Kabla ya kuchagua chama
gani ukipe madaraka ya kuongoza nchi kwanza fikiria uwezo wa
chama hicho kitaasisi.Chama cha mapinduzi (CCM) ni miongoni vyama vichache
duniani ambavyo vimejitengenezea muundo bora wa kitaasisi kwa ajili ya kuongoza
nchi. Vyama vya aina hii huwa na viongozi wenye uwezo mkubwa wa kuongoza nchi
bila kutetereka na kujenga imani kwa wananchi kwa kuwa na uhakika wa kuishi na
kujiendeleza kwa usalama na bila woga wowote.Kwa hali hiyo CCM ni chama ambacho
watu wengi wamekuwa wakija Kutoka
nchi mbalimbali kupenda kujifunza kutoka Tanzania ni jinsi gani kimeweza
kuongoza nchi kwa ustadi shrikishi na kwa mafanikio makubwa.
Tangia uhuru CCM ilitamka
rasmi kazi kubwa iliyopo mbele ya Taifa letu ni
kupambana maadui wakuu watatu wakiwemo Umasikini, Ujinga na Maradhi.Maadui hawa
ni maeneo nyeti ambayo CCM iliyaona kuwa tukifanikiwa hapa maisha ya mwananchi
yatakuwa bora zaidi. Serikali imetoa kipaumbele katika vita
dhidi ya umaskini. Katika
kufanya hivyo, inatekeleza malengo ya Dira ya Maendeleo ya Taifa 2025, na
vilevile mpango wa kimataifa wenye dhamira ya kutokomeza umaskini kwa nusu ya
kiwango cha sasa ifikapo mwaka 2015 na kuutokomeza kabisa ifikapo mwaka 2025.
Serikali kwa kushirikiana na wadau wengine, iliandaa Mkakati wa Taifa wa
Kusimamia Utekelezaji wa Sera za Kuondoa Umaskini
Kwa
mujibu wa ujibu wa ilani na nyaraka mbali mbali za CCM, Masuala makuu
yaliyobainishwa katika kupiga vita umaskini na Serikali ni pamoja naKukuza uchumi
unaoshirikisha watu wengi kuzingatia shughuli zinazofanywa na wadau mbalimbali
kama vile wakulima wadogo wafanyabiashara wadogo, viwanda vidogo na vya kati, Kuendeleza
huduma muhimu za kijamii na kiuchumi, Kuweka mazingira mazuri ya umilikaji wa
uchumi yanayovutia wawekezaji; Kuwa na usimamizi mzuri wa hifadhi ya mazingira
kwa maendeleo endelevu; Kuimarisha miundombinu hasa barabara na mawasiliano; Utawala
bora kuwa hasa vita dhidi ya rushwa,
uzingatiaji wa utawala wa sheria, demokrasia, uwazi, uwajibikaji na ushirikishwajiwa
wadau na
Kuwa na mfumo imara wa ufuatiliaji.
Kwa
watanzania ambao walikuwa bado hawajui hadi leo, ni kwmaba Serikali ya CCM imeonyesha
kasi kubwa kuibadili Tanzania na imewezesha
nchi kusamehewa baadhi ya madeni yake chini ya Mpango wa Msamaha wa Madeni na
Mkakati wa Kupunguza Umaskini. Pia Serikali imeandaa Mkakati wa Misaada wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania unaolenga kuboresha usimamizi wa misaada ya
wafadhili, ili kuielekeza misaada hiyo katika maeneo ya kipaumbele yaliyoainishwa
katika kupunguza umaskini. Katika kuhakikisha kuwa jamii maskini zinapata
huduma za msingi kwa gharama zinazolingana na uwezo wao kiuchumi, hatua
mbalimbali zimechukuliwa ikiwa ni pamoja na kufuta ada zote katika shule za
msingi na kupunguza ada katika shule za sekondari za Serikali, kutoa ruzuku kwa
shule za sekondari za binafsi, kutoa ruzuku ya mbolea na kuondoa kodi katika
pembejeo na zana muhimu za kilimo na mifugo na kuondoa kodi ya makisio kabla ya
kuanza biashara. Hatua hizo zimesaidia kupunguza kero zinazowakabili wananchi.
Ili
kuongesa kasi kuushinda Umasikini, Serikali ya CCM ilianzisha Idara ya kuondoa Umaskini ili
kuimarisha shughuli za uratibu na utekelezaji wa mipango ya kuondoa umaskini.
Idara hiyo ina kazi kuu ya kuratibu na kusimamia jitihada za kupunguza umaskini
nchini. Vita dhidi ya umaskini inachukuliwa kama agenda kuu ya Taifa na hivyo
kuchukua hatua za kuongeza bajeti ya fedha zinazotengwa katika sekta za
kipaumbele. Kwa mujibu wa Uchambuzi wa utafiti uliofanyika mwaka 2000/001, umeonyesha
kuwa idadi ya watu wanaoishi katika umaskini imepungua kutoka asilimia 38.6
mwaka 1991/92 kufikia asilimia 35.3 mwaka 2000/2001. Uchambuzi huo unabainisha
kuwa idadi ya watu wanaoishi katika umaskini uliokithiri, imepungua kutoka
asilimia 21.6 mwaka 1991/92 kufikia asilimia 17.7 mwaka 2000/01.
Ili
kuleta unafuu wa maisha Serikali ya CCM pia imeweza kusimamia mfumko wa bei na
kupata mafanikio makubwa ya kupungua kwa
kiwango cha mfumko wa bei kutoka asilimia 27.1 mwaka 1995 hadi asilimia 4.1
mwezi Novemba, 2004. Mafanikio hayo yametokana na utekelezaji makini wa sera za
kudhibiti ongezeko la ujazi wa fedha na karadha; kuongezeka kwa makusanyo ya
mapato ya Serikali; mkakati na mfumo wa kudhibiti matumizi ya Serikali; juhudi
za wananchi katika kuongeza uzalishaji kwenye baadhi ya mazao ya chakula; na
upatikanaji na usambazaji mzuri wa bidhaa muhimu za matumizi ya kawaida. Lengo
la Serikali ni kuendeleza sera hizo ili kiwango cha mfumko wa bei kiendelee
kushuka na kilingane na cha nchi tunazofanya nazo biashara kwa wingi. Mwenendo
wa kupungua kwa Mfumko wa Bei umeonyeshwa katika
Ili
kuongeza kasi ya kukuza uchumi na kuonge ajira Serikali ya CCM imefanya juhudi
kubwa ya kuvutia wawekezaji wa ndani na nje kwa kuweka mazingira mazuri ya
kibiashara. Kwa mujibu wa ripoti mbali mbali kuanzia mwaka 1995 hadi Desemba
2004, Kituo cha Uwekezaji (TIC) kimeidhinisha jumla ya miradi 2,321
inayokadiriwa kutoa nafasi za ajira 447,290. Kati ya miradi hiyo, 1,598 ilikuwa
mipya na miradi 723 ni ya zamani. Miradi 1,003 sawa na asilimia 43.2
inamilikiwa na wawekezaji wa ndani, miradi 610 sawa na asilimia 26.3 na
wawekezaji wa nje na miradi 708 sawa na asilimia 30.5 ni ya ubia kati ya
wawekezaji wa ndani na wa nje. Thamani ya uwekezaji katika miradi yote hiyo ni
Shilingi 7,587,078 milioni.
Kwa
kuongeza nguvu na kasi na ushiriki wa kila mwananchi Serikali ya CCM ilianzisha Mkakati wa
Kupunguza Umaskini Awamu ya Pili ujulikanao kama Mkakati wa Kukuza Uchumi na
Kuondoa Umaskini Tanzania (MKUKUTA) wa mwaka 2004. Mkakati utatekelezwa na
Serikali kwa kushirikiana na wadau mbalimbali kwa miaka mitano kuanzia mwaka
2005/06 hadi 2009/10.
Pia Serikali kwa
kutambua tatizo la ajira nchini, ilianzisha mradi wa kutoa mikopo midogo
uliotokana na mkopo wa Dola za Marekani 10.7 milioni kutoka Benki ya Maendeleo
ya Afrika. Utekelezaji wa mradi huo ulianza kwa
majaribio katika mikoa sita iliyobainika kuwa nyuma kimaendeleo. Mikoa hiyo ni Mtwara, Lindi, Pwani, Morogoro,
Dodoma na Singida. Kati ya mwaka 2000 na 2004, Mradi umeweza kutoa mikopo ya Shilingi
bilioni 3.7 ambayo ni asilimia 42 ya fedha za mkopo zinazokusudiwa kutolewa kwa
wananchi. Fedha zilizotolewa chini ya mradi huo, zimewafikia walengwa 17,404
ambao ni asilimia 53 ya walengwa waliokusudiwa. Asilimia 61 ya walengwa
waliofikiwa ni wanawake. Mikopo hiyo imewafikia wananchi kupitia asasi 73 za
kifedha ambazo asilimia 68 ni Vyama vya Ushirika vya Akiba na Mikopo.
Serikali
ilianzisha Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) kwa lengo la kuboresha huduma za
jamii ikiwa ni hatua mojawapo ya kupambana na umaskini kwa kusaidia shughuli za
wananchi katika sekta za afya, elimu, maji, miundombinu, mazingira na
mafunzo.vile vile Katika kutekeleza mwelekeo wa sera za CCM na Ilani za
Uchaguzi, Serikali imechukua hatua kadhaa ili kuhakikisha kwamba wananchi wa
Tanzania wanakuwa na uwezo zaidi wa kushiriki katika uchumi wa nchi yao. Katika
kuboresha zaidi mazingira ya uwezeshaji wa wananchi hususan kwa kutumia
rasilimali zilizopo, Serikali imefanya maandalizi ya Programu Maalum ya
Kurasimisha Rasilimali za Sekta isiyo Rasmi kuwa sekta rasmi (MKURABITA) kwa
nia ya kuwawezesha wananchi kutumia mali walizonazo kama dhamana ya kukopa
fedha kutoka benki kwa ajili ya kukuza shughuli zao za kiuchumi na hivyo
kupunguza umaskini.
Inawezekana bado kuna watu hawaamini mafanikio
haya.Kwa mujibu wa waraka uliotolewa na shirika la masuala ya Uchumi
duniani
”World Economic Forum (WEF)’’ Tanzania imepanda
kwa kasi na kuruka nafasi 11 ikilinganishwa na mchakato wa mwaka jana
ambapo kwanza ilikuwa chini ya Kenya na Uganda. kwa mujibu wa waraka huo Tanzania
ilikuwa nchi ya 71 kati ya nchi 117 zilizofanyiwa tathnini hiyo.nchi ya Uganda
ilikuwa ya 87 na Kenya ilikuwa ya 92.Awali
Tanzania ilikuwa ya 82 wakati Kenya ilikuwa ya 78 naUganda 79. katika
mchakato huo vitu vitatu viliangaliwa pia
uimara wa uchumi, ubora wa taasisi za umma na utayari wa kiteknologia..Tanzania
ilioneshwa kuwa na uimara mkubwa wa taasisi za umma na kuwa na nafasi ya 60, wakati uimara wa
Uchumi ilikuwa ya 72 na utayari wa kiteknologia..ilikuwa
nchi ya 86
Kwa maana hiyo una sababu za kuichagua CCM katika kiti cha Urais, Ubunge na Udiwani.Kidumu chama cha Mapinduzi.
Nguvu ya Hoja,