MTAALA WA MAFUNZO YA ITIKADI KWA WANACHAMA

NA VIONGOZI WA CHAMA CHA MAPINDUZI

 

 

Wakati wa mfumo wa siasa wa Chama kimoja, Chama cha Mapinduzi kilikuwa na utaratibu wa kutoa mafunzo ya itikadi kwa wananchi waliopenda kujiunga nacho.  Wakati huo, hakuna aliyeruhusiwa kujiunga na Chama kama hakupitia mafunzo katika madarasa ya itikadi yaliyokuwa yakiendeshwa matawini.

 

Utaratibu huo uliachwa baada ya Tanzania kuingia katika mfumo wa siasa wa vyama vingi mwaka 1992.  Tokea wakati huo, wananchi wengi wamejiunga na Chama bila ya kuijua na kuielewa vyema misingi ya kiitikadi na kimaadili ya Chama Cha Mapinduzi.  Wapo miongoni mwa wanachama wa aina hiyo waliofikia hadi kuwa viongozi wa ngazi mbalimbali katika Chama na Serikali zake.

 

Taathira za hali hiyo zimeanza kujitokeza katika dalili za kumong’onyoka kwa misingi ya mshikamano wa kiitikadi miongoni mwa wanachama na viongozi.  Zimeanza pia kudhihirika dalili za kuporomoka kwa maadili.

 

Dalili hizo zilipoanza kujitokeza, Chama kilianzisha utaratibu wa kutoa mafunzo kwa njia ya warsha na semina kwa viongozi, hasa baada ya chaguzi za Chama.  Chama pia kilianza kuhimiza kufufuliwa kwa madarasa ya itikadi matawini ili kutoa mafunzo kwa wanachama, hasa wale wapya.

 

Wito kuhusu madarasa ya itikadi uliitikiwa kwa misisimko tofauti katika maeneo mbalimbali ya nchi kulingana na hamasa na utashi au mwamko wa viongozi.  Yako maeneo ambayo yamefufua madarasa, lakini pia yapo maeneo mengi tu ambako hukuti vuguvugu la madarasa ya itikadi.

 

 

 

 

Kwa upande mwingine, wito wa Chama kufufua madarasa ya itikadi haukufuatana na kutolewa kwa mtaala mahususi wa kitaifa wa mafunzo hayo.  Matokeo yake ni kwamba hata katika maeneo yalikofufuliwa madarasa ya itikadi, maudhui ya mafunzo yalitofautiana kulingana na utashi wa viongozi wa kila eneo.  Hali hii haiwezi kujenga mazingira ya mshikamano wa kiitikadi ndani ya Chama.

 

Ni katika jitihada za kuondoa dosari hii, ndipo zilipoanza juhudi za kutunga mtaala wa kitaifa wa mafunzo ya itikadi kwa wanachama na viongozi yatakayotolewa katika mdarasa ya itikadi nchi nzima.  Matokeo ya jitihada hizo ni mtaala huu unaoambatishwa na maelezo haya ya utangulizi.

 

Mtaala huu umepitishwa rasmi na Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama Cha Mapinduzi katika kikao chake cha tarehe 29-30 Aprili, 2006 kilichofanyika Dodoma.

 

Inatarajiwa sasa baada ya kupatikana kwa mtaala huu, vuguvugu la madarasa ya itikadi matawini na katika maeneo mengine ya uongozi wa Chama litafukuta nchi nzima.  Hilo likitokea, tutakuwa tumeweka utaratibu wa uhakika wa kuwajenga wanachama wetu kiitikadi na kimaadili katika mazingira ya sasa.  Kwa kufanya hivyo, tutajihakikishia zaidi kupata viongozi walioandaliwa kiitikadi na kimaadili.

 

Inawezekana.  Tutimize wajibu wetu.

 

 

Omar R. Mapuri,

KATIBU WA HALMASHAURI KUU YA TAIFA

ITIKADI NA UENEZI

CHAMA CHA MAPINDUZI

06/06/2006

 

 


MTAALA WA MAFUNZO YA ITIKADI KWA WANACHAMA

NA VIONGOZI  WA CCM

 

SOMO/MADA

VIPENGELE

MADHUMUNI

WALENGWA

REJEA

1. Historia ya

    CCM Tangu

    TANU na ASP

a) TANU

- Kuundwa kwake

- Malengo na madhumuni ya TANU

- Kuenea kwa TANU

- Kuelekea Uhuru

 

b) ASP

- Kuundwa kwake

- Malengo na madhumuni ya ASP

- Kuelekea Mapinduzi

- Misukosuko iliyokabiliana nayo ASP

- Uhuru wa Tanganyika, Mapinduzi ya    

  Zanzibar na Muungano wa

  Tanganyika na Zanzibar.

 

c) CCM

- Kuundwa kwake

- Madhumuni na sera za CCM

- Misukosuko iliyohimiliwa na CCM

Kuwaelimisha wanachama na viongozi umuhimu wa Historia ya CCM – kwamba CCM imetoka  wapi, iko wapi na inakwenda wapi.

Wanachama na Viongozi wa CCM

Historia ya CCM tangu TANU na ASP uk. 1-20 kwenye Kitabu cha Sera za Msingi za CCM

2. Katiba ya CCM

-Imani ya CCM

-Malengo na Madhumuni ya CCM

-Wajibu wa Mwanachama wa CCM.

-Haki ya Mwanachama wa CCM.

-Ahadi za Mwanachama wa CCM.

Kuwaelimisha wanachama wa CCM na Jumuiya zake, Imani, Madhumuni na malengo ya Katiba ya CCM.  Aidha ni vema viongozi na wanachama waelimishwe umuhimu wa kuzingatia Kanuni na Katiba ya CCM katika kutekeleza majukumu yao.

Wanachama wa CCM na Jumuiya zake.

Katiba ya CCM – Toleo la Mei 2005 Ibara –

4 (1-3)

5 (1-19)

14 (1-5)

15 (1-9)

- Nyongeza “A” ya Katiba ya   

  CCM 2005

 

SOMO/MADA

VIPENGELE

MADHUMUNI

WALENGWA

REJEA

3. Ujenzi wa

     Chama

-Kazi ya Chama ndani ya Chama

 

-Kazi ya Chama ndani ya jamii.

 

-Jumuiya za CCM kama kielelezo cha 

  Uhai wa Chama.

 

-Tathmini ya Uhai wa Chama katika

  Matawi na Mashina.

Kuwaelimisha wana-CCM umuhimu wa Uhai wa Chama kwa lengo la kushinda Uchaguzi

Wanachama na Viongozi wa CCM

- Programu ya CCM ya 1987-

  2002,  Sura ya 8

 

- Mwongozo wa CCM wa 1981

   Ibara 44-53

 

- Makala ya  “Ujenzi wa

  Chama” iliyotolewa katika   

  Semina za Halmashauri

  Kuu za Mikoa,

 Juni 14-  21,2003.

4. Sera za Msingi

     za CCM 

a) Azimio la Arusha

    -Siasa ya Ujamaa na Kujitegemea

    -Ujamaa na Maendelea Vijijini

    -Siasa ni Kilimo

    -Ushirika

    -Kila mtu mwenye uwezo wa kufanya

     kazi afanye kazi.  

Kuwaelimisha wanachama na Viongozi kwamba Ujamaa na Kujitegemea ndio chimbuko la sera za Msingi za CCM.

Wanachama na Viongozi wa CCM.

Katiba ya CCM Toleo la Mei 2005

- Azimio la Arusha

- Ilani ya Uchaguzi 2000-

  2005 na 2005-2010.

5. Mwelekeo wa

    Sera za CCM

    katika Kipindi    

    husika

- Kujenga Msingi wa Uchumi wa Kisasa    

  wa Taifa linalojitegemea.

- Mikakati ya Uwezeshaji wa Kiuchumi   

   wa wananchi katika kupambana na           

   umaskini.

-  Utawala bora na Madaraka

   ya wananchi.

- Chama Cha Mapinduzi na umoja wa           

  Kitaifa; Amani na Utulivu na Mapinduzi    

  ya uchumi.

- Vipengele vingine kwa mujibu wa   

  mwelekeo uliopo.

 

Kuwaelimisha wana-CCM na viongozi maudhui ya Mwelekeo wa Sera za CCM katika kipindi husika, mfano miaka ya 2000-2010.

Wanachama na Viongozi wao.

- Mwelekeo wa Sera za CCM

  Katika Miaka ya 2000-2010

  ukurasa wa 9-75 na

  mielekeo mingine ya sera

  kadri itavyotoka.

6. Utekelezaji wa

    Ilani za 

    Uchaguzi za   

     CCM         

- Maana ya Ilani

- Mafanikio ya Utekelezaji katika nyanja   

   za:-

- Ustawi wa Jamii; Elimu na Afya.

- Miundombinu, Huduma za Kiuchumi.

  Mawasiliano na Uchukuzi:

- Uchumi na Biashara

- Kilimo, Utalii na Madini

- Nishati na Maji

- Ulinzi na Usalama.

- Kero za wananchi

Kuwaelimisha wana-CCM na viongozi wao kuhusu Ilani kama zana ya kutafsiria sera za Chama katika vitendo katika kipindi fulani. 

Wanachama na Viongozi wao

- Taarifa ya Utekelezaji wa

  Ilani ya Uchaguzi katika

  Halmashauri za Wilaya na

  Kata/Wadi katika kipindi

  husika.

 

- Taarifa ya Utekelezaji wa

  Ilani ya Uchaguzi ya CCM

  katika kipindi husika.

7. Demokrasia 

    katika Mfumo

    wa vyama

    vingi vya

    siasa.

- Umuhimu wa demokrasia katika nchi

  yetu.

- Kujikosoa na kukosoana.

- Mashindano ya vyama katika kuwania

  dola.

- Kupingana bila kupigana.

Kuwaelimisha wana-CCM na viongozi umuhimu wa kutumia demokrasia kama chombo cha kutwaa madaraka ya dola

Wanachama na Viongozi wa CCM.

-Tujielimishe

 

-Mwongozo wa CCM wa                  

  1981, Sehemu ya Pili

 

- Elimu ya Uraia.

 

8. Wanachama

    kama Askari  

    wa Mstari wa

    Mbele wa  

    harakati za

    Mapambano

    wakati wa 

    Uchaguzi.                

Majukumu/Nafasi ya Mwanachama wa CCM/Jumuiya wakati wa Uchaguzi katika:-

(a) Kushiriki kumpata Mgombea Mzuri.

(b) Umuhimu wa kupiga kura –

     kumchagua mgombea wa CCM.

(c) Kuhamasisha wapenzi wa CCM

     kutunza shahada kisha kupiga kura                             

     kumchagua mgombea wa CCM.

(d) Kushiriki kufanikisha kampeni za CCM.

(e) Kufichua njama/hila za wapinzani.

 

Kuwawezesha wanachama wa CCM na Jumuiya zake kuelewa nafasi na majukumu yao katika kuipatia CCM ushindi.

Wanachama wa CCM na Jumuiya zake.

1. Mwongozo wa CCM wa

    1981.

              

2. Kanuni za Utendaji Kazi

    Katika Chama Ndani ya

    Mfumo wa Vyama Vingi

    vya Siasa Sura ya 2.

 

SOMO/MADA

VIPENGELE

MADHUMUNI

WALENGWA

REJEA

9. Miiko na Maadili ya    

    Uongozi

-Maadili ya wanachama na viongozi

-Miiko ya uongozi

-Uadilifu katika kutafuta uongozi.

-Vita dhidi ya rushwa

-Vita dhidi ya hulka ya kujilimbikizia mali kwa kutumia madaraka

Kuwaelimisha wanachama na viongozi wa CCM na Serikali zake kuhusu wajibu wao wa kupambana na hulka na vitendo vya kukiuka miiko na maadili

Wanachama na viongozi wa CCM na Jumuiya zake na wa Serikali zake.

1. Azimio la Arusha.

 

2. Mwongozo wa CCM

     wa 1981.

 

3. Katiba ya CCM

 

4. Kanuni za Maadili za CCM

10. Utandawazi

-Maana ya Utandawazi

-Historia ya Utandawazi

-Wadau wa Utandawazi

-Athari za Utandawazi

-Mikakati ya kukabiliana

  na utandawazi.

Kuwaelimisha wanachama wa CCM na Jumuiya zake, hali halisi ya mwenendo wa Dunia ya leo – kisiasa, kiuchumi na kijamii.

- Wanachama wa CCM

    na Jumuiya zake.

- Sera za Msingi za  

   CCM  Uk. 36-37.

 

 

Umetolewa na Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama Cha Mapinduzi, Aprili, 2006