nchi yetu iingie katika mfumo wa vyama vingi vya siasa (Julai 1, 1992) na huu ukiwa ni takribani mwaka wa 13, mwelekeo wa sera za vyama vya upinzani haujabadilika hata kidogo.

Badala yake zimeendelea kuwa ni sera zinazojenga mfarakano (shari), sera zinazotoa vitisho vinavyoashiria kuvuruga amani na utulivu hapa nchini. Bila hata aibu baadhi ya viongozi wa vyama vya siasa vya upinzani wamefikia hata kutamka au kuutangazia umma wa Watanzania kwamba wasipotwaa madaraka ya kuongoza nchi Oktoba 2005 ati damu itamwagika, nchi itawaka moto au kutotowalika. Je, viongozi wa aina hiyo wanatutakia mema au balaa?

Aidha mwelekeo wa itikadi za baadhi ya vyama vya siasa ni kutumia udini, ukabila, ubaguzi wa rangi au umajimbo ama ukanda kama njia ya kuingia Ikulu. Je, nani hajui madhara ya sera za udini au ukabila?

Je, mateso wanayopata wananchi wa Burundi na Rwanda msingi wake ni nini kama si ukabila? Au mapambano ya muda mrefu ya wananchi wa kusini mwa Sudan na kaskazini ni nini kama si udini?

Baadhi ya viongozi wa vyama vya siasa vya upinzani wanapopata fursa ya kuhutubia mikutano ya hadhara wanajazwa jazba, hasira kali huku wakiendelea kuporomosha matusi mazito na kuwaandama viongozi wa Chama Tawala kwa matusi ya nguoni na kashfa za kila aina.

Wapinzani wanapoandaa maandamano wananchi wanakosa amani. Kwa sababu maandamano yao mara nyingi hujaa vitimbi vya kila aina. Si mara chache hutakosa kuwasikia wakitamka mambo mazito kama vile jino kwa jino, ngangari, chechenia, ukanda wa gaza na kadhalika.

Mabango yao yakiwa yameandikwa kwa kauli mbiu zinazoashiria , vurugu na kejeli mbali mbali. Siku hizi umezuka mtindo wa viongozi wa vyama vya upinzani nchini kuyaona maandamano kama njia ya mkato ya kutatua matatizo mbalimbali yanayowakabili wananchi.

Wananchi badala ya kutumia muda wao kwa kazi za kujiletea maendeleo, wanapoteza muda mwingi kushiriki katika maandamano ya kwenda Ikulu.

Hali kama hiyo pia hudumaza jitihada za serikali za kupambana na umaskini, ujinga na maradhi. Wakati baadhi ya viongozi wa vyama vya siasa vya upinzani wamekuwa wakichukua muda mwingi kuandaa maandamano, wananchi wanapaswa kujiuliza, Je, maandamano ndio jibu la kupambana na umaskini, ujinga na maradhi?