WAPINZANI FUNGUENI MACHO MUONE MAENDELEO YALIYOLETWA NA CHAMA CHA MAPINDUZI

 

           

Katika kipindi hiki cha uchaguzi hasa wakati huu wa kampeni imekuwa ni jamabo la kawaida kwa kila mpinzani anayesimama jukwaani kujinadi, kuelezea mapungufu ya CCM tu bila ya kuelezea ni kitu gani atawafanyia wananchi wananchi kwa ajili ya maendeleo yao: Si vibaya sana kufanya hivyo ila tukumbuke kuwa unapoelezea mapungufu fulani uwe umetangulia kuelezea mafanikio ya taasisi husika.

 

            Hivi ni kweli kuwa CCM haijafanya lolote la maana katika kipindi chote ilichotawala kama ambavyo wanadai wapinzani? Je Tanzania tuliyonayo hii ya leo ndiyo ile ile iliyoachwa na Wakoloni? Au ndiyo ile ile ilyokuwa kabla ya kuzaliwa kwa chama cha Mapinduzi? Ni kweli kuwa  mboni za macho ya upinzani hazioni kabisa Neema ya maendeleo yaliyoletwa na chama cha mapinduzi? Tunachelea kusema kwamba wapinzani wanakope nzito zinazofunika kabisa mboni za macho yao na kuyazuia yaone mema ya chama cha Mapinduzi.  Labda tuwasaidie wapinzani kwa kuwaonesha maendeleo ya dhahiri yaliyofanywa na serikali ya awamu ya tatu ya chama cha Mapinduzi.

 

            Imekuwa kawaida kwa wapizani kuwadanganya wananchi kwamba Serikali ya CCM imeshindwa kuwapatia watoto wao elimu. Lakini takwimu inaonyesha kwamba idadi ya wanafunzi wa shule za msingi imeongezeka kutoka milioni tatu na nusu mwaka 1995 na kufikia zaidi ya milioni saba na nusu kwaka 2005. Wakati huo huo wanafunzi wa shule za secondary wameongezeka zaidi ya maradufu kutoka wanafunzi 190,000 mwaka 1995 hadi wanafunzi 520,000 mwaka 2005.

 

            Serikali ya chama cha Mapinduzi haikuishia kwenye elimu za msingi na sekondari tu, bali hata elimu ya juu iliangalia kwa umakini .  Serikali ya CCM imeongeza idadi ya wanafunzi wa vyuo vikuu kutoka wanafunzi 7785 mwaka 1995 hadi kufikia wanafunzi 32,181 mwaka 2005. Ili kuhakikisha kuwa kila mtoto anapata elimu, Serikali ya Chama cha Mapinduzi imefuta ada kwa shule za msingi na kupunguza kwa kiasi kikubwa ada ya shule za sekondari. Je wapinzani hawajayaona haya maendeleo katika sekta ya elimu? Na kama wanayaona mbona hawayazungumzii hata kidogo? Au maendeleo wanayotaka wao ni ya aina gani?. Kama kweli wanawatakia mema wananchi, ni vyema wapinzani wanyanyue ndimi  ndimi za vinywa vyao kuelezea maendeleo haya.

 

            Wapinzani wanadai serikali ya CCM haikufanya lolote katika sekta ya afya: Hivi ni kweli hawana macho ya kuona wala masikio ya kusikia mambo yanayofanywa na Serikali ya CCM katika kuendeleza sekta ya afya? Tunashawishika kusema kwamba Wapinzani wameweka pamba masikioni mwao. Na hizo pamba si za kawaida kwani zinachuja mambo kadhaa na kuruhusu yale wanayopenda kuasikia na kuyanena wao.

 

            Hata hivyo hatuchoki na hatutachoka kuwakumbusha na kuwaeleza wapinzani maendeleo yaliyofanywa na serikali ya CCM katika Serikali mbalimbali. Wapinzani tuambieni ya kwamba kipindi cha Serikali ya awali ya Tatu kimetoa mfano mzuri ya mafanikio katika sekta ya Afya. Kwa mfano upatikanaji wa dawa katika hospitali, vituo vya afya na Zahanati za Serikali umeongezeka sana kwa vile kiasi cha fedha kwa ajili ya ununuzi wa dawa na vifaa kimeongezeka kutoka shilingi bilioni kumi mwaka 2000 hadi shilingi bilioni 30 mwaka 2004/05. Aidha huduma za chanjo kwa watoto umeinarika na kuongezeka kutoka asilimia 30 mwaka 1995 hadi asilimia 90 mwaka 2004. Pia wilaya zote miepatiwa x-ray, ultra sound machine na majokofu mapya. Mbona wapinzani hamtaki hata kidogo  kuyatupia macho haya? Au mlizaliwa kwa ajili ya kukosoa tu?

 

            Tunatambua ya kwamba suala la upatikanaji wa maji ni tatizo sugu katika sehemu kubwa ya bara la Afrika na duniani kwa ujumla. Hata hivyo serikali ya CCM imefanya kazi nzuri katika sekta ya maji kwa kupanua na kuongeza upatikanaji wa maji nchini  na pia kwa kuanzisha miradi mikubwa ya maji kama ule wa kutoa maji ya ziwa Victoria na kuyapeleka katika mkoa wa Shinyanga, mradi wa maji wa Chalinze katika Mkoa wa Pwani na mradi wa maji wa Dodoma mjini. Serikali ya awamu ya tatu ya CCM imewezesha visima vingi vya maji kuchimbwa na visima hivi vinatumiwa hata na Wapinzani wenyewe:  Lakini bado wapinzani wamekuwa wakiwaeleza wananchi kwamba CCM haijafanya juhudi zozote katika kuwapatia huduma ya maji.

 

            Hivi huku kama sio kukosa shukurani ni nini? Wapinzani wanaoga, wanafua na wanakunywa maji hivi hawajiulizi  yametokea wapi? Au wanayafuata wenyewe kwenye vyanzo vyake? Ni dhahilri kuwa Wapinzani hawana tofauti na mtoto anayemfinya mama yake mashavu hali ya  kuwa amebebwa mgongoni kwa mama huyo.

 

            Tunawashangaa sana wapinzani wanapoona tu sehemu za barabara na madaraja zenye kasoro na kutoona kabisa barabara nzuri na madaraja ya kuvutia yaliyotengenezwa na serikali ya CCM.

 

            Huko nyuma tulizoea Wapinzani wakiongelea kero ya usafiri katika kivuka cha mto Rufuji. Cha ajabu ni kwamba baada ya serikali ya CCM kutengeneza daraja imara lililoondoa kabisa kero ya usafiri mto Rufiji hakuna hata upinzani mmoja aliyeruhusu kinywa chake kupongeza jambo hilo. Au hilo daraja limeshishwa kutoka Mbinguni? Tuseme wapinzani hawajawahi hata siku moja kusafiri kupitia Rufiji tangu daraja hilo kujengwa? Na kama ni hivyo basi tuanachukua nafasi hii kuwafahamisha wapinzani kuwa sa Rufiji kuna daraja daraja zuri sana lililojengwa kwa juhudi za serikali ya CCM waende wakalione. Pia kuna madaraja mengi tu makubwa na madogo madogo yaliyojengwa chini ya serikali safi ya CCM na wapinzani wanayafahamu.

 

            Tunaomba wapinzani waache unafiki na kuwa eleza wananchi kinagaubaga jinsi serikali ya CCM ilivyoziwezesha sekta binafsi kuchangia kuleta maendeleo ya nchi yetu: seckta binafsi imenezeshwa kupunguza kero mabalimbali kama vile kero ya usafiri, elimu na afya: sasa hivi tunashuhudia jinsi miji mbalimbali ya nchi ilivyopambwa a daladala nyingi zinazotoa huduma ya usafiri kutoka eneo moja hadi lingine. Boti ziendazo kwa kasi zinatoka huduma nzuri na za haraka katika miji ya Da-es-salaam, Unguja na na hivi karibuni mikoa ya Mwanza na Bukoba: Shule za watu binafsi na vyuo vya elimu ya juu vimeongeza idadi ya Watanzania wanaopata Elimu. Zahanati vituo vya afya na hata hospitali za watu binafsi nazo zimesaidia kuboresha huduma ya afya  kwa watanzania.  Huduma hizi tunauhakika hata wapinzani wanazipata ila tunashangazwa na tabia yao ya kudharau na kubeza maendeleo yaliyofanyika chini ya serikali ya  CCM. Tunashangaa sana tunaposikia  wapinzani wakibeza maendeleo yaliyofanywa na CCM katika kuimarisha sekta ya mawasiliano.

 

Ni dhahiri kwamba chini ya utawala bora wa serikali ya CCM mawasiliano ya aina zote yameismarishwa kwa kiasi kikubwa.  Sasa hivi idadi kubwa ya watanzania wanamudu kuwasiliana na ndugu na jamaa zao, katika mikoa tofauti na hata nje ya nchi kwa urahisi mno.   Chini ya utawala wa CCM makampuni mbalimbali ya simu na mawasiliano mengine yameweza kueneza huduma hii muhimu mpaka katika baadhi ya vijiji.  Wapinzani wenyewe wanawasiliana sana tu kwa kutumia simu za viganjani.  Na cha ajabu ni pale wanapotumia mawasiliano hayo hayo kubeza maendeleo yaliyoletwa kutokana na kuimarishwa kwa huduma za mawasiliano.  Hapa tatutokosea tukiwalinganisha wapinzani na mtu anaekata tawi la mti alilolikalia. 

 

Wapinzani wanatumia utitiri wa vyombo vya habari kueneza propaganda zao, lakini wanasahau kuwa wingi huu wa vyombo vya habari umetokana na utawala makini wa CCM.  Chini ya utawala wa CCM vyombo vya habari vimeongezeka kwa kiasi kikubwa mno, idadi ya magazeti, redio, na hata vituo vya television vya watu binafsi vimeongezeka kwa kiasi kikubwa mno.  Ongezeko hili la vyombo vya habari, linakwenda sambamba na uhuru wa vyombo vya habari unaochochewa na demokrasia imara iliyojengwa chini ya utawala imara wa Chama cha Mapinduzi.  Chaajabu ni pale wapinzani wanapodhubutu kuudanganya umma wa watanzania, kuwa CCM haikufanya lolote katika kuimarisha huduma hii itolewayo na vyombo vya habari.  Au wapinzani walitarajia kuwaona na kuwasikia viongozi wa CCM wakitangaza vipindi mbalimbali kwenye Television na radioni ndipo waamini kwamba CCM inajali vyombo vya habari?

 

Maendeleo na ustawi wa jamii yoyote hutegemea kwa kiasi kikubwa amani na utulivu katika jamii husika. Serikali za awamu zote za CCM. Zilijitahidi na zilifanikiwa kuhakikisha kuwa jamii ya watanzania wote bila kujali itikadi zao, rangi na imani zao inaishi katika mazingira mazuri ya amani na utulivu.   Wapinzani kwa nyakati tofauti wamekuwa wakibeza sera ya CCM ya kuwahakikishia wananchi wa Tanzania amani ya kudumu na utulivu wa uhakika;   Wapinzani wakumbuke ya kwamba ni amani iliyojengewa mazingire mazuri na CCM inayowawezesha hata wao kusimama majukwani na kunadi sera za vyama vyao.  Serikali ya chama cha mapinduzi imedumisha amani na utulivu ndani na nje ya mipaka yetu.   Tukiwasikia wapinzani wanasema amani iliyolindwa na CCM wakati inawanufaisha hata wao, tunakumbuka usemi wa wahenda usemao “baniani mbaya kiatu chake dawa”.  

 

Tukiwasikiliza wapinzani wanapokuwa majukwaani tunashawishika kujiuliza je wapinzani ni malaika ambao daima huwa sahihi kwa asilimia mia moja?  Je wapinzani huwa hawakosei hata sikumoja?   Hatutaki kuwakumbusha wananchi watanzania juu ya wale wabunge wawili kwa tiketi ya chama kimoja cha upinzani waliotumia madaraka yao kwenda  kinyume na maadili ya bunge na hatimaye kulidhalilisha bunge letu na nchi yetu mbele ya uso wa kimataifa.  Je hii ndiyo staili wanayoitaka wapinzani?  Kama wao kweli huona mapungufu tu mbona hili hawalisemi? Au wamesahau?;  wengine kwa kukosa hoja  wanadai eti viongozi wengi wa CCM in wazee, hivyo hawafai, wakumbuke kuwa  umri na rangi ya paka si hoja mradi anakamata panya.

 

Nguvu ya Hoja,

Abiyani Chuo Kikuu.