JEE, TUMEACHANA
NA SIASA YA UJAMAA NA KUJITEGEMEA? LA HASHA
[Na Omar
R. Mapuri]
UTANGULIZI:
Tokea mwanzoni mwa miaka ya
tisini,
Katika makala haya tutajaribu
kusahihisha dhana hizo ambazo tunaamini kwa kiasi kikubwa ni matokeo tu ya
ubabaikaji uliosababishwa na mageuzi.
Tutajitahidi kuonyesha kwamba CCM haijaachana na siasa yake ya Ujamaa na
Kujitegemea, bali ambacho kimekuwa kikibadilika kulingana na wakati na
mazingira, ni mikakati tu ya kufikia lengo
UCHANGANUZI WA MANENO ”FALSAFA”,
“IMANI”, “SIASA”, “SERA”, “ILANI” n.k.
Kabla ya kuitazama kwa undani
siasa ya Ujamaa na Kujitegemea, inafaa kwanza kuchanganua maneno ya “falsafa”,
“imani”, “siasa”, “itikadi”, “sera”, “maamuzi” na “ilani” ambayo yanatumika
sana katika kuielezea dhana nzima ya ujamaa na kujitegemea katika mikutadha
mbali mbali.
Falsafa:
Falsafa inayosarifu dhana na
nadharia za Chama Cha Mapinduzi, na nchi nzima kwa jumla ni usawa wa
binadamu na mtu kuthaminiwa kwa utu wake.
Falsafa hii inabeba dhana za uhuru, demokrasia, haki, udugu na
amani. Falsafa hii inaashiriwa katika
Ahadi ya
“12. – (1) Binadamu
wote huzaliwa huru, na wote ni sawa.
(2) Kila mtu anastahili heshima ya kutambuliwa na kuthaminiwa utu
wake.
Ibara ya 11 ya Katiba ya
Inathibitika kwa hivyo kwamba
falsafa hii si ya CCM peke yake, bali ni ya nchi nzima. Hatujapata kusikia chama hata kimoja cha
siasa kinachoipinga falsafa hii.
Imani/Siasa/Itikadi:
Ni imani ya CCM kwamba ujamaa na
kujitegemea ndiyo njia pekee ya kujenga nchi ya watu walio sawa, huru na
wanaoheshimiana. Kwa hivyo, hiyo ndiyo siasa au itikadi ya msingi ya CCM. Ibara ya 4 ya Katiba ya CCM inaweka bayana
imani ya CCM
4. CCM kinaamini kwamba:
(1) Binadamu wote ni sawa
(2) Kila mtu anastahili heshima
ya kutambuliwa na kuthaminiwa utu wake.
(3) Ujamaa na kujitegemea ndiyo
njia pekee ya kujenga jamii ya watu walio sawa na huru
Kwa upande wa Katiba ya Jamhuri
ya Muungano wa
Ibara ya 3(1) ya Katiba ya
Jamhuri ya Muungano wa
Tukizilinganisha Katiba za nchi
na ile ya CCM katika muktadha wa siasa ya ujamaa na kujitegemea, inadhihirika
kwamba neno “kujitegemea” halikutumika katika Katiba za nchi. Tafsiri yetu ya tofauti hiyo ni kwamba katika
siasa ya Ujamaa na Kujitegemea, ncha ya ujamaa ni ya nchi nzima lakini ncha
ya kujitegemea inatoa fursa kwa vyama vya siasa kutofautiana kwa sera. Ingawa kuna vyama vya upinzani ambavyo
husikika vikitaka kipengele cha Ujamaa kiondoshwe katika Katiba ya nchi,
lakini ukizitazama kwa undani sera za vyama hivyo, utagundua kwamba zimejengwa
juu ya msingi huo huo wa ujamaa. Na vipo
vyama ambavyo hujinasibu kwa wananchi kwamba eti ndivyo vyenye uwezo
mkubwa zaidi wa kuzitekeleza sera za CCM
kuliko CCM yenyewe. Vyama kama hivyo
vinakiri usahihi wa siasa ya Ujamaa lakini vinadai kuwa eti CCM haina uwezo wa
kuitekeleza. Lakini zaidi ya yote,
hatujapata kusikia chama cho chote cha siasa nchini
Sera na Dira:
Baada ya kubainisha siasa yake ya
Ujamaa na Kujitegemea iliyojengwa juu ya msingi wa falsafa ya usawa wa binadamu na mtu
kuthaminiwa kwa utu wake, TANU mnamo
mwaka wa 1967 ilipitisha Azimio la Arusha lililoandaa mazingira na kuweka dira ya utekelezaji wa siasa
hiyo. Sera ni mkakati wa utekelezaji wa siasa kwa kipindi
fulani kulingana na uchambuzi wa dira uliofanywa kwa ajili ya kipindi
hicho. Sera huweza kubadilika kulingana
na mahitaji ya wakati. Kwa hivyo,
wakati siasa ya Ujamaa na Kujitegemea ni ya kudumu na Azimio la Arusha kama dira yake ya utekelezaji nalo ni la
kudumu kwa kiasi fulani, sera na mikakati ya utekelezaji huweza kubadilika kila
baada ya muda, kulingana na mabadiliko ya mahitaji ya wakati. Na
kweli uzoefu katika TANU na ASP na baadaye CCM unaonyesha kwamba baada ya kila
kipindi cha wastani wa miaka 10, Chama kimekuwa kikitathmini utekelezaji wa
siasa ya Chama na kuzitazama upya sera zake za msingi kwa lengo la kuzifanya
zikidhi mahitaji ya wakati. Baada ya
kufanya mapitio hayo Chama huja ama na mwongozo unaojikita katika ufafanuzi na
kuyawekea mkazo maeneo fulani au huja na sera mpya kabisa, lakini lengo kuu likiwa ni lile lile la
kutekeleza siasa ya Ujamaa na Kujitegemea kwa kuzingatia misingi ya Azimio la
Arusha. Ndiyo maana katika kipindi cha
toka 1971 hadi sasa, CCM imetoa nyaraka nne zifuatazo za kisera za msingi:-
(1)
Mwongozo wa TANU wa 1971 ambao
ulijenga hamasa ya utekelezaji wa Azimio la Arusha.
(2)
Mwongozo wa
CCM wa 1981 ambao ulijielekeza katika kukabiliana na
mmong’onyoko wa maadili uliokuwa unasababishwa na hali ngumu ya uchumi
iliyochangiwa na vita vya nduli Idi Amin.
(3)
Mwelekeo wa Sera za CCM katika Miaka ya Tisini
uliozingatia haja ya kujihami na
taathira za upepo wa mageuzi makubwa ya kiuchumi na kisiasa uliokuwa ukivuma
Duniani na kuziangusha dola kubwa za kijamaa za Ulaya ya Mashariki likiwemo la
Urusi yenyewe ya Kisovieti.
(4)
Mwelekeo wa Sera za CCM katika Miaka ya 2000-2010 unaozingatia
zaidi suala la matumizi ya teknolojia (modenaizesheni) katika ujenzi wa uchumi
wa kisasa.
Kwa
jumla, chimbuko la sera zote za CCM ni Azimio la Arusha na zinapoandaliwa,
yanazingatiwa pia malengo na madhumuni ya CCM yaliyobainishwa katika ibara ya 5
ya Katiba ya CCM. Baba wa
Taifa, Mwalimu Julius K. Nyerere katika “Kujitawala ni Kujitegemea” aliyaelezea
ifuatavyo mahusiano baina ya Azimio la Arusha na Sera za Chama:-
Azimio la
Arusha ndilo linaloeleza itikadi ya chama chetu. Ndiyo kauli kuu ya lengo letu na misingi
yetu; ndilo msingi wa maamuzi yote ya sera za Chama na Serikali.
Aidha
Mwalimu alitambua haja ya kupitia upya sera kila mara na kurekebisha
Azimio. Alisema tena katika “Kujitawala
ni Kujitegemea:-
Kila
miaka inavyopita, kauli yo yote muhimu kupitiwa mara kwa mara kuona
Maneno
hayo yanatosha kuwasuta wale wanaodai kwamba eti Mwalimu hakutaka mabadiliko ya
Azimio na Sera.
Maamuzi:
Ndani ya utekelezaji wa sera ya
msingi, Chama huweza kupitisha maamuzi yenye lengo la kutoa msukumo wa
utekelezaji wa jambo fulani mahsusi au kukabili tatizo fulani la utekelezaji. Ni kwa msingi huo ndio TANU na baadaye CCM
ilipitisha maamuzi mengi yakiwemo yafuatayo:-
(1)
Siasa ni kilimo (Azimio la Iringa) (1972)
kwa lengo la kutoa msukumo katika suala zima la kilimo.
(2)
Mpango wa Elimu kwa Wote (UPE)
(Azimio la Musoma), (1974) uliotoa msukumo wa kuharakisha kufikisha elimu kwa
wote ikiwa ni pamoja na suala la elimu ya watu wazima.
(3)
Mtu ni Afya (1976): Kutoa msukumo kwa sera
ya kinga kuliko tiba.
(4)
Mpango wa Kujihami Kiuchumi
(1980/81) ili kukabiliana na hali ngumu ya uchumi wa nchi.
(5)
Maamuzi ya
Ilani:
Kama ilivyokwishabainishwa, sera
za msingi huchukua upeo wa muda mrefu kidogo, na kwa uzoefu wa CCM, ni
Baada ya uchanganuzi huo wa maneno “falsafa”,
“siasa”, “itikadi” “sera”, “maamuzi” na “ilani”
kama yanavyotumika katika msamiati wa CCM, imedhihirika kwamba falsafa
na siasa ni vitu vya kudumu, au ni malengo ya muda mrefu, lakini sera, maamuzi
na ilani ni vitu vinavyobadilika kila baada ya muda. Na hapa ndipo penye siri ya mafanikio ya
CCM. Ingawa CCM ni chama kikongwe,
lakini kila baada ya muda hujirekebisha kwa mujibu wa mazingira ya wakati,
lakini bila ya kupoteza lengo. Kwa
ufupi, CCM inafuata kanuni ya mwezi ambao katika mzunguko wake huanza na
uchanga (ukiwa na umbo la hilali), ukafikia upevu (ukiwa na umbo la sahani) na
kurejea tena uchanga ambapo unakuwa tunu tena. Ni kutokana na kanuni hiyo ndiyo maana
wananchi hawaichoki CCM pamoja na ukongwe wake, kwani wakati wote inawaletea
matumaini mapya.
UJAMAA NA KUJITEGEMEA KAMA SIASA
YA CHAMA:
Siasa ya Ujamaa:
Siasa ya Ujamaa imechambuliwa na wanafalsafa wengi
wakubwa waDunia hii wakiongozwa na Karl Marx na Vladmir Lenin. Pia imechambuliwa kwa kina na Mwalimu Julius
K. Nyerere kwa mazingira ya
Kugawana au kusambaza kwa wote utajiri wa nchi (si kwa kugawana fedha bali kwa kuhakikisha upatikanaji wa huduma za kijamii kwa wote) ni sura moja tu ya Ujamaa. Lakini pia kuna sura ya pili ambayo ni ya kuuchuma huo utajiri wenyewe wa kugawana. Katika Azimio la Arusha, unafafanuliwa utaratibu wa kuchuma utajiri bila ya kunyonyana. Mkakati uliowekwa ni wa njia kuu za uchumi wa nchi kuwekwa chini ya wakulima na wafanyakazi kupitia vyombo vya Serikali
Siasa ya Kujitegemea:
Siasa ya Kujitegemea imechambuliwa kwa kina katika Sehemu
ya Tatu ya Azimio la Arusha. Siasa hii
inajikita katika kuleta maendeleo ya kweli ya nchi na ya wananchi wenyewe hasa
wanyonge. Hoja inajengwa kwamba huwezi kuzungumzia maendeleo ya kweli
kama maendeleo hayo ni ya vitu tu na si ya watu wenyewe na
Kwa mnasaba huo, Siasa ya
Kujitegemea inasisitiza kwamba: maendeleo ya nchi huletwa na watu, hayaletwi
na fedha. Fedha ni matokeo siyo msingi
wa maendeleo. Ili tuendelee twahitaji
vitu vinne: (i) Watu; (ii) Ardhi; (iii) Siasa
Siasa ya Kujitegemea imebainisha
masharti mawili ya maendeleo. Masharti
hayo ni Juhudi na Maarifa.
Juhudi inaashiria kufanya kazi kwa kujituma na Maarifa ni
kiashirio cha matumizi ya utaalamu na teknolojia kwa lengo la kuziongezea tija
juhudi.
Kwa jumla, mtu hahitaji utafiti wa kina kubaini kwamba
karibu yote yaliyoelezewa kuhusiana na Siasa ya Kujitegemea yalikuwa na ukweli
mwaka 1967 na bado yana ukweli hadi leo.
Aidha, yote hayo yanaendelea kupendwa na Watanzania waliowengi ambao siyo tu wameyakubali, bali
pia wanajitahidi kuyatekeleza. Kwa mfano
Watanzania pamoja na unyonge wao, hawakubali kuonewa wala kunyanyaswa. Pia, Watanzania wamejiletea maendeleo mengi
(shule, zahanati, visima, njia, maji n.k.) kwa kujitegemea bila ya kusubiri
fedha. Na zaidi ya yote, Watanzania
wanajituma kwa bidii kubwa. Kwa
kuzingatia ukweli huo, mtu hapaswi kupata taabu
BAADHI YA MAENEO YALIYOHITAJI
MAREKEBISHO YA SERA
Katika makala haya tumedhihirisha
kwa uhakika na bila ya kigugumizi kwamba Siasa ya Ujamaa na Kujitegemea ndiyo
siasa ya CCM na tumelitambua Azimio la Arusha kuwa ndiyo dira kuu inayoongoza
uandaaji wa sera za utekelezaji wa siasa hiyo.
Baadhi ya watu wasioitakia mema CCM wamekuwa wakiihukumu siasa hiyo kwa
vigezo visivyokuwa sahihi, na ndio waliochangia kwa sehemu kubwa katika
kuwababaisha wanachama na viongozi wa CCM.
Watu kama hao wamekuwa wakiitangaza siasa hiyo kuwa iliyoshindwa na
kwamba sasa ubepari ndio umejikita.
Kigezo wanachotumia ni sifa za nchi yenye ujamaa kamili zilizotajwa
katika Azimio la Arusha
Kwa hivyo, usahihi wa mambo ni
kwamba Ujamaa na Kujitegemea ni lengo la muda mrefu ambalo kulifikia kutachukua
miaka mingi
Hapa tutazungumzia mifano mitatu
tu ya maeneo ambayo kutokana na kubadilika kwa mazingira na mahitaji ya wakati,
CCM ilibidi izifanyie marekebisho sera zake za msingi. Maeneo hayo yanahusu udhibiti wa njia kuu
za uchumi, mazingatio ya maarifa katika kujenga msingi wa kujitegemea na suala la masharti au
miiko ya uanachama. Ni maeneo haya
hasa ndiyo yanayojengewa hoja na wapinzani wetu kwamba CCM imeachana na Siasa
ya Ujamaa na Kujitegemea.
Tatizo la pili lilihusu
utaifishaji wa hata hizo njia kuu za uchumi zilizotakiwa na Azimio la
Arusha. Baada ya muda wa utaifishaji,
mashirika ya umma na viwanda vingi vilijikuta vinapungukiwa na tija kutokana na
ubadhirifu, uajiri uliozidi mahitaji na ufinyu wa mitaji. Njia kuu hizo za uchumi zikawa zinaingiza
hasara Serikalini badala ya faida.
Serikali ikajikuta inatumia fedha nyingi kufidia mashirika na viwanda
hivyo badala ya kugharamia huduma za kijamii kwa wananchi
Katika mazingira hayo, CCM
ilibidi kuzitathmini sera zake ili kujiridhisha
Katika kuelekeza njia ya kuondokana na matatizo yaliyojitokeza kuhusiana na zoezi la kuimilikisha Serikali njia kuu za uchumi, Mwalimu Nyerere alisema yafuatayo katika “Kujitawala ni Kujitegemea” mwaka 1987”.
Lakini
Azimio halikutaja mpango wa kuonyesha ni shughuli gani imilikiwe na Taifa zima,
ni sehemu gani imilikiwe na Serikali za Mitaa, na sehemu gani ishikwe na Vyama
vya Ushirika. Wala Azimio halikusema ni sehemu gani inaweza kudhibitiwa kwa njia
nyingine isiyokuwa ya kumiliki.
Kadhalika Azimio linasema kwamba ardhi lazima imilikiwe na umma; lakini
halisemi “shamba lile la eka 100
Kwa hiyo
tunapopata tatizo jipya, tunajadili tena na kuamua sehemu gani ya shughuli
ishikwe na umma, na shughuli gani za uchumi katika nchi yetu zinaweza
kudhibitiwa kwa njia nyingine kama leseni, kodi au utaratibu mwingine.
Ilikuwa ni katika mazingatio hayo ndiyo Mwelekeo wa Sera
za CCM Katika Miaka ya Tisini ulipotungwa.
Mwelekeo huo unaelezewa kwa majumuisho na kifungu cha 1 (Sura ya Tatu)
cha “Ilani ya Uchaguzi ya CCM, Uchaguzi Mkuu, Oktoba 1955”
1. Ujamaa
na Kujitegemea:
Katika kuendeleza kuufufua na
kuujenga uchumi wa Taifa Serikali ya CCM itaongozwa na Siasa ya Ujamaa na
Kujitegemea inayolingana na wakati tulionao.
Shabaha ya Ujamaa katika kipindi hiki, ni kuwafanya wananchi wenyewe kuwa ndio wamilikaji wakuu wa uchumi, na dola kuwa zaidi mhimili wa uchumi wa Taifa. Kwa mantiki hiyo, wananchi wamiliki uchumi wa kilimo, ufugaji, uvuvi, viwanda, madini nakadhalika, moja kwa moja kila mtu binafsi, wamiliki kwa vikundi vya ushirika wa aina mbali mbali, wamiliki kwa kununua hisa katika makampuni ya wananchi au kununua hisa katika makampuni ya ubia.
Kimsingi
mabadiliko hayo hayakuugusa msingi wa Azimio la Arusha wa uchumi kumilikiwa na
wananchi. Kilichobadilishwa ni msisitizo
wa umilikaji huo kufanywa na Serikali kwa niaba ya wananchi, na badala
yake sasa unatakiwa ufanywe na wananchi wenyewe moja kwa moja kwa njia mbali
mbali. Uamuzi huo una dhamira ya
kuwaongezea wananchi uwezo wa kumiliki uchumi wa nchi
Mabadiliko
hayo ndiyo msingi wa sera ya uchumi wa soko ambapo sekta ya
binafsi imetambuliwa na kupewa fursa ya kushiriki katika kukuza uchumi (kujenga
utajiri wa nchi). Mabadiliko hayo pia
ndio msingi wa sera ya ubinafsishaji ambayo si mada ya makala haya.
Ni kweli
uchumi wa soko na ubinafsishaji ni miongoni mwa viashiria vya ubepari. Lakini ni kweli pia kwamba uzoefu ulimwenguni
kote unaonyesha kwamba njia hizo za kujenga uchumi zina ufanisi mkubwa katika
kukuza uchumi. Ujamaa una malengo
makubwa
Kwa hivyo, hata kwa CCM, “Mwelekeo wa Sera za CCM Katika Miaka ya Tisini” na baadaye “Mwelekeo wa Sera za CCM Katika Miaka ya 2000-2010” ni mkakati mpya wa Chama wa kujenga uwezo wa kiuchumi utakaohimili mahitaji ya malengo ya Ujamaa.
Lakini
pia ingefaa ieleweke kwamba ingawa Serikali imepunguziwa kwa kiasi kikubwa
jukumu la umiliki wa njia kuu za uchumi, lakini bado imeachiwa jukumu la kuutawala
au kuudhibiti uchumi kwani
Tunapenda
kusisitiza kwamba mabadiliko haya hayakufanywa kwa kubahatisha bali
yalizingatia kwa ukamilifu mambo ya msingi ya Azimio la Arusha na maelekezo ya
Baba wa Taifa. Wapo baadhi ya wanasiasa
na wasomi wanaoitaka CCM itangaze kwamba sasa inajenga ubepari nchini, eti kwa
sababu tu ya kuwapo nchini kwa viashiria vya ubepari. Wanasema hayo wakijua kwamba nchi za kibepari
zimekwa kwa muda mrefu sasa zikitumia mazuri ya Ujamaa kupunguza makali ya
ubepari. Mazuri hayo ni pamoja na kutoa
fursa sawa za elimu na huduma nyingine za jamii, kuboresha maslahi na mazingira
ya kazi kwa wafanyakazi (tofauti na yale aliyoyashuhudia Karl Marx wakati
akiandika nadharia yake ya ujamaa wa kisayansi) na kuwatoza kodi kubwa kubwa
matajiri ili Serikali ipate fedha za kuwahudumia maskini. Mataifa ya kibepari yanapochukua hatua kama
hizo ambazo kimsingi ni za kijamaa, hayajiiti ya kijamaa, hayasemi yanajenga
Ujamaa na wala hayana lengo la kujenga Ujamaa.
Kwa nini CCM inapopanga mkakati wa kuyatumia yale ya kibepari yanayoweza
kusaidia kujenga Ujamaa ilazimishwe kujitangaza kuwa sasa ni Chama cha kibepari
au kinachojenga ubepari? Wanaoitaka CCM
itangaze kuwa inajenga ubepari wana
agenda ya siri ya kutaka CCM ikose imani ya Watanzania na wao wapate mwanya wa
ubabaishaji wa kujitangaza kuwa wao ndio wajamaa na watetezi wa wanyonge. Aghlabu ni watu hao hao ambao hivi sasa eti
wanajinasibisha na Baba wa Taifa lakini wakati alipokuwa Mkuu wa Nchi na Chama
akiongoza ujenzi wa Ujamaa katika mazingira ya wakati ule, wakimlaumu na
kumkosoa hata kama ni kwa siri. Kama si
wanafiki ni nani?
Mazingatio
ya Maarifa Katika Kujenga Msingi wa Kujitegemea:
Tumekwishaeleza
kwamba Azimio la Arusha limeyataja juhudi na maarifa kuwa ndiyo
masharti ya maendeleo. Tumeeleza vile
vile kwamba uzoefu unaonyesha kwamba Watanzania wamekuwa wakitumia zaidi juhudi
kuliko maarifa, hasa katika kilimo na hivyo uzalishaji wa mali haujawa na tija
ya kutosha. Matokeo yake ni kwamba
uchumi wa nchi umeendelea kuwa ulio nyuma na tegemezi. Lakini tumekwishaonyesha pia kwamba malengo
ya Ujamaa ni makubwa na kamwe hayatoweza kufikiwa kama uchumi wa nchi
utaendelea kuwa wa namna hii.
Ni katika
mazingatio ya ukweli huu ndiyo “Mwelekeo wa Sera za CCM Katika Miaka ya 2000
Hadi 2010” ulipotungwa. Mwelekeo huu
wa sera umetoa msisitizo kwenye kujenga msingi wa uchumi wa kisasa wa taifa
linalojitegemea na kutumia mkakati wa “modenaizesheni”, yaani
matumizi ya teknolojia ya kisasa katika kilimo, ufugaji, uvuvi, viwanda n.k.
ili kukuza tija na hivyo utajiri wa nchi.
Sura ya
Pili ya Mwelekeo huu wa sera inalichambua kwa kina suala hili. Itoshe tu hapa kunukuu ibara za 19 na 20 za
Mwelekeo kama ifuatavyo:-
19.
Uzoefu wa dunia unaonyesha kuwa huduma za kiuchumi
na za kijamii za kisasa; barabara, mahakama, elimu, afya, maji n.k. zote
zinagharamiwa na uchumi wa kisasa. Hivi
ndivyo ilivyo Ulaya, Marekani n.k. na hakuna mgongano. Nchi za Asia ambazo mara nyingi
tunazitolea mifano zimeelewa hilo na wamechukua na wanaendelea kuchukua
hatua za kuufanya uchumi wao uwe wa kisasa zaidi ili umudu kubeba gharama za
huduma za jamii, mahakama, barabara n.k. kutokana na misaada na mikopo kutoka
kwa wahisani. Hili si jawabu la
kudumu. Jawabu la kudumu ni kujenga
nguvu za uchumi wetu za kulipia gharama hizo za lazima za maendeleo yetu.
20. Katika azma ya
kujenga msingi wa uchumi wa kisasa (Modenaizesheni) wa taifa linalojitegemea
msukumo wetu uelekezwe kwenye maeneo
yafuatayo (ambayo yamebainishwa na kuchambuliwa. Maeneo hayo ni elimu ya kisasa; kilimo,
ufugaji na uvuvi wa kisasa; viwanda; madini; utalii; miundombinu ya kiuchumi;
sera muafaka za fedha na biashara; na kazi, maarifa, nidhamu, idadi ya watu na
maendeleo ya uchumi.
Nayo kwa upande wake, “Ilani ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba, 2000” inafanya majumuisho kama ifuatavyo katika ibara yake ya pili:-
2. Mwelekeo wa
Sera za CCM za Miaka ya 2000 hadi 2010 unaunganisha malengo makuu haya ya
Mwelekeo wa Sera za CCM Katika Miaka ya Tisini na kuendeleza utekelezaji wake
ili kujenga msingi wa uchumi wa kisasa wa Taifa linalojitegemea na
uwezeshaji wa kiuchumi wa wananchi.
Uchumi wa sasa wa Tanzania ni uchumi ulio nyuma na tegemezi. Nchi haiwezi kujitegemea kiuchumi wakati
uchumi wake uko nyuma na pia uchumi wake hauwezi kuwa ulioendelea kama
haujitegemei. Kadri uchumi unavyozidi
kuwa wa kisasa, yaani modenaizesheni ya uchumi wa taifa, ndivyo nchi
inavyoingia katika mkondo wa kujitegemea kiuchumi … Uchumi wa kisasa utajengwa kwa kuhakikisha
kuwa sayansi na teknolojia ya kisasa inapenyezwa katika sekta zote ili hatimaye
kuutokomeza umaskini nchini.”
Katika juhudi hizo zinazofanywa na CCM za kujenga msingi wa uchumi wa Taifa linalojitegemea katika mazingira ya utandawazi unaosukumwa na ubepari, tunahitaji mitaji mikubwa na teknolojia ya kisasa. Walionazo nyenzo hizo za msingi kwa sasa ni mabepari. Kwa hivyo hakuwezi kuwa na njia ya mkato katika kuzipata nyenzo hizo ila kuwakaribisha kama wawekezaji. Hiyo ndiyo mantiki ya sera za ubinafsishaji na kuvutia vitega uchumi hata vya nje, nchini. Lakini katika kuwalinda wanyonge na kuwawezesha nao kuhimili ushindani, ndiyo maana CCM imeweka mkakati wa kuwawezesha wananchi, ambao ni mada iliyo nje ya upeo wa madhumuni ya makala haya.
Masharti/Miiko
ya Uanachama:
Sehemu ya
Tano ya Azimio la Arusha inaweka masharti sita yafuatayo kwa viongozi:
1.
Kiongozi wa TANU (baadaye CCM) au wa
Serikali sharti awe mkulima au mfanyakazi na asishiriki katika jambo lo lote la
kibepari au kikabaila.
2.
Asiwe na hisa katika makampuni yo yote.
3.
Asiwe mkurugenzi katika kampuni ya kikabaila au
kibepari.
4.
Asiwe na mishahara miwili au zaidi.
5.
Asiwe na nyumba ya kupangisha.
6.
Viongozi tunaofikiria hapa ni wajumbe wa Halmashauri
Kuu ya Taifa, Mawaziri, Wabunge, Wakuu wa Vyama vilivyoshirikishwa na TANU (baadaye
Jumuiya za CCM), Wakuu wa Mashirika ya Kiserikali, Viongozi kutokana na
kifungu cho chote cha Katiba ya TANU (baadaye ya CCM), Madiwani, na
Watumishi wa Serikali wenye vyeo vya kati na vya juu. (Kwa mujibu wa kifungu hiki kiongozi ni mtu
na mkewe au mke na mumewe).
Lengo la msingi la masharti haya lilikuwa ni kujenga maadili mema ili miongoni mwa viongozi wasitumie madaraka yao kujinufaisha binafsi.
Hata
hivyo, kufuatia “Mwongozo wa 1981”, masharti hayo ya uongozi yakafanywa ya
wanachama wote na kuingizwa kwa namna hiyo katika Katiba ya CCM ya
1982. Utekelezaji wa masharti haya
ulifikia hatua ya kuwafukuza watu uanachama hata kwa sababu ya kufuga kuku 500
tu au kupangisha vibanda vyao. Hali hiyo
ilitoa picha kama kwamba ujamaa ni umaskini na kwamba kila ukiwa maskini zaidi
ndiyo unakuwa mjamaa zaidi. Watu wakaogopa kufanya shughuli za kuchuma
mali hata zile za halali. Ubunifu wa
kujikwamua na umaskini ukavia katika jamii.
Hili siyo lengo la Ujamaa.
Ujio wa
mabadiliko makubwa ya kiuchumi, kijamii na kisiasa katika miaka ya tisini
kuliifanya CCM iitazame upya mikakati yake ya kujenga Ujamaa. Kwanza iliona ina wajibu wa kuwaondoa
Watanzania katika utamaduni wa kuthamini umaskini uliokuwa unaanza kujengeka
kwa jina la Ujamaa na Azimio la Arusha.
Pili, katika mazingira ya mfumo wa vyama vingi, haikuona uhalali wa
kuendelea kuwafunga mikono wanachama wa CCM tu na kuwaacha wengine wafaidike
peke yao na mageuzi ya kiuchumi yaliyokuwa yanaandaliwa.
Ni kwa
msingi na mazingatio hayo na mengineyo ndipo CCM katika Maamuzi ya Zanzibar
ya 1991 (ambayo huitwa Azimio la Zanzibar kwa makosa na baadhi ya watu)
ilipopitisha maamuzi ya msingi yafuatayo:-
(1)
Masharti ya uanachama yarejeshwe kuwa ya viongozi tu
kama ilivyokusudiwa katika Azimio la Arusha.
(2)
Msisitizo wa masharti ubaki katika kuhakikisha
maadili mema miongoni mwa viongozi na kuwaongezea uwajibikaji kama
ilivyokusudiwa katika Azimio la Arusha badala ya kuwazuwia kushiriki katika
shughuli halali za kujipatia riziki.
(3)
Zaidi ya wakulima na wafanyakazi, wananchi wengine
wenye kufanya shughuli nyingine halali za kujipatia riziki (wakiwemo
wafanyabiashara) waruhusiwe kujiunga na CCM.
Katika
eneo hili pamekuwa na upotoshaji makubwa kwamba eti viongozi wameondolewa
masharti na miiko na kwamba kwa hivyo eti, Maamuzi ya Zanzibar yalikiuka Azimio
la Arusha. Hii si sahihi hata
kidogo. Viongozi bado wanafungika na
masharti ya msingi ya Azimio la Arusha.
Na katika kuhakikisha hivyo, ibara ya 17 ya Katiba ya CCM (toleo la
1997) inataja sifa za Kiongozi na ibara ya 18 imeiweka bayana miiko ya
Kiongozi. Tunazinukuu hapa chini ibara
hizo ili kuondoa shaka:-
17. Pamoja
na kutimiza masharti ya Uanachama kama
yalivyoelezwa katika Katiba, Kiongozi sharti pia awe na sifa zifuatazo:-
(1)
Awe ni mtu aliyetosheka, na asiwe mtu aliyetawaliwa
na tamaa.
(2)
Awe ni mtu anayependa kueneza matunda ya uhuru kwa
wananchi wote kwa ajili ya manufaa yao na maendeleo ya Taifa kwa jumla.
18. (1) Ni mwiko kwa kiongozi kutumia madaraka
aliyopewa ama
kwa ajili
ya manufaa yake binafsi au kwa upendeleo, au kwa namna yoyote ambayo ni kinyume
cha lengo lililokusudiwa madaraka hayo.
(2)
Ni mwiko kwa kiongozi kupokea mapato ya kificho,
kutoa au kupokea rushwa au kushiriki katika mambo yoyote ya magendo au mambo
mengine ambayo ni kinyume cha lengo lililokusudiwa madaraka hayo.
Miiko hii inalinda misingi ya masharti ya uongozi ya Azimio la Arusha na kamwe haipingani nayo wala kuidhoofisha au kuifuta kama inavyodaiwa na baadhi ya wanasiasa na wasomi.
HITIMISHO:
Tumeonyesha
katika makala haya kwamba CCM haijaachana kamwe na Ujamaa na Kujitegemea. Ujamaa na kujitegemea ndiyo siasa au itikadi
ya CCM. Ujamaa na Kujitegemea ndilo
lengo la msingi na la kudumu la CCM. Kwa
CCM, lengo hilo halibadiliki. Tunaamini
hivyo hata kwa nchi kwani Watanzania wanapenda Ujamaa na wanachukizwa na
ubepari.
Tumeonyesha
pia kwamba Azimio la Arusha linaendelea kuwa dira ya CCM katika safari ndefu na
ngumu ya kujenga Ujamaa na Kujitegemea.
Kwa hivyo, wale wanaodai kuwa CCM haina dira ama hawajaelewa, au ni
wababishaji tu au mbaya zaidi, ni wapotoshaji wa makusudi wenye agenda ya siri
ya kuipaka matope CCM kwa lengo la kujinufaisha kisiasa. Azimio siyo tu ni dira, bali ndilo chimbuko
la sera mbali mbali za CCM za utekelezaji wa siasa ya Ujamaa na
Kujitegemea. Mara chache sana Azimio
huweza kubadilika na wakati kwa vipengele visivyokuwa vya msingi, bila ya
kuathiri lengo na madhumuni ya msingi.
Mabadiliko ya aina hiyo yaliridhiwa hata na Baba wa Taifa mwenyewe. Na ndiyo maana alikuwa miongoni mwa watu wa
kwanza walionunua hisa za Benki ya CRDB ilipobinafsishwa.
Aidha
tumeonyesha katika makala kwamba kinachobadilika kila baada ya muda ni sera na
mikakati ya utekelezaji wa Siasa ya Ujamaa na Kujitegemea. Sera hutungwa kwa ajili ya kutoa mwelekeo
katika jambo mahsusi kwa kipindi fulani, ndani ya upeo wa dira kuu (Azimio la
Arusha) na kwa kulenga lengo kuu (Ujamaa na Kujitegemea). Vivyo hivyo kwa mikakati ya utekelezaji wa
sera hizo.
Pia,
katika makala haya, tumekiri kama linavyokiri Azimio la Arusha lenyewe kwamba
Tanzania si nchi ya ujama kamili. Na
wala haijawahi hata siku moja kuwa nchi ya ujamaa kamili. Lakini chini ya CCM, Ujamaa na Kujitegemea ndilo
lengo kuu ambalo kulifikia kwake si kazi rahisi wala ya muda mfupi.
Tumejenga
pia hoja kwamba kuwepo kwa viashiria vya ubepari nchini (ambavyo vimekuwapo
toka enzi za ukoloni na wakati Azimio linaandikwa na baadaye kutekelezwa)
haiwezi ikawa sababu ya kuitaka CCM itangaze kuwa inajenga ubepari kama baadhi
ya wanasiasa na wasomi wanavyotaka. CCM
inayatumia yale ya ubepari yanayoweza kusaidia katika ujenzi wa Ujamaa, kama
vile yanavyofanya mataifa ya kibepari
ambayo yamefanikiwa kuyatumia mazuri ya Ujamaa katika kupunguza makali ya
ubepari. Kwa hivyo, CCM kwa mazingira ya
wakati huu, kutumia sera za uchumi wa soko na ubinafsishaji kisiwe kioja.
CCM
inajua inachokifanya kama ibara ya 9 ya”Ilani ya Uchaguzi Oktoba, 2000”
inavyobainisha; yaani:-
9.
Chama Cha Mapinduzi kinasimamia
utekelezaji wa mageuzi ya kisiasa na kiuchumi huku kikielewa kwamba katika
kipindi cha awali cha utekelezaji wake, uchumi wa soko huwanufaisha walionacho
na wajanja wachache. Kwa msingi huo
Chama Cha Mapinduzi kitaendelea kuchukua hatua madhubuti za kisera ili kuwalinda
na kuwawezesha kiuchumi wanaoathirika na ushindani na uchumi wa soko. Lengo ni kutekeleza uchumi wa soko na
wakati huo huo kuelekeza faida na ziada
zitokanazo na sekta za umma na binafsi katika kupambana na umaskini.
Matokeo
ya hatua hizo yatachukua muda kuonekana na hivyo si sahihi kuzihukumu hivi
sasa, kiasi cha miaka kumi tu toka zianze kuchukuliwa, kama baadhi ya wanasiasa
na wasomi wanavyofanya bila ya kupendekeza hatua mbadala.
Tumeonyesha
pia katika makala haya kwamba kubwa lililofanywa na Maamuzi ya Zanzibar ni
kuwaondolea wanachama wa CCM mzigo wa masharti ya uongozi na badala yake
kuyaacha kwa viongozi wenyewe tu kama ilivyokusudiwa na Azimio la Arusha. Kwa hivyo, madai kwamba Maazimio ya Zanzibar
yamelidhoofisha au kuliua Azimio la Arusha si sahihi na ni upotoshaji mtupu.
Tunamalizia
kwa kusisitiza kwamba mabadiliko ya sera hayafanywi kwa kukurupuka tu. Yanafanywa kwa uangalifu mkubwa kwa
kuhakikisha kwamba juhudi za kujenga Ujamaa hazivurugiki na lengo halipotezwi. Azimio la Arusha lenyewe limeacha wazi
milango ya mabadiliko na Baba wa Taifa mwenyewe aliridhia uwezekano huo mwaka
1987 katika hotuba yake maarufu ya “Kujitawala ni Kujitegemea”.