MAPAMBANO
DHIDI YA UMASIKINI NI NDOTO
Katika wiki hizi chache zilizobakia kufikia tarehe ya kupiga kura ya Rais wabunge na madiwani, wapo wananchi ambao hadi sasa bado hawajafanya uamuzi juu ya nani watakayempigia kura ifikapo tarehe therathini mwezi huu kwa madai kwamba mambo yatajiipa huko huko kituoni. Katika kipindi chote kilichopita cha wagombe kujinadi ,juu ya kipi kitakachofanyika baada ya vyama hivyo kushinda na kuingia madarakani , kila mtu anmatumaini mabubwa kwa wapiga kura wake kwamba wamemwelewa vilivyo na mategemeo makubwa kwa kila anayeingia katika uwanja wa mashindano ni kupata ushindi ,uwe wa kishindo, wa tsunami ,ushindi ni ushindi tu.Ushindi unaotarajiwa kwa kila chama ni kuona wagombea wake wanakubalika katika kila daraja , nikiwa na maana ya ushindi wa kiti cha urais, kiti cha ubunge, na kiti cha udiwani.
Wapo baadhi ya wapiga kura ambao tayari wameshafanya uamuzi wa Rais wao mtarajiwa , lakini bado wana kigugumizi cha Mbunge yupi atakayewafaa, na kwa upande wa Diwani ndio kabisaa hawajui wamchague yupi.Kigugumizi hiki kinatoka wapi basi? Ninaamini kuwa kila chama kumefanya maamuzi makini na sahihi katika kuchagua wagombea wa viti vyote vinavyotakiwa kupigiwa kura na watanzania siku ya siku itakapowadia.
Vipo vyama ambavyo
sera zake zinaonekana kuwa makini sana
, na baadhi ya sera hizo zimekwishaonyesha matokeo mazuri kwa watanzania na kilichobakia ni kuendelezwa na kuboreshwa zaidi
kinachotakiwa ni kuhakikisha kuwa kura yako inalenga
kwa wagombea watakaokuwa wamepitishwa wa chama kimoja ili kuonyesha ukomavu wa fikra, na
utumiaji wa uhuru wako wa
kuchagua chama kinachofaa kuiongoza nchi yetu kwa
kipindi 2005-2010 Tunapochagua
Rais tuchague na wasaidizi wake watakaomwezesha kufanya maamuzi sahihi katika kutekeleza ilani ya chama kilichomweka
madarakani. Kwa kuwa kila
chama kin
Tanzania chini ya chama cha mapinduzi imekuwa mbali kiushindani kiuchumi mbali zaidi ya Kenya and Uganda katika mwaka 2005 mchakato wa ushindani
huo.Kwa mujibu wa waraka uliotolewa
na shirika la masuala ya Uchumi
duniani
“”World Economic Forum (WEF)’’ Tanzania imepanda kwa kasi
na kuruka nafasi 11 ikilinganishwa na mchakato wa
mwaka jana ambapo kwanza ilikuwa chini ya Kenya na Uganda.kwa mujibu
wa waraka huo Tanzania ilikuwa nchi ya 71 kati ya nchi 117 zilizofanyiwa tathnini hiyo.nchi ya Uganda ilikuwa ya 87 na
Kenya ilikuwa ya 92.Awali Tanzania ilikuwa
ya 82 wakati Kenya ilikuwa ya 78 naUganda
79 katika mchakato huo vitu vitatu
viliangaliwa pia uimara wa uchumi, ubora
wa taasisi za umma na
utayari wa kiteknologia..
Katika mafanikio ya ushirikiano
wa
Katika kuzikabili gharama kubwa za utoaji wa elimu hasa
katika mwelekeo huu mpya, itabidi Serikali iongeze kipaumbele katika bajeti ya
elimu na pia kuimarisha zaidi shirkiano(“partnership”) na wahisani, sekta
ya binafsi na jamii kupitia vyombo na taasisi zake mbali mbali (k.v. NGOs.
Jumuiya za Wananchi,n.k) Aidha, itabidi jitihada ziongezwe za kuwaelimisha
wazazi juu ya jukumu lao la msingi la kuchangia gharama za elimu ya watoto wao na kuweka utaratibu wa kuwasaidia
wale wasiokuwa na uwezo. Katika kipengele hiki , ni vigumu sana kwa taifa
kufanikiwa endapo hakutakuwa na uhishirikiano kati ya wananchi na kwa maana ya
wazazi wa watoto, uongozi wachama tawala
kwa maana ya watu hao watatu, Diwani, mbunge na rais wa serikali.Kama rais
atapata kura nyingi za kutosha na madiwani pamoja na wabunge wa chama chake
wakakosa kura katika majimbo yao ya uchaguzi , hakuna
kitakachowezekana kwa kuwa itakuwa ni sawa na ule msemowa wahenga usemao figa
moja haliinjiki chungu.
Wataalam wanatuelezea kwamba Uchumi wa Tanzania umekuwa
ukibadilika mwaka hadi mwaka. Kubadilika huku kwa uchumi kumetokana na
mabadiliko ambayo yamekuwa yakijitokeza ndani ya nchi na nchi nyingine duniani.
Tanzania sio kisiwa katika dunia hii ambacho kitapitwa na mabadiliko hayo,
hivyo nayo imeathiriwa kwa namna moja au nyingine.Tunapozungumzia uchumi tuna
maana mfumo mzima wa uzalishaji mali, matumizi (consumption) na
ugawaji/usambaji wa mazao hayo pamoja na
huduma. Uchumi unazungumzia pia kudhibiti rasilimali, kugharamia mapato na
matumizi ya jamii, biashara na viwanda. Kwa maana hiyo uchumi wa dunia umekuwa
unabadilika hasa kwa kuongezeka kwa ushindani katika masoko ya dunia pamoja na
kuongezeka kwa kasi ya maendeleo ya sayansi na teknolojia. Nchi ambazo
zitashindwa kwenda sambamba na mabadiliko hayo zina hatari ya kuathiriwa vibaya na kuzidi kuachwa nyuma kimaendeleo.
Mafanikio ya jitihada za Serikali ya Awamu ya Tatu ya CCM
katika kuzingatia mambo hayo, na kuboresha uchumi, ni dhahiri. Tumefanikiwa
kuongeza maradufu ukuaji halisi wa uchumi wetu kutoka 3.6% mwaka 1995 hadi 6.7%
mwaka 2004. Matarajio ni ukuaji wa 6.9% mwaka huu, 2005. Mfumuko wa bei
umeshuka kutoka 27.4% mwaka 1995 hadi
kufikia 4.2% mwezi Juni 2005. Akiba ya
fedha za nje leo ni kubwa kuliko wakati wowote ule katika historia yetu. Uchumi
wetu sasa umejengwa katika misingi imara, na unao uwezo wa kuhimili misukosuko
ya ndani au nje ya nchi. Mafanikio ya ukuaji wa uchumi wetu pia yameimarisha
ukusanyaji mapato. Wakati Serikali yangu inaingia madarakani, tulikuwa
tunakusanya wastani wa mapato ya kodi Sh.25 bilioni kwa mwezi. Sasa mwelekeo ni kukusanya zaidi ya Sh.150
bilioni kwa mwezi, yaani zaidi ya mara sita ikilinganishwa na 1995. Haya ni
mafanikio ya kujivunia kwa Serikali na wananchi wake, na ni sifa kwa utendaji
wenu Lakini kama si kwa usimamizi wa viongozi makini wa chama cha CCM kwa Maana ya Diwani mbunge na
Rais hayo yangekuwa na dosari na tusingefika hapo tulipo.
Ni kweli kwamba kuna nyufa ndogo za umasikini katika
jamii ya watanzania,lakini kama tutakuwa makini katika kufanya maamuzi sahihi
juu ya viongozi hao watatu, nyufa hizo zitazibika kwa kipindi kifupi kama dalili njema
zilivyojionyesha katiaka awamu ya tatu ya uongozi wa CCM. Maadam tuwe na Imani madhubuti kwa
hao waliopitishwa kugombea uogozi,, na sisi wenyewe kwa wenyewe tuaminiane. Wananchi tukiaminiana tutaleta kile kinachoitwa mtaji wa
kijamii (social capital). Kuaminiana ni mtaji kwa sababu kunawezesha watu
kushirikiana katika kutatua
matatizo mbalimbali -,ya kijamii, kiuchumi na kisiasa.
Mtaji wa kijamii ukiwa mkubwa, uwezo wa umaskini kuleta rabsha katika siasa
unapungua, au kuisha kabisa. Kadhalika, imani ya wananchi kwa viongozi au
serikali huleta kile kinachoitwa mtaji wa kisiasa (political capital). Penye
mtaji mkubwa wa kisiasa malalamiko ya wananchi yanapungua (au yanasemwa chini
chini kwa sauti ndogo) na hivyo rabsha za kisiasa zinapungua
Kwa nia njema na ufanisi katika uchaguzi wa mwaka
2005-2010 kama tusipokuwa makini kuhakikisha safu yetu ya wagombea wa CCM wote
wanapata kura na kibali cha kuwatumikia watanzania itakuwa ni sawa na lile
zoezi la wataalamu wa kilimo
wanapojitahidi kubebesha (buding) kwa baadhi ya mazao kwa kutegemea
kupata mazao bora na mengi na bora zaidi na kujikuta kile kitawi kinanyauka au
ksababisha hata lile shina mama kufa kabisa kwa ajili ya misukasuko iliyotokea
katika ubebeshaji usiozingatia utafiti na ushauri wa kutaalam Tusifanye makosa
ya namna hiyo katika kupiga kura ,kwa kuwachagua viongozi watakaokuwa kikwazo
cha maendeleo,na utekelezaji wa ilani za chama
zenye lengo la kuleta ufanisi na maendeleo kwa watanzania kwa
kuangalia mfano mmoja wa wa ilani ya uchaguzi wa mwaka 2005-2010,
“Sura ya nane kipengele cha 120 cha ilani ya CCM, kinazungumzia wanawake na kuahidi
kuwa katika kipindi cha 2005 hadi 2010,ambapo inaahidi kuzielekeza serikali
zake, kutekeleza mambo mengi ikiwa ni pamoja na kuongeza ushiriki wao katika
ngazi mbalimbali za uongozi. Chama kinakusudia kuwashirikisha wanawake
kiutendaji na katika kufanya maamuzi ili kufikia asilimia 50 ifikapo mwaka
2010, kama inavyoelekezwa na mkataba wa Umoja wa Afrika (OAU)Pia Chama kinaahidi
kuongeza nafasi za viti maalumu katika chaguzi za mitaa, vijiji , kamati za
zahanati, nkkamati za bunge na za taifa , ubunge na uwakilishi, CCM katika muda
huo, inaahidi kukamilisha majadiliano ya kuwezesha kuanzishwa benki ya
maendeleo ya wanawake. Kipengele cha 66, cha Sura ya Sita inazungumzia huduma
za jamii, na suala la elimu afya maji na maendeleo ya makazi sula la afya limezungumzia ambapo raia wengi wa nchi
hii, au wanawake wanaahidiwa kimaandishi kuwa serikali itashughulikia suala la
afya za wanawake ili kupunguza vifo vya wazazi “Kupunguza vifo vya watoto
wachanga waliozaliwa hai pamoja na wale wenye umri wa chini ya miaka mitano. Kupunguza
vifo vya wazazi kutoka 529 katika kila wazazi 100,000 na kuongeza kiwango cha
wazazi kuzalishwa na wakunga waliopata mafunzo bora …”
Ilani ya NCCR -Mageuzi
inaahidi kujenga usawa baina ya jinsia ya kiume na kike, kutokomeza maonevu ya
kihistoria na mila potofu zinazodhalilisha wanawake. Inaahidi kuwapa nafasi na
fursa maalumu, ili kuboresha athari za maonevu waliyopata katika historia.
Inazungumzia kuwawezesha kutumia vifaa vya kisasa majumbani, ili iwe rahisi kwa
jinsi zote kushiriki katika kazi za kuhudumia familia. Inatoa ahadi ya kuundwa
benki ya kuwakopesha wawekezaji wanawake itakayoendeshwa na wanawake. Kwa
upande wa siasa, itakuwa na idadi iliyo sawa ya wanaume na wanawake katika
vyombo vya uwakilishi, na kupanua mfumo wa uwakilishi wa uwiano. Kuridhia na
kutekeleza mikataba yote ya Umoja wa Mataifa, Umoja wa Afrika na Jumuiya ya
Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika kwa manufaa ya Watanzania, ili kujenga
jamii yenye kutamalaki uvunjwaji wa haki za binadamu na yenye kufurahia usawa
kati ya wanaume na wanawake na kuwaweka katika ngazi mbalimbali muhimu za
uongozi
Tukumbushane sasa kila mtu na mwenzi wake tusifanye kosa
la kumchagua Rais na tukawaacha wawezeshaji wake wakuu yaani , Wabunge na
madiwani wa CCM vinginevyo tutashindwa kuujenga ule mnara wa babeli kwa kukosa
lugha inayofanana katika kufanya maamuzi sahihi ya maendeleo ya nchi yetu na
watu wake. Au tukashindwa kupata mavuno mengi kwa kushindwa kuzingatia tafiti
na maelekezo ya wataalam.
Flora Rugambarara na Cosmas
Bahali
Nguvu ya Hoja,