Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete

Alizaliwa Oktoba 7, mwaka 1950 katika kijiji cha Msoga Wilaya ya Bagamoyo mkoani Pwani.

Elimu.

1958-1961 - Shule ya Msingi Msoga
1962-1965 - Shule ya Msingi ya Kati ya Lugoba
1966-1969 - Shule Sekondari Kibaha
1970-1971 - Shule ya Sekondari Tanga
1972-1975 - Chuo Kiku cha Dar es Salaam, Shahada ya kwanza ya Uchumi
1976-1977 - Mafunzo ya Afisa wa Jeshi na Mafunzo ya Uongozi wa Jeshi Monduli
1983-1984 - Mafunzo ya Makamanda wa Jeshi

Nafasi alizowahi kushika

1975-1977 - Katibu msaidizi wa TANU wa Mkoa
1977-1980 - Katibu Msaidizi wa CCM, Kisiwani Zanzibar
1980-1981 - Afisa Utumishi wa CCM makao makuu
1981-1983 - Katibu wa CCM Mkoa Tabora
1983-1986 - Mkufunzi wa Siasa katika Chuo cha uongozi wa Jeshi Monduli
1986-1988 - Katibu wa CCM Wilaya ya Nachingwea na baadaye Masasi
1988-1990 - Naibu Waziri wa Nishati na Madini
1990-1994 - Waziri wa Nishati, Madini na Maendeleo ya Maji
1994-1995 - Waziri wa Fedha
1995- 2005 -  Mbunge wa Chalinze
1995-2000 - Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa
2000-2005 -  Aliteuliwa tena kuuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa. Wadhifa ambao anaushikilia mpaka sasa.