MGOMBEA URAIS WA CCM KWENDA KUCHUKUA FOMU TUME

 

Siku ya Jumatatu tarehe 1/08/2005, Mgombea Urais wa CCM wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Ndugu Jakaya Mrisho Kikwete atakwenda kuchukua Fomu ya Uteuzi wa Kugombea Urais katika Ofisi za Makao Makuu ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi zilizopo Posta House, Dar es Salaam.

 

Maandalizi yote ya zoezi hilo la uchukuaji Fomu yamekamilika na Ofisi ya CCM ya Mkoa wa Dar es Salaam imeandaa Ratiba ya kumsindikiza Ndugu Kikwete kwenda kuchukua Fomu ambayo itawashirikisha wanachama wa CCM wa Wilaya zote za Mkoa wa Dar es Salaam pamoja na Jumuiya za CCM za Wanawake (UWT), Wazazi na Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM).

 

Ratiba kamili ya Tukio hilo muhimu la Jumatatu mtakabidhiwa baadaye na Katibu wa CCM wa Mkoa wa Dar es Salaam, Ndugu Mattson Chizi ambaye pia ni Mkuu wa Kitengo cha Uchaguzi cha Chama Cha Mapinduzi.

 

Ratiba hiyo inaonyesha kwamba msafara huo wa kumsindikiza Mgombea Urais wa CCM wa Muungano utaanzia Olfisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Mtaa wa Lumumba na kupitia katika barabara za Mkunguni; Bibi Titi Mohamed, Ohio hadi Makao Makuu ya Tume. 

 

Baada ya kukabidhiwa Fomu za Uteuzi wa Kugombea Urais na Mkurugenzio wa Uchaguzi, Ndugu R.R. Kiravu, Ndugu Kikwete na msafara wake watarejea Ofisi Ndogo za Makao Makuu ya CCM ambapo atawasalimu wanachama wa CCM