TANU na ASP toka mwanzo vilikuwa ni vyama
vya ukombozi vilivyojengeka kwenye msingi wa demokrasia.
Kwa mfano, pendekezo la Mwalimu Julius K. Nyerere la kuunganisha
vyama lilipitishwa na TANU na ASP kwa njia ya kidemokrasia.
TANU na ASP walipeleka suala zima la kuunganisha
vyama kwa wanachama wenyewe kwani ndio wenye vyama.
Wanachama hao katika matawi yao walitakiwa
wajadili nakutoa maoni yao kuhusu suala la kuunganisha TANU
na ASP ili kiundwa Chama kimoja cha Mapinduzi.
Kazi hiyo ilifanyika kwa ufanisi kama ilivyoagizwa
na Halmashauri Kuu za Taifa za TANU na ASP. Licha ya wanachama
kujadili na kutoa maoni yao, kwa Zanzibar viongozi wa ASP
walipwewa nafasi ya kujadili na kutoa maoni yao katika vikao
vyote vya Chama.
Wanachama walijadili na kutoa maoni yao kwanza
ndipo wakafuata viongozi katika Halmashauri za vikao mbalmblai
vya ASP. Angalia majedwali na. 1 na 2 ambayo yanaonyesha
matokeo ya maoni ya wanachama wa TANU na ASP kuhusu kuunganishwa
vyama. Matokeo ya Maoni ya Wnachama wa TANU kuhusu kuunganishwa
TANU na ASP
| Matawi |
Idadi
|
Asilimia
|
| Idadi
ya Matawi ya TANU |
6,639
|
100.00
|
| yaliyokutana |
6,427
|
96.81
|
| yaliyokutana |
212
|
3.19
|
| yaliyokubali |
6,424
|
99.95
|
| yaliyokataa |
3
|
0.05
|
| Idadi
ya matawi madogo ya TANU |
38
|
100.00
|
| Matawi
Madogo yaliyokutana |
38
|
100.00
|
| Matawi
Madogo yaliyokubali |
38
|
100.00
|
| Matawi
Madogo yaliyokataa |
Hakuna
|
0.00
|
|
Chanzo:
Chuo cha CCM Kivukoni (1981) Historia ya Chama cha TANU
1954 hadi 1977, (Dar es Salaam : Mpiga Chapa wa Serikali)
Takwimu hizi zinaonyesha kuwa zaidi ya asilimia
99 ya matawi yote ya TANU yaliyokutana, yalikubali Chama
chao kiunganishwe na ASP ili kiundwe Chama kimoja cha Mapinduzi.
Matokeo ya Vikao na Wanachama wa ASP kuhus Maoni ya Kuunganishwa
TANU na ASP. Matawi Idadi ya matawi ya ASP yaliyokubali
yaliyokataa Wanachama Idadi ya wanachama wote Idadi ya wanachama
waliokubali Idadi ya wanachama waliokataa Idadi 257 257
Hakuna Idadi 103,983 103,574 409 Asilimia 100.00 100.00
0.00 Asilimia 100.00 99.00 0.04 Chanzo: Taarifa na Mapendekezo
ya Tume kuhusu Mfumo wa Siasa Nchini Tanzania, Kitabu cha
Kwanza (Dar es Salaam: KIUTA, 1991) Ibara ya 125 ASP, kama
ilivyokuwa kwa TANU, ilifanya zoezi hili kwa uangalifu mkubwa.
Matokeo yanaonyesha kwamba, matawi yote ya
ASP 257 yalikubali ASPiunganishwa na TANU na kiundwe Chama
kimoja cha Mapinduzi. Aidha, wanachama wa ASP zaidi ya asilimia
99 waliunga mkono pendekezo la kuviunganisha vyama vya TANU
na ASP.
Baada ya vyama hivyo kupokea matokeo ya maoni
ya wanachama wao, Halmashauri Kuu ya Taifa ya TANU na ile
ya ASP, zilikutana na kufanya kikao cha pamoja mwezi Oktoba
1976.
Katika mkutano huo iliteuliwa Tume ya watu
20 iliyopewa jukumu la kutayarisha Katiba ya Chama kipya.
Mwenyekiti wa Tume hiyo alikuwa Marehemu Sheikh Thabit Kombo
na Katibu wake alikuwa Mheshimiwa Pius Msekwa.
Tarehe 21 Januari 1977 Mkutano Mkuu wa pamoja
wa Vyaa vya ASP na TANU ulipitisha pendekezo la Halmashauri
Kuu za ASP na TANU. Pendekezo hilo lilisema: "Sisi wajumbe
wa Mkutano Mkuu wa Taifa, wa pamoja wa TANU na ASP tuliokutana
leo tarehe 21 Januari 1977, Mjini Dar es Salaam, chini ya
Uongozi wa pamoja wa Mwalimu Julius K. Nyerere, Rais wa
TANU na Ndugu Aboud Jumbe, Rais wa ASP, kwa kauli moja tunasema
na kutamka rasmi kuvunjwa kwa Tanganyika African Natoinal
Union (TANU) na Afro-Shirazi Party (ASP) ifikapo tarehe
5, Februari 1977 na wakati huo huo kuundwa kwa Chama kpya
cha pekee na chenye uwezo wa mwisho katika mambo yote kwa
mujibu wa Katiba."
Azimio hilo lilisisitiza kwamba TANU na ASP
havikuamua kujivunja kama vyama kwa kuwa vimeshindwa kutekeleza
majukumu yao.
Kwa hakika TANU na ASP ni vyama vilivyopata
mafanikio ya kipekee katika Afrika katika kuyatekelezamajukumu
yao ya kihistoria na mafanikio hayo ndio yaliyowezesha vyama
hivyo kujivunja vyenyewe.
Katika Mkutano Mkuu huo a pamoja, Mwalimu
J.K. Nyerere alichaguliwa kuwa Mwenyekiti wa CCM, Ndugu
Aboud Jumbe kuwa Makamu wa Mwenyekiti wa CM na Ndugu Pius
Msekwa kuwa Katibu Mtendaji Mkuu wa CCM. Chini ya uongozi
wao CCM ilipata mafanikio makubwa.