BAADHI YA MAMBO YA MSINGI YALIYOMO KATIKA
ILANI YA UCHAGUZI YA CCM YA MWAKA 2005
1.
Kikao
cha Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM cha tarehe 15 Agosti, 2005 kilichofanyika
2.
Siasa
ya Chama Cha Mapinduzi ni ya ujamaa na kujitegemea inayozingatia
mazingira ya wakati. Mwelekeo wa sera za
msingi za CCM za kujenga ujamaa kwa kipindi fulani huzingatia ukweli na hali
halisi ya wakati huo. Ndiyo maana katika
Mwelekeo wa Sera za CCM Katika Miaka ya Tisini ulioandaliwa katika
mazingira ya mageuzi makubwa ya kiuchumi, kisiasa na kijamii yaliyoikumba dunia
nzima mwishoni mwa miaka ya themanini na mwanzoni mwa tisini, CCM ilibainisha
ifuatavyo katika ibara za 5 na 6 za Mwelekeo huo:-
5. Siasa ya msingi ya
Chama Cha Mapinduzi itaendelea kuwa UJAMAA NA KUJITEGEMEA kwa kuzingatia kwamba
ndiyo iliyotuundia mazingira ya amani, utulivu na umoja wa Taifa letu, na ndiyo
siasa inayolingana na matarajio ya wananchi walio wengi.
6. Lengo la Ujamaa
na Kujitegemea katika miaka ya tisini litakuwa kuhakikisha kwamba wananchi
wenyewe wanamiliki na kuendesha uchumi wa nchi yetu, mmoja mmoja, kwa kupitia
vyama vyao huru vya ushirika wa aina mbalimbali, kwa kupitia makampuni ya
wananchi na ya ubia ambamo maelfu ya wananchi watanunua hisa
Kwa mtazamo huu wa CCM, sehemu kubwa ya
uchumi wa nchi inakusudiwa umilikiwe na wananchi wenyewe ili kuinua hali ya
maisha yao na kutosheleza mahitaji yao ya msingi. Dola
itaendelea kushika nafasi ya muhimili
wa uchumi wa Taifa.
3.
Ikumbukwe
kwamba kabla ya hapo, ujenzi wa ujamaa ulisimama juu ya msingi wa wananchi
kumiliki uchumi wa Taifa kupitia dola, na siyo moja kwa moja.
4.
Mwelekeo
wa Sera za CCM Katika Miaka ya 2000 Hadi 2010 ambao ndio sera ya msingi ya CCM ya wakati huu, ni
mwendelezo wa malengo makuu ya Mwelekeo wa Sera za CCM Katika Miaka ya
Tisini. Katika ibara zake za 11, 12
na 13, Mwelekeo huo (wa 2000-2010) unabainisha ifuatavyo:-
11. Malengo makuu ya Mwelekeo wa sera za
CCM Katika Miaka ya Tisini yalikuwa mawili.
12. Pili, Mwelekeo wa Miaka ya Tisini
ulisisitiza kwamba lazima nguvu na uwezo wetu uelekezwe kwenye kuinua
kiwango cha nguvu za uzalishaji
13. Malengo haya makuu ya Mwelekeo wa Sera
za CCM za Miaka ya Tisini yanatuunganisha na majukumu ya Mwelekeo wa Sera za
CCM za Miaka ya 2000 hadi 2010. Kwa
kuendeleza malengo hayo mawili kazi iliyo mbele yetu ni kujenga msingi wa
kisasa wa Taifa linalojitegemea na uwezeshaji wa kiuchumi wa wananchi.
5. Hii ndiyo inatupeleka kwenye chimbuko la
Ilani ya sasa.
6. Chimbuko la Ilani ya Uchaguzi ya CCM kwa Ajili ya Uhaguzi
Mkuu wa Mwaka 2005 ni Mwelekeo wa Sera za CCM Katika Miaka ya 2000 Hadi 2010. Ilani hii itakuwa ni kipindi cha pili na cha
mwisho cha utekelezaji wa Mwelekeo huo.
Kwa hivyo, imeandaliwa kwa kuzingatia majukumu makuu mawili yafuatayo ya
Mwelekeo huo:-
(a)
Kujenga
msingi wa uchumi wa kisasa wa taifa linalojitegemea; yaani modenaizesheni
ya uchumi.
(b)
Kutekeleza
Sera ya Kuwawezesha Wananchi Kiuchumi.
MAFANIKIO YA SERIKALI YA AWAMU YA TATU NA AZMA YA KUYAENDELEZA
7. Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa
Ari mpya, Nguvu mpya na Kasi mpya.
KUJENGA MSINGI WA UCHUMI WA KISASA WA TAIFA LINALOJITEGEMEA
8. Mafanikio ya Serikali ya Awamu ya Tatu katika utekelezaji wa
jukumu la kujenga msingi wa uchumi wa kisasa wa taifa linalojitegemea
yanajidhihirisha kwa ujumla katika kuongezeka kwa kasi ya ukuaji wa uchumi
kutoka asilimia 3.6 mwaka 1995 hadi asilimia 6.7 mwaka 2005. Lengo la Ilani hii katika kuyaendeleza
mafanikio hayo ni kasi ya ukuaji wa uchumi kufikia asilimia 10 ifikapo mwaka
2010 kwa kutumia mikakati iliyomo katika Mkakati wa Kukuza Uchumi na Kupunguza
Umaskini
9. Lengo la kukuza uchumi wa nchi ni kwamba hatimaye manufaa ya
kukua huko kwa uchumi yawafikie wananchi.
Kuna aina mbili za manufaa wanayotarajia kuyafaidi wananchi. Aina ya kwanza ni ile ya wananchi
kufaidika kwa pamoja kwa njia ya huduma zilizoimarishwa za kijamii na
miundombinu kama vile elimu, afya, maji, barabara, umeme, mawasiliano n.k. Aina ya pili ya manufaa ya kukua kwa uchumi
yanayotarajiwa na wananchi ni ile ambapo mwananchi mmoja mmoja anafaidika kwa
njia ya kuongezeka kwa kipato chake na cha familia yake.
10. Katika lugha ya wanaharakati wa mapambano dhidi ya umaskini,
aina ya kwanza ya manufaa huhusishwa na kupunguza kile kinachoitwa umasikini
usiokuwa wa kipato na ile aina ya pili huhusishwa na kile kinachoitwa umasikini
wa kipato.
11. Kwa kutumia ukuaji wa uchumi wa taifa uliopatikana katika
kipindi cha miaka 10 iliyopita, Serikali ya Awamu ya Tatu imefanikiwa
12. Jitihada pia zimefanyika na zinaendelea kufanyika za kukabiliana
na umasikini wa kipato, yaani kuwafikishia wananchi manufaa ya kukua kwa uchumi
kwa wao kufaidika mmoja mmoja. Hili
ndilo hasa eneo ambalo Sera ya Uwezeshaji wa Wananchi kiuchumi inahusika nalo. Agenda kuu katika eneo hili ni:-
(a)
Uwezeshaji
(b)
Kupambana
na umasikini
(c)
Kushiriki
katika uchumi wa nchi, na
(d)
Ajira.
13. Eneo hili la kuyafikisha kwa wananchi manufaa ya kukua kwa
uchumi wa nchi ndilo agenda kuu na changamoto ya msingi ya Ilani ya Uchaguzi ya
CCM ya Mwaka 2005. Na mbinu kuu za
kuikabili changamoto hii ni pamoja na zifuatazo ambazo zote ni sehemu ya MKUKUTA:-
(a)
Kuendelea
kukua kwa uchumi wa nchi kwa kasi kubwa zaidi (kufikia asilimia 10 ifikapo
mwaka 2010).
(b)
Kuongezeka
kunakoendelea, kwa wingi na ubora wa huduma za jamii hasa elimu, afya, maji
n.k. na miundombinu hasa barabara, madaraja, mawasiliano, umeme n.k.
(c)
Modenaizesheni
ya harakati mbalimbali
za kiuchumi zinazowapatia ajira za kujiajiri na kipato wananchi, hasa kilimo,
ufugaji, viwanda vidogo, uvuvi, uchimbaji madini, n.k.
(d)
Kuzipa
uhai rasilimali mfu za wananchi ili ziweze kutumika
(e)
Kuwawezesha
wananchi kutumia fursa mbalimbali za maendeleo zilizopo kujiongezea kipato na
kushiriki katika uchumi wa nchi, ikiwa ni pamoja na kuwawezesha kumiliki hisa
katika makampuni mbalimbali,
(f)
Mkakati
wa Uanzishaji wa Maeneo Maalumu ya Uchumi (Special Economic Zones
Strategy)
(g)
Kuimarisha
taasisi zinazotoa mikopo kwa wananchi.
14. Kwa vile lengo la juhudi zote hizi zinazobainishwa na Ilani ni
kuyafanya maisha ya Watanzania yawe bora zaidi, CCM imebuni kaulimbiu mbili
zifuatazo:-
(a)
Maisha
bora kwa kila Mtanzania,
(b)
Kwa
ari mpya, nguvu mpya na kasi mpya,
KUZINGATIA DIRA ZA 2025 NA 2020 NA MALENGO YA MAENDELEO YA MILENIA
15. Ilani hii ya mwaka 2005 imezingatia pia malengo ya Dira ya
Taifa ya 2025 na Dira ya Maendeleo ya
DONDOO
ZA YALIYOMO KATIKA ILANI
16.
Dondoo za mambo yaliyomo katika Ilani hii ya uchaguzi
zinatolewa hapa sura kwa sura.
(a) Sura ya Utangulizi
Sura hii
imechambua hali ilivyo duniani wakati huu na kuiweka
(b) Sura
ya Kwanza
Sura hii
inabainisha kwa muhutasari mafanikio ya kiuchumi na kijamii ya miaka 10 ya
Serikali ya Awamu ya Tatu. Mafanikio
hayo yameelezewa kwa uchambuzi zaidi katika kitabu cha Mafanikio ya Serikali
ya Awamu ya Tatu na Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya Mwaka 2000.
(c) Sura ya Pili
Sura hii
imeweka mkakati wa kuendeleza utekelezaji wa jukumu kuu la kwanza la Mwelekeo
wa Sera za CCM Katika Miaka ya 2000 hadi 2010, yaani jukumu la kujenga msingi wa uchumi wa kisasa wa taifa
linalojitegemea. Inasisitiza umuhimu wa mapinduzi ya kilimo (pamoja na ufugaji na uvuvi) ambacho ndicho sekta msingi wa uchumi wetu, na pia
mapinduzi ya viwanda ambavyo
vinatambuliwa na Ilani hii kama sekta
kiongozi wa uchumi wa kisasa. Sura
hii hatimae inaweka malengo makuu ya jumla ya Ilani kuwa ni haya yafuatayo:-
(i)
Kukuza uchumi kwa kiwango cha zaidi ya asilimia kumi (10%)
kwa mwaka ifikapo mwaka 2010 kutoka ukuaji wa sasa wa asilimia sita nukta saba
(6.7%).
(ii)
Kuanza kupunguza umasikini wa kipato wa watu wetu kwa namna
iliyo dhahiri.
(iii)
Kuendeleza safari ndefu ya kujitegemea kwa kuwa na uwezo wa
kulipia gharama za bidhaa tunazoziagiza toka nje zinazohitajika kusukuma
maendeleo yetu, kwa kutumia mapato ya ziada yatakayotokana na ongezeko kubwa la
thamani ya mazao na bidhaa tutakazouza nje ya nchi.
(d) Sura ya Tatu
Sura hii
inaweka malengo na mbinu za utekelezaji kwa sekta za uzalishaji
(e) Sura ya Nne
Sura hii
inabainisha malengo ya Ilani katika sekta za miundombinu na huduma za
kiuchumi. Sekta hizo ni ardhi, nishati,
barabara, usafiri, uchukuzi, mawasiliano na fedha. Miongoni mwa malengo makuu ni kurasimisha
umilikaji wa ardhi na nyumba kwa Watanzania wanyonge wenye rasilimali hizo bila
ya kuzisajili. Zoezi
(e) Sura ya Tano
Sura hii ya
Ilani inajikita katika utekelezaji wa sera ya uwezaji wa wananchi
kiuchumi. Sehemu ya utekelezaji wa sera
hii inayomlenga mwananchi moja kwa moja,
ni kuwaanda wananchi na kuwatengenezea
mazingira mazuri ili waweze kuzitumia ipasavyo fursa zilizopo na
zitakazoanzishwa na uwezeshaji kiuchumi.
Maandalizi hayo ni pamoja na elimu
na mafunzo, ujasiriamali, urasilimishaji wa rasilimali (MKURABITA) na kujiunga
katika ushirika, hususani wa kuweka na kukopa (SACCOS).
Maeneo matatu
mahususi ya uwezeshaji wa wananchi yamepewa uzito wa aina yake. Maeneo hayo ni Ajira, Mifuko ya Hifadhi ya
Jamii na Harambee za Kuwezeshana Kupambana na Umaskini.
(i) Ajira
Ajira ziko za
aina mbili zifuatazo:-
·
Aina ya kwanza ni ajira
katika maana ya kazi ya kulipwa mshahara katika sekta ya umma (Serikalini na
vyombo vyake) na katika sekta binafsi (iliyo rasmi na isiyo rasmi). Katika aina hii ya ajira, baada ya utafiti wa
kina, inaweza kusemwa kwa uhakika kwamba zitaweza kupatikana nafasi mpya zaidi
ya milioni moja katika kipindi cha Ilani.
Tulifanya utafiti huo ili kujiepusha na kutoa ahadi ya njozi
isiyotekelezeka
Nafasi hizo
mpya kwa upande wetu zitapatikana kutokana na kukua kwa uchumi ambako
kutawezesha kuongezeka kwa harakati za kiuchumi na kupanuka kwa hduuma mbali
mbali za kijamii, ulinzi, miundombinu n.k.
Katika sekta ya umma, pamoja na nafasi za ajira zitakazotokana na watu
kustaafu na kufariki, kutakuwa na ajira mpya nyingi kwenye sekta ya ualimu
kutokana na upanuzi unaoendelea wa shule za msingi, sekondari na vyuo
vikuu. Sekta ya afya pia itatoa ajira
nyingi kwa upande wa waganga na wauguzi
kwa vile sekta hii lazima ipanuke
kukidhi mahitaji ya wananchi. Sekta ya ujenzi vile vile ina nafasi ya kutoa ajira
nyingi mpya. Kwa upande mwingine katika
sekta ya binafsi, Serikali za CCM zitaendelea kuvutia wawekezaji katika
viwanda, migodi, kilimo cha biashara (mashamba makubwa) n.k. ili nafasi za
ajira ziendelee kuongezeka. Mkakati mpya
wa Serikali wa kuanzisha maeneo maalum ya uchumi (Special Economic Zones)
umekusudiwa kuibua nafasi nyingi mpya za ajira.
·
Aina ya pili ya ajira
katika maana ya kujiajiri binafsi katika kilimo, ufugaji, uvuvi, viwanda,
biashara, kuchimba madini, udereva, ufundi, ualimu, uhasibu, kuendesha mgahawa,
ushonaji, uandishi, uanasheria, uhandisi, ukandarasi n.k. Eneo hili ndilo lenye nafasi tele za ajira
katika nchi yetu. Katika kipindi cha
Ilani hii, CCM itaweka mkazo kwenye kuwawezesha wananchi, hasa vijana na wanawake kwenye shughuli za kujiajiri vijijini na mijini. CCM
inatoa wito kwa wananchi wajitokeze kuitikia wito wa kujiajiri na pia wakubali
kutobagua kazi maana wahenga wanasema mchagua jembe si mkulima. Kwa njia hiyo ya Serikali kuwawezesha
wananchi walio tayari, nafasi mpya za ajira zitapatikana kwa mamilioni zaidi ya
zile milioni moja za kuajiriwa, na kiwango cha ukosefu wa ajira (unemployment)
kitapungua
(ii) Eneo la Pili la Uwezeshaji litakaloibuliwa
ni Mifuko ya Hifadhi ya Jamii
Pamoja na suala
la kukaribisha wawekezaji nchini, kuna umuhimu wa kufikiria uwezekano wa
kuutumia uwezo mkubwa wa fedha uliopo katika mashirika ya hifadhi za jamii
(pensheni) yaani NSSF, PPF, LAPF na Mfuko wa Pensheni wa Serikali. CCM itaelekeza Serikali kufanya mashauriano
ya msingi na uongozi wa mifuko hii ili kupata njia muafaka za kuifanya mifuko
hii ishiriki katika uwekezaji na hivyo kuliongeza nguvu taifa, ya kukuza uchumi
wake kwa kasi zaidi na kuwawezesha wananchi wake kiuchumi kwa kuwaongezea
nafasi za ajira.
(iii) Eneo la tatu la uwezeshaji litakalopewa
mwelekeo mpya ni Harambee za Kuwezeshana
katika Kupambana na Umaskini
Watanzania wa
asili mbali mbali wana jadi ya kuungana mkono kwa hali na
CCM itawahimiza
wananchi kwenye michango (harambee) ya kuwezeshana katika fani za elimu, afya
na uchumi (mitaji) kwani hizi ni nyenzo za msingi katika kupambana na umaskini.
(g) Sura ya Sita
Sura hii
inahusu malengo ya Ilani katika sekta ya huduma za jamii. Sekta zinazohusika ni elimu, afya, maji na
maendeleo ya makaazi. Upanuzi mkubwa
(i) Kuongeza idadi ya wanafunzi wa msingi
watakaoendelea na elimu ya sekondari kufikia asilimia 50 ya watahiniwa wa
Darasa la
(ii) Kupunguza vifo vya watoto wachanga
kutoka 95 kwa watoto 100 wanaozaliwa
hadi watoto 50.
(iii) Kuwafikishia huduma ya maji
(h) Sura ya Saba
Sura hii ni ya
mazingitio maalum ya Ilani kuhusu
(i) Kuendelea kuyatambua na kuyaenzi
Mapinduzi ya
(ii) Kuendelea kutambua kwamba Mapinduzi
hayo sio tu ni ngao ya uhuru wa wananchi wa
(iii) Kuendelea kuyalinda na kuyaendeleza
kwa nguvu zote mafanikio yaliyoletwa na Mapinduzi hayo, hususan katika sekta za
ardhi, ustawi wa jamii, huduma za jamii kama vile elimu na afya, na kukuza
uchumi na matumizi endelevu ya rasilimali pamoja na kuwajengea wananchi uwezo
wa kutumia fursa zilizopo ili kupambana na umaskini.
(iv) Kuendelea kuheshimu haki za binadamu,
demokrasia na utawala bora.
Malengo
mahususi ya kisekta yamezingatia misingi hiyo na yamewekwa kwa mtindo ule ule
(i) Sura ya Nane
Sura hii inahusu
maeneo mengine muhimu, hususan demokrasia, utawala bora, madaraka ya umma,
mapambano dhidi ya rushwa, ulinzi na usalama, hifadhi ya mazingira, kukabili
majanga, utafiti na maendeleo, vyombo vya habari, mambo ya nje, utamaduni,
michezo, kuyaendeleza makundi mbalimbali na kuhamia Makao Makuu Dodoma.
Katika eneo la
utafiti na maendeleo (R&D), CCM inalenga katika Serikali kutenga asilimia
1.0 ya bajeti ya kila mwaka kwa ajili ya utafiti. Msukumo maalum utatolewa katika kulinda
hakimiliki za matokeo ya utafiti na kuyafikisha matokeo ya utafiti kwa wananchi
ili wayatumie kujiongezea tija.
Inatarajiwa pia
Katika eneo la
mambo ya nje, mkazo utaelekezwa katika utekelezaji wa Sera ya Diplomasia ya Uchumi.
Katika eneo la
kuyaendeleza makundi mbalimbali, yamelengwa makundi ya watoto, wanawake,
vijana, wazee, walemavu, wafanyakazi n.k.
Kwa makusudi kabisa ya kutoa msukumo kwa makundi
(j) Sura ya Tisa
Sura hii
inahusu Chama chenyewe, hasa viongozi. Viongozi wa CCM wanahimizwa kuongoza kwa
kuonyesha njia katika utekelezaji wa yote yaliyomo katika Ilani, hususan yale
yanayohitaji kufanya kazi kwa bidii na maarifa.
Kuhusu Muungano wa
HITIMISHO
Ilani ya Uchaguzi ya CCM
Kwa Ajili ya Uchaguzi Mkuu wa 2005 imesheheni mambo yenye kuleta matumaini kwa
wananchi. Imeandaliwa juu ya msingi wa nguvu ya hoja na si hoja ya nguvu. Inaahidi mambo iliyoridhika kuwa
yatawezekana, kufuatia utafiti wa kina ilioufanya kabla. Kwa hivyo, wagombea wa
CCM wa ngazi zote
Kwa Ilani hii ya Uchaguzi,
CCM inaahidi mambo makubwa matatu ya jumla yafuatayo:-
Maisha Bora kwa Kila Mtanzania
Ari Mpya, Nguvu Mpya na Kasi Mpya katika
kukuza uchumi wa nchi na kupambana na umaskini.
Idara ya Itikadi na Uenezi
CCM MAKAO MAKUU.