NEC YATEUA WAGOMBEA WA NAFASI ZA KITAIFA KATIKA JUMUIYA ZA WAZAZI NA VIJANA
Katika kikao chake cha tarehe 28/1/2004, Halmashauri
Kuu ya Taifa ya CCM iliyokutana mjini Dar es Salaam chini ya Mwenyekiti wa CCM,
Mheshimiwa Rais Benjamin William Mkapa ilifanya uteuzi wa mwisho wa wanachama
watakaogombea nafasi mbali mbali za uongozi wa Jumuiya ya Wazazi, ngazi ya Mkoa
na Taifa.
Walioteuliwa kugombea nafasi ya Mwenyekiti wa Wazazi
Taifa ni Ndugu Idd Mohamed Simba, Ndugu Kisase Marwa Ginche na Ndugu Abioud Mugini
Maregesi.
Aidha Halmashauri Kuu ya Taifa imemteua Ndugu
Ramadhani Suleiman Nzori kugombea nafasi za Makamu Mwenyekiti wa Wazazi Taifa.
Aidha, kikao hicho cha NEC imewateua wanachama wa CCM watatu kugombea
nafasi ya Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa CCM Taifa.
Walioteuliwa na Halmashauri Kuu ya Taifa kugombea
nafasi hiyo ni Ndugu Nape Mosses Nnauye, Dr. Emmanuel Nchimbi na Ndugu Jane
Claude Mihanji.
Vijana wa CCM watatu pia waliteuliwa kugombea nafasi
ya Makamu wa Mwenyekiti wa UVCCM Taifa.
Hawa ni Ndugu Mtumwa Khatib Ameir, Ndugu Amina Idi Mbarouk na Ndugu Ali
Suleiman Othman.
Uchaguzi wa viongozi hao wa Kitaifa wa Jumuiya za
Wazazi na Vijana utafanywa na Mikutano Mikuu ya Jumuiya hizo hivi karibuni.
Katika kikao chake cha tarehe 28/1/2004, Halmashauri
Kuu ya Taifa ya CCM pia imewateua Ndugu Ali Hassan Gwaja, Ndugu Ali Mohamed
Mtopa na Ndugu Ibrahim Chande Ngongono kugombea nafasi ya Mwenyekiti wa CCM wa
Mkoa wa Lindi ambayo iliachwa wazi kufuatia kifo cha aliyekuwa Mwenyekiti wake,
Marehemu Ahmed M. Lilai aliyefariki dunia tarehe 17/3/2003.
Walioteuliwa kugombea nafasi ya Mjumbe wa NEC kupitia
mkoa wa Kaskazini Pemba ni Ndugu Ramadhani Khamis Feruzi, Ndugu Mbarouk Rashid
Omar na Ndugu Salim Hamad Saleh. Nafasi
hiyo imekuwa wazi kufuatia kifo cha Ndugu Borafia Mtumwa Borafia kilichotokea
tarehe 1/10/2002.