ITIFAKI YA MATUMIZI YA BENDERA YA

 CHAMA CHA MAPINDUZI

 

 

1.0.0 UTANGULIZI

 


          1.0.1 Katiba ya Chama Cha Mapinduzi ibara ya 3 inaainisha wazi wazi umuhimu na nafasi ya bendera kama ifuatavyo: Bendera ya CCM itakuwa rangi ya   kijani kibichi ambayo itakuwa na alama ya jembe (alama ya mkulima) na nyundo (alama ya mfanyakazi) kwenye pembe ya juu upande wa mlingoti.

 

          1.0.2 Ni dhahiri basi kuwa bendera hiyo ni alama muhimu iliyobuniwa ili kuwa   kielelezo cha umoja pamoja na kudhihirisha azma na madhumuni ya CCM          ya kutetea haki na maslahi ya wakulima na wafanyakazi.

 

          1.0.3 Wakati  wa mfumo wa chama kimoja, bendera ya Chama ilitumika kwa      matumizi  rasmi tu kwenye ofisi za Chama, magari ya viongozi na ofisini        kwenye meza za viongozi husika n.k.  Hata hivyo, baada ya kuingia kwa          mfumo wa vyama vingi, bendera hiyo imejikuta ikitumika pia kwa shughuli     za kiuenezi na hamasa, hasa wakati wa kampeni za Uchaguzi wa Dola.            Katika mazingira hayo, wanachama na wapenzi wa CCM huitumia bendera           hiyo kwenye  baiskeli, majumbani mwao, vijiweni mwao, kwenye magari         yao na hata wenyewe tu  mmoja  mmoja kupeperusha mikononi au hata          kuivaa.  Pia, bendera hiyo hutumika kwa mapambo kwenye mikutano ya    hadhara na shughuli nyingine za Chama.

 

          1.0.4 Kwa kuzingatia kwamba matumizi yote hayo yana manufaa makubwa        kwake, Chama kimeamua kutoa  itifaki hii ili iwe mwongozo rasmi wa         matumizi ya bendera hii  ya Chama.  Kimsingi, itifaki hii inabainisha     matumizi mawili makubwa  ya bendera hii.  Matumizi hayo ni yale rasmi     kwa ajili ya ofisi na vingozi wa Chama kwa upande mmoja, na yale ya      uenezi na uhamasishaji kupitia wanachama wa kawaida, wapenzi na     mashabiki wa CCM kwa upande wa pili.

 


2.0.0 MATUMIZI RASMI YA BENDERA YA CCM

 

2.0.1      Bendera kwa ajili ya matumizi  rasmi zitakuwa za aina mbili kuu zifuatazo:-

 

          (a)   Bendera za Viongozi Wakuu wa CCM

                   (b)   Bendera za Viongozi Wengine wa Chama na Majengo ya Ofisi za Chama

 

2.1.0      Bendera za Viongozi Wakuu wa CCM

 

          2.1.1  Bendera hizi zitakuwa na utepe wa rangi ya manjano upande wa    mlingoti na zitapambwa kwa urembo wa nyuzi za rangi hiyo hiyo kuizunguka bendera yote ukiondoa ule upande wa mlingoti utakaokuwa na utepe.

 

          2.1.2  Bendera za aina hii zitapeperushwa  na viongozi wakuu wafuatao tu:-

(a)      Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi.

(b)     Makamo wawili wa Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi.

(c)      Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi.

(d)     Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mgombea Urais wa Zanzibar na Mgombea Mwenza wa Jamhuri kwa tiketi  ya Chama Cha Mapinduzi wakati wa kampeni ya Uchaguzi Mkuu wa Dola, au chaguzi nyingine zozote ambapo Chama kitakuwa na Mgombea au Wagombea wa nafasi hizo.

 

 

 

 

 

          2.1.3  Bendera hizi za Viongozi Wakuu zitatumika kama ifuatavyo:-

 

(a)      Kwenye gari la Kiongozi kwa kuegeshwa kwenye mlingoti upande wa kushoto wa mbele wa gari hilo, wakati wote awapo ndani ya gari safarini.

 

(b)       Bendera ya aina hiyo hiyo iliyotengenezwa kwa ajili ya          kuwekwa mezani itakuwa mezani kwenye meza ya ofisi ya     Kiongozi wakati wote kwani ni udhihirisho wa mamlaka yake.

 

(c)        Bendera ya mezani itatumika pia na kuwepo mezani wakati   wa mikutano yote ya chama na wakati wa mazungumzo   baina ya CCM na chama au vyama vingine, mfano vyama rafiki na vya kidugu.

 

(d)       Bendera kubwa nyumbani kwa Kiongozi Mkuu na kwa           kuegesha ofisini mwake.

 


2.2.0 Bendera za Viongozi Wengine wa Chama Na Majengo Ya Ofisi za Chama

 

2.2.1  Bendera hizi zitakuwa na utepe wa manjano upande wa mlingoti tu. Hazitokuwa na urembo ule uliobainishwa kwa bendera za Viongozi Wakuu.

 

 

 

 2.2.2 Viongozi   wataostahiki kupeperusha bendera hizi kwenye meza      ofisini, magari, pikipiki na baiskeli ni hawa wafuatao:- 

 


 

(a)      Makatibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa wanaoongoza Idara   za Chama.

(b)               Wenyeviti na Makatibu Wakuu wa Jumuiya za CCM ngazi ya Taifa.

(c)                Wajumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM.

(d)               Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, Wenyeviti na Makatibu wa CCM wa Mikoa na Wilaya.

(e)                Wabunge na Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi wanaotokana na CCM.

(f)                 Makatibu wa CCM wa Majimbo, Kata/Wadi na Matawi.

 

 

2.2.3  Ofisi za Chama zitazostahiki kupeperusha bendera hizi ni za ngazi zote kuanzia Shina (yakiwemo Mashina ya Wakereketwa na Maskani) hadi Taifa.  Ofisi za Jumuiya za Chama na taasisi nyingine za Chama zitastahiki kupeperusha bendera za Chama za matumizi rasmi.

 

2.3.0      Vipimo Vya Bendera za Chama Kwa Ajili ya Matumizi Rasmi

         

          2.3.1  Bendera za Chama kwa ajili ya matumizi rasmi zitakuwa na vipimo                      vifuatavyo:-

 

 

AINA YA BENDERA KWA MUJIBU WA MATUMIZI

VIPIMO (milimita)

Urefu

Upana

1

Bendera za Mashina

1350

900

2

Bendera za ofisi nyingine zote za Chama, Jumuiya na Taasisi zake

1800

1200

3

Bendera za majumbani na kuegesha ofisini kwa Viongozi Wakuu

1800

1200

4

Bendera za mezani

220

150

5

Bendera za magari na vyombo vingine vya usafiri

300

200


 

 


2.4.0  Masharti ya Matumizi Rasmi ya Bendera:-

         

          2.4.1  Matumizi rasmi ya bendera ya CCM yataambatana na masharti yafuatayo:-

 

          (a)      Bendera ziwe za vipimo vilivyobainishwa.

 

          (b)     Zitundikwe kwenye milingoti rasmi.  Kwa Mashina ya majumbani zinaweza kutundikwa juu ya nyumba          husika kulingana na mazingira ya pahala.

 

          (c)      Kwenye magari, bendera zipeperushwe kwenye          mlingoti rasmi wa gari, usawa wa mkono wa         kushoto wa gari husika.     Bendera iondolewe au           kufunikwa isipepee mara tu kiongozi anapokuwa        halitumii kwa muda mfupi au mrefu gari hilo.

         

          (d)     Kiongozi anapoendesha mwenyewe gari asipeperushe           bendera ya matumizi rasmi.

 

          (e)      Ukiondoa bendera za kwenye magari ambazo   hazitopepea wakati kiongozi hayumo garini, bendera     nyingine zote za      CCM zitapepea wakati wote.            Isipokuwa kwamba, pale   ambapo bendera ya CCM   inapepea sambamba na bendera        ya Taifa, utafuatwa utaratibu wa bendera ya Taiufa wa kupandisha           na kushusha bendera.

 

2.5.0 Mtoaji wa Bendera

 

2.5.1  Bendera zote kwa matumizi rasmi zitatengenezeshwa na       kutolewa       na Makao Makuu ya CCM pekee na    zitatengenezwa kwa kutumia        vitambaa rasmi vilivyothibitishwa na Shirika la Viwango (TBS). Vitambaa hivyo ni Pantone 109C (Kijani) na Pantone 256 C (manjano).

 

3.0.0 MATUMIZI KWA AJILI YA UENEZI WA CHAMA

 

 

3.0.1  Bendera za CCM kwa ajili ya matumizi ya uenezi na hamasa hazitokuwa   na utepe  wala urembo wa aina yoyote.    Zitaweza kutumiwa na wanachama, wapenzi na mashabiki wa CCM           wakati wote ama kwa kupeperusha wenyewe mikononi,        kwenye baiskeli zao, pikipiki, magari, sehemu zao za kazi, za    mazungumzo, nyumbani  n.k.  Bendera hizi pia ndizo           zitakazotumika kwa ajili ya kupamba maeneo ya mikutano na         shughuli nyingine za Chama.

 

3.1.0    Masharti

 

3.1.1  Bendera hizi hazitohusika na masharti yote yaliyobainishwa kwa ajili ya matumizi rasmi, isipokuwa yale yaliyoainishwa kwenye Katiba ya CCM kwa mujibu wa Ibara ya 3.

 

3.2.0    Mtoaji wa Bendera

 

3.2.1  Bendera hizi zitaweza kutengenezeshwa na/au kutolewa na ofisi za CCM za Mikoa na Wilaya au kwa ruhusa/idhini za ofisi hizo.