RATIBA YA ZOEZI LA KUWAPATA WAGOMBEA WA CCM KATIKA
UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA VIJIJI NA VITONGOJI – TANZANIA BARA MWAKA 2004
1.0 UTANGULIZI
1.1 Kwa
kuzingatia ratiba ya Wizara ya Serikali za Mitaa na Tawala za Mikoa iliyotolewa
kwa ajili ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, Vitongoji na Vijiji mwaka 2004; na
kwa kuzingatia Katiba ya CCM toleo la 1997 ambayo inaelekeza taratibu za CCM
kwa chaguzi hizo kupitia vikao vya kutoa maoni, kuchuja, kupendekeza na
hatimaye kufanya uteuzi wa mwisho kwa mujibu wa Ibara 27:3; 34:4(e); 37:8(e);
39:5(b-c) na 49:6(c); Chama Cha Mapinduzi Makao Makuu kimeandaa Ratiba ya kuzingatiwa.
1.2
CCM
imedhamiria kwa mara nyingine kushinda kwa kishindo Vitongoji, Mitaa na Vijiji
vyote nchi nzima. Hilo ndilo lengo
la CCM na ni vema lizingatiwe. Ushindi
mkubwa utakaopatikana katika uchaguzi wa Vitongoji, Mitaa na Vijiji utaijengea
CCM msingi imara wa kushinda kwa kiwango cha juu katika uchaguzi Mkuu wa 2005.
2.0 KURA
ZA MAONI
2.1 Utaratibu
wa CCM kuwapata wagombea wake ni wa kupitia kura za maoni. Hivyo baada ya kuzingatia ratiba ya Serikali taratibu zilizoandaliwa ndani ya
CCM zinatoa fursa ya kushiriki uchaguzi huo na kushughulikia malalamiko
yatakayojitokeza kabla ya siku ya kuchukua fomu za Serikali zitakazotolewa
kuanzia tarehe 28/10/2004.
2.2 Ratiba
ya taratibu za kura za maoni, uchujaji na uteuzi wa Wagombea wa CCM iwe kama
ifuatavyo kwa Mikoa yote Tanzania Bara:-
1.
Tarehe 20-26/9/2004
Waombaji uongozi kuchukua na kurejesha fomu kwa Katibu wa CCM wa Tawi. (Kurejesha tarehe 26/9/2004 kabla ya saa 10
jioni).
2.
Tarehe 28/9/2004 –
2/10/2004 Kura za Maoni ngazi za Vitongoji, Mitaa.
3.
Tarehe 3-7/10/2004 Kura
za Maoni ngazi ya Vijiji.
4.
Tarehe 9/10/2004 –
13/10/2004 Vikao vya Kamati za Siasa za Matawi kuchuja na kupendekeza majina ya
waombaji wa Vitongoji, Mitaa na Vijiji.
5.
Tarehe 15/10/2004 –
18/10/2004 vikao vya Halmashauri Kuu za Matawi
(a)
Kuteua majina ya
wagombea Uongozi wa Vitongoji na Mitaa.
(b)
Kupndekeza majina ya
waombaji uongozi wa Serikali za Vijiji na kuwasilisha mapndekezo hayo kwenye
Kata..
6.
Tarehe 20/10/2004 –
26/10/2004 vikao vya Kamati za Siasa za Kata kuteua majina ya wagombea nafasi
za Uongozi wa Serikali za Vijiji na
kurejesha majina kwenye Matawi.
7.
Tarehe 28/10/2004 –
30/10/2004 wagombea uongozi walioteuliwa na Chama kugombea Uongozi wa
Vitongoji, Mitaa na Vijiji kuchukua fomu za uteuzi za Uchaguzi kwa wasimamizi
wa uchaguzi wa Serikali.
8.
Tarehe 1-2/11/2004 CCM
kuhakiki Ujazaji wa fomu za wagombea na kuzirudisha kwa wasimamizi wa Uchaguzi
wa Serikali.
9.
Tarehe 4/11/2004
Wasimamizi wa Uchaguzi wa Serikali kuteua majina ya wagombea uongozi wa
Mitaa, Vitongoji na Vijiji.
10.
Tarehe 3-5/11/2004
Uteuzi wa Mawakala wa CCM.
11.
Tarehe 5/11/2004 CCM
kuwasilisha pingamizi au malalamiko dhidi ya uteuzi kwa wasimamizi wa uchaguzi
wa Serikali (kama ipo haja ya kufanya hivyo).
12.
Tarehe
8/11/2004-19/11/2004 Kampeni za Uchaguzi.
13.
Tarehe
21/11/2004-27/11/2004 Uchaguzi wa Viongozi wa Vitongoji na Mitaa.
14.
Tarehe 28/11/2004
Uchaguzi wa Viongozi wa Vijiji.
3.0 RATIBA
YA KUZINGATIWA KATIKA KUWAPATA WAGOMBEA WA CCM KATIKA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA
MITAA, VIJIJI NA VITONGOJI MWAKA 2004
|
NA. |
TAREHE |
SHUGHULI |
MHUSIKA AU WAHUSIKA |
|
1. |
20-26/9/2004 |
Uchukuaji
wa fomu za Uongozi wa Vitongoji,Mitaa na
Vijiji |
Makatibu
CCM wa Matawi na Kata |
|
2. |
26/9/2004 |
Urejeshaji
wa fomu za Uongozi kwa Katibu wa Tawi kwa ngazi za Vitongoji, Mitaa na
Vijiji. (kabla ya saa 10.00 jioni). |
Wagombea
wote Makatibu wa CCM wa Matawi na Kata. |
|
3. |
28/9/2004
-2/10/2004 |
Kura
za Maoni kwa Wagombea Uongozi Ngazi ya Vitongoji na Mitaa |
Kamati
za Siasa za Matawi na Kata |
|
4. |
3-7/10/2004 |
Kura
za Maoni kwa Wagombea Uongozi Ngazi ya Vijiji |
Kamati
ya Siasa za Matawi, Kata na Wilaya |
|
5. |
9-13/10/2004 |
Vikao
vya Mapendekezo kuhusu Wagombea wa Vitongoji, Mitaa, Vijiji na Wajumbe wa Serikali za Vijiji na Mtaa |
Kamati
za Siasa za Matawi |
|
6. |
15-18/10/2004 |
(a)
Vikao vya uteuzi kwa
nafasi ya Wenyeviti wa Vitongoji, Mitaa na Wajumbe wa Serikali za Mitaa. (b)
Kutoa mapendekezo ya
wagombea ngazi ya Vijiji. |
Halmashauri
Kuu za Matawi |
|
7. |
20-26/10/2004 |
Vikao
vya Uteuzi wa mwisho kwa nafasi za Wenyeviti na Wajumbe wa Serikali za
Vijiji. |
Kamati
za Siasa za Kata |
|
8. |
28-30/10/2004 |
Siku
ya kuchukua fomu za uteuzi kwa Msimamizi wa Uchaguzi wa Serikali |
1.
Mgombea wa CCM aliyeteuliwa kwa kila nafasi 2.
Makatibu wa CCM wa Matawi na Kata. |
|
9. |
1-2/11/2004 |
Kuhakiki
fomu za Wagombea na kuzirudisha kwa Msimamizi wa Uchaguzi wa Serikali |
1.Mgombea aliyeteuliwa 2.Makatibu
wa CCM wa Matawi na Kata. |
|
10. |
4/11/2004 |
Wasimamizi
wa Uchaguzi kuteua majina ya wagombea |
Wasimamizi
wa Uchaguzi wa Serikali |
|
11. |
3-5/11/2004 |
Uteuzi
wa Mawakala wa CCM |
Kamati
za Siasa za Matawi na Kata |
|
12. |
5/11/2004 |
Kuwasilisha pingamizi/Malalamiko
dhidi ya Uteuzi kwa Msimamizi wa
Uchaguzi |
Wagombea
wa CCM walioteuliwa |
|
13. |
8-19/11/2004 |
Mikutano
ya Kampeni za Uchaguzi |
Kamati
za Siasa za Matawi na Kata. |
|
14. |
21/11/2004
|
Uchaguzi
wa Viongozi wa Vitongoji na Mitaa. |
-
Makatibu CCM Kata na Matawi -
Wasimamizi wa Uchaguzi |
|
15. |
28/11/2004 |
Uchaguzi
wa Viongozi wa Vijiji. |
-Makatibu
wa CCM wa Kata na Matawi -Wasimamizi wa Uchaguzi. |
KIAMBATISHO
RATIBA ILIYOTOLEWA NA
SERIKALI ZA MITAA NA TAWALA ZA MIKOA KUHUSU UTEKELEZAJI WA UCHAGUZI WA VIONGOZI
WA NGAZI ZA VIJIJI, VITONGOJI NA MITAA KWA MWAKA 2004
|
NA. |
TAREHE |
SHUGHULI |
MHUSIKA AU WAHUSIKA |
|
1. |
29/1-29/2/2004 |
ORTAMISEMI
kufanya mapitio ya Kanuni za Uchaguzi za 1999 na kuandaa mapendekezo |
ORTAMISEMI |
|
2. |
20/3-28/3/2004 |
ORTAMISEMI
kuandaa makisio ya gharama ya uchaguzi na kuwasilisha Hazina |
ORTAMISEMI |
|
3. |
17/4/2004 |
ORTAMISEMI
kuandaa na kuendesha mkutano na viongozi wa Kitaifa wa vyama vya Siasa |
ORTAMISEMI |
|
4. |
10/6-24/6/2004 |
ORTAMISEMI
kuandaa na kuendesha mkutano wa Wadau (Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Tume ya
Uchaguzi, Wakuu wa Mikoa na Wakuu wa Wilaya) |
ORTAMISEMI |
|
5. |
25/6-31/7/2004 |
ORTAMISEMI
kuandaa na kuendesha mkutano wa Wadau, Wakurugenzi wa Halmashauri na Mameya/Wenyeviti |
ORTAMISEMI |
|
6. |
21/8/2004 |
Waziri
kutoa Tangazo kwa umma kuhusu Uchaguzi |
WAZIRI |
|
7. |
24/8-6/9/2004 |
Wasimamizi
Wasaidizi kuandaa orodha za wapiga kura kutoka kwenye rejesta ya wakazi |
WASIMAMIZI
WASAIDIZI WA UCHAGUZI |
|
8. |
23/8-1/9/2004 |
ORTAMISEMI
kuandaa mada za kufundishia Wasimamizi wa Uchaguzi |
ORTAMISEMI |
|
9. |
6/9/-13/9/2004 |
Wasimamizi
kubandika orodha ya Wapiga Kura |
WASIMAMIZI
WASAIDIZI WA UCHAGUZI |
|
10. |
9/9-13/9/2004 |
Wasimamizi
wa Uchaguzi kupokea na kusikiliza
pingamizi dhidi ya orodha ya wapiga kura |
WASIMAMIZI
WASAIDIZI WA UCHAGUZI |
|
11. |
4/9-18/9/2004 |
-
ORTAMISEMI kupokea vifaa vya
uchaguzi toka kwa Mpiga Chapa wa Serikali/Wazabuni wengine -
Kununua vifaa
visivyopatikana kwa Mpiga Chapa wa Serikali. |
ORTAMISEMI |
|
12. |
19/9-8/10/2004 |
ORTAMISEMI
kusafirisha vifaa vya uchaguzi kwenda kwenye Halmashauri |
ORTAMISEMI |
|
Wasimamizi
wa Uchaguzi kuendesha Semina za Wasimamizi Wasaidizi wa Uchaguzi |
WASIMAMIZI
WA UCHAGUZI |
||
|
13 |
9/10-23/10/2004 |
Msimamizi
wa Uchaguzi kusambaza vifaa vya uchaguzi kwenye Vijiji, Mitaa na Vitongoji |
WASIMAMIZI
WA UCHAGUZI |
|
14. |
23/10/2004 |
Wasimamizi
wa Uchaguzi kutoa maelekezo ya uchaguzi |
WASIMAMIZI
WA UCHAGUZI |
|
15. |
28/10-4/11/2004 |
Katibu
Tawala wa Mkoa kuteua Kamati ya Rufaa |
KATIBU
TAWALA WA MKOA |
|
Siku
ya kuchukua na kurudisha fomu za uteuzi |
WASIMAMIZI
WA UCHAGUZI |
||
|
16. |
4/11/2004 |
Siku
ya uteuzi |
WASIMAMIZI
WA UCHAGUZI |
|
17. |
5/11/2004 |
Kuwasilisha
pingamizi malalamiko dhidi ya uteuzi |
WASIMAMIZI
WASAIDIZI WA UCHAGUZI |
|
18. |
6/11-7/11/2004 |
Kusikiliza
malalamiko/pingamizi ya uteuzi |
WASIMAMIZI
WASAIDIZI WA UCHAGUZI |
|
19. |
8/11-19/11/2004 |
Mikutano
ya Kampeni |
WAGOMBEA |
|
20. |
20/11/2004 |
Wasimamizi
wa Uchaguzi kutoa tangazo la mdomo juu ya uchaguzi kesho yake 21/11/2004 |
WASIMAMIZI
WA UCHAGUZI |
|
21. |
21/11/2004 |
Siku
ya Uchaguzi wa Vitongoji. |
-
WAPIGA KURA -WASIMAMIZI
WA UCHAGUZI |
|
22. |
27/11/2004 |
Wasimamizi
wa Uchaguzi kutoa taarifa ya mdomo juu ya Uchaguzi wa Vijiji |
WASIMAMIZI WA UCHAGUZI |
|
23. |
28/11/2004 |
Siku
ya Uchaguzi wa Vijiji na Mtaa |
-
WAPIGA KURA -
WAGOMBEA -
MSIMAMIZI WA UCHAGUZI |
|
24. |
6/12-11/12/2004 |
Kuitishwa
kwa mikutano ya kwanza ya Halmashauri mpya za vijiji na Kamati za Mitaa |
MAAFISA
WATENDAJI WA VIJIJI NA WENYEVITI WA MITAA |