RAIS MKAPA AMTEUA NDUGU CHARLES MAKONGORO NYERERE (CCM) KUWA MBUNGE

 

Rais Benjamin Mkapa, amemteua Ndugu Charles Makongoro Nyerere kuwa Mbunge.

 

Taarifa ya Ikulu ilisema uteuzi huo unaanza rasmi Jumatatu ijayo.  Rais Mkapa amefanya uteuzi huo kulingana na kifungu cha 66(1)(e) kinachompa madaraka ya kuwateua Wabunge wasiozidi kumi kulingana na sifa zilizoainishwa katika Katiba.

 

Ndugu Makongoro anakuwa Mbunge wa kumi wa kuteuliwa na kwa hiyo anatimiza idadi ya Wabunge ambao Rais anapaswa kuwateua kwa mujibu wa Katiba.

 

Wengine ni Ndugu Kingunge Ngombale-Mwiru (CC), Ndugu Omar Ramadhan Mapuri (CCM), Brigedia Jenerali (mstaafu) Hassan Ngwilizi (CCM) na Ndugu Hamad Rashid Mohamed (CUF).

 

Taarifa iliwataja wengine kuwa ni Dkt. Abdulkader Shareef (CCM), Chifu Abdallah Fundikira (CCM), Bi Anne Kione Malecela (CCM), Dkt. Masumbuko Lamwai (CCM) na Bi Mwaidi Hassan Makame (CCM).