CCM BADO NI CHAMA BORA NA
KINASTAHILI KUPEWA RIDHAA YA KUONGOZA TANZANIA KATIKA AWAMU HII YA NNE
Yapata miaka minne sasa tangu Mheshimiwa Rais Benjamin
Mkapa alipotanngaza rasmi mpango wa elimu kwa wote,
yaani elimu ya bure kwa watoto wa shule za msingi. Kufutwa kwa
ada iliyokuwa ikitozwa kwa kila mwanafunzi ili kupata elimu ya msingi
kumechochea ongezeko kubwa la idadi ya watoto walioandikishwa kuanza elimu ya
msingi na hivyo kuleta matumaini makubwa kwa taifa hasa tunapozingatia ukweli
kuwa watoto ni akiba na nguvu kazi ya taifa la kesho.
Elimu kwa wote ni sera ama mpango wa dunia
nzima kufuatia makubaliano ya Jomtien huko nchini Thailand ya mwaka 1990
yaliyopitiwa na kuwekewa malengo katika mkutano wa wakuu wa nchi za Umoja wa Mataifa
Septemba 2000, na kuwekwa kama lengo mojawapo na mahsusi katika malengo ya
milenia.
Lengo la sera ama mpango huo wa elimu kwa wote
ni kuwezesha hasa wale watoto wanaotoka katiaka familia zenye hali duni ya
kimaisha/kiuchumi, yatima watokanao na UKIMWI watoto wa mitaani na wengine
wanaoishi katika mazingira magumu kupata elimu ya msingi, ikiwa na lengo la
kuwawezwesha kushiriki katika kujenga maisha yao ya baadaye na pia kujenga
uchumi wa taifa letu. Hatua ya kutoa elimu ya msingi kwa wote ni hatua ya utambuzi kuwa watoto ni hazina kubwa
kwa taifa linalonuiya kujenga uchumi endelevu.
Matarajio ya mpango huo wa
elimu kwa wote ni kumwezesha kila mtoto Mtanzania kupata elimu ya msingi bila
kubaguana, yaani katika hali fulani ya usawa. Japo zipo shule za msingi zenye
viwango mbalimbali vya ubora, tukizingatia huduma za ziada ambazo hutolewa
katika shule hizo – hasa zile za watu binafsi – bado kila mtoto wa kitanzania anaweza kupatiwa elimu nzuri na ya kuridhisha
katika shule za serikali ambazo idadi yake sasa imeongezeka na zile
zilizokuwepo zimepanuliwa katika mpango wa MMEM. Ikumbukwe kuwa haya yote ni kwa maendeleo endelevu ya nchi masikini duniani zikiwemo
zile za Afrika: Kusini mwa Jangwa la Sahara.
Tanzania ni moja
kati ya nchi chache sana masikini duniani, zilizofanikiwa kwa
kiasi kikubwa katika kutekeleza mpango wa dunia nzima wa Elimu Kwa Wote. Hapa
tunaweza kutaja mipango ya MMEM na MEMKWA kama sehemu tu ya mafanikio hayo. Chini
ya mpango kabambe wa MMEM, idadi ya madarasa
yanayotumiwa na watoto katika shule za msing imeongezeka, kila shule ikipatiwa
walao darasa moja. Pia zipo shule nyingine nyingi zilizojengwa ama zinazojengwa
katika harakati nyingine za kuhakikisha kuwa kila kijiji kinakuwa na walao shule moja ya msingi na hata zaidi.
Takwimu zinaonyesha kuwa kufuatia mabadiliko
hayo yaliyotokea ama yanayotokea katika sekta ya elimu, idadi ya watoto
walioandikishwa katika shule za msingi iliongezeka kutoka watoto millioni 4.4
mwaka 2000 hadi kufikia millioni 7.5 mwaka 2004 ikiwa ni zaidi ya asilimia 94
ya watoto wote Tanzania waliofikia umri wa kuanza shule ya msingi. Sambamba na hilo idadi ya walimu wa shule za msingi
imeongezeka na kusababisha tofauiti katika uwiano wa mwalimu kwa wanafunzi. Pia
vyuo vya walimu vimeongezeka na mipango maalum ya
kufundisha walimu imekuwepo.
Kufuatia mafanikio makubwa yanayoonekana
dhahiri kutokana na mipango ya MMEM na MEMKWA,
wananchi wamehamasika na wamekuwa na mwamko chanya wa elimu. Hilo linathibitika katika juhudi
mbalimbali za wananchi, katika sehemu mbalimbali hapa nchini, kuamua kuunga
mkono juhudi za serikali ya awamu ya tatu chini ya utawala wa
Chama Cha Mapinduzi, kwa kuweka mipango ya kujenga
shule za Sekondari za Kata. Ama kweli aliye na macho
haambiwi tazama. Shule za Sekondari (za kata) zinamea kote nchini kwa juhudi za wananchi. HEKO CCM kwa
kujenga mazingira mazuri ya kuwawezesha wananchi kutambua na kuchukua jukumu
lao la kuendeleaza elimu hapa nchini.
Ikumbukwe kuwa elimu bora ni
silaha mbadala ya kupambana siyo tu na umasikini uliokithiri kwenye nchi
zilizoko kusini mwa Jangwa la Sahara, Tanzania ikiwa mojawapo, bali ni ngao
mahsusi ya kuliwezesha taifa lolote (mataifa masikini na hata mataifa tajiri)
kupambana na wimbi la utandawazi. Ndani ya utandawazi sera ni
ushindani, na hilo linawezekana pale ambapo taifa husika limejiandaa vilivyo, likiwa na
wasomi wa kutosha katika fani mbalimbali, zikiwemo zile za sayansi na
teknolojia, biashara, sanaa, sheria na nyinginezo.
Inafaa tukumbuke kuwa haya yote hayatawezekana
pasipokuwa na msingi imara katika sekta ya elimu na katika
serikali kwa ujumla. Tunapokaribia uchaguzi mkuu ni
vizuri tukajiuliza maswali machache yanayohusiana na maendeleo ya taifa letu.
Je sisi tupo wapi tukijilinganisha na wenzetu katika
nchi zilizoendelea? Tunaelekea wapi? Tutafika? Kama tutafika,tuzingatie
mambo gani? Nani anaweza kutufikisha lengo hilo, yaani kule ambako matarajio yetu
yameelekea?
Hivi sasa Watanzania tupo katika hatua muhimu sana ya kujiandaa kufanya uchaguzi hapo
tarehe 30 mwezi Oktoba 2005 . Tusipokuwa
makini tutatumbukia katika shimo la nyoka hatari wenye sumu kali, ambao bila
shaka watatuangamiza. Tuufananishe huu wakati kama vile tupo ufukweni tukisuburi
chombo tuende upande mwingine wa ziwa. Tunahitaji kufanya maamuzi makubwa na tusipokuwa makini ama tusipotumia busara, tutaweza kujikuta
tumepanda meli mbovu isiyokuwa na nahodha mahiri na hivyo kujiweka katika
hatari kubwa ya kuangamiza maisha yetu. Tukumbuke kwamba tusipofanya maamuzi ya
busara, ambayo hadi siku ya kupiga kura yatakuwa ya
hiari, tutalazimika kuteseka kwa kipindi kirefu, pengine kisichopungua miaka
mitano. Nani ana uwezo wa kutuongoza na kutufikisha
tuendako? Pia ni nani ama chama gani zaidi ya CCM
kinachoweza kuendeleza mafanikio makubwa ambayo tayari yameshapatikana katiaka
sekta mbalimbali hapa nchini ikiwemo ile ya elimu? Ikiwa Chama Cha Mapinduzi
kimesimamia na Kuwezesha mafanikio makubwa namna hii kwa
kipindi kifupi cha miaka kumi kilipokuwa madarakani tangu kuanzishwa vyama
vingi vya siasa hapa nchini, ni kwa sababu gani tusiamini kuwa CCM inaweza
kufanya mengi na makubwa zaidi kwa kipindi kijacho?
Itambulike wazi kuwa
suala la maendeleo si la mzaha hata kidogo.
Maendeleo hayaji kwa kusema tu katika majukwaa kama wanavyofanya
wanasiasa mbalimbali katika kipindi hiki cha kampeni za uchaguzi mkuu wa rais
na wabunge. Mabadiliko katika maendeleo hayaji kwa
muda mfupi kama ambavyo wapinzani mbalimali wamekuwa wakiahidi. Labda
watuhakikishie uwezo wao wa kufanya miujiza, na ikiwa
hivyo wafanye michache tuione kabla ya kuwapigia kura katika uchguzi mkuu
unaokaribia. Ni jambo la busara tukatilia maanani kuwa taifa kubwa na lenye heshima kama hili la Tanzania, haliwezi kugeuzwa kuwa uwanja wa majaribio na wanasiasa ambao
hawajakomaa.
Wote tunatambua kuwa iIli kuleta maendeleo
endelevu, katika taifa lolote lile tunahitaji sera ambazo zitaliongoza taifa
katika sekta zote, Mbili kuwepo na viongozi wenye
uzalendo na wanaojituma kwa moyo wao wote katika shughuli mbalimbali za ujenzi
wa taifa, wasio na ubinafsi na wenye utayari wa kuwatumikia wapiga kura. Tatu:- Kuwepo na demokrasia ya kweli yenye kuheshimu haki na utu
wa binadamu, na utawala wa sheria. Haya yote lazima yaanze
ama yaonekane dhariri kwenye chama chochote husika. Nne:- Kuwepo kwa dhamira na mchakato wa kupambana na rushwa. Tano:
-kuwepo na viongozi mahiri na wenye uzoefu wa kutosha
kuliongoza taifa.
Wakati sifa zilizoanishwa hapo juu ni mhimili wa maendeleo ya taifa katika nyanja mbalilimbali,
wote tunakiri kwamba sifa hizo hazipatikani katika vyama vingine vya siasa
isipokuwa Cha Mapinduzi (CCM). Kwa mantiki hiyo inakuwa vigumu kuona ni kwa namna gani maemdeleo tuliyokwisha kuyapata yatakuwa
endelevu ikiwa tutawachagua wapinzani kukamata Dola.
Wananchi tujihadhari na
ahadi za uongo zinazogubika karibia katika majukwaa yote ya vyama vya upinzani
wakati huu wa kampeni. Ahadi kama zile za kuwajengea wananchi wote wa sehemu
fulani nyumba bora na za kisasa ili waepukane na adha ya kuishi katika nyumba
za nyasi, kufuta umasikini kwa asilimia mia moja kwa muda mfupi mara tu
wakiingia madarakani, na nyingine zinazofanana na hizo ni bora zikafanyiwa
utafiti na wananchi kabla ya kuaminika. Hapa yafaa ikumbukwe kuwa kusema
jambo ni kitu kimoja na kulitimiza ni kitu kingine.
Wananchi tujiulize, ni kwa namna gani viongozi wa
namna hiyo watatimiza ahadi hizo bila ya kuwa na sera na matayarisho ya
kutosha. Tujiepushe na wanasiasa wanaohahidi
kujenga madaraja hata katika sehemu ambazo hazina mito.
Pengine ni jambo
la ukweli kabisa kwamba vyama vyote vya siasa vya upinzani vimekuwa ni sehemu
ya maisha ya wananchi wengi wa taifa la Tanzania.
Ingekuwa vyema vyama vya upinzani wakaliambia taifa hili ni
kwa namna gani wao kama sehemu ya uhai wa taifa hili wamejaribu kutatua matatizo hayo wanayoyahubiri
katika majukwaa ya kisiasa na sio tu kungojea hadi watakapoingia madarakani.
Tukumbuke kuwa wapinzani siyo tu kwamba nao ni sehemu
ya jamii hii ya watanzania bali wengine wengi kati yao wamewahi
kushikilia nafasi mbalimbali katika kuliongoza taifa hili. Ikiwa walishindwa
kuwatumikia wapiga kura wakati ule wa uongozi wao, leo hii ni lipi jipya
watakalolifanya? Labda lile la kufoji pasi za kusafiria
kwenda ngambo kulidhalilisha taifa. Kama kweli wapinzani
wameguswa na wana uchungu na hali duni za baadhi ya
wanachi, basi waonyeshe kwa vitendo wakati wote na sio tu kuyazunguzia hayo
katika majukwaa hasa wakati uchaguzi mkuu unapokaribia. Inasikitisha sana na pia inakera kuona kuwa wapinzani hugundua matatizo ya wananchi
pale tu uchaguzi mkuu unapokaribia. Kwa maneno mengine bado tunasisitiza kuwa Chama Cha Mapinduzi bado
kina kila sababu ya kuendelea kuaminiwa na wananchi na
hivyo kupewa ridhaa ya kuongoza Tanzania,
kwani CCM imekuwa inaishi kila siku na kila wakati sambamba na maisha ya
Watanzania. Tofauti na Vyama vya Upinzani ambavyo
vinakuwa hai na uwezo wao wa kuwaona wananchi hutokea wakati wa uchaguzi pekee.
Ndugu Watanzania Kura zote za NDIYO tuipe CCM. Hapo tarehe 30 Oktoba 2005.
Nguvu ya Hoja,
Abiyani Chuo Kuu.