HOTUBA YA MHE. JAKAYA MRISHO KIKWETE, RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA
TANZANIA NA MWENYEKITI MPYA WA CCM KWENYE MKUTANO MKUU WA SABA WA CHAMA CHA
MAPINDUZI, CHIMWAGA – DODOMA, 25 JUNI 2006
Ndugu Mwenyekiti Mstaafu,
Mheshimiwa Benjamin William Mkapa;
Mwenyekiti Mstaafu, Ali Hassan Mwinyi
Ndugu zangu, wanachama wenzangu,
Nimesimama kutoa shukrani kwenu
wajumbe wenzangu wa Mkutano Mkuu wa Taifa wa Chama chetu kwa uamuzi wenu wa
kunichagua tena kwa kishindo, kuwa
Mwenyekiti wa Nne wa Chama Cha Mapinduzi.
Natafuta maneno mazuri ya kuelezea
//shukrani zangu
shukrani zangu kwenu lakini
Kiswahili hakina maneno zaidi ya Ahsanteni Sana.
Kwa mara nyingine tena natoa
shukrani zangu za dhati kwa Halmashauri
Kuu ya Taifa ya Chama chetu kwa imani yao kwangu na hivyo kuamua kunileta mbele
yenu kwa uchaguzi huu mlioufanya leo.
Namshukuru
kwa namna ya kipekee mzee wangu na mwalimu wangu Mheshimiwa Benjamin William
Mkapa, Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na sasa Mwenyekiti
Mstaafu wa Chama chetu. Kwanza
namshukuru kwa kunilea na kunilinda mpaka nimefika hapa. Alikuwa mwalimu wangu wa masuala ya
diplomasia kwa kipindi chote cha miaka 10 nilichokuwa Waziri wake wa Mambo ya
Nje. Nimeingia wizarani nikiwa sijui
//chochote kuhusu
chochote
kuhusu masuala ya uhusiano wa kimataifa lakini nimeondoka nikiwa nimehitimu.
Na, hata kabla ya hapo tulipokuwa wote katika Baraza la Mawaziri ambapo mimi
nilipojiunga nilimkuta yeye ni Waziri Mwandamizi alinisaidia kwa mengi. Lakini, pia nilijifunza mengi kuhusu Ubunge
na uongozi wa ngazi za mwanzo kutoka kwake kule Wilayani Masasi wakati
nilipokuwa Katibu wa CCM wa Wilaya na yeye akiwa Mbunge wa Jimbo la
Nanyumbu.
Pili, namshukuru sana kwa imani
yake na mapenzi yake kwangu wakati wa
mchakato, baada ya uteuzi, wakati wa uchaguzi na baada ya uchaguzi.
//Na sasa nikiwa Rais,
Na sasa nikiwa Rais, amekuwa mshauri wangu wa kutumaini. Ni mtu mwepesi na hana taabu ninapomuomba
ushauri na msaada kwa jambo lolote ninapoona anaweza kunisaidia. Sina shaka kwamba
hata kwa masuala ya Chama nayo ataniwekea milango yake wazi ili niweze kuchota
kutoka kwenye hazina yake kubwa ya busara, hekima na maarifa.
Ushahidi
mwingine mkubwa wa upendo na imani yake kwangu, ni uamuzi wake wa kuacha
Uenyekiti kabla ya wakati wake na kunipendekeza mimi nichukue nafasi hiyo. Ni imani iliyoje kwangu mtu anayoweza
kuionyesha zaidi ya hii. Aliponiambia
Februari, 2006 kuwa ameamua kuacha Uenyekiti na kuniachia, nilimwambia kuwa
naona ilikuwa mapema mno, mimi ningependa kwanza
//nipate nafasi
nipate nafasi ya kujiimarisha katika Serikali kabla
ya kuchukua Uongozi wa Chama. Nakumbuka kumwambia “Unajua Mzee nina miezi
miwili tu sina haraka, endelea mpaka 2007”.
Mzee Mkapa akanijibu
kuwa na yeye
alipokea hivyo hivyo kutoka kwa Mzee Mwinyi.
Alisisitiza kuwa huu ni utaratibu mzuri, ni bora kuudumisha. Akanisihi
kuwa nikubali maombi yake. Nikamjibu
sawa ila “siyo sasa”. Akaniambia:
“Haitakuwa ghafla” na hata Mzee Mwinyi alimkabidhi zaidi ya miezi sita
baada ya kuchaguliwa, hivyo alidhani mwezi Juni ungekuwa wakati muafaka. Nikamwambia “Ndiyo Mzee!”. Muafaka ukafikiwa na maelewano yetu hayo ndiyo yamezaa shughuli
hii ya leo.
// Waheshimiwa Wajumbe;
Waheshimiwa Wajumbe;
Nilipokuwa
namuomba Mwenyekiti Mkapa aendelee mpaka 2007 nilifanya hivyo sio kwa sababu ya
kutokujiamini kumudu madaraka ya Mwenyekiti wa Chama bali ni kutokana na kutaka
kujipa nafasi ya kujijenga na kujiimarisha katika kazi kubwa mliyonipa ya
kuongoza Serikali. Nimeikubali haja ya
kuunganisha kofia sasa. Naukubali mzigo
huu mpya kwa moyo mkunjufu na bila ya hofu.
Nasema sina hofu kwa sababu ninyi
wenzangu mpo. Ninyi wenye Chama chenu
mpo tena mna hamasa kubwa. Jirani zangu
Wazigua wanao msemo maarufu usemao, “Zumbe ni wan’tu” maana yake ni kwamba,
“kiongozi ni watu”. Hali kadhalika
Mwenyekiti wa Chama ni wanachama.
Maadamu
//wanachama wa CCM
wanachama wa CCM wapo na viongozi
na makada wake wapo tena walio imara, sioni sababu kwa nini nisifanikiwe katika
kazi yangu ya Uenyekiti. Mzee Malecela
yupo. Rais Karume yupo. Hali kadhalika Kamati Kuu na Halmashauri Kuu ipo.
Sekretariet yenye uwezo wa kiutendaji ipo. Siwezi kushindwa.
Sababu nyingine inayonipa imani
kuwa mzigo huu unabebeka “hata na mie ambaye si Mnyamwezi”, ni ule ukweli
kwamba narithi Chama imara, chenye wanachama na viongozi wenye msimamo,
mshikamano na hamasa ya hali ya juu.
Chama ambacho ni imara kwa muundo wake na bora kwa sera zake. Chama ambacho kimeweka misingi endelevu ya kupata
viongozi na kubadilishana uongozi wa juu bila ya kelele wala mikwaruzo. Sote
//tunaona mchakato
tunaona mchakato huu unavyofanyika
katika mazingira ya utulivu na upendo. Tumeona
pia kwa namna gani hata mchakato wenye ushindani mkubwa kama ule wa kutafuta
Mgombea Urais ulivyoendeshwa na kumalizika salama. Tulianza kumi na moja na
mitandao kumi na moja lakini sasa tuko wamoja, kitu kimoja na mtandao mmoja tu
wa CCM. Waliodhani kuwa Chama chetu
kingemeguka walitahayari. Hata kura zilizopigwa zinathibitisha ukweli huo.
Tamaa ya fisi tu, mkono wa mwanadamu haukudondoka.
Tuimarishe Chama Chetu
Ndugu Wajumbe;
Pamoja
na ukweli huo, kuhusu uimara na ubora wa Chama chetu natambua hoja na haja ya
kuchukua hatua zaidi za kukiimarisha na kukiboresha zaidi
//Chama Cha Mapinduzi.
Chama Cha Mapinduzi. Ni makusudio yangu kushirikiana kwa karibu na
wanachama wenzetu na ninyi viongozi wenzangu katika kufanikisha kazi hii
muhimu.
Ndugu Wajumbe;
Chama
imara ni kile ambacho viungo vyake vimekamilika na vinafanya kazi vizuri. Chama ni wanachama, viongozi, vikao,
watendaji, rasilimali na Jumuiya za Chama.
Kukamilika
kwa viungo vyote hivyo na kwa kila kiungo kuwa kinafanya kazi ipasavyo, ndio
uimara wa Chama Cha Mapinduzi. Kwanza
kabisa, hatuna budi kuhakikisha kuwa wanachama wa Chama chetu ni madhubuti,
wanaongezeka kwa idadi na kwamba wako mstari wa mbele kukitetea na kukipigania
Chama chao. Wanachama wanaotimiza
ipasavyo
//wajibu wao
wajibu wao wa kikatiba. Wanaolipa ada zao kwa wakati, wanaotoa
michango yao na kushiriki kwa ukamilifu vikao vya Chama vinavyowahusu na
shughuli mbalimbali za Chama. Naomba kwa
pamoja tupime ubora wa kiungo hiki na kubaini mapungufu yaliyopo na
kuyarekebisha.
Wajumbe wenzangu,Wajumbe wenzangu;
Katika kuimarisha Chama chetu hatuna budi tuhakikishe kuwa
kiungo cha viongozi kiko imara kweli kweli. Safu za Uongozi ziwe zimekamilika
ipasavyo, hakuna mapengo na kwamba viongozi hao wako mstari wa mbele kutimiza
wajibu wao wa uongozi. Kiongozi ndiye
mwonyeshaji njia, lazima viongozi wa Chama Cha Mapinduzi tuifanye kazi hiyo kwa
umahiri mkubwa. Viongozi pia lazima
waongoze kwa mfano na siyo kwa maneno.
Kauli za
//fuata maneno
fuata maneno yangu usijali matendo
hazina nafasi katika uongozi wa Chama cha watu. Tuseme tunayotenda ili tujenge
moyo kwa watu kutuamini.
Kwa vile Chama chetu ni Chama
tawala, viongozi wetu wanao wajibu wa kuifanya kazi hiyo ndani ya Chama na nje
ya Chama ndani ya Umma. Ni ukweli
usiofichika kwamba, viongozi wa Chama chetu hawaifanyi vya kutosha kazi ya
uongozi miongoni mwa umma. Wakati
mwingine ukitulinganisha na viongozi wa vyama vya upinzani, viongozi wa Chama
Cha Mapinduzi hatufanyi sana mikutano ya hadhara na umma. Mikutano ya hadhara ni nyenzo ya kuwavutia
watu upande wetu. Inatoa fursa ya kufafanua
masuala mbalimbali yahusuyo sera na siasa ya Chama chetu. Naomba wenzangu tubadilike ili tuzuie
upotoshaji na
//kuhakikisha kuwa
kuhakikisha kuwa wananchi wanapata
ukweli wa mambo kutoka midomoni mwetu.
Tutaendelea
kuhimizana kuhusu kuzingatia jambo hili
muhimu. Kadhalika tutalipa umuhimu
unaostahili suala la mafunzo ya viongozi na makada wetu. Kwa ajili hiyo tutafuatilia kwa karibu uamuzi
wa NEC wa kuwa na Chuo cha Chama pale Ihemi, Iringa. Baada ya muda si mrefu tutaanza kuchukua
hatua za utekelezaji wake.
Waheshimiwa Wajumbe wenzangu;
Kama
tulivyosikia katika taarifa ya Chama kuwa hali ya ufanyikaji wa vikao vya Chama
siyo nzuri hasa kwa ngazi za mwanzo za Chama chetu. Huko ndiko waliko wanachama na huko ndiko
kiliko Chama. Hivyo udhaifu huu ni jambo
lisilofurahisha hata kidogo. Hatuna budi
tubadilike. Kama tujuavyo
//maamuzi ya Chama
maamuzi ya Chama hufanywa kwenye vikao tofauti na
Serikali ambapo Rais, Waziri, Mkuu wa Mkoa na Mkuu wa Wilaya wanaweza
kuamua wenyewe bila vikao. Katika Chama maamuzi hufanywa kupitia vikao
na hata Mwenyekiti wa Chama na viongozi
wa Chama hawana maamuzi yao binafsi labda iwe kutelekeza maamuzi yaliyofanywa
kabla au maagizo ya katiba na kanuni.
Hivyo basi, kutokufanyika vikao
vya Chama vya ngazi husika kunadhoofisha sana mfumo mzima wa maamuzi ndani ya
Chama. Kutofanyika vikao kunaua dhana nzima ya demokrasia ya ndani ya Chama na
dhana ya uongozi wa pamoja. Wanachama
na wajumbe wa vikao husika wawe wakali kudai kufanyika kwa vikao vya ngazi
zao. Naomba tubadilike ili kiungo hiki
muhimu sana
//tukipe nafasi
tukipe nafasi stahiki ya uhai
wake.
Ndugu Wajumbe;
Watendaji
ni kiungo cha msingi kabisa katika uhai na maendeleo ya Chama chetu. Ndicho kiungo unganishi kwa shughuli zote za
Chama. Ndicho kiungo kitendaji cha Chama
chetu. Bila ya kiungo hicho mambo yetu
yatakuwa mabaya au hayatowezekana.
Hatuna budi basi kukiangalia vizuri kiungo hiki. Tuhakikishe kuwa Chama chetu kina watendaji
waliokamilika ipasavyo kwa mujibu wa ikama.
Watendaji wa Chama chetu wawe ni
watu wenye ujuzi, maarifa na uwezo wa
hali ya juu wa kazi zao za kiutendaji. Aidha, ni wajibu wetu kuwawezeshea watendaji
wetu kutimiza ipasavyo majukumu yao kwa maana ya mafunzo, zana na vifaa vya
kazi.
//Pamoja na hayo,
Pamoja na hayo, tuwatengenezee
mazingira mazuri ya kufanyia kazi:
maofisini na katika hali ya maisha yao.
Lakini,
tunapozungumzia watendaji, zana na vitendea kazi vya Chama tunazungumzia suala
zima la kujenga uwezo wa raslimali na kifedha wa Chama chetu ulio mkubwa zaidi
kuliko ilivyo sasa.
Ni lazima tukae chini kuzungumzia
kujenga uwezo wa kifedha na rasilimali wa Chama chetu. Hili ni jambo la msingi
sana. Hakuna majawabu rahisi kuhusu nini
na vipi tufanye, lakini lazima tufanye kwani hakuna badala yake. Tufanye hivyo katika
kila ngazi ya Chama chetu. Nawaomba wenzangu kila kiongozi na kila mwanachama
katika ngazi yake alipe suala hili uzito unaostahili. Tuchune bongo zetu, tubuni mikakati, mbinu na
mipango ambayo
//itakiingizia Chama
itakiingizia Chama chetu fedha na kukipatia
rasilimali za kufanyia kazi kwa uhakika.
Waheshimiwa Wajumbe;
Nalisemea hili kwa sababu ya
umuhimu wake na kwa sababu naamini wote tunautambua ukweli huo. Sasa wakati umefika kwa Chama chetu
kuondokana na maisha ya kutafuta fedha na rasilimali za kufanyia shughuli zake
kwa taratibu za zimamoto. Kufanya hivyo
kuna hatari ya siku moja kujikuta moto umekuwa mkubwa mno na hauzimiki kwa
urahisi. Lakini jambo baya zaidi ni
hatari ya kuhusishwa na watu tusiokuwa
na uhakika nao na kupata hatari ya kuishia kupata fedheha.
Waheshimiwa Wajumbe;
Jumuiya
za Chama ni kiungo chenye nafasi ya pekee kwa Chama chetu. Jumuiya ziliundwa kwa nia
//ya kukisogeza Chama
ya kukisogeza Chama chetu karibu
na umma wa Watanzania. Ni chombo
kilichoundwa kukipatia Chama chetu wanachama, marafiki, wapenzi na washabiki
miongoni mwa makundi mbalimbali ya jamii pana ya Watanzania. Na kwa wakati huu siasa ya vyama vingi
jumuiya ni chombo muhimu cha kukitafutia Chama chetu kuungwa mkono na Watanzania
walio wengi wakati wa uchaguzi. Hivyo
basi kwa Jumuiya za Chama Cha Mapinduzi kuwa imara ni jambo ambalo halina
mjadala.
Naomba wana CCM wenzangu tuelewe hivyo. Hasa
naomba viongozi na wanachama wa UWT, Vijana na Wazazi watambue umuhimu wao huo. Naomba watambue kuwa, Jumuiya kuwa imara ni
kwa maslahi mapana ya Chama chetu. Hatuna budi tufanye kila tuwezalo
kuhakikisha kuwa Jumuiya
//zetu zinaimarishwa
zetu zinaimarishwa ipasavyo kwa
ngazi zote. Napenda kuitumia fursa hii
kuwahakikishia wana CCM na wanachama na viongozi wa jumuiya zetu ushirikiano wangu wa hali ya juu katika
jitihada za kujenga na kuimarisha jumuiya zetu.
Ndugu Wajumbe wenzangu;
Leo
tunakutana kwa mara ya kwanza tangu Mei Nne mwaka wa jana, wakati wa Mkutano
Mkuu Maalum wa uteuzi wa Mgombea Urais kwa tiketi ya CCM. Pia, ni mara ya
kwanza tangu uchaguzi kuisha.
Kwa
mara nyingine napenda kuwashukuru
Lakini,
shukrani kubwa zaidi nazitoa kwa kwenu
kwa jinsi mlivyokipigania Chama chetu
//wakati
wa kampeni
wakati
wa kampeni na kukiwezesha kupata ushindi mnono ambao umewashangaza wengi.
Nimeiona nguvu ya viongozi, wanachama na makada wa Chama wanapoamua kukipigania
Chama chao. Hakuna mfano wake.
Nakosa
maneno mazuri ya kuelezea shukrani na pongezi zangu kwenu kwa jitihada zenu
kubwa zilizokipatia ushindi mkubwa
Ndugu
zangu, Wajumbe wenzangu;
Mzee
Mkapa alitukumbusha jana kuwa, mwisho wa uchaguzi mmoja ndiyo mwanzo wa
uchaguzi mwingine. Maandalizi ya uchaguzi wa 2010
//yalitakiwa
kaunza
yalitakiwa
kuanza saa 10 jioni siku ya tarehe 14
Desemba, 2005 baada ya kupiga kura. Hembu tujiulize:- Je, tumeanza au bado
tunasherehekea ushindi? Ndugu zangu
tuanze sasa kwa kujenga na kuimarisha Chama chetu na kutafuta nyenzo na vifaa
muhimu vya kuendeshea kampeni. Wachina
wana msemo “Jasho jingi wakati wa amani, damu kidogo wakati wa vita”.
Ndugu Wajumbe wenzangu;
Wakati
tunazindua kampeni za uchaguzi za chama chetu pale Uwanja wa Jangwani, tarehe
21 mwezi wa nane mwaka jana, Mwenyekiti wetu wa CCM wa wakati ule, Mheshimiwa
Benjamin William Mkapa, alinikabidhi Ilani ya Uchaguzi ya Chama chetu ili nikainadi
kwa wananchi kwa niaba yenu.
//Kazi
hiyo nimeifanya
Kazi
hiyo nimeifanya kwa nguvu na uwezo wangu wote na ninyi wenzangu ni mashahidi.
Tena, tumeifanya sote kwa ushirikiano na mafanikio makubwa.
Vilevile,
siku ile Mwenyekiti Mkapa alinikabidhi
Ilani sio tu kwa ajili ya kuinadi tu,
bali pia iwe ndio dira ya Serikali ya Awamu ya Nne pindi wananchi watakapokuwa
wametupa ridhaa ya kuwaongoza. Sasa Chama chetu kimekamata dola, na mchakato wa
utekelezaji wa Ilani mliyotukabidhi tumeuanza. Tena tumeianza kazi hiyo
Katika
kipindi chote ambacho tumekuwa madarakani, tumetumia kila mwanya kukumbusha na
kusisitiza kwa watumishi wa umma kwamba Ilani
//ya
CCM ndio dira
ya
CCM ndio dira na mwongozo wa Serikali ya Awamu ya Nne,
Pili,
nilifanya ziara katika Wizara zote na Idara mbalimbali za Serikali nikiwa
nimebeba Ilani ya chama chetu mkononi. Nia yangu ilikuwa
//kuwakabidhi
watumishi
kuwakabidhi
watumishi wa umma Ilani hiyo na kuwakumbusha kwamba katika utumishi wao
Serikalini wanao wajibu kutekeleza Ilani
ya Chama kilichopata ridhaa ya wananchi hata kama utashi na mapenzi
Ndugu Wajumbe;
Kwa
ujumla,
Ndugu
Wajumbe;
Tumepanga
kutekeleza kauli-mbiu hiyo ya Chama chetu kwa kuongeza na kuboresha huduma za
kijamii na kiuchumi kwa Watanzania na kukuza
//kipato
cha Watanzania
kipato
cha Watanzania wakulima na wanyakazi walioko mijini na vijijini. Kwa upande wa huduma mkazo utawekwa katika
sekta za afya, maji, elimu, umeme, barabara n.k.
Tumesikia maoni ya wajumbe wakati wa kuchangia
taarifa za Serikali. Tutayatafakari na
kuyafanyia kazi. Kwa upande wa barabara, nimesikia sauti za
//mazuri.
mazuri. Hivyo hivyo kwa umeme.
Waheshimiwa
Wajumbe;
Mimi na wenzangu Serikalini tunatambua kuwa
maisha bora kwa Watanzania yatawezekana tu kwa kuhakikisha kwamba kipato cha
Watanzania kinaongezeka. Ndiyo, maana tumeamua kuweka mkazo maalum kwenye
kuongeza tija na uzalishaji katika shughuli wanazojihusisha nazo Watanzania
walio wengi ambazo ni kilimo, uvuvi na ufugaji. Tutaimarisha sekta
zitakazochangia kukua kwa kilimo, hasa viwanda vya usindikaji wa mazao ya
kilimo na kuzalisha bidhaa zinazotakiwa na sekta hiyo.
Ndugu
zangu;
Katika
suala la kilimo, ninalo ombi maalum kwenu, Viongozi wa CCM. Chama chetu kina
historia
//ya
muda mrefu
ya
muda mrefu na ya kutukuka ya kuwa mstari wa mbele katika kuhamasisha, kusukuma
na kusimamia mageuzi ya kilimo nchini. Tulikuwa tukiwahamasisha wakulima wakati
wa utayarishaji wa mashamba, kupanda, kupalilia, kuvuna na hata wakati wa
kuhifadhi mazao. Chama chetu kilikuwa mstari wa mbele katika kutoa miongozo kwa
wakulima wetu juu ya kanuni za kilimo bora. Lakini, siku hizi, majukumu haya ya
msingi tumeyaacha. Matokeo yake ni maendeleo ya kilimo kurudi nyuma.
Ndugu
zangu, wanachama wenzangu na viongozi wenzangu, Tumewaahidi Watanzania mageuzi
ya kilimo. Nawasihi turudie ule utaratibu wetu mzuri wa zamani. Lazima tufanye
hivyo ili tufanikiwe katika azma yetu hii. Ilani hii ni yetu sote. Na, sote,
katika Chama na Serikali, tutapimwa na
//wananchi
kwa mafanikio
wananchi
kwa mafanikio ya utekelezaji wake.
Ndugu
Wajumbe;
Katika mikakati ya kuongeza kipato kwa
Watanzania, lipo suala zima la kuwapatia ajira wasiokuwa na ajira. Tumeanza
kuchukua hatua za kukuza ajira Serikalini. Vilevile tumeanza kuweka mazingira
ya kuwawezesha vijana, wanawake na Watanzania kwa ujumla wanaotaka kujiajiri
kufanya hivyo. Waziri Mkuu atalifafanua
vizuri zaidi kesho. Ninachosema ni kuwa,
tunajali na tunaheshimu ahadi zetu. Tunajiandaa pia kukuza uwekezaji ili tukuze
ajira na kukuza uchumi.
Ndugu
zangu, utekelezaji wa Ilani yetu unahitaji uwezo mkubwa wa kirasilimali wa
Serikali. Tunafanya jitihada kuhakikisha kwamba uwezo huo unakuwepo.
Tutahakikisha kwamba mapato ya
//Serikali
yataendelea
Serikali
yataendelea kukua. Vilevile, mimi na wenzangu Serikalini tunaendelea na juhudi
za kujenga mahusiano mazuri na nchi wahisani, marafiki na mashirika ya
Kimataifa ili tuendelee kupata misaada ya kutuwezesha kutekeleza mipango yetu.
Nafurahi kwamba hadi sasa juhudi za Serikali yetu zimepokelewa vizuri duniani
kote. Na kila nilipoenda kwenye ziara nje, nimepewa matumaini ya kuungwa mkono
katika jitihada zetu. La msingi zaidi
katika kujenga uwezo wetu ni kuhakikisha kwamba uchumi wetu unakuwa mkubwa
zaidi ili tuweze kujitegemea wenyewe. Hii lazima iwe azma yetu ya muda mrefu.
Kwahiyo,
ndugu zangu, Ilani ya chama chetu iko katika mikono salama. Tutahakikisha
inatekelezwa.
//Na,
kwa kweli
Na,
kwa kweli Bajeti yetu ya kwanza iliyopitishwa kwa kishindo na Bunge Jumatatu
inathibitisha dhamira yetu ya kutekeleza yale tuliyoyaahidi katika Ilani ya
Chama chetu.
Ni dhahiri kwamba yote
tuliyoyaahidi hayataonekana kwenye bajeti ya mwaka huu. Ilani yetu ni ya miaka
mitano na ahadi zetu tulizotoa zitatekelezwa ndani ya kipindi hicho.
Ndugu wajumbe wenzangu;
Leo
hii tunajigamba juu ya uwezo wetu wa kutekeleza Ilani ya Chama chetu na
kuendesha mambo yetu kwa sababu moja
kuu: nayo ni msingi mzuri aliotujengea
na kutuachia Rais wetu na Mwenyekiti wetu Mstaafu, Mhe. Benjamin William Mkapa.
Ndugu
zangu, mkiniona natembea kifua mbele,
//kama
ambavyo
kama
ambavyo chama changu kinanitegemea niwe, mkiniona nasimama kwa kujiamini,
Misingi
aliyotuachia Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere inaifanya kazi yetu ya kudumisha na
kuendeleza umoja, mshikamano na utulivu wa taifa letu iwe rahisi. Misingi
aliyotuachia Mzee Mwinyi inaifanya kazi yetu ya kuhubiri uvumilivu wa tofauti
zetu za kisiasa na kijamii isiwe ngumu. Na, misingi imara ya kiuchumi
aliyotuachia Mzee Mkapa inalifanya jukumu la msingi la Serikali ya Awamu ya
//Nne-
jukumu la kukuza
Nne
– jukumu la kukuza uchumi, kuinua kipato cha Watanzania na kuwaletea maisha
bora – liwezekane.
Ndugu
zangu, sisi
Mzee
wetu Mkapa, umelifanyia Taifa letu kazi
//kubwa
na nzuri
kubwa
na nzuri na umeiletea heshima kubwa nchi
yetu. Tunakushukuru
Kabla
ya kumaliza naomba nisemee mahusiano na vyama vingine vya siasa nchini na nje
ya nchi. Napenda kuwahakikishia kuwa, tutaendelea kujenga uhusiano mwema na
vyama vyote vya siasa nchini na vyama rafiki nje ya nchi. Tunatambua umuhimu wa
vyama vya siasa kwa kuendeleza demokrasia nchini mwetu. Nawaahidi ushirikiano wa karibu. Utaratibu aliouonyesha Mwenyekiti Mkapa wa
mawasiliano na vyama vya siasa nitauendeleza kwa kasi mpya,
//nguvu
mpya na ari mpya.
nguvu
mpya na ari mpya. Tunajenga nyumba moja si busara kugombea
fito. Tutashindana wakati wa uchaguzi,
ukiisha sote tujenge nchi yetu.
Ndugu
Wajumbe;
Leo najiona
nimezaliwa upya katika historia ya maisha yangu na katika historia ya uanachama
wangu kwa Chama chetu. Nilipojiunga na
utumishi wa Chama cha TANU Aprili 2, 1975 na kuanza kazi pale Singida sikujua
na wala sikuotea kuwa hatimaye safari yangu ile iliyopitia Kisiwandui, Ofisi
Ndogo, Tabora, Monduli, Nachingwea, Masasi na katika Umoja wa Vijana, NEC na Kamati Kuu hatimaye itanifikisha hapa nilipofikia leo.
Nitakuwa
mwizi wa fadhila kama sitatambua na kutoa neno la shukrani kwa Umoja wa Vijana
wa
//TANU na Umoja
TANU na Umoja wa Vijana wa CCM. Umoja wa Vijana wa TANU na
Umoja wa Vijana vilikuwa uwanja muhimu na darasa lililonipatia mbinu na maarifa
ya Uongozi. Kadhalika, lilikuwa darasa
la kujifunzia siasa na sera za Chama na kuniandaa kuwa mwanachama wa TANU na
CCM.
Nawashukuru
wazee na walezi wangu wa kisiasa hususan Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage
Nyerere, Mzee Rashid Kawawa, Mzee Ali Hassan Mwinyi kwa malezi mazuri. Sitomsahau Mzee Pius Msekwa katika orodha
hiyo.
Namshukuru Mwenyezi Mungu kwa
kunijaalia rehema zake. Na, nazidi kumuomba Mola wetu anijalie karama zake
nimudu vyema majukumu ya Uenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi na yale ya Urais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Lakini, pia
//nawashukuru
sana
nawashukuru sana Viongozi wangu
na wanachama wenzangu wa TANU na sasa CCM kwa malezi yao, ushirikiano wao na
msaada wao. Bila ya ushirikiano huo
nisingekuwa hivi nilivyo sasa. Nategemea kwa kiasi kikubwa ushirikiano wenu
katika jukumu hili kubwa na zito la Uenyekiti wa Chama chetu. Kwa pamoja,
tunaweza kukijenga, kukidumisha na kukiimarisha Chama chetu ili kiendelee kuwa
tumaini na kimbilio la Watanzania. Naamini inawezekana. Mwalimu Nyerere alipata kusema “it can be
done, play your part”
Kwa mara nyingine, napenda
kuwashukuru kwa imani kubwa mliyoinyesha kwangu.
Nawashukuru sana kwa
kunisikiliza. Sasa, naufunga rasmi mkutano huu. Nawatakia safari njema ya
kurejea nyumbani.
KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI