RATIBA YA UTEUZI WA WAGOMBEA NAFASI YA SPIKA WA BUNGE LA JAMHURI YA MUUNGANO NA SPIKA WA BARAZA LA WAWAKILISHI ZANZIBAR KUPITIA CCM MWAKA 2005

 

1.0            UTANGULIZI

 

1.1             Uchaguzi wa Maspika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Baraza la Wawakilishi Zanzibar utafanyika mwezi Novemba 2005 baada ya Wabunge/Wawakilishi wapya kupatikana.

 

1.2             Zoezi la kumpata Spika kwa mujibu wa Sheria na Kanuni za Uchaguzi linahusisha vyama vyote vya siasa nchini.

 

1.3             Chama Cha Mapinduzi kwa upande wake, kina utaratibu wa kupendekeza wanachama wake watakaokwenda kugombea nafasi hizo.

 

 

2.0            UTARATIBU WA UTEUZI NDANI YA CHAMA

 

2.1             Waombaji wa nafasi ya Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar.

 

A:      KUCHUKUA NA KURUDISHA FOMU

 

(a)              Nafasi ya Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

 

(i)                Kuchukua fomu tarehe 1/11/2005

 

(ii)              Tarehe ya mwisho ya kurudisha 3/11/2005 kabla ya saa 10 jioni.

 

(iii)            Fomu zitachukuliwa na kurejeshwa kwa Katibu Mkuu wa CCM.

 

(b)              Nafasi ya Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar

 

(i)                Fomu zitachukuliwa tarehe 1/11/2005

 

(ii)              Tarehe ya mwisho wa kurudisha fomu ni 3/11/2005 kabla ya saa 10 jioni.

1

 

(iii)            Fomu zitachukuliwa na kurejeshwa kwa Naibu Katibu Mkuu Zanzibar.

 

(c)               Gharama ya kuchukua fomu kwa nafasi zote mbili za Uspika ni Tsh. 500,000/=.

 

B:       VIKAO VYA UCHUJAJI NA UTEUZI

 

(i)                Tarehe 5/11/2005 Kamati Maalum kuwachuja Waombaji wa Nafasi ya Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar.

 

(ii)              Tarehe 8/11/2005 Kamati ya Wawakilishi wote wa CCM kufanya uteuzi wa mwisho wa wagombea wa CCM.

 

(iii)            Tarehe 12/11/2005 Sekretarieti ya Halmashauri Kuu ya Taifa kutoa mapendekezo kuhusu uteuzi wa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

 

(iv)            Tarehe 13/11/2005 Kamati Kuu kuwachuja Wagombea wa nafasi ya Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

 

(v)              Tarehe 14/11/2005 Kamati ya Wabunge wote wa CCM kufanya Uteuzi wa Mwisho wa wagombea wa CCM.

 

3.0             Utaratibu wa kugombea, kuchuja na Uteuzi wa Manaibu wa Spika utafanywa na Vikao vya Kamati za Wabunge/Wawakilishi wote wa CCM.

 

 

 

 

 

 

2