MWENYEKITI WA CCM, RAIS BENJAMIN WILLIAM MKAPA AKUTANA NA WENYEVITI WA CCM WA MIKOA MJINI DAR ES SALAAM
Mwenyekiti wa CCM, Mheshimiwa Rais Benjamin William
Mkapa tarehe 30/1/2004 alikutana na Wenyeviti wa CCM wa Mikoa yote ya Tanzania
Bara na Tanzania Zanzibar kubadilishana mawazo juu ya mambo mbali mbali
yanayohusu Chama Cha Mapinduzi.
Kikao hicho pia kilihudhuriwa na Katibu Mkuu wa CCM,
Ndugu Philip J. Mangula.
Wakati huo huo, Sekretarieti ya Halmashauri Kuu ya
Taifa ya CCM chini ya Mwenyekiti wake, Katibu Mkuu wa CCM, Ndugu Philip J.
Mangula tarehe 29/1/2004 ilikutana na Makatibu wa CCM wa Mikoa katika Ofisi
Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Mtaa wa Lumumba Dar es Salaam.
Kikao hicho pia kilihudhuriwa na Makatibu Wakuu wa
Jumuiya za CCM za Umoja wa Wanawake (UWT), Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) na
Wazazi ambao kwa mujibu wa Katiba ya CCM wote hao ni Wajumbe wa Sekretarieti ya
Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM.
Viongozi hao walipeana majukumu ya kufuatilia
utekelezaji wa maamuzi ya kikao cha siku tatu (27-29/1/2004) cha Halmashauri
Kuu ya CCM ya Taifa kilichokutana Dar es Salaam.