| | |||||||||||||||||||||
| | |||||||||||||||||||||
| Uchaguzi Mkuu wa CCM wa mwaka 2002 ulikuwa halali na wa mafanikio makubwa | |||||||||||||||||||||
| Walioshindwa wakubali kwamba kuna kushinda na kushindwa katika uchaguzi | |||||||||||||||||||||
| Katika mkutano wake wa mwezi uliopita wa Septemba, Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM miongoni mwa mengine ilipokea taarifa ya Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa kuhusu maamuzi iliyofanya baada ya kusikiliza na kuyajadili malalamiko yaliyotolewa na baadhi ya wagombea wa nafasi mbali mbali za uongozi katika ngazi ya Mkoa katika Uchaguzi Mkuu wa CCM uliofanyika mwaka jana (2002). Kamati Kuu haikupata lalamiko hata moja kuhusiana na uchaguzi wa Ngazi ya Taifa uliofanyika Chimwaga mwezi Oktoba, 2002. Kuhusiana na chaguzi za Ngazi ya Mkoa, Kamati Kuu ilipokea malalamiko kutoka Mikoa ya Arusha, Dar es Salaam, Iringa, Kagera, Mara, Mbeya, Mwanza, Rukwa na Singida. Kwa jumla, malalamiko mengi yalijikita juu ya tuhuma za rushwa. Walalamikaji na walalamikiwa wote walipewa fursa ya kutosha ya kujieleza katika vikao husika na Kamati Kuu yenyewe kupitia Kamati ya Maadili ya CCM ilifanya uchunguzi wa kina wa kila tuhuma katika kipindi cha karibu mwaka mzima. Lakini hakuna hata tuhuma moja iliyothibitika. Kilichobainika kwa malalamiko yote ni uchungu tu wa kushindwa ulioambatana na ugumu wa kukubali kushindwa. Lakini hayo ndiyo maisha katika ushindani wowote; kuna kushinda na kushindwa. Kwa hiyo, uamuzi wa Kamati Kuu ni kwamba matokeo ya uchaguzi yaliyotangazwa katika mikoa yote iliyolalamikiwa ni halali na yanabaki yalivyo. Kwa mujibu wa Ibara ya 29 ya Kanuni za Uchaguzi wa CCM, uamuzi huo ni wa mwisho. Halmashauri Kuu ya Taifa imeridhika kwamba si uchaguzi wa ngazi ya Taifa tu ambao haukuathiriwa na rushwa, bali pia hata chaguzi za ngazi ya Mkoa. Kwa hivyo, Halmashauri Kuu ya Taifa imeungana na kauli ya Mwenyekiti wa CCM, Mheshimiwa Rais Benjamin Mkapa aliyoitoa katika hotuba yake ya ufungaji wa Mkutano Mkuu pale Chimwaga ambapo aliutangaza uchaguzi mkuu wa Chama kuwa na mafanikio makubwa. Kwa maneno yake Mwenyekiti, "mafanikio hayo makubwa yameonyesha pia kuwa CCM si mali ya mtu, ni mali ya watu, ambao ni wanachama." Halmashauri Kuu ya Taifa imeridhika | 2005. CCM inawataka wanachama wake na wananchi wote kwa jumla wasimame kidete kufichua vitendo vya kweli vya rushwa (siyo dhana tu), lakini wasikubali kuingizwa katika mtego wa mikakati ya uchaguzi ya wapinzani. | ||||||||||||||||||||
| pia kwamba mjadala kuhusu rushwa ndani ya Chama ambao umekuwa ukikuzwa sana na magazeti na vyombo vingine vya habari kwa kiasi kikubwa ni mkakati tu wa wapinzani wa CCM kukichafulia jina Chama wakati wakijiandaa kwa Uchaguzi Mkuu wa | |||||||||||||||||||||
| Buriani Mzee Ibrahim Raha Jongo | |||||||||||||||||||||
| · CCM itakukumbuka daima | |||||||||||||||||||||
| Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, Mzee Ibrahim Raha Jongo (66) amefariki dunia tarehe 29/8/2003 usiku mjini Dar es Salaam. | alimueleza marehemu kuwa alikuwa mtu wa watu na ni mtu aliyetoa mchango mkubwa sana wakati wa kampeni za Uchaguzi Mkuu wa Serikali wa mwaka | ||||||||||||||||||||
| | |||||||||||||||||||||
| Enzi za uhai wake, Mzee Jongo akiwa jukwaani huko Shinyanga akiifanyia kampeni CCM | |||||||||||||||||||||
| 1995 na 2000. Marehemu alishika nafasi mbalimbali za uongozi ndani ya CCM na katika Jumuiya ya CCM ya Wazazi. Mzee Jongo alikuwa Mjumbe wa NEC tangu mwaka 1997 hadi umauti wake ulipomfika. | |||||||||||||||||||||
| Mzee Jongo ambaye alifariki dunia katika Hospitali ya Tumaini ambako alikuwa amelazwa kutokana na kusumbuliwa na afya yake alizikwa tarehe 31/8/2003 kijijini kwake Chamazi, katika Wilaya ya Temeke mkoani Dar es Salaam. Katibu Mkuu wa CCM, Ndugu Philip Mangula aliongoza maelfu ya viongozi wa CCM, Serikali na wanachi kwenye mazishi ya Mzee Jongo ambaye alizikwa kwa heshima zote za Chama. Katika salaam zake za rambirambi kwa niaba ya Halmashauri Kuu ya Taifa, wanachama wa CCM na wananchi kwa ujumla, Ndugu Mangula aliusifu mchango wa marehemu kwa kutumia kipaji chake cha usanii katika kukitetea na kukiimarisha Chama. Aidha, Katibu Mkuu wa CCM | |||||||||||||||||||||
| | |||||||||||||||||||||
| Marehemu Mzee Jongo | |||||||||||||||||||||
| | ||||||||||||||
|
| ||||||||||||||
| | ||||||||||||||
| Tuna kila sababu ya kujivunia Mkapa na Karume kwani | ||||||||||||||
| Mkapa ana uwezo mkubwa wa uongozi Karume ameirejeshea heshima Zanzibar | utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2000-2005. Katika hotuba hiyo ambayo imechapishwa katika ukurasa wa pili wa jarida hili , Mwenyekiti alitoa changamoto kwa viongozi na wanachama wa CCM kuwa mstari wa mbele kutetea rekodi nzuri ya Chama na Serikali zake badala ya kuwaachia wapinzani wanaojaribu kupuuza au kukebehi rekodi hiyo, usahihi wa Sera za CCM na umakini wa utekelezaji wake. Halmashauri Kuu ya Taifa imempongeza pia Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Amani Abeid Karume kwa kazi nzuri anayoifanya Zanzibar ambayo matunda yake yanaonekana. Uchumi wa Zanzibar hivi sasa umekua kutoka aslimia 3.2 mwaka 2000 hadi asilimia 5.6 mwaka 2002. Mfumko wa bei umeshuka kutoka aslimia 6.2 mwaka 2000 hadi kufikia aslimia 5.2 mwaka 2002. Miundombinu hasa ya barabara na mawasiliano pamoja na shule imekuwa bora zaidi hivi sasa kote Unguja na Pemba na mabadiliko yanaonekana kwa kila mtu. Tangu Serikali ilipozundua mpango wa kupunguza umaskini mwezi Mei 2002 imekuwa ikiweka mkazo mkubwa katika uimarishaji wa sekta ya elimu, mawasiliano, afya na maji. Aidha, Rais Karume ameirejeshea Zanzibar heshima mbele ya Jumuiya ya Kimataifa kama inavyodhirishwa na kurejeshwa kwa misaada ya wahisani. Kutokana na mafanikio hayo makubwa, Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM imezipongeza Serikali zote mbili, yaani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na ile ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa kutekeleza vizuri Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2000 na kuwataka Watanzania wajivunie mafanikio hayo. Pia Serikali zote mbili zimepongezwa kwa juhudi zake za kuondoa kero mbali mbali za wananchi. | |||||||||||||
| Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama Cha Mapinduzi iliyokutana mwezi Septemba ilijadili kwa kina miongoni mwa mengine, hali ya kisiasa nchini. Kwa jumla, Halmashauri Kuu ya Taifa imeridhika na hali ya amani na utulivu wa nchi ukiondoa matukio ya hapa na pale ya uhalifu. | mpango wa kuzifuatia madeni nchi maskini duniani (HIPC). (2) Tanzania hivi sasa inapokea misaada mingi na mikubwa ya wahisani kuliko wakati mwingine wowote; na tena misaada hiyo inaingizwa moja kwa moja katika bajeti ya Serikali ukiwa ni ushahidi wa kutosha wa jinsi wahisani | |||||||||||||
| | ||||||||||||||
| Mwenyekiti mpya wa SADC, Rais Mkapa akivishwa beji baada ya kukabidhiwa madaraka hayo na Rais Dos Santos wa Angola. | ||||||||||||||
| Halmashauri Kuu ya Taifa imempongeza kwa dhati Mheshimiwa Benjamin William Mkapa, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi kwa kuchaguliwa kuwa Mwenyekiti wa SADC kwa mwaka 2003/2004. Imempongeza pia kwa kufanikisha kwa kiwango kikubwa Mkutano wa Wakuu wa Nchi za SADC uliofanyika Mjini Dar es Salaam tarehe 26-27 Agosti, 2003. Halmashauri Kuu ya Taifa imeendelea kumpongeza Rais Mkapa kwa uwezo wake mkubwa wa uongozi ambao umeijengea heshima kubwa Tanzania na Chama Cha Mapinduzi ndani na nje ya nchi yetu. Rais Mkapa amejibainisha waziwazi kwa sasa kuwa tegemeo kubwa la kuzisemea nchi za Kiafrika na nyingine za Dunia ya Tatu katika medani za Kimataifa, hasa katika wadhifa wake wa heshima kubwa wa Mwenyekiti Mwenza wa Tume ya Utandawazi Duniani. Lakini pia, kwa haiba yake ya uongozi, Rais Mkapa amejitokeza kuheshimika sana hata mbele ya macho ya nchi zilizoendelea. Kutokana na kuheshimika huko, ameweza kujenga imani kubwa ya nchi hizo siyo kwake yeye binafsi tu bali hata kwa nchi yetu. Imani hiyo inajidhihirisha katika mambo makuu yafuatayo miongoni mwa mengi mengine:- (1) Tanzania ni miongoni mwa nchi chache sana zilizofanikiwa kuingia katika | ||||||||||||||
| wanavyotuamini kuwa tunazitumia vizuri fedha zao. (3) Hivi sasa Tanzania ni miongoni mwa nchi zinazoongoza katika kuvutia vitega uchumi vya nje katika Bara la Afrika. Halmashauri Kuu ya Taifa ilijadili pia hotuba ya ufunguzi wa Mwenyekiti ambayo ilibainisha mafanikio makubwa ya jumla katika maeneo ya siasa, uchumi na huduma za jamii wakati tukiwa tumemaliza nusu ya kipindi cha | ||||||||||||||
| | ||||||||||||||
| Madarasa ya Skuli ya Chwale, Wete, Pemba yaliyojengwa chini ya Mfumo wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) | ||||||||||||||
|
· | ||||||||||
|
| ||||||||||
|
| ||||||||||
|
| ||||||||||
|
Tamko la Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM kuhusu Palestina | ||||||||||
|
· NEC yaunga mkono Wapalestina katika harakati zao za kujikomboa · Yataka Israel isimuhamishe Arafat nchini mwake · Na Jumuiya ya Kimataifa yatakiwa kusimamia utekelezaji wa Road-Map | ||||||||||
|
Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama Cha Mapinduzi imesema kwamba imepokea kwa mshangao na masikitiko makubwa, uamuzi wa Serikali ya Israel wa kutaka kumuondoa kutoka nchini mwake Rais wa Palestina, Mheshimiwa Yassir Arafat.
Katika tamko lililotolewa hivi karibuni Mjiji Dodoma, NEC ambayo ilikutana chini ya Mwenyekiti wa CCM, Rais Benjamin Mkapa imesema kwamba uamuzi huo wa fedheha una shabaha ya kuvuruga jitihada zinazoendelea sasa za kuleta amani kati ya Israel na Palestina na katika Mashariki ya Kati kwa jumla. "Hii inathibitisha kwa mara nyingine tena jinsi ambavyo Serikali ya Israel isivyokuwa na dhamira ya dhati wala utashi wa kisiasa wa kupata ufumbuzi muafaka na wa kudumu wa mgogoro baina yao na Wapalestina", tamko la NEC lilisema. Aidha, uamuzi huo na matendo kadhaa ya kikatili yanayofanywa na Israel dhidi ya Wapalestina vinadhihirisha wazi nia mbaya ya Serikali ya Israel ya kutaka kukwamisha Mpango wa sasa wa amani Mashariki ya Kati, maarufu kwa jina la Road Map, Mpango ambao hatimaye ungewezesha kuzaliwa kwa Taifa la Wapalestina lililo huru, na linaloishi bega kwa bega na kwa amani na Taifa la Israel. | ||||||||||
|
| ||||||||||
|
Kiongozi wa Palestine, Yasser Arafat akiongoza mkutano wa Kamati Kuu ya Chama cha PLO (Palestine Liberation Organization) | ||||||||||
|
Katika tamko lake NEC imeazimia kuwa: "Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama Cha Mapinduzi inapenda kuelezea kutokufurahishwa kwake na uamuzi huo, na kuulaani vikali. Kutekelezwa kwa uamuzi huo hakutaongeza usalama kwa Israel bali kutazidisha chuki na kuchochea ghasia zaidi. Hivyo basi, Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama Cha Mapinduzi inaitaka |
Serikali ya Israel kubadili uamuzi wake huo. Kimsingi Halmashauri Kuu ya Taifa inaisihi Serikali ya Israel kurudi kwenye mstari wa utekelezaji wa Mpango wa Amani wa sasa na Mkataba wa Oslo". "Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama Cha Mapinduzi inatoa wito kwa Jumuiya ya Kimataifa, hususan Umoja wa Mataifa na nchi za Marekani, Urusi, Uingereza na Ufaransa zilizotayarisha |
Road Map kufanya kila linalowezekana kusimamia na kuhakikisha utekelezaji wake". "Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama Cha Mapinduzi inapenda kukariri msimamo wake wa kuwaunga mkono watu wa Palestina katika harakati zao za kujikomboa na kupata Taifa lao lililo huru wanaloliendesha wenyewe". | ||||||||
|
| ||||||||||||||
| | ||||||||||||||
| Serikali za zatakiwa ziandae sherehe kabambe za miaka 40 ya Mapinduzi na Muungano mwakani kwani | ||||||||||||||
| · Muungano wetu ndio mfano pekee Barani Afrika · Kauli mbiu ya MAPINDUZI DAIMA iendelezwe | ||||||||||||||
| ujasiri wa TANU na ASP chini ya Baba wa Taifa, Marehemu Mwalimu Julius Nyerere na Jemedali Mkuu wa Mapinduzi ya Zanzibar wa kuziunganisha nchi mbili za Tanganyika na Zanzibar na kuwa Tanzania tarehe 26 Aprili, 1964. Karibu miaka 40 sasa, Muungano wa Tanzania ndio mfano pekee Barani Afrika wa mafanikio ya utekelezaji wa dhamira ya Waafrika kuungana kikweli. Kamati Kuu ina fahari kubwa kwamba vyama vya TANU na ASP na hatimaye CCM vimeweza kudumisha Muungano wetu kwa kipindi chote cha miaka 40 na kuujengea msingi imara wa kudumu milele, licha ya juhudi zinazofanywa na maadui wa Muungano za kutaka kuudhoofisha na kuusambaratisha ambazo zimegonga ukuta. Kwa kuzingatia na kuthamini mafanikio hayo makubwa na kuwapa heshima wanayostahili waasisi wa Mapinduzi na Muungano, Kamati Kuu ya CCM imezitaka Serikali zote mbili za CCM ziandae sherehe kubwa za kuadhimisha miaka 40 ya Mapinduzi ya Zanzibar hapo tarehe 12 Januari, 2004 na miaka 40 ya Muungano wa Tanzania hapo tarehe 26 Aprili, 2004. Kamati Kuu ya CCM inawataka wananchi wote bila kujali tofauti zao za kisiasa kushiriki katika sherehe hizo muhimu na kamwe wasikubali kurubuniwa na wezi wa fadhila wanaotaka tarehe hizo muhimu katika historia ya nchi yetu zisahaulike. | ||||||||||||||
| Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM imezitaka Serikali zote mbili za CCM za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ziandae sherehe kubwa za aina yake kuadhimisha miaka 40 ya Mapinduzi ya Zanzibar hapo tarehe 12 | wa Chama cha Afro-Shiraz, Mzee Abeid Amani Karume, ambao walijitoa mhanga wa maisha yao kwa ajili ya uhuru wa kweli wa Wazanzibar na kuutokomeza kabisa utawala mkongwe wa Kisultani. Katika kikao chake hicho, Kamati Kuu ilitamka kwamba Chama Cha | |||||||||||||
| | ||||||||||||||
| Mwalimu Nyerere akichanganya udongo wa Tanganyika na Zanzibar kudhihirisha muungano wa nchi hizo mbili hapo tarehe 26 Aprili, 1964 | ||||||||||||||
| | ||||||||||||||
| Januari, 2004 na miaka 40 ya Muungano wa Tanzania zitakazofikia kilele chake tarehe 26 Aprili, 2004. Katika kikao chake cha siku mbili kilichofanyika mjini Dar es Salaam hivi karibuni chini ya Mwenyekiti wa CCM, Rais Benjamin William Mkapa, Kamati Kuu ilizingatia ujasiri wa Afro-Shiraz Party wa kuikomboa Zanzibar kutoka katika makucha ya wakoloni wa Kiingereza na utawala wa Masultani walowezi tarehe 12 Januari, 1964. Wajumbe wa Kamati Kuu waliuthamini na kuuenzi mchango mkubwa wa mashujaa wa Mapinduzi ya Zanzibar chini ya uongozi thabiti wa Rais | ||||||||||||||
| Mapinduzi kina fahari kubwa kuona kwamba ASP na hatimaye CCM baada ya kuungana na TANU imeweza kuyalinda, kuyaendeleza na kuyadumisha Mapinduzi ya Zanzibar kwa karibu miako 40 sasa na kuyawekea msingi imara wa kuyadumisha milele. Kutokana na ukweli huu, Kamati Kuu imesisitiza kwamba kauli mbiu ya MAPINDUZI DAIMA iendelee kutumika kama kielelezo cha dhamira ya kweli ya kuyadumisha mapinduzi hayo na matunda yake ambayo kila Mzalendo wa kweli wa Zanzibar na Tanzania nzima anapaswa kujivunia. Aidha, Kamati Kuu ilitafakari pia | ||||||||||||||
| Rais Nyerere anamvisha nishani ya uaminifu na ushujaa Rais wa
ASP Mheshimiwa Abeid Amani Marume tarehe 19/2/1967 kwenye jengo la
Makao Makuu ya ASP Kisiwandui | ||||||||||||||
|
| ||||||||||
|
| ||||||||||
|
TASAF Chachu ya maendeleo na inayoondoa umaskini nchini | ||||||||||
|
Chama cha Mapinduzi (CCM) kimewapongeza waanchi na Serikali kwa juhudi za waziwazi zinazoonekana za kuondoa umaskini nchini. Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) ulianzishwa na Serikali mwaka 2000 kutokana na mkopo wa Dola za Kimarekani 60 milioni toka Benki ya Dunia. Serikali ya Jamhuri ya Muungano ya Tanzania nayo imetoa Dola za Kimarekani 3.2 milioni kuchangia juhudi za wananchi katika kuondoa umaskini. TASAF imejitanua katika wilaya 40 za Tanzania Bara na wilaya zote za |
Unguja na Pemba ambapo imeshughulikia jumla ya miradi mingi kote nchini. Inatazamiwa kwamba katika miaka miwili ijayo, shughuli za TASAF zitaenea katika wilaya zote za Tanzania Bara. Miradi iliyokamilishwa hadi sasa ni pamoja na madarasa ya shule za msingi 1,888; nyumba za walimu 481; vyoo vya matundu 277; zahanati 272; nyumba za waganga 330; visima 244; mabwawa 6; barabara za vijijini kilomita 1,354; bustani za miche na mingineyo kadhaa. Kwa mujibu wa taarifa ya Serikali |
iliyowasilishwa hivi karibuni kwenye kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, TASAF hadi sasa imetoa ajira kwa wananchi 69,699 ambao kati yao hawa wanawake ni 32,800. Halmashauri Kuu ya Taifa ambayo ilikutana chini ya Mwenyekiti wa CCM, Rais Benjamini Mkapa imeridhika na mafanikio haya makubwa yaliyokwisha patikana na imewataka wananchi kushiriki katika ujenzi wa miradi hiyo ili isaidie kuwaondolea au kuwapunguzia tatizo la umaskini. | ||||||||
| | | |||||||||
|
Ujenzi wa Zahanati wa Zingwe Zingwe, Unguja ni moja ya miradi ya TASAF. |
Wananchi wakishiriki kutoa maoni yao juu ya ujenzi wa mira iliyo chini ya TASAF. | |||||||||
|
| ||||||||||
|
Tovuti (Website) ya CCM hii hapa | ||||||||||
|
Tovuti (Website) ya CCM ilizinduliwa rasmi tarehe 5 Februari, 2002 na Mwenyekiti wa CCM, Mheshimiwa Rais Benjamin Mkapa wakati wa sherehe za Jubilel ya miaka 25 ya Chama Cha Mapinduzi zilizofanyia Zanzibar. Hata hivyo, muda mfupi baada ya uzinduzi huo, Tovuti ilikabiliwa na matatizo kadhaa yaliyosababisha isiwepo kwenye mtandao kwa kipindi kirefu. Kutokana na kasoro hiyo, hatua za kuifufua Tovuti iyo zilichukuliwa hivi karibuni. Hivi sasa Tovuti ya CCM ambayo ni www.ccmtz.org au www.ccmtz.com imeundwa upya na ipo hewani. Taarifa nyingi za Chama Cha Mapinduzi zinaendelea kujazwa katika Tovuti hiyo. Baadhi ya mambo muhimu yaliyowekwa ili kuitangaza CCM ni pamoja na Hotuba mbali mbali; Mwelekeo wa Sera za CCM katika miaka ya 2000 hadi 2010; Katiba ya CCM; ILANI ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2000; Historia ya TANU na ASP na mambo megine kadhaa.
Mtandao wa Internet: Kazi ya uundaji wa Tovuti imekwenda sambamba na uunganishaji wa mtandao wa kisasa wa INTERNET katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba Dar es Salaam. Kazi hiyo imekwishakamilika na hivi sasa kompyuta ya Ofisi ya Katibu Mkuu wa CCM imekwisha unganiswa na INTERNET. Ili kila kompyuta katika jengo iweze kupata INTERNET, kazi ya kuweka mtandao wa ndani (Local Area Network- LAN) imekwishaanza. | ||||||||||
| | ||||||||||||||
|
| ||||||||||||||
| | ||||||||||||||
| Baada ya hali ya amani na utulivu kurejea Zanzibar | ||||||||||||||
| · Karume asambaza maendeleo Pemba na Unguja · Sera za `Jino kwa Jino' zimefifia · Na heshima ya SMZ inang'ara | ||||||||||||||
| imerejea na umoja na mshikamano wa Kitaifa unaendelea kujengeka tena. · Sera za chuki na uhasama (jino kwa jino) za CUF zilizokuwa zikiwavutia wafuasi wengi wa chama hicho zimefifia kwa kiasi kikubwa. · Hadhi na heshima ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na Mheshimiwa Rais Amani Abeid Karume imerejea na inaendelea kuimarika siku hadi siku. · Kupitishwa kwa marekebisho ya sheria za Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC) kumewezesha kufanyika kwa amani na utulivu chaguzi ndogo za majimbo 17 | ||||||||||||||
| Matokeo ya Uchaguzi wa Rais wa Zanzibar yalitangazwa tarehe 7 Novemba, 2000. Kufuatia matokeo hayo, mgombea wa Urais kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mheshimiwa Amani Abeid Karume alishinda kwa kishindo kwa kupata kura 248,095 (65%), ambapo mgombea wa nafasi hiyo hiyo kupitia CUF, Seif Shariff Hamad alipata kura 122,000 (33%). | Mapinduzi ya Zanzibar pamoja na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Kwa kutekeleza Ilani ya Uchaguzi ya CCM kuhusu ujenzi wa mshikamano na umoja wa Kitaifa, awamu ya pili ya mazungumzo ya kujenga maelewano ya kisiasa baina ya vyama vikuu vya siasa vya CCM na CUF yalifanyika. Baada ya miezi 9 ya majadiliano na mashauriano | |||||||||||||
| | ||||||||||||||
| Katibu Mkuu wa CCM, Ndugu Philip Mangula akipeana mkono na Katibu Mkuu wa CUF, Seif Shariff Hamad baada ya kutiwa saini Muafaka baina ya vyama vyao viwili tarehe 10/10/2001 Ikulu Zanzibar | ||||||||||||||
| Hata hivyo, kumalizika kwa Uchaguzi Mkuu wa 2000 kulizaa hali ya mivutano mikubwa ya kisiasa, vurugu baadhi ya nyakati na hujuma dhidi ya mali za Serikali na wananchi. Mivutano hiyo ilipelekea fujo na maandamano haramu ya tarehe 26 na 27 Januari, 2001 huko Pemba, fujo zilizosababisha kupotea kwa maisha ya watu 23, wengine kujeruhiwa na baadhi ya wananchi kukimbilia Shimoni-Kenya. Tukio hili liliisikitisha sana Serikali ya | ||||||||||||||
| Muafaka ulifikiwa kati ya CCM na CUF na ulitiwa saini tarehe 10 Oktoba, 2001 Ikulu Zanzibar. Hatua kadhaa zilichukuliwa na Serikali zote mbili za Muungano na ya Zanzibar ili kuhakikisha kwamba vurugu za aina hiyo zilizotokea Pemba hazirudiwi tena. Faida zilizokwishapatikana kutokana na kutekelezwa kwa Muafaka ni pamoja na:- Hali ya maelewano katika jamii | ||||||||||||||
| Kisiwani Pemba tarehe 18 Mei, 2003. Matokeo yake ni kwamba CUF ilipata viti 11 na CCM ilipata viti 6. Kutokana na mafanikio hayo, mazingira mazuri yamejengeka Zanzibar ambayo yameiwezesha Serikali ya CCM ya Zanzibar kuendelea kutekeleza Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2000 kwa ufanisi mkubwa na kuharakisha maendeleo. | ||||||||||||||
| Inaendelea Uk. 19 | ||||||||||||||
|
| ||||||||||||
|
| ||||||||||||
|
Baada ya hali ya amani na utulivu kurejea Zanzibar | ||||||||||||
|
Inatoka Uk. 18 |
uimarishaji wa sekta ya elimu, mawasiliano, afya na maji. Serikali imeshatekeleza mambo yafuatayo:- · Imeandikisha asilimia 98 ya watoto waliofikia umri wa kwenda skuli. ·. Mpango Mkuu wa Elimu umefanyiwa mapitio. · Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar kimeshatimiza mwaka wa pili tangu kilipofunguliwa rasmi mwaka jana. Chuo |
baada ya Rais Amani Abeid Karume kuchukuwa madaraka mwaka 2000. Kuanzia Novemba 2000 hadi Juni 2003, jumla ya wafanyakazi 3,741 wameshalipwa viinua mgongo yenye thamani ya shilingi 2,914 milioni. Kadhalika wafanyakazi 1662 wameshalipwa malimbikizo ya pensheni zao. Wakati Rais Karume anaingia madarakani, Serikali ilikuwa inadaiwa | ||||||||||
|
Katika kipindi cha mwaka 2000-2003 uchumi wa Zanzibar umekuwa kutoka asilimia 3.2 mwaka 2000 hadi asilimia 5.6 mwaka 2002. Mfumko wa bei umeshuka kutoka asilimia 6.2 mwaka 2000 hadi asilimia 5.2 mwaka 2002. Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) ulioanzishwa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa | ||||||||||||
| | | |||||||||||
|
"Sasa mambo safi", Naibu Katibu Mkuu CCM (Zanzibar), Ndg. Saleh R. Ferouz |
Wake kwa waume wakishiriki katika mradi wa TASAF wa ujenzi wa kusambaza maji wa Kiuyu Mnungwini (Pemba) | |||||||||||
|
mkopo wa Benki ya Dunia umesaidia kupunguza matatizo ya wananchi wa Zanzibar hasa vijijini. Mfuko huu umetenga shilingi bilioni 3 kwa ajili ya miradi ya maendeleo katika sekta za elimu, afya na huduma za maji. Mpaka sasa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii umeshatekeleza miradi 65, Unguja 37 na Pemba 28. Miradi hii ina thamani ya shilingi bilioni 1,737,218,255. Katika fedha hizo, wananchi wamechangia shilingi milioni 239,505,855 kama nguvu kazi na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii umetoa shilingi bilioni 1,497,712,400. TASAF pia inaifadhili miradi miwili ya kilimo cha umwagiliaji maji katika vijiji vya Mtwango na Ndijani, Unguja. Halikadhalika TASAF inayafanyia utafiti maeneo ya mto Mwanakombo, Upenja, Chaani na Kibokwa kwa Unguja na Weni pamoja na Gae la Mtungi kwa Pemba ili kuangalia uwezekano wa kuyatumia maeneo hayo kwa ajili ya kilimo cha kumwagilia maji. Tangu Serikali ilipozindua mpango wa kupunguza umaskini mwezi Mei, 2002 imekuwa ikiweka mkazo mkubwa katika |
hiki kina wanafunzi 54 wanaochukua shahada ya ualimu na sanaa. · Imejenga barabara zenye urefu wa kilomita 60 kwa kutumia fedha za Serikali. · Zabuni ya utanuzi wa uwanja wa ndege wa Zanzibar tayari zimeshatangazwa. · Inaimarisha huduma za maji safi katika maeneo mbalimbali ya Unguja na Pemba. · Serikali ya Japani iko katika hatua za mwisho inashughulikia ombi la mradi wa maji katika Manispaa ya Zanzibar wenye thamani ya shilingi bilioni 11. · Serikali imeyatengeneza majenereta ya umeme Pemba kwa thamani ya shilingi 497,000,000/=. · Katika sekta ya kilimo, Serikali inakiimarisha Chuo cha Kizimbani kwa ajili ya shughuli za utafiti wa kilimo na mifugo. Serikali pia inayafanyia utafiti mabonde 57 ya Unguja na Pemba yenye ukubwa wa hekta 17,042. Kwa kuwa Ilani ya Uchaguzi ya CCM inatilia mkazo suala la ustawi wa jamii wa wananchi wake katika utekelezaji wa ahadi za Serikali, suala la mafao ya wastaafu lilishguhulikiwa mara moja |
mafao ya viinua mgongo vya wastaafu wapatao 4967 yenye thamani ya shilingi 5,325 milioni. Wastaafu 2293 pia walikuwa wanaidai Serikali shilingi 1,092.2 milioni kama malimbikizo ya pensheni. Malipo hayo yamefanywa kwa wadai wote wa Unguja na Pemba. Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar katika kutekeleza Ilani ya Uchaguzi ya CCM pia imeweka mkazo katika ujenzi wa barabara mijini na vijijini. Katika kipindi cha miaka miwili na nusu ya utekelezaji wa Ilani, Serikali imeweza kujenga barabara Unguja na Pemba ili kuimarisha miundo mbinu ya uchumi.
UNGUJA barabara zilizojengwa ni:-
· Kitogani-Paje Kilomita 11-2 · Barabara ya Bambi _ kilomita 6.0 · Jang'ombe-Mpendae _ kilomita 0.6 · Kaebona-Kaepwani _ kilomita 4.5 | ||||||||||
|
Inaendelea Uk. 20 | ||||||||||||
|
| ||||||||
| | ||||||||
| Baada ya hali ya amani na utulivu kurejea Zanzibar | ||||||||
| Inatoka Uk. 19 | ||||||||
| | ||||||||
| Rais Karume akikagua ujenzi wa barabara mpya ya Kilindini - Micheweni huko Pemba | ||||||||
| · Makunduchi-Mtende _ Kilomita 5.5
PEMBA barabara zilizojengwa ni:-
· Chake-Wesha _ kilomita 7.0 · Chake-Vitongoji _ kilomita 7.0 · Kilindi-Micheweni _ kilomita 6.0 Jumla ya shilingi 2,282 bilioni zimetumika kugharamia ujenzi wa barabara hizi. Kati ya hizo, shilingi 1.319 bilioni zimetolewa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na shilingi 963 milioni ni msaada wa lami kutoka Serikali ya Libya. Barabara zinazoendelea kujengwa hivi sasa kwa nguvu za Serikali ni kwa upande wa Unguja barabara ya Mahonda-Donge yenye urefu wa kilomita 14; na Pemba ni barabara ya Mtu Haliwa-Chokocho ya kilomita 12. Barabara nyingine zinazojengwa kwa msaada wa wafadhili ni:- · Kidimni-Kitope _ kilomita 29.6 · Mkoani-Chake _ kilomita 30.5 Mafanikio yote haya yameweza kupatikana katika kipindi cha miaka miwili na nusu tu cha uongozi wa Rais Amani Abeid Karume. | ||||||||
| | ||||||||
| Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM na Waziri Kiongozi wa SMZ akizindua mradi wa maendeleo Zanzibar. | ||||||||
| | ||||||||||||
| | ||||||||||||
| Tumeachana na Siasa ya Ujamaa na Kujitegemea? La hasha | ||||||||||||
| Tokea mwanzoni mwa miaka ya tisini, Tanzania imo katika mageuzi makubwa ya kisiasa, kiuchumi na kijamii ambayo yanakwenda sambamba. Mageuzi ya kisiasa yametuingiza katika mfumo wa vyama vingi vya siasa baada ya zaidi ya miaka 40 ya mfumo wa chama kimoja. Mageuzi ya kiuchumi yametutoa katika uchumi hodhi uliokuwa ukimilikiwa na dola na kutuingiza katika mfumo wa uchumi wa soko unaotoa nafasi ya ushiriki wa sekta ya binafsi. Mageuzi ya kijamii ni pamoja na kupanuka kwa uhuru wa vyombo vya habari pamoja na mambo mengine mengi ambayo aghlabu ni matokeo ya mageuzi ya kiuchumi na kisiasa. Kama ilivyo kawaida ya mageuzi, mageuzi haya makubwa na mengi yanayokwenda sambamba yamewa-fadhaisha na hata kuwa- babaisha wananchi wengi | [Na Omar R. Mapuri] | Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na ile ya Zanzibar. Katika Utangulizi wa Katiba zote mbili unapata maneno yafuatayo: " tumeamua rasmi na kwa dhati kujenga katika nchi yetu jamii inayozingatia misingi ya uhuru, haki, udugu na amani." Pia Katiba hizo zinaendelea: " . Misingi hiyo yaweza tu kutekelezwa katika jamii yenye demokrasia " Ibara ya 12 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania haikuvunga vunga maneno katika kuibainisha falsafa hii ya msingi. Ibara hiyo inasomeka kama ifuatavyo:- "12. - (1) Binadamu wote huzaliwa huru, na wote ni sawa. (2) Kila mtu anastahili heshima ya kutambuliwa na kuthaminiwa utu wake. Ibara ya 11 ya Katiba ya Zanzibar ina maneno hayo hayo. Inathibitika kwa hivyo kwamba falsafa hii si ya CCM peke yake, bali ni ya nchi nzima. Hatujapata kusikia chama hata kimoja cha siasa kinachoipinga falsafa hii. Imani/Siasa/Itikadi: Ni imani ya CCM kwamba ujamaa na kujitegemea ndiyo njia pekee ya kujenga nchi ya watu walio sawa, huru na wanaoheshimiana. Kwa hivyo, hiyo ndiyo siasa au itikadi ya msingi ya CCM. Ibara ya 4 ya Katiba ya CCM inaweka bayana imani ya CCM kama ifuatavyo:- 4. CCM kinaamini kwamba:
(1) Binadamu wote ni sawa
(2) Kila mtu anastahili heshima ya kutambuliwa na kuthaminiwa utu wake.
(3) Ujamaa na kujitegemea ndiyo njia pekee ya kujenga jamii ya watu
walio sawa na huru Kwa upande wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, sehemu ya Utangulizi imeelezea madhumuni ya kutungwa kwa Katiba hiyo kuwa ni kujenga jamii yenye demokrasia na pia kwa ajili ya kuhakikisha kwamba Tanzania inaongozwa na Serikali yenye kufuata misingi ya demokrasia na ujamaa. Maneno kama hayo yamerejewa pia katika Katiba ya Zanzibar. Ibara ya 3(1) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inaitangaza rasmi Tanzania kuwa ni nchi ya kidemokrasia na ya kijamaa, yenye kufuata mfumo wa vyama vingi vya siasa. Ibara ya 8(1) ya Katiba ya Zanzibar nayo imeitangaza hivyo hivyo Zanzibar isipokuwa tu imetumia maneno | ||||||||||
| kutamka mwanzoni mwa vuguvugu la mageuzi kwamba eti CCM haina dira. Aidha, wapo wasomi wanaojaribu kuonyesha kwamba CCM imeachana na ujamaa na kwamba sasa inaendesha sera wanazoziita za kiliberali. Zaidi ya yote, vipo hata vyama vya upinzani vilivyodiriki kujinasibu kwamba eti vyenyewe ndivyo sasa vyenye sera za ujamaa eti kuziba pengo lililoachwa na CCM iliyoutelekeza ujamaa. Katika makala haya tutajaribu kusahihisha dhana hizo ambazo tunaamini kwa kiasi kikubwa ni matokeo tu ya ubabaikaji uliosababishwa na mageuzi. Tutajitahidi kuonyesha kwamba CCM haijaachana na siasa yake ya Ujamaa na Kujitegemea, bali ambacho kimekuwa kikibadilika kulingana na wakati na mazingira, ni mikakati tu ya kufikia lengo hilo kuu la muda mrefu. UCHANGANUZI WA MANENO "FALSAFA", "IMANI", "SIASA", "SERA", "ILANI" n.k. Kabla ya kuitazama kwa undani | ||||||||||||
| "Siasa ya Ujama na Kujitegemea ipo pale pale," Katibu Mwenezi wa CCM Taifa, Ndg. Omar R. Mapuri akiwaeleza waandishi wa habari hivi karibuni | ||||||||||||
| wakiwemo wana CCM. Ilivyokuwa mageuzi hayo yameletwa, yanaendeshwa na kusimamiwa na CCM, wapo wana CCM wanaojiuliza kama CCM imeachana na sera zake za msingi, hasa Siasa ya Ujamaa na Kujitegemea na dira ya utekelezaji wake ambayo ni Azimio la Arusha. Wapo pia wanachama wa CCM wachache, wakiwemo hata viongozi, ambao hawajiulizi tena, bali wanaamini hasa kwamba CCM imekwishaachana na sera zake. Katika nyakati fulani wapo hata viongozi wa CCM waliosikika wakitoa kauli kama vile: "tulipokuwa tukijenga ujamaa ." au "enzi zile za Azimio la Arusha ." kama vile ujenzi wa ujamaa haupo tena au enzi za Azimio la Arusha zimekwisha. Yupo hata kiongozi mkubwa wa CCM aliyewahi | siasa ya Ujamaa na Kujitegemea, inafaa kwanza kuchanganua maneno ya "falsafa", "imani", "siasa", "itikadi", "sera", "maamuzi" na "ilani" ambayo yanatumika sana katika kuielezea dhana nzima ya ujamaa na kujitegemea katika mikutadha mbali mbali. Falsafa: Falsafa inayosarifu dhana na nadharia za Chama Cha Mapinduzi, na nchi nzima kwa jumla ni usawa wa binadamu na mtu kuthaminiwa kwa utu wake. Falsafa hii inabeba dhana za uhuru, demokrasia, haki, udugu na amani. Falsafa hii inaashiriwa katika Ahadi ya Kwanza ya Mwanachama wa CCM isemayo: "Binadamu wote ni ndugu zangu na Afrika ni moja". Falsafa hii ndiyo pia iliyoweka misingi ya Katiba ya | |||||||||||
| Inaendelea Uk. 22 | ||||||||||||
| | |||||||||||
|
| |||||||||||
| | |||||||||||
| Tumeachana na Siasa ya Ujamaa na Kujitegemea? La hasha | |||||||||||
| Inatoka Uk. 21 | |||||||||||
| "haki za kijamii" badala ya neno "ujamaa". Hata hivyo madhumuni ni yale yale. Tukizilinganisha Katiba za nchi na ile ya CCM katika muktadha wa siasa ya ujamaa na kujitegemea, inadhihirika kwamba neno "kujitegemea" halikutumika katika Katiba za nchi. Tafsiri yetu ya tofauti hiyo ni kwamba katika siasa ya Ujamaa na Kujitegemea, ncha ya ujamaa ni ya nchi nzima lakini ncha ya kujitegemea inatoa fursa kwa vyama vya siasa kutofautiana kwa sera. Ingawa kuna vyama vya upinzani ambavyo husikika vikitaka kipengele cha Ujamaa kiondoshwe katika Katiba ya nchi, lakini ukizitazama kwa undani sera za vyama hivyo, utagundua kwamba zimejengwa juu ya msingi huo huo wa ujamaa. Na vipo vyama ambavyo hujinasibu kwa wananchi kwamba eti ndivyo vyenye uwezo mkubwa zaidi wa kuzitekeleza sera za CCM kuliko CCM yenyewe. Vyama kama hivyo vinakiri usahihi wa siasa ya Ujamaa lakini vinadai kuwa eti CCM haina uwezo wa kuitekeleza. Lakini zaidi ya yote, hatujapata kusikia chama cho chote cha siasa nchini Tanzania kinachojitambulisha na ubepari. Sera na Dira: Baada ya kubainisha siasa yake ya Ujamaa na Kujitegemea iliyojengwa juu ya msingi wa falsafa ya usawa wa binadamu na mtu kuthaminiwa kwa utu wake, TANU mnamo mwaka wa 1967 ilipitisha Azimio la Arusha lililoandaa mazingira na kuweka dira ya utekelezaji wa siasa hiyo. Sera ni mkakati wa utekelezaji wa siasa kwa kipindi fulani kulingana na uchambuzi wa dira uliofanywa kwa ajili ya kipindi hicho. Sera huweza kubadilika kulingana na mahitaji ya wakati. Kwa hivyo, wakati siasa ya Ujamaa na Kujitegemea ni ya kudumu na Azimio la Arusha kama dira yake ya utekelezaji nalo ni la kudumu kwa kiasi fulani, sera na mikakati ya utekelezaji huweza kubadilika kila baada ya muda, kulingana na mabadiliko ya mahitaji ya wakati. Na kweli uzoefu katika TANU na ASP na baadaye CCM unaonyesha kwamba baada ya kila kipindi cha wastani wa miaka 10, Chama kimekuwa kikitathmini utekelezaji wa siasa ya Chama na kuzitazama upya sera zake za msingi kwa lengo la kuzifanya zikidhi mahitaji ya wakati. Baada ya kufanya mapitio hayo Chama huja ama na mwongozo unaojikita katika ufafanuzi na kuyawekea mkazo maeneo fulani au huja na sera mpya kabisa, lakini lengo kuu likiwa ni lile lile la kutekeleza siasa ya Ujamaa na Kujitegemea kwa kuzingatia misingi ya Azimio la Arusha. Ndiyo maana katika kipindi cha toka 1971 hadi | sasa, CCM imetoa nyaraka nne zifuatazo za kisera za msingi:- (1) Mwongozo wa TANU wa 1971 ambao ulijenga hamasa ya utekelezaji wa Azimio la Arusha. (2) Mwongozo wa CCM wa 1981 ambao ulijielekeza katika kukabiliana na mmong'onyoko wa maadili uliokuwa unasababishwa na hali ngumu ya uchumi iliyochangiwa na vita vya nduli Idi Amin. (3) Mwelekeo wa Sera za CCM katika Miaka ya Tisini uliozingatia haja ya kujihami na taathira za upepo wa
mageuzi makubwa ya kiuchumi na kisiasa uliokuwa ukivuma Duniani na kuziangusha
dola kubwa za kijamaa za Ulaya ya Mashariki likiwemo la Urusi yenyewe
ya Kisovieti. Kwa jumla, chimbuko la sera zote za CCM ni Azimio la Arusha na zinapoandaliwa, yanazingatiwa pia malengo na madhumuni ya CCM yaliyobainishwa katika ibara ya 5 ya Katiba ya CCM. Baba wa Taifa, Mwalimu Julius K. Nyerere katika "Kujitawala ni Kujitegemea" aliyaelezea ifuatavyo mahusiano baina ya Azimio la Arusha na Sera za Chama:- Azimio la Arusha ndilo linaloeleza itikadi ya chama chetu. Ndiyo kauli kuu ya lengo letu na misingi yetu; ndilo msingi wa maamuzi yote ya sera za Chama na Serikali. Aidha Mwalimu alitambua haja ya kupitia upya sera kila mara na kurekebisha Azimio. Alisema tena katika "Kujitawala ni Kujitegemea:- Kila miaka inavyopita, kauli yo yote muhimu kupitiwa mara kwa mara kuona kama misingi yake bado inahitajiwa katika mazingira mapya Hata mimi nakubali kwamba (Azimio la Arusha) linahitaji marekebisho. Maneno hayo yanatosha kuwasuta wale wanaodai kwamba eti Mwalimu hakutaka mabadiliko ya Azimio na Sera. Maamuzi: Ndani ya utekelezaji wa sera ya msingi, Chama huweza kupitisha maamuzi | ||||||||||
| yenye lengo la kutoa msukumo wa utekelezaji wa jambo fulani mahsusi au kukabili tatizo fulani la utekelezaji. Ni kwa msingi huo ndio TANU na baadaye CCM ilipitisha maamuzi mengi yakiwemo yafuatayo:- (1) Siasa ni kilimo (Azimio la Iringa) (1972) kwa lengo la kutoa msukumo katika suala zima la kilimo. (2) Mpango wa Elimu kwa Wote (UPE) (Azimio la Musoma), (1974) uliotoa msukumo wa kuharakisha kufikisha elimu kwa wote ikiwa ni pamoja na suala la elimu ya watu wazima. (3) Mtu ni Afya (1976): Kutoa msukumo kwa sera ya kinga kuliko tiba. (4) Mpango wa Kujihami Kiuchumi (1980/81) ili kukabiliana na hali ngumu ya uchumi wa nchi. | |||||||||||
| | |||||||||||
| (5) Maamuzi ya Zanzibar (1991) ambayo yaliwaondolea wanachama wa kawaida wa CCM masharti ya uongozi yaliyoainishwa katika Azimio la Arusha. Maamuzi hayo yalikuwa na lengo la kuwawezesha wanachama wa CCM kushiriki katika harakati za kiuchumi katika mazingira mapya yaliyokuwa yanaingia ya uchumi wa soko. Masharti ya uongozi yalibaki kwa viongozi tu kama ilivyokuwa imekusudiwa katika Azimio la Arusha. Ilani: Kama ilivyokwishabainishwa, sera za msingi huchukua upeo wa muda mrefu | |||||||||||
| Inaendelea Uk. 23 | |||||||||||
| | ||||||||||
|
| ||||||||||
| | ||||||||||
| Tumeachana na Siasa ya Ujamaa na Kujitegemea? La hasha | ||||||||||
| Inatoka Uk. 22 | ||||||||||
| Azimio la Arusha zimekuwa zikichukua sura za kusambaza huduma za jamii (elimu, afya, maji n.k.) kwa wote, kujenga misingi ya fursa sawa za kujiendeleza, kuondoa unyonyaji, kupiga vita kila aina ya ubaguzi na dharau, kuwatetea wanyonge na kuwasaidia kujikwamua na kadhalika.Uamuzi wa kuanzisha vijiji vya ujamaa katika miaka ya sabini ulikuwa na lengo la kurahisisha utekelezaji wa juhudi hizi. Pamoja na matatizo ya hapa na pale ya utekelezaji, tunaamini Watanzania walio wengi hasa wanyonge, bado wanapenda kufikiwa kwa malengo hayo. Ndiyo maana tunasema Siasa ya Ujamaa ni ya kudumu. Kugawana au kusambaza kwa wote utajiri wa nchi (si kwa kugawana fedha bali kwa kuhakikisha upatikanaji wa huduma za kijamii kwa wote) ni sura moja tu ya Ujamaa. Lakini pia kuna sura ya pili ambayo ni ya kuuchuma huo utajiri wenyewe wa kugawana. Katika Azimio la Arusha, unafafanuliwa utaratibu wa kuchuma utajiri bila ya kunyonyana. Mkakati uliowekwa ni wa njia kuu za uchumi wa nchi kuwekwa chini ya wakulima na wafanyakazi kupitia vyombo vya Serikali Siasa ya Kujitegemea: Siasa ya Kujitegemea imechambuliwa kwa kina katika Sehemu ya Tatu ya Azimio la Arusha. Siasa hii inajikita katika kuleta maendeleo ya kweli ya nchi na ya wananchi wenyewe hasa wanyonge. Hoja inajengwa kwamba huwezi kuzungumzia maendeleo ya kweli kama maendeleo hayo ni ya vitu tu na si ya watu wenyewe na kama maendeleo hayo yamejengwa juu ya msingi wa utegemezi wa fadhila za nje. Inasisitizwa kwamba fedha si msingi wa maendeleo bali ni matokeo ya maendeleo. Kwa hivyo mkakati unaotiliwa mkazo ni wa kujituma katika kujiletea maendeleo bila ya kusubiri fedha kwanza au misaada na mikopo kutoka nje. Vitu hivyo kama vitapatikana vije tu kusaidia juhudi zetu za kujitegemea na kamwe visiruhusiwe kuhatarisha uhuru wetu. Kwa mnasaba huo, Siasa ya Kujitegemea inasisitiza kwamba: Maendeleo ya nchi huletwa na watu, hayaletwi na fedha. Fedha ni matokeo siyo msingi wa maendeleo. Ili tuendelee twahitaji vitu vinne: (i) Watu; (ii) Ardhi; (iii) Siasa safi na (iv) Uongozi bora. Kwa kuzingatia ukweli kwamba nchi yetu ina watu wengi na eneo kubwa la ardhi, mkakati wa siasa ya kujitegemea unabainisha kwamba maendeleo yataletwa na kilimo na hivyo pia unamjali zaidi mkulima vijijini. | ||||||||||
| Siasa ya Kujitegemea imebainisha masharti mawili ya maendeleo. Masharti hayo ni Juhudi na Maarifa. Juhudi inaashiria kufanya kazi kwa kujituma na Maarifa ni kiashirio cha matumizi ya utaalamu na teknolojia kwa lengo la kuziongezea tija juhudi. Kwa jumla, mtu hahitaji utafiti wa kina kubaini kwamba karibu yote yaliyoelezewa kuhusiana na Siasa ya Kujitegemea yalikuwa na ukweli mwaka 1967 na bado yana ukweli hadi leo. Aidha, yote hayo yanaendelea kupendwa na Watanzania waliowengi ambao siyo tu wameyakubali, bali pia wanajitahidi kuyatekeleza. Kwa mfano Watanzania pamoja na unyonge wao, hawakubali kuonewa wala kunyanyaswa. Pia, Watanzania wamejiletea maendeleo mengi (shule, zahanati, visima, njia, maji n.k.) kwa kujitegemea bila ya kusubiri fedha. Na zaidi ya yote, Watanzania wanajituma kwa bidii kubwa. Kwa kuzingatia ukweli huo, mtu hapaswi kupata taabu sana kuelewa kwa nini Siasa ya Kujitegemea inaendelea kuwa siasa ya CCM. Kama ilivyo katika siasa ya ujamaa, bila shaka yamejitokeza hapa na pale matatizo ya kiutekelezaji. Yapo matatizo yaliyo nje ya uwezo wetu kama vile matatizo ya kiuchumi ya dunia ambayo yalipotukumba na sisi yaliathiri utekelezaji wetu. Lakini pia yapo matatizo yaliyotokana na kasoro zetu wenyewe kama vile kuweka mkazo mdogo katika maarifa na badala yake kukazania tu juhudi ambapo matokeo yake yamekuwa ni tija ndogo katika uzalishaji hasa katika kilimo. Maeneo kama haya ya matatizo na kasoro ndiyo yanayotoa fursa ya kuzipitia upya baadhi ya sera za Chama kama tutakavyobainisha baadaye. Mwandishi wa Makala hii ni Katibu Mwenezi wa CCM Taifa, Ndugu Omar R. Mapuri ambaye katika toleo lijalo la jarida hili atamalizia Makala yake kwa kueleza juu ya:- Baadhi ya maeneo yaliyohitaji
marekebisho ya Sera
Shabaha ya Ujamaa katika kipindi
hiki.
Masharti na miiko ya Uanachama | ||||||||||
| kidogo, na kwa uzoefu wa CCM, ni kama miaka 10 hivi. Ndani ya kipindi hicho, Chama huchambua sera na kujipangia malengo ya utekelezaji kwa vipindi vifupi vifupi, aghlabu vya miaka mitano mitano. Hapo ndipo tunapopata ilani za uchaguzi ambazo huwasilishwa kwa wananchi kwa ajili ya kuombea kura katika chaguzi za dola ambazo hufanywa kila baada ya miaka mitano. Baada ya uchanganuzi huo wa maneno "falsafa", "siasa", "itikadi" "sera", "maamuzi" na "ilani" kama yanavyotumika katika msamiati wa CCM, imedhihirika kwamba falsafa na siasa ni vitu vya kudumu, au ni malengo ya muda mrefu, lakini sera, maamuzi na ilani ni vitu vinavyobadilika kila baada ya muda. Na hapa ndipo penye siri ya mafanikio ya CCM. Ingawa CCM ni chama kikongwe, lakini kila baada ya muda hujirekebisha kwa mujibu wa mazingira ya wakati, lakini bila ya kupoteza lengo. Kwa ufupi, CCM inafuata kanuni ya mwezi ambao katika mzunguko wake huanza na uchanga (ukiwa na umbo la hilali), ukafikia upevu (ukiwa na umbo la sahani) na kurejea tena uchanga ambapo unakuwa tunu tena. Ni kutokana na kanuni hiyo ndiyo maana wananchi hawaichoki CCM pamoja na ukongwe wake, kwani wakati wote inawaletea matumaini mapya. UJAMAA NA KUJITEGEMEA
KAMA SIASA YA CHAMA: Kama siasa ya Chama, Ujamaa na Kujitegemea ni lengo la kudumu. Ni kwa msingi huo ndiyo tunasema kwamba Chama Cha Mapinduzi bado kabisa hakijaachana na siasa hiyo. Katiba na sera za CCM zinabainisha wazi wazi msimamo huo kama ilivyokwishaelezewa. Baada ya kuuelewa msimamo huo, ni muhimu pia kuelewa tunapozungumzia Ujamaa na Kujitegemea tunakusudia nini. Tutajaribu kwa kutumia lugha nyepesi kabisa, kutoa ufafanuzi huo katika sehemu hii ya makala haya. Kama inavyojieleza yenyewe, siasa ya Ujamaa na Kujitegemea ina ncha mbili, yaani ya Ujamaa na ile ya Kujitegemea. Katika Azimio la Arusha, umefanywa uchanganuzi wa kina ambapo Sehemu ya Pili ya Azimio hilo inachambua Siasa ya Ujamaa na Sehemu ya Tatu inachambua Siasa ya Kujitegemea. Kwa maneno mengine siasa yetu hii ni siasa mbili ndani ya moja. Nasi kwa ufupi kabisa tutafanya uchanganuzi kama huo. Siasa ya Ujamaa: Siasa ya Ujamaa imechambuliwa na wanafalsafa wengi wakubwa waDunia hii wakiongozwa na Karl Marx na Vladmir Lenin. Pia imechambuliwa kwa kina na Mwalimu Julius K. Nyerere kwa mazingira ya Tanzania katika vitabu vyake mbali mbali, ambapo majumuisho yake yaliwekwa katika Azimio la Arusha. Sisi katika makala haya hatukusudii kurejea uchambuzi wa kifalsafa bali tu tunajaribu kumwelezea mwananchi wa kawaida maana pana na nyepesi inayokusudiwa katika Siasa ya Ujamaa. Kwetu sisi Ujamaa maana yake ni kugawana utajiri wa nchi kwa usawa na kwa haki katika misingi ya kuheshimiana. Jitihada zetu za kiutekelezaji katika kufikia lengo hilo kama zinavyoongozwa na | ||||||||||
|
| ||||||||
|
| ||||||||
|
| ||||||||
|
| ||||||||
|
| ||||||||
|
|
Sio elimu, sio mali, sio dini; bali ni ... | |||||||
|
Na Muhammed Seif Khatib | ||||||||
|
Nnachojivunia. Ni kipi? Sio elimu. Sio utajiri. Sio dini. Sio kabila. Kwangu mimi, vyote sio muhimu. Kwa nini? Twahibu!, vyote ni pambo tu. Kama ni mali; mali yako. Wachache huipata. Wengi ni mafukara. Wachache wao hupata kihalali. Wengi wao chori chori! Ukiwa na elimu ni mali yako. Si yetu sote. Kumpa mwingine ni kupenda tu. Ni wewe ujinga utakayeutoroka. Naam! Nayo dini ni imani. Imani hutofautiana. Wapo wasioamini cho chote. Wao, wapo wapo tu! Huko paradise hao watakaokwenda hadi leo hawajijui! Kufika huko nako, sio kwa leo au kesho. Safari ni ndefu! Kujivunia kabila, ni ubozi na ubahaluli. Zinauzwa wapi kabila? Si unaikuta tu. Asokabila sio mtu? Nnachojivunia nini? Uwanachama wa chama changu: Chama cha siasa chenye historia. Chama kilichofanya matendo makubwa Afrika. Ni chama hiki kilichotoka ndani ya mifupa na damu ya vyama vya ukombozi. Vipi hivyo, ni ASP na TANU. Naam! Vyama vya Waafrika. Vyama vya ukombozi. Vyama vilivyoona mbali. Vyama vya Nyerere na Karume. Viongozi waanzilishi. Viongozi waasisi wa taifa letu. Vyama vyao viliunganisha Waafrika. Viliwahamasisha. Vikawaamsha katika maruirui ya kutawaliwa. Walilemazwa ili kujiona sio watu kama watu. Waliamini kuwa wao ni watwana na wajakazi tu. Utu wao ulidhalilishwa! ASP na TANU, waasisi wa uanachama wangu, vikaweka mikakati ya kudai haki za Waafrika. Vikakataa katu kutawaliwa. Vikadai uhuru wa Tanganyika. Vikagombania uhuru wa Tanganyika. Vikagombania uhuru wa Zanzibar. Vilimkataa mkoloni. Vilimkataa Sultani. Mapambano yakapamba moto. Wakoloni wakasalimu amri Tanganyika. Masultani wakatimuliwa huko Zanzibar. Nchi zetu zikawa huru. Uhuru wa Mwafrika. Uhuru wa mtu mweusi. Hiki nnajivunia. Nnachojivunia. Ni uwanachama wangu. Chama hiki kilichorithi historia hii ya ukombozi. Bila historia hii bado leo tungekuwa watwana na wajakazi katika nchi yetu ya asili. Naionea fahari |
vyombo vya usalama ikiwemo Jeshi, Polisi na Usalama wa Taifa! Hili haliji wenyewe. Ni kazi ya busara na hekima iliyojengwa. Raia wanaheshimiwa na vyombo vinaheshimiwa. Utaifa unapewa umbele. Mipaka na majukumu ya kazi hayaingiliani. Uadilifu unapewa kipaumbele. Hakuna mfarakano. Hili katika nchi nyingine haliwezekani. Nnajivunia ufanisi wa chama changu katika kujenga kuaminiana huku katai ya vyombo vya usalama raia na vyombo vingine vikiwemo Serikali, Bunge na Mahakama! Nnachojivunia chama changu kwa sera sahihi zinazokubalika na kutekelezeka! Sera zenye uhalisi wa mambo. Hazibuniwi kuwalaghai watu, la hasha! Hazibuniwi kufurahisha watu tu! Ila hilo. Zinabuniwa kuondolewa watu umasikini. Zinabuniwa kuwaletea watu maendeleo. Ni sera zinazosimamiwa vizuri na Serikali zetu. Zinawekewa mikakati ili zilete tija na fanaka. Ufanisi wa utekelezaji huo katika ngazi zote. Kila mwanachama miongoni mwetu aangalie kitongoji na kijijini pake nini kimetekelezwa. Hakuna shule iliyojengwa au kukarabatiwa? Nyumba za walimu, vyoo na kadhalika zimejengwa? Hakuna zahanati mpya? Hakuna soko au gulio? Hakuna kuboreka kwa huduma za madawa za mahospitali, huduma za wakunga na watoto? Mwanachama wa CCM kama mimi anayejivunia chama chake lazima atajivunia ufanisi wa utekelezaji wa sera zake. Yapo ya kusemea kifua mbele katika kitongoji au kijiji. Tena utayasemea kwa uhakika na mifano. Ikiwezekana utoe takwimu na gharama zote. Si hivyo tu ipo miradi katika kata, tarafa, wilaya na hata mkoa. Lakini ukiweza unaweza kuisemea miradi ya kitaifa kama ya barabara, madaraja, umeme, gesi, nyumba, hospitali na kadha wa kadha. Lakini sio lazima kama hauelewi. Mimi Nnachojivunia, umahiri wa chama changu katika utendaji wake na uongozaji wake. Taifa hili linajizolea sifa kemkem duniani kote. Hilo wewe hujivunii? Mimi nnajivunia. Tujivuniye. | |||||||
|
historia hiyo. Nnachojivunia uwanachama wangu wa Chama Cha Mapinduzi. Chama kilichorithi heshima ya kuwa mkombozi. Hakuna chama kingine kinachoweza kujinasibisha na hilo. Huo ni ukweli. Hiyo nayo ni hoja nzito. Nnachojivunia kuwa mwanachama wa chama kikongwe. Sio ukongwe na kuishiwa au kukongoroka! La hasha. Ukongwe wenye busara na hekima. Chama kizoefu katika kuendesha nchi. Chama kiongozi. Chama kinachoongoza na vingine vinajikongoja! Chama kilichoonyesha na kubainisha umahiri wake. Kimeunganisha umma wa Tanzania kuwa kitu kimoja. Hakuna ufa wala mpasuko ndani ya Taifa. Kimefanikiwa kujenga umoja na utangamano wa kweli. Macho yanachukia kuona damu inamwagika ya binadamu! Tumezoea kununia mfarakano. Ni mfarakano wa dini, kabila ama rangi. Amani na upendo ni chaguo la watu wa nchi hii. Nnachojivunia mafanikio hayo yaloletwa na chama changu. Nnachojivunia kuwepo kwa umoja thabiti wa kitaifa. Umoja wenye kukumbatisha makabila yote, dini zote, jinsia zote na maeneo yote. Umoja wa Waafrika wa nchi zetu mbili walioungana miaka arobaini iliyopita. Ni umoja wa Waafrika wa Tanganyika na Zanzibar. Lakini budi ifahamike umoja huo ulianza mwaka 1957. Ni pale African Association ya Zanzibar na Shiraz Association zilipounda Afro-shirazi Party. Mshikamano huo ukaimarika na kuongoza Mapinduzi halali ya mwaka 1964. Umoja huo ni wa kidugu na kihistoria. Kuuvunja itakuwa ni kosa kubwa. Nnajivunia kuwa chama changu kimerithi na kuendeleza umoja huo! Chama kipi kingine cha siasa nchini chenye historia ya kuunganisha umma wa Tanzania na kusimamia kwa dhati umoja huu? Hakuna zaidi ya chama changu. Hivyo budi nnajivunia hili. Nnajivunia uhusiano mzuri uliojengwa na chama changu kati ya | ||||||||