MKUTANO MKUU WA NANE WA TAIFA WA CCM NOVEMBA, 2007

 

nembo.gif

 

Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama Cha Mapinduzi inawakaribisha Wajumbe wote Mkoani Dodoma kwa ajili ya kuhudhuria Mkutano Mkuu wa Nane wa Taifa, utakaofanyika tarehe 3 – 4 Novemba 2007.  Mkutano huo utakuwa ni wa uchaguzi.

 

Mkutano Mkuu utafanya kazi ya kuwachagua Viongozi wa Chama, watakaokuwa madarakani kwa kipindi cha miaka mitano; (2007 – 2012).  Aidha, Mkutano Mkuu utapokea taarifa ya kazi za Chama, kwa kipindi cha mwaka 2002 hadi 2007 na taarifa za Serikali za utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2000 hadi 2005.

 

Kamati ya Utendaji ya Maandalizi ya Mkutano Mkuu imeandaa na kupanga huduma mbali mbali za malazi, chakula, usafiri, matibabu, burudani na huduma nyinginezo muhimu kwa wajumbe. Huduma hizo zitapatikana kwa wajumbe kwa muda wote watakapokuwepo hapa mjini Dodoma, kwa lengo la kufanikisha Mkutano.  Maelezo kamili kuhusu huduma hizo yanapatikana katika kitabu hiki.

 

Ikiwa utatokea upungufu au kasoro ya aina yoyote katika kipindi cha mkutano, Wajumbe wanaombwa wasisite kuwaarifu viongozi wa Kamati zinazohusika, ili waweze kuwahudumia mara moja.

 

KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI

……………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………

UTARATIBU WA MAPOKEZI, HUDUMA ZA MAKABRASHA NA VITAMBULISHO

 

Mapokezi

Mabasi yote kutoka Mikoani yaende moja kwa moja Makao Makuu ya CCM Dodoma ambako watawakuta waelekezaji (guides) na kuwaongoza mahali pa kwenda.

 

Makabrasha ya Mkutano Mkuu wa Taifa wa CCM na Vitambulisho, vitatolewa na Kamati zinazohusika.

 

Makatibu Wasaidizi/Wahasibu wa CCM wa Mikoa ndio wenye wajibu wa kuwachukulia Wajumbe wa Mikoa yao Makabrasha na Vitambulisho vyao.

 

 

Huduma ya Posho

Malipo ya posho na malipo mengine yanayohusu Mkutano Mkuu wa CCM wa Taifa, yatalipwa na Kamati ya Fedha.

 

Makatibu Wasaidizi/Wahasibu wa CCM wa Mikoa ndio wenye wajibu wa kufuatilia malipo ya Wajumbe na Waasisi wa Mikoa yao.

 

Huduma ya Afya

Vituo vya afya vitakavyowahudumia Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Nane wa Taifa wa CCM, vimeandaliwa katika maeneo yafuatayo:

(i)                   Makao Makuu ya CCM

(ii)                 Ukumbi wa Kizota

(iii)                St. Gasper

 

 

 

 

 

 

Ulinzi na Usalama

               

Suala la Ulinzi na Usalama wa Mkutano Mkuu wa Nane wa Taifa wa CCM ni jukumu la kila Mjumbe na lipo mikononi mwa kila mmoja.

 

Ingawa ulinzi na usalama umeimarishwa katika sehemu zote za malazi, burudani, eneo la Kizota na Mji wa Dodoma kwa ujumla, Wajumbe wanatahadharishwa na kushauriwa kutotembea mmoja mmoja, hususan wakati wa usiku.

 

Vitambulisho vitatolewa kwa Wajumbe wote, Wasikilizaji, Waalikwa, Maafisa, Waandishi wa Habari na Wahudumu.  Hakuna mtu atakayeruhusiwa kuingia ndani ya Ukumbi wa Mkutano bila kitambulisho.  Kwa hiyo, ni muhimu kwa kila mhusika wakati wote kuwa na kitambulisho chake.

 

 

 

Mpangilio wa Malazi ya Wajumbe