MAAMUZI YA ZANZIBAR, 1991
HOTUBA YA MWENYEKITI WA CCM, RAIS ALI HASSAN MWINYI WAKATI AKIZUNGUMZA NA WAZEE WA CHAMA,
VIONGOZI WA TAIFA, MASHIRIKA YA UMMA NA WATU BINAFSI JUU YA UFAFANUZI WA
MAAMUZI YA HALMASHAURI KUU YA TAIFA KATIKA KIKAO CHAKE CHA
Ndugu Mwenyekiti wa Chama Cha
Mapinduzi, Mkoa wa
Ndugu Katibu Mkuu,
Ndugu Mwenyekiti wa Wazee wa
Ndugu Viongozi wa Chama na
Serikali na
Ndugu zetu waalikwa,
Kabla ya yote, labda niseme kwamba kwa
kuwa tumo katika mwezi wa pili tokea kuanza kwa mwaka mpya, nami sijapata
nafasi ya kukutana nanyi wazee, na vyema nitumie nafasi hii kwanza kukutakieni
heri ya mwaka mpya, na baraka zote za mwaka 1991. (Makofi).
Ninakuombeeni uzima, nguvu, baraka na mafanikio.
Pili, tuna kawaida katika nchi yetu,
kwamba kila linapotokea jambo muhimu katika Taifa, tunatafuta nafasi ya
kukutana nanyi na kukuelezeni. Hivyo,
leo napenda kuzungumza nanyi wazee wa dar es Salaam na, kupitia kwenu, iwe ninazungumza
na Wazee wenzenu wa
Hivi karibuni Halmashauri Kuu ya Taifa
ilifanya kikao chake cha kawaida
LAZIMA TWENDE NA WAKATI
Inaelekea kuna hofu kwamba Azimio la Arusha linageuzwa. Kwa hiyo, tokea mwanzao, kabla ya kusema
lolote, nataka tuelewane kwamba siasa
yetu bado ni ile ile ya Ujamaa na Kujitegemea.
(Makofi). Haikugeuka wala hatutazamii kuigeuza. Kwa hali
yoyote sisi Wanachama wa Chama Cha Mapinduzi hatutaigeuza Siasa
hii. (Makofi)
. Kule Zanzibar tulizungumza mambo
mengi, miongoni mwao, ni kutoa tafsiri ya baadhi ya vipengele vya Azimio ili
vifanane na wakati tulionao.
Azimio la Arusha,
Kwa hivyo ni dhahiri kwamba jamii ya
Tabia ya wakati ni
Hapa Afrika, kwa
mfano, imeanzishwa mipango mbalimbali ya ushirikiano wa uchumi. Mipango hiyo ni pamoja na Ushirikiano wa Nchi
za Kusini mwa Afrika (SADCC) na Eneo la Soko Nafuu (PTA). Afrika pia imeazimia kuunda Jumuiya ya
Uchumi. Nchi zinazoendelea nazo
zimedhamiria kuzidisha ushirikiano miongoni mwao. Nchi yetu lazima ifanye mabadiliko ili iweze
kushiriki kwa ukamilifu katika shughuli zote hizo zinazosaidia maendeleo yetu.
KILA
Ndugu Wazee, Msahafu
wa Waislam unasema ‘LIKULLI AJALIN KITABU” Mwingereza mmoja kaitafsiri aya hiyo
hivi: ‘ TO EVERY AGE ITS BOOK” yaani “Kila zama ina Kitabu (Mwongo) chake”. Na sisi Wana-CCM tunakubali kuwa “kila
Mojawapo ya malengo
ya maamuzi ya
Mwaka 1967
lilitangazwa Azimio la Arusha. Mwaka
1971 ulifuatiwa na tamko la Iringa la “Siasa ni Kilimo”. Tamko hili lilikuwa ni mbinu na msisitizo wa
Siasa yetu ya Kujitegemea. Zlilipanua
tafsiri ya Azimio la Arusha. Katika
mwaka 1981 ilionekana kuna haja ya kutolewa mwongozo mwingine kulingana na
wakati ule ambao nao ni upanuzi wa tafsiri ya Azimio. Ulitangazwa ili kukidhi haja ya wakati ule.
Aidha, kabla ya
hapo, katika mwaka 1974, Chama kilipitisha Agizo la Musoma kuhusu Elimu ya
Kujitegemea ambalo madhumuni yake yalikuwa kutazama upya suala la uingizaji
wanafunzi Chuo Kikuu na kupanua Elimu ya Msingi ili kutoa fursa kwa watoto wote
wenye umri wa kwenda shule kufanya hivyo.
Maandiko yote hayo
hayakupingana na Azimio la Arusha ila yakiongeza mwangaza kwa mambo ambayo
yalihitaji yafanane na wakati wake. Na
lazima iwe hivyo, kwani bila ya kwenda na wakati tungechekesha.
Kwa mfano
wakati wa Azimio la Arusha, mtakumbuka
kuwa tafsiri ya neno Kiongozi ni pamoja na yule mwenye mshahra uliofikia
shilingi 1,066/= kwa mwezi. Tungeng’ang’ania tafsiri hii tu, basi leo pasingekuwapo
wafuasi. Wafanyakazi wote wangetafsirika
kuwa ni viongozi wa CCM. Kwani ukiacha
wakulima wafanyakazi wote sasa kwa tafasiri ya 1987 ni viongozi tena maradufu. Maana kima cha chini sasa ni Sh.2,500/=,
ambazo ni zaidi ya mara mbili ya Sh.1,066/=.
Ndiyo maana tukasema jamii yetu italazika Kufanya marekebisho kila inapokuwa lazima
kufuatana na wakati. Tutafanya hivyo
bila ya kuachana na misingi ya siasa yetu.
Kwa hivyo,
tulichokifanya kule
CHIMBUKO LA AZIMIO LA ARUSHA
Historia ya Azimio la Arusha tunaijua
sote. TANU ilipigania kwa maneno mpaka
nchi ikapata UHURU wake.
Tabia hiyo ilizusha
manung’uniko ya watu. Jamii ilianza
kugawanyika makundi mawili; manaizi na makabwela. Kitendo hicho ndio chimbuko la kutangazwa kwa
Azimio la Arusha. Azimio lilikuja kutoa
mwongozo wa maadili ya wanachama na viongozi wa TANU. Kwa hivyo nia ya Azimio la Arusha, miongoni
mwa mambo mengine, ilikuwa ni kuwazuia viongozi kutumia uongozi wao
kujitajirisha.
ATATIZO LA SASA NI UCHUMI TEGEMEZI
Mtu anaweza kuuliza
je sasa kuna tatizo gani? Tatizo letu
katika miaka ya tisini na kuendelea ni lile la uchumi tegemezi. Tatizo letu sasa ni kwamba uchumi wetu ni
duni mno. Wakati idadi yetu inaongezeka,
mapato ya Taifa, hasa ya fedha za
kigeni, hayaongezeki. Wakati wa Uhuru
idadi yetu ilikuwa ni watu milioni tisa.
Lakini leo, tuko milioni tisa na tisa tena na nusu ya tisa. Lakini mapato yetu ya pesa za kigeni yapo
pale pale, $ milioni 400. Wakati Azimio
la Arusha lilitutaka tujitegemee, hali halisi ni kuwa tumekuwa wategemezi
wakubwa. Maana Taifa letu hizi sasa, kwa
pato
MBINU ZA KUJITEGEMEA
Ilani ya Uchaguzi
inasema hivi:
“Makusudi
ya Chama katika kipindi cha miaka mitano ijayo ni kwa Taifa kukusanya nguvu
zote za wananchi kwa kusaidiana na Serikali zao (Mbili), na kuzitumia katika
kila eneo la maendeleo ili kutoa msukumo mpya wa utekelezaji wa siasa ya Ujamaa
na Kujitegmea”.
Hivyo, Chama na Serikali zake zinawajibika kuwarahisishia wananchi wao kujitegemea kwa
chakula, kujitegemea kwa mavazi na kujitegemea kwa malazi. Ili kutimiza lengo
Je wananchi wakituuliza: hivi ni mbinu
gani mlizofanya kumshirikisha kila mmoja wetu kutumia nguvu zake zote katika
kuzalisha
“Mimi sikuweza kutumia nguvu zangu
zote katika kufanya kazi ya kuzalisha kwa sababu nimezuiwa na Azimio la
Arusha.”
MWANACHAMA KUCHANGIA UCHUMI
KIKAMILIFU
Azimio la Arusha
lipo. Narudia tena kusema kuwa
wanaohusika na tafsiri hii ni wanachama. Sisemi Viongozi, bali wanachama wa
CCM. Tunataka kumpa Mwanchama wa CCM,
kama mwanachama mwingine yeyote, uhuru zaidi wa kuzalisha ili kuchangia kadiri
ya uwezo wake katika pato
Ili tujitoe,
kitaifa, kwenye shimo la utegemezi tulimo hivi sasa, mbinu bora ni kutoa
uhuru kwa kila mwananchi wa kila Kaya,
wa kila Kata, wa kila Tarafa, wa kila Wilaya na wa kila Mkoa kutumia nguvu zake zote katika
kuzalisha. Matokeo ya hatua hii ni
kumwezesha kila mtu katika Kaya, Kata, Tarafa, Wilaya na Mkoa kujigemea. Tukifika hapo ndipo Taifa litapokuwa
limeondokana na hali ya sasa ya uchumi tegemezi.
KUPANGISHA NYUMBA
Jambo la kupangisha
nyumba nalitaja tu, kwani si lazima kwa sababu si jipya; hata hivyo ni vyema
nalo litajwe. Mwenyekiti Mstaafu alilisemea jambo hili mahali pengi
“Nasharti
hayo yanamkataza kiongozi wetu kuishi kikabaila kwa mbinu za kupangisha majumba.
Lakini
sharti hili halimkatazi mtu mwenye vyumba vya ziada katika nyumba yake anamoishi kuvipangisha kwa watu wengine
kwa kodi nafuu, Hili ni jambo la kawaida kabisa katika nyumba zetu za
“Waswahili”’ na upangishaji huu mimi nimekuwa
nikiutetea tangu zamani. Utaratibu
huu unawasaidia
Ni kweli kwamba huko nyuma
tumekuwa wakali mno
katika kutafsiri msharti haya.
Azimio la Arusha
linachokataa ni unyonyaji. Hivyo maskini
ya Mungu mwenye kijumba chake cha mbavu za mbwa akimwona maskini mwenziwe
anapata taabu, hana pakukaa, asimpangishe?
Je akimpangisha atakuwa anamnyonya?
Au anamstiri? Kwa hiyo tangu
zamani kustiriana ni ruhusa (Makofi).
Hatukuishia hapo
kule
Sisi tunaamini
kwamba baada ya kipindi kirefu cha utumishi, mtu aweze kuwa na nyumba ili, hata
akiwa kipofu angalau aweze kupapasa kuta zake na kusema: Hii ni nyumba
yangu niliyoipata kwa jasho langu la
kazi ya miaka 30. Tunataka awe na
kitu. Lakini, Ndugu Wazee, bahati nzuri
wanachama wa CCM,
Vinginevyo tutakuwa
tunamfanyia mzaha mtu huyo. Maana
atachukua mkopo, ajenge nyumba, kisha ashindwe kulipa huo mkopo. Waliomkopesha wataikama hiyo nyumba na kuiuza
ili kurudisha fedha
Kwa hivyo Ndugu
Wanachama, huko ndiko kwenda na wakati, vinginevyo tutapwelewa. Mtu kama huyu aruhusiwe kupangisha nyumba
yake, iwe nusu ya nyumba, ama robo ya nyumba au yote: (makofi).
BIASHARA YA KUPANGISHA MAJUMBA
BADO NI MWIKO
Lakini kikao cha
Vile vile,
Mwanachama wa CCM, hata akiwa kiongozi katika mazingira maalum, aruhusiwe kukodisha nyumba yake, ikiwa haihitaji
kuikaa wakati ule. Inawezekana haihitaji kuishi katika nyumba
yake kwa kuwa kapata uhamisho. Mfano,
mtu kahamishiwa Iringa kwa kazi wakati nyumba yake iko
Ni mwanachama wa
aina hii ndiyo tulisema huko
HISA KATIKA MAKAMPUNI YA UMMA, KUPUNGUZA
UKWASI!
La pili
lililoamuliwa huko
Mfano kuna mwananchi
mmoja alikwenda kwenye kiwanda cha Umma kutaka huduma ya kusafishiwa ngozi
zake. Alipofika hapo alikuta “pamelala
paka” Yaani palikuwa kimya, hapakuwa
na kazi yoyote inayofanyika. Kumbe kile
kiwanda kilikuwa kimefungwa kwa kukosekana fedha za kukiendeshea ...........
umeme ulikatwa na wafanyakazi walipewa likizo.
Meneja alimfahamisha
huyo mteja kuwa kiwanda kimefungwa kwa sababu ya deni la maji na umeme pamoja
na pesa za mishahara ya wafanyakazi.
Huyo mteja alikubali kulipa arubuni (advance ) ya milioni saba ili
kukikwamua kiwanda. Wiki ya pili yake
kiwanda kilianza kufanya kazi zake za kuzalisha
Kisa cha kiwanda
hicho kusimama kazi ni kukosa fedha za kuendeshea. Kiswahili cha siku hizi huitwa ukwasi. Kwa hiyo kazi ilisimama.
Katika hali
UBIA WA UMMA NA DOLA KATIKA
SHIRIKA
Narudia,
watakaoruhusiwa kununua hisa ni wananchi wowote watakaopenda pamoja na wakulima
wa pamba, korosho, kahawa, tumbaku na wafanyakazi wa
Endapo shirika la
umma litataka kuwashirikisha wananchi na wafanyakazi wake kwa kulichangia ili
kuondoa tatizo la Ukwasi, jambo
Katika sera ya
uwekezaji rasilimali tunaruhusu ubia
katika uchumi wetu. Ubia huo
unaweza kuwa baina ya watu wa ndani ya
nchi peke
WAFANYAKAZI KUSIMAIA UWAJIBIKAJI
Nia nyingine ya
kufanya hivyo inatokana na kutambua kuwa wafanyakazi wenye hisa katika kiwanda
watakuwa wasimamizi wakereketwa wa uwajibikaji katika viwanda hivyo. Watakereketwa zaidi pakiwa na ubadhirifu au
kutowajibika.
Hivi leo baadhi ya
mashirika ya Umma ni mashirika ya umma kwa jina tu. Watu wanayaibia wakidai wanachukua chao. Pengine wanashindana kufanya hivyo ili
wasipunjwe. Baadhi ya mashirika ya Umma
yanahujumiwa kana kwamba hayana wenyewe.
Baada ya maamuzi ya
MWONGOZO WA 1981 KUHUSU UWAJIBIKAJI
Maamuzi ya
“Imezuka
tabia ya aibu nchini ambayo imekuwa ikiongezeka ya vitendo vya kuharibu na
kuvitumia vibaya vyombo muhimu vya kazi na
Lakini ikiwa watu pale pale wenyewe wana hisa katika
kampuni au shirika - mfano - TANESCO kuwa Mkurugenzi katika kampuni ya
Kibepari. Napenda suala hili lieleweke vizuri ili kujibu fikra
zilizojengeka kuwa uamuzi huo umevunja Azimio la Arusha.
Lakini kuna
Mkurugenzi wa aina nyingine ambaye ni tofauti kabisa na Mkurugenzi mwenye
Azimio la Arusha
bado lilo pale pale kwa wale wakurugenzi wa aina ya kwanza. Wao Azimio linawabana, hawawezi kuwa wanachama wa CCM. Lakini huyu wa aina ya pili aliyeajiriwa tu,
akija kuomba uwanachama tunamkubali.
Azimio la Arusha kamwe halijamkataa
mfanyakazi mwenziwao kwa “koa” la kutumikia Kampuni ya Kibepari, hivyo ndivyo
tulivyoamua
MWANA
- CCM KUWA NA HISA KATIKA KAMPUNI YA KIBEPARI
Jambo jingine ambalo
halikueleweka vizuri na linahitaji ufafanuzi ni lile la kumruhusu mwanachama wa
CCM kuwa na hisa katika kampuni ya Kibepari.
Hili nalo tumeliruhusu huko
Ni vyema
kukumbushana kuwa yapo makampuni ya kibepari ambayo tumekuwa nayo hata kabla ya
Azimio la Arusha. Kampuni hizo zimekuwa
zikidhi kiasi fulani cha ajira ya Watanzania, pamoja na Wanachama wa CCM.
Ni jambo hili
lieleweke vizuri, nitatoa mfano tu wa Kampuni ya mtu binafsi. Mwenye Kampuni ya binafsi anaweza kabisa akaamua kwa hiari yake kuuza baadhi
ya hisa kwa wafanyakazi wake ili
kuwapa motisha ya kazi Tajiri yeyote akiamua kufanya hivyo, Chama na Serikali
vitamwona kuwa amechukua hatua ya kimaendeleo.
Kitendo chake hicho ni halali.
Kwa sababu itakuwa ameuzimua ubepari kwa kuifanya kampuni yake ni ya
ubia kati yake na wananchi aliowaajiri.
Kwa kweli kampuni hiyo itakuwa
Katika hali hiyo,
hata Mwanachama wa CCM anaruhusiwa kupokea/kununua hisa alingane na wafanyakazi
wenzie.
Ni mazingira maalum
ya namna hii tu ndiyo yanayoruhusu Mwanachama wa CCM,
MISHAHARA MIWILI KWA MWANA-CCM
Kuhusu mishahara
miwili, Azimio la Arusha linasema hivi:
“Kwamba
kila mtu anayo haki ya kupata malipo ya haki kutokana na kazi yake”.
Kufuatana na ukweli
huo, anayefanya kazi mbili za halali anastahiki kupata malipo ya kazi ya
pili. Tuchukue mfano wa Profesa ambaye
mchana kutwa anasomesha Chuo Kikuu.
Baada ya saa za kazi anaweza kuamua kufanya azi ya akili, kwa mfano
kutoa ushauri au kuandika mradi kwa aliyemwomba huduma hiyo.
Mwanachama huyo
atastahiki kupata malipo ya kazi hiyo.
Hili si geni, katika sherehe za kuadhimisha miaka 20 ya Azimio la
Arusha, baba wa taifa alisema hivi:
“Lile
sharti la kutopokea mishahara miwili kwa kweli ni sharti la tahadhari tu. Ni vigumu
Jambo la msingi ni
kwamba lazima twende na wakati. Mwaka
1987 lilipotungwa Azimio la Arusha ilikuwa hakuna haja ya kuwa na mishahra au
malipo ya kazi zaidi ya moja kwa sababu wakati ule mshahara mmoja ulikuwa
unatosha kukidhi mahitaji yote muhimu.
Kwa mfano, mimi, mwenyewe,
mshahara wangu wakati ule ulikuwa shilingi 2,200/= kwa mwezi. Mshahara huo, hasa kwa
Wazee wangu
watakumbuka kwamba wakai ule kule kitunguu, pilipili na bizari -yote hivyo kwa
senti tano tu. Ilikuwa inawezekana pia
kununua samaki mkubwa kiasi kwa senti
ishirini mpaka 50 tu; au kununua kuni za kuweza kupikia mlo mzima kwa senti
kumi tu.
Siku hizo
iliwezekana mnunuzi kujaziwa mafuta ya kupikia au samli kikombe kizima kwa
senti ishirini hasitini tu.
Halikadhalika kwa senti ishirini tu mtu aliweza kununua matunda,
Katika hali hiyo, kulikuwa hakuna ulazima wa
kufanya kazi ya pili. Afanyae kazi zaidi
ya moja huonekana ni mlafi au ana tamaa.
Kwa mshahara huo huo niliweza kudunduliza pesa na mwishowe kununua gari
mpya kabisa. Gari
HALI IMEBADILIKA
Lakini leo mambo yamebadilika. Gharama ya maisha imepanda san. Serikali yenyewe imeungama waziwazi kuwa
haina uwezo wa kumlipa mfanyakazi wake mshahara unaomwezesha kumudu gharama za maisha. Kutokana na hali hiyo, wafanyakazi wengi,
wanashindwa kukidhai mahitaji
KOFIA MBILI MSHAHARA MMOJA
Lakini lazima
tuelewane kuwa hii mishahara miwili tunayozungumzia haimhusu kiongozi mwenye
kofia mbili. Kwa mfano, Mkuu wa Mkoa na
Mkuu wa Wilaya, ambao vile vile ni Katibu wa Chama wa Mkoa au Wilaya,
hawaruhusiwi kupokea mishahara miwili.
Hawa watalipwa mshahara mmoja tu, maana hii kazi ya pili ni sehemu tu ya
ile ya kwanza. Lakini wanaruhudiwa kufanya kazi za ziada kama vile
kilimo, ufugaji na kadhalika, baada ya saa
za kazi,
MWANA-CCM MKULIMA NA MFUGAJI
Watanzania wengi ni wakulima, wakulima ndio wengi
zaidi. Mkulima kwa maana pana ni pamoja
na mfugaji. Katika siku za nyuma, baadhi
ya wanachama waliwahi kutiwa msukosuko
kwa kuwa na mashamba makubwa au kufuga
kuku 500. Lakini baadaye Chama
kilijisahihisha
“Chama
Cha Mapinduzi ni Chama kinachokua (haikudumaa).
Kinakaa katika nadharia na falsafa yake, (ili kwenda na wakati)”.
Hii ndio
ilivyokifanya Chama kijisahihishe kila kinapokosea.
Kwa hiyo
class=Section2>
Kuhusu ufugaji, kuna
baadhi ya wenzetu katika makabila ya
Huko Zanzibar
tulifikria labda tuweke kiwango maalum
cha mifugo,
Hiyo ndio hali
halisi iliyotufanya tukubaliane kuwa mfugaji yeyote anaetaka kuwa
mwanachama bila ya kujali idadi ya
mifugo yake. Mwenye mshahara mkubwa,
vile cvile hata wa malaki, maadam ni mshahara wa kazi halali, naye pia
aruhusiwe kuwa mwanachama wa CCM.
MAFUNZO YA MIEZI MITATU
BIASHARA NDOGO NDOGO
Huko Unguja
hatukuishia hapo. Tuliamua kuwa Mwanachama wa CCM wa kawaida naye pia
aruhusiwe kuwa na biashara ndogo ndogo ili kumwongezea kipato. Biashara hizo, ambazo sharti zifanywe baada
ya saa za kazi, ni pamoja na uvuvi, kuwa na gari ndogo au pick-up ya kukodisha
kwa kuchukulia abiria au mizigo, kushona, kusindika matunda, mafuta na mashine
ya kukoboa au kusaga unga.
Mwanachama mwenye
mashine ya kusaga unga hanyonyi bali anatoa huduma kwa jirani zake
kijijini. Chama na Serikali vimo mbioni
kuhimiza na kutafuta teknolojia ya kumrahisishia kazi Mtanzania, hasa
wanawake. Ni vyema kukaribisha
teknolojia ya kuwasaidia wanawake waondokane na kufanya kazi ngumu ngumu
zinazoweza kuwapotezea wakati na kuathiri afya zao,
Ndugu Wazee, haya
kwa muhtasari ndio yaliyoamuliwa
Mshairi mmoja
amesema:-
“Kutaraji
uongofu bila kupitia njia zake ni
jahazi kutembea nchi kavu”
Ndugu Wazee
Ahsanteni