RATIBA YA UTEUZI WA WAGOMBEA URAIS, UBUNGE, UWAKILISHI,   UDIWANI NA VITI MAALUM WANAWAKE

 

 

Katika kikao chake cha tarehe 15/02/2005 Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM iliyokutana Mjini Dodoma chini ya Mwenyekiti wa CCM, Rais Benjamin Mkapa imepitisha ratiba ya uteuzi wa wagombea Urais, Ubunge, Uwakilishi,   Udiwani na Viti Maalum Wanawake.

 

Ratiba iliyopitishwa ni kama ifuatavyo:-

 

(A)     KUCHUKUA NA KURUDISHA FOMU

 

 

MWAKA

NAFASI YA UONGOZI

MWANZO WA KUCHUKUA FOMU

MWISHO WA

KURUDISHA FOMU

 

2005

Rais wa  Zanzibar  na Mwenyekiti Baraza la Mapinduzi

 

 

1 Machi 2005

15 Aprili  2005 Kabla ya Saa 10:00 jioni

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

1 Machi 2005

15 Aprili  2005 Kabla ya Saa 10:00 jioni

 

(B)     VIKAO  VYA UCHUJAJI NA UTEUZI WA WAGOMBEA  URAIS

 

 

 

MWAKA 2005

 

 

TUKIO

 

 

27  Aprili 2005

 

 

Kamati Maalum ya Halmashauri Kuu ya Taifa kuwajadili waombaji wa  Nafasi ya Rais wa Zanzibar

 

 

29  Aprili 2005

 

 

Sekretarieti ya Halmashauri Kuu ya Taifa

 

 

  2 Mei 2005

 

 

Kamati Kuu Kutoa Mapendekezo kwa Halmashauri Kuu ya Taifa

 

 

  3 Mei 2005

 

 

Halmashauri Kuu ya Taifa kuchagua jina moja la Mgombea Kiti cha Rais wa  Zanzibar na kupendekeza jina/majina ya Wagombea

U-Rais  wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

 

 

  4 Mei 2005

 

 

Mkutano Mkuu Maalum wa Taifa Kuchagua Jina moja la mgombea Kiti cha  Rais wa  Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

 

 

 

 

2.0     WAGOMBEA UBUNGE NA UWAKILISHI/VITI MAALUM - WANAWAKE

 

(A)    KUCHUKUA NA KURUDISHA FOMU

 

MWAKA

NAFASI YA UONGOZI

MWANZO WA KUCHUKUA FOMU

MWISHO WA KURUDISHA FOMU

 

2005

Ubunge

1/08/2005

3/08/2005 kabla ya saa 10.00 jioni

Uwakilishi

1/08/2005

3/08/2005 kabla ya saa 10 .00 jioni

 

(B)     UTEUZI WA WABUNGE/WAWAKILISHI/VITI MAALUM WANAWAKE

 

MWAKA 2005

TUKIO

4-6 Agosti 2005

Kura za maoni katika Majimbo

7 Agosti 2005

Mikoa kuchagua wagombea 5 wa kila Mkoa (UWT)

8 Agosti

Kamati za Siasa za Wilaya

 

9 – 10 Agosti 2005

 

Kamati za Siasa za Mikoa zitajadili

Pia wagombea Ubunge/Uwakilishi Viti Maalum Wanawake

Kamati Maalum ya Halmashauri Kuu ya Taifa kuwajadili wagombea Ubunge/Uwakilishi wa aina zote.

11 Agosti 2005

Baraza Kuu la UWT kuandaa orodha ya wagombea wote nchini

12-13 Agosti 2005

Sekretarieti ya Halmashauri Kuu ya Taifa.

15 Agosti 2005

Kamati Kuu Maalum

16 Agosti 2005

Halmashauri Kuu ya Taifa kuteua wagombea Ubunge na  Uwakilishi wa jimbo na Viti Maalum Wanawake

17 Agosti 2005

Kutangaza Uteuzi

 

 

3.0              RATIBA YA UTEUZI WA MADIWANI

 

         3.1     Tarehe 22 - 29 Juni 2005

Kuchukua na kurudisha fomu

 

3.2     Tarehe 01 -  05 Julai, 2005

 

(i)     Mikutano Mikuu  ya CCM Maalum ya Kata/Wadi kuwapigia  kura za maoni wagombea Udiwani wa Kata/Wadi

 

(ii)              Tarehe 08 - 10 Julai 2005 Mikutano Mikuu ya UWT Wilaya kuwapigia kura za maoni Wagombea Udiwani wa Viti Maalum  Wanawake.  Kila Katibu wa UWT Wilaya apange  na kuitisha Mkutano Mkuu huo katika kipindi hicho.

 

3.3     Tarehe 11 - 12 Julai, 2005

Kamati za Siasa  za Kata/Wadi kuwajadili wagombea Udiwani  wa Kata/Wadi

 

3.4     Tarehe 13 -  20 Julai  2005 ,

(i)       Kamati za Siasa za Wilaya kuwajadili Wagombea Udiwani wa aina zote na kuandaa orodha ya majina ya wagombea Udiwani wa Viti Maalum kwa kuzingatia idadi inayotakiwa kwa mujibu wa Sheria ya Uchaguzi (hivi sasa idadi hiyo itakuwa kubwa kidogo kuliko robo ya Kata/Wadi zote zilizomo katika Jimbo la Uchaguzi)  Orodha hiyo itawasilishwa kwa Tume ya Uchaguzi.

 

(ii)              Tarehe 24 - 26 Julai 2005, Kamati za Siasa za Mikoa kuwajadili wagombea wote wa Udiwani wa Kata/Wadi katika Mikoa.

 

3.5     Tarehe 24-26 Julai  2005

Kamati za Siasa za Mikoa kutoa mapendekezo ya wagombea Udiwani wa aina zote.

 

3.6     Tarehe 9 – 10  Agosti 2005

Halmashauri Kuu za Mikoa zitateua wagombea Udiwani wa Kata/Wadi/Viti Maalum.  Mara baada ya uteuzi huo, Wenyeviti na Makatibu wa CCM  wa Mikoa wataondoka kwenda kuhudhuria Mkutano Maalum wa Halmashauri Kuu ya Taifa wa tarehe 14-16  Agosti, 2005. 

 

NB: Majina ya walioteuliwa yatatangazwa siku moja na ya   wagombea Ubunge/Uwakilishi kwa tiketi ya CCM.

 

3.7            Tarehe 16 -17  Agosti, 2005

 

Siku za kutangaza majina yote ya wagombea Udiwani wa Kata/Wadi,  Uwakilishi na Ubunge kwa tiketi ya CCM.  Utaratibu huu utazuia kutokea kwa migogoro baina ya wagombea Udiwani na Ubunge kwa upande mmoja na wagombea Udiwani na Uwakilishi kwa upande mwingine

 

3.8             Tarehe ……(Nomination Day) kwa mujibu wa Tume ya Uchaguzi (NEC na ZEC)

 

(1)              Atakayechukua fomu kugombea kiti cha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania atatakiwa apate wadhamini wa-CCM 250 kutoka Mikoa isiyopungua 10.  Kati ya hiyo, Mikoa 2 iwe ya Zanzibar.

 

(2)              Atakayechukua fomu ya kugombea kiti cha Rais wa Zanzibar atatakiwa apate wadhamini wana-CCM 250 kutoka  Mikoa isiyopungua 3 ya Zanzibar.  Kati ya hiyo, Mkoa mmoja uwe wa Pemba .

 

(3)              Wagombea kiti cha Urais hawapigiwi kura za maoni.  Wao hutafuta wadhamini Wana-CCM 250 kwa mujibu wa Kanuni za uteuzi katika kipindi kilichowekwa.

 

(4)              Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (NEC) hawaruhusiwi kuwadhamini Wagombea Urais kwa kujaza fomu za Wagombea wa nafasi hizo.