USHINDI   WA CCM UKO   WAZI   WAZI

 

 Hakukosea hata kidoga mgombea urais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi ndugu Jakaya Mrisho Kikwete aliposema kwamba ushindi kwa CCM ni wa asilimia 90. Ni dhahiri ndugu Kikwete alikuwa na sababu za msingi aliposema maneno hayo mbele ya umati mkubwa wa wananchi wa mjini Sikonge mkoa wa Tabora tarehe 9/10/2005. Na ni dhahiri kuwa watanzania walio wengi wanaamini ya kwamba CCM ndicho chama bora kuliko vyama vingine vyote vya siasa.

 

Kielezo kimoja wapo cha nguvu na umakini wa Chama Cha Mapinduzi ni wingi na ubora wa makada wake. Chama Cha Mapinduzi kina kila sababu ya kujivunia ubora wa mtaji huu. Tunapokiongelea Chama Cha Mapinduzi tunaongelea itikadi, malengo na sababu sahihi za Chama kikubwa na chenye historia inayotukuka.  Na kamwe sio nasaba na umaarufu wa mtu mmoja mmoja ndani ya chama kama vilivyo vyama vya upinzani hapa nchini. Tunaamini ya kwamba hakuna hata mwananchi mmoja mwenye uelewa wakutosha atakayethubutu kukipa kura ya ndiyo chama ambacho muhimili wake ni mtu mmoja kwani kwa kufanya hivyo atakuwa ameiweka nchi yetu rehani na katika hatari ya kupelekwa katika kiza kinene cha mapungufu ya mtu huyo. Kwa mantiki hiyo basi tuna hakika ya ushindi wa asilimia 90 na pengine hata zaidi. Aidha, Chama Cha Mapinduzi kimesheheni wagombea wenye kutambua na kuyajali matatizo ya wananchi. Na kwa kuwa itikadi na malengo ya CCM vinalenga katika kuwaletea maendeleo ya kweli wananchi wa Tanzania ndio maana CCM ina kila sababu za kujiamini.

 

Wagombea udiwani, ubunge na urais wa Chama Cha Mapinduzi hata uwaamshe saa nane usiku watakuambia historia, madhumuni, itikadi, malengo, na hata mwelekeo wa Ilani ya Chama chao. Uelewa na umakini huu wa Makada wa CCM ni jambo nadra kulikuta kwa wagombea wa vyama vya upinzani. Udhaifu na mapungufu haya kwa viongozi wa vyama vya upinzani, utatufanya tuwe na mashaka kuhusu mwelekeo wa vyama hivyo. Ndiyo maana tunakila sababu ya kuamini kuwa vyama vya upinzani vinalenga kuitumbukiza nchi yetu katika machafuko.makubwa. Mapungufu haya ya viongozi wa vyama vya upinzani ya kushindwa hata kuelewa vema vyama vyao, haiyumkini ndiyo sababu ya viongozi hao kushindwa kuweka mipaka kati ya siasa zinazolinda maslahi ya Tanzania za amani, utulivu, na maendeleo na saiasa za chuki na vurugu. Imekuwa ni tabia kwa wapinzani kutumia hamasa hasi za wafuasi wao kuendesha kampeni kwa njia ya vitisho, vurugu na kusababisha maafa.

 

Haingii akilini hata kidogo kwa ngombea uraisi katika nchi yenye misingi imara ya amani na utulivu kama Tanzania kunukuliwa na waandishi wa vyombo vya habari kuwa ameacha kugombea ubunge kwa sababu hapendi namna mawaziri wanavyojibu maswali ndani ya bunge. Je mtu huyo akiwa rais si tunaweza kusikia siku moja amewaondoa pasipo kufuata mantiki ya hoja na sheria mawaziri wake kwenye kikao kwa sababu wametofautiana hoja? Hii itasababisha uvunjifu wa amani na kujenga hofu kwa mawaziri na hata watendaji wengine wa serikali. Watanzania tupo tayari kuilinda amani ya nchi yetu hivyo ni dhahiri kuwa hatutamchagua mtu anayeongozwa na utashi binafsi kuwa rais. Ndiyo maana tunaamini kuwa CCM itashinda kwa kishindo.

 

Wapinzani bado ni dhaifu mno na wakati mwingine huwa hawatambui cha kuwafanyia watanzania. Ndio maana hata katika kampeni zao badala ya kuelezea sera zao, hutumia muda mwingi kukikashfu Chama Cha Mapinduzi, na hata kuwadanganya wananchi kwa kuwapa taarifa za uongo. Mfano, yuko mgombea ambaye aliwaeleza wananchi kuwa Baba wa Taifa ndiye alitoa wosia kwa CCM kwamba watanzania wasipewe elimu wala fursa za kujiendeleza kiuchumi, kwamba itakuwa ni vigumu kwa CCM kutawala wasomi na matajiri. Mgombea huyu kamwe hana hofu ya Mungu. Anasahauu kuwa wananchi wanajua fika kuwa CCM imekuwa na sera nzuri na zinazotekelezeka kuhusu elimu na uwezeshwaji kiuchumi wa mtu mmoja mmoja tangu vyama asisi vya TANU/AFRO-SHIRAZ. Na kiashiria kikubwa cha kukubalika na kuaminika kwa CCM hata kabla ya uchaguzi tayari ina Wagombea wasiopungua 8 wa ubunge na madiwani wanaozidi 120 wa CCM wamekosa upinzani. Kadiri tunavyoelekea ukikongoni, vyama vya upinzani watazidi kuingia mitini. Hakika CCM itashinda kwa kishindo 2005.

 

Ushindi wa kishindo wa Chama Cha Mapinduzi unathibitishwa zaidi na matokeo ya uchaguzi wa Serikali za Mitaa uliofanyika Novemba 2004 ambapo CCM ilionesha kuwa ni maji ya kina kirefu ambacho hakipimwi kwa miguuu miwili. Katika uchaguzi huo Chama cha Mapinduzi kilijizolea ushindi wa siyo chini asilimia 96 na kuwaacha wapinzani wakiwa hoi bin taaban. Kwa kuwa ni wananchi walewale ndio watakopiga kura kuchagua rais, wabunge na madiwani, hapana shaka ushndi kwa CCM ni utakuwa katika kiwango cha uwiano kama hicho cha Serikali za Mitaa.

 

Wagombea wa CCM wanafahamu kuwa maendeleo kwa watanzania kamwe hayataletwa kwa miujiza kama ambavyo ahadi za wapinzani zinavyosema. Ndiyo maana siko zote CCM, imeweka bayana kuwa, wananchi wakukubali kuwa kujitegemea kwa kufanya kazi kwaa bidiii na maarifa ndio msingi wa maendeleo na kutokomeza umasikini. Kila mtu mwenye uwezo wa kufanya kazi anawajibu wa kufanya kazi na kushirikiana na serikali kubuni na kutekeleza mbinu bora zaidi za uwezeshaji wananchi. Aidha, mtaji wa masikini ni ari, nguvu, kasi na akili zake mwenyewe. Uwezeshaji ni njia ya kumuunga mkono.

 

Kwa vyama vya upinzani, kuwaahidi wananchi kuwa vitawaletea maendeleo bila ya kuunganisha nguvu zao katika kufanya kazi ni uongo na unafiki mkubwa unaopaswa kupigwa vita. Wapinzani walitarajia kukiona Chama cha Mapinduzi kikiwaletea watanzania maendeleo kwa njia ya “akadabla(mazingaombwe), hili ni jambo lisilowezekana: Hata wayunani wakale walisema, “Impossibilium nullaest obligation” yaani hakuna mwenye kupaswa kutenda lisilo wezekana: Tuna imani na wananchi wa Tanzania kuwa ni watu wenye uwezo wa kuzitambua pumba na kuziweka mbali na mchele.

 

Wapinzani hawaelewi watanzania wanataka nini ndio maana mara nyingi wamekuwa wakitumia kampeni za vitisho na wakati mwingine wafuasi wao wakihatarisha amani na utulivu uliojengeka miongoni mwa watanzania. Watanzania hawahitaji vitisho, watanzania, haawahitaji kuona damu ya raia wema ikimwagika. Watanzania tumezoa Amani, utulivu na mshikamano wa kitaifa. Hivyo wapinzani wanaotumia kampeni za vitisho wasitegemee kupata kura za watanzania:

 

Wakati kampeni za uchaguzi za 2005 zinaanza wapinzani walikuwa wanafanana na mvuvi anayeng’ang’ania kuwawakilisha wakulima au mwalimu anayetaka kuwa mwakilishi wa daktari. Kadiri siku zinavyokwenda wapinzani wanachukua sura ya mbabaishaji anayeng’ang’ania kuwa mweka hazina wa umoja wa raia wema. Watu hawa wakifanikiwa kutimiza azma yao, maisha na rasilmali za raia hawa wema vitakuwa mashakani.Wapinzani wajiandae kushindwa kwa kishindo 2005.

 

Kwa muda mrefu majukumu ya wapinzani yamekuwa ni kudai ruzuku kutoka serikalini kwa nguvu zote, kuudanganya umma wa watanzania kwa kutoa ahadi zisizotekelezeka, kuwatishia wananchi wanaonekana kuwa na msimamo na imani na Chama Cha Mapinduzi na kulalamika bila ya sababu za msingi. Hivi kamwe havitoi mvuto kwa watanzania wa kuvikuchagua vyama hivi vya upinzani.

 

Wapinzani bado ni wachanga mno katika ulingo wa siasa. Kuwa wachanga sio kosa. Kosa kubwa la wapinzani ni kwamba hawataki kukua. Kama vyama vya upinzani vingekuwa tayari kukua na kukomaa kisiasa basi viongozi na wafuasi wa vyama hivyo wangekuwa tayari kujifunza kutoka hata kwa mtoto mdogo wa miaka miwili: Watoto wadogo huwa wanaangalia na kujali hali halisi, huwa hawaendishwi na yale ambayo  hawawezi kupambana nayo. Kama wapinzani wamejifunza hili, wangekubaliana na hali halisi ya kutokukubalika kwao mbele ya wananchi waliyo wengi na hivyo wasingepoteza nguvu na muda mwingi katika kupambanana na mkongwe Chama cha Mapinduzi kwa kuwadanganya watanzania na kutumia mkakati na mbinu duni kama vitisho ili kutafuta ridhaa za watanzania.

 

Ni jambo la kushangaza kwa mtanzania mwenye akili zake timamu kung’ang’ania kuingia katika kinyang’anyiro ambacho amekuwa akitupwa nje kwa kipindi cha miaka kumi na mitano bila kuona aibu. Hivi mtu huyu anatarajia malaika washuke kutoka mbinguni waje kumwambia kuwa hakubaliki kwa watanzania ndio afike kikomo? Na inakuaje kuwa mtu mwingine ambaye anatembea na ofisi za chama chake kwenye kikapu, kuomba kura ili aingie ikulu?Hivi watu kama hawa kama hawana lengo la kuwachekesha watanzania wana malengo gani? Na inakuwaje kwa mtu anayejiita mpinzani kuacha kupanga mikakati ya kampeni na badala yake kwenda kwenda mahakamani kudai ruzuku kwa ajili ya chama chake ambacho hakijui hata rangi za bendera ya taifa letu? Hiii sio aina ya wapinzani tuliyoikusudia tulipo ridhia kuingia katika mfumo wa vyama vingi.

 

Kwa kuwa wanatambua wazi kuwa hawakubaliki kwa watazania waliyo wengi hivyo hawataingia Ikulu wala bungeni, lakini bado wanang’ang’ania kuzunguka huku na kule kujinadi. Tunashawishika kuamini kuwa wengi wao hawapo kwa ajili ya maslahi ya watanzania. Pengine hiki ndicho kinachowafanya wengi wao watumie nguvu nyingi sana katika kudai ruzuku kuliko kupanga mikakati ya kuwaletea watanzania maendeleo. Hii imewafanya wapinzani wengi kukosa mwelekeo sahihi hata kama inapotokea baadhi yao kuingia bungeni, huwa si jambo la ajabu kwao kusahau kilichowapeleka bungeni na badala yake kufanya mambo ya kihuni ambayo hupelekea baadhi yao kutimuliwa bungeni. Tunaimani na wananchi wa Tanzania hawataharibu kura zao kwa kuwapa watu hawa badala yake watakichagua Chama cha Mapinduzi kwa kura nyinngi iwezekanavyo hivyo kupelekea kupatikana kwa Ushindi wa Kishindo, kwa maisha bora ya kila Mtanzania.

 

Nguvu ya Hoja

Abiyani Chuo Kikuu.